Ndoto: Kumvuta mtu mkono ili atoke kwenye shimo la maji taka

Meaning?

SSP-0300.jpg
 
Habari wanajamvi,usiku wa manane nimeota nipo na zuchu nimemshika mkono tukitembea kimadaha sana,sijui wakuu hii ndoto ina maana gani hasa ukizingatia imenijia saa nane za usiku
 
Kuna mdogo wangu wa kike alifariki mwaka 2017, kifo chake kiukweli kilikuwa na utata.. Japo tulimswalia na tulimzika na mazishi yake niliyasimamia mimi mwenyewe, sasa hii ni mara ya pili naota analia kwa uchungu huku ameniangalia, usiku wa leo nimeota ananingalia huku analia kwa uchungu sana mwisho wa siku ilibidi nimkumbatie kwa kumbebeleza na akanyamaza na ndio nikashtuka usingizini
Nenda parokia iliyokaribu uliza ofisi wanakoandikisha nia za misa, andikish nia ya misa ya kumuombea marehemu mdogo wako, hiyo hali haitajirudia. Misa inasaliwa kila siku hivyo siyo lazima uende jumapili. Nimeandika kwa kutambua kupitia mwandiko wako kuwa wewe siyo mkatoliki ila kwa vile binadamu wote tukishakufa dini tunakuwa dini moja nenda kaweke nia ya misa kwa ajili yake.
 
Tumekuwa tukiota ndoto kila siku za aina mbalimbali na katika matukio tofauti tofauti wakati mwingine tumekuwa tukijiuliza kuwa kwani ndoto hii ilimaanisha nini lakini tumekuwa tukibakia njia panda tukiwa na maswali mengi sana.

Leo hii ntakusogezea aina za alama (symbolism) ambazo ni common au tuseme ujirudia mara kwa mara kwa waotaji walio wengi kiasi cha maana zake kuwa bayana kwa wafasiri ndoto, kwa kuwa ndoto ni njia ya pili ya akili kuzungumza yenyewe na kujipatia ufumbuzi kiroho na kimwili.

Ndoto zimegawanyika katika pande kuu mbili; Ndoto zinazoacha Kumbukumbu na Ndoto zinazosahulika baada ya kitendo cha kuota.

Ndoto zinazoacha Kumbukumbu ambazo ndizo hasa uleta maswali mengi ugawanyika katika makundi makuu manne;
(a) Ndoto za Kufurahisha
(b) Ndoto za Kutisha
(c) Ndoto tulivu lakini nje ya mipaka ya kifikra (maono)
(d) Ndoto za fedheha

Kwa kuwa kitendo cha kuota huwa kinakuwa mara nyingi ni kama stori na kina matukio mengi na kila mtu uota kivyake, hatuwezi kumtafsiria kila mtu ndoto yake bali katika kila ndoto kuna ile dhima kuu/ishara ambayo kila mtu uiona kwa wakati wake kwenye ndoto na asijue maana yake, hicho ndicho ntakachokusogezea hapa.

1. Kuendesha Gari

Ukiota unaendesha gari (na haikuwa matamanio ya akili yako) jua kuwa umefikia hatua ya kuweza kuyaongoza maisha yako mwenyewe, hongera.

Lakini ukiota kuwa kuna mtu mwingine ndiye kashika usukani na wewe ni abiria- kama ukimbaini sura basi tambua mtu huyo ndiyo anayeshikilia hatima ya maisha yako na kama usipombaini jua kuwa umewaachia usukani wa maisha yako watu wengine ndiyo wakuamulie.

2. Kufanya mitihani

Ulishamaliza shule lakini umekuwa bado muhanga wa kufanya mitihani ndotoni-unaandamwa na mitihani ya kimaisha na utapitia magumu mpaka ufahulu ndo usonge mbele.

3. Kurudia maisha ya shule

Unaota matendo uliyokuwa ukitenda mara kwa mara ulipokuwa shule licha ya umri ulionao- kuna jambo unakumbushwa juu ya maisha yako ya nyuma kipindi ulipokuwa na displine ya kila kitu ikiwemo muda, urafiki, uvumilivu n.k jaribu kuijeuza katika maisha yako ya sasa uishi vyema au ufanikiwe.

4. Kufanya mapenzi

Je unafanya mapenzi na mtu unayemfahamu au uliyemtaka kimapenzi hata kama haikufanikiwa- hii ni starehe ya akili tu haina shida ni sawa na ndoto nyevu.

Je, unaota unafanya mapenzi na mtu usiyemjua, kiumbe cha ajabu au umefedheheka au kujihisi karaha baada ya ndoto- jua kuwa unaandamwa na roho za mapepo au jini.

5. Mbwa

Imetokea katika ndoto zako umemwona mbwa, umeng'atwa na mbwa,unakimbizwa au unachezea mbwa (na wewe si mtu anayependa mbwa au kuwa nao muda mwingi) - hii ni ishara kuwa roho ya uzinzi ishakuvaa kama unaendekeza ngono badili mienendo yako.

6. Kupanda

Ukiona kwenye ndoto unapanda chochote iwe ni ngazi, kamba au chochote kile kuelekea juu- hii ni ishara njema kuwa utafanikiwa au utapandishwa cheo kazini.

7. Kushuka

Kushuka kwa namna yeyote ile kutoka juu na kurudi chini- ni ishara mbaya ya kuporomoka kimaisha.

8. Kuofia kudondokea shimoni/kujiona unadondokea katika umbali mrefu ambao hujui mwisho wake.

Ni ishara inayoashiria kuwa bado unasafiri ndefu katika maisha yako ya hapa duniani, subira na tahadhari ni muhimu mpaka kufikia lengo.

9. Kupaa

Ukiota unapaa iwe una mabawa, au unapaa mithili ya superman na ikiwa kitendo hiki ukupatia furaha- jua kuwa ni roho yako imefikia kiwango cha juu cha utulivu hivyo kinastarehe na hamna tatizo.

10. Kuoga

Kuota unaoga ni ishara ya kuondokana na mabaya iwe ni matendo,laana au dhambi hivyo umekuwa msafi kiroho,

Endapo ukibaini katika ndoto maji unayoogea ni masafi basi ni habari njema ila kama ni machafu ni ishara ya mabalaa au magonjwa kukuandama.

11. Kula nyama

Kula nyama ya haina yoyote ile ndotoni iwe ni mbichi, iliyopikwa au choma ni ishara mbaya ya kukumbwa na mikosi au kuandamwa na roho za kuzimu.

12. Kula pamoja na wengine/familia

Ukijiona unakula na wengine katika kundi au wanafamilia na marafiki huku mood yenu ni yenye furaha hii ni ishara kuwa maisha unayoishi hivi sasa ni yenye kukupa furaha.

Tofauti na hapo kula peke yako au na watu usiowajua si ishara njema lakini ikitokea wakati wa kula ujafanikiwa kula hii ni ishara njema ya kuwa na bahati nzuri katika mambo yako.

13. Kunywa maziwa

Ikitokea unakunywa maziwa hasa freshi katika ndoto huku ukiwa na furaha pasina shaka hii ni ishara njema ya kufanikiwa kimaisha lakini ikitokea maziwa haya yanakutia mashaka,au ulishinikizwa kuyanywa au yananuka ni ishara ya kurogwa au kuharibikiwa.

14. Nyoka

Ukimwona nyoka yeyote yule katika ndoto yako ni ishara ya uadui. Ikitokea ukamuua-hiyo ni ishara njema kuwa umeishinda roho ovu

Na ikitokea akakugonga wakati unapambana nae ni ishara kuwa adui yako au mchawi amefanikiwa au anakaribia kukudhuru hivyo wapaswa kujilinda zaidi.

15. Kuua

Ukiona umetekeleza kitendo chochote cha mauaji katika ndoto iwe kwa kukusudia au pasipo kukusudia wakati jambo hilo halikuwa na umuhimu wowote katika kujiokoa- jua unaandamwa na roho ya mauti.

16. Kufa

Ukiota umekufa ni ishara ya mwanzo mwema wa maisha mapya au phase nyingine tena ya maisha ya hapa duniani imeanza tena na ni ishara ya kuishi maisha marefu.

17. Kuota marehemu

Ukiota marehemu anaongea na wewe au anakuomba umpe au umfanyie kitu fulani au mnapiga stori za kawaida -jua ni kweli kuwa roho zenu bado zina mawasiliano na unapaswa kufikiria ni ujumbe gani marehemu anajaribu kukupa au ni kitu gani hakukamilisha anachotaka umsaidie kukikamilisha.

18. Kuongea kiingereza

Kama ujuhi hata kingereza cha salamu lakini ghafla huko zako ndotoni unatiririka ung'eng'e bila taabu- ni ishara ya kupata ufumbuzi juu ya jambo ulilohisi haliwezekani kwa njia itakayokustaajabisha.

19. Kuimba

Kuota unaimba ndotoni na unajikuta unafatisha beti na stanza zake pasipo kukosea huku ukihisi mpaka na ala za muziki unazisikia -ni ishara kuwa unatakiwa kuamka na ukazime mziki uliouacha ukiimba kwani unaufanya ubongo wako ushindwe kupumzika.

20. Kuota umeamka na unajaribu kutoka kitandani na haiwezekani

Ni ishara ya kuhamka katika mwili wa ndotoni (kuhisi umehamka kumbe bado unaota) hii haina madhara yeyote zaidi ya kukupa uzoefu namna ubongo wako unavyotenda kazi.

21.Kuota huna nguvu mwilini kabisa

Kuota kuwa nguvu zimekuishia kiasi kwamba huwezi inua hata kidole au unapumua kwa taabu au umekabwa- Ni ishara ya mlalo mbaya hivyo akili inajaribu kukukumbusha ufanye lolote mwili upate oksijeni ya kutosha, aidha uvute hewa mara nyingi kisha ujitingishe ghafla ili mwili upate nguvu na wewe uweze kujigeuza au kuhitimisha haina uhusiano wowote na zimwi.

22. Kuota unatenda hisani/watoa msaada

Ni ishara ya kufanikiwa kwa kutenda yaliyo mema.

23. kuota unawanga au unawangiwa na watu unaowafahamu hasa ndugu, familia au marafiki

Ni ishara kuwa wachawi wanakupumbaza na wanakutumia katika shughuli zao za kishirikina hivyo unapaswa kuwa makini kabla ya kutoa shutuma.

24. Kuota anga iwe ni nyota, mwezi au jua

Ni ishara ya kuanza au kufunguka kwa jicho la kiroho na hivyo jumbe nyingi utazozipata kwa namna hii ni maono.

25. Kuota mtu maarufu

Kumwota mtu yeyote maarufu awe ni msanii, mwanasiasa, mchezaji n.k ni ishara nzuri ya kufanikiwa au kujitwalia heshima au umaarufu.

26. Kuota unalia/una wasiwasi

Ni ishara nzuri kuwa utafanikiwa katika magumu yako na utakuwa na mwenye furaha.

27. Kuota uko uchi mbele za watu

Ni ishara kuwa kuna jambo lisilo zuilika litakutia fedheha au aibu.

28. Kuota unafanya mapenzi na ndugu au mzazi

Ni ishara ya upendo usio na mashaka kati yako na uliyemwota, hivyo usifikirie ni ndoto mbaya kwa kuwa imeenda kinyume na ulivyodhania.

29. Kuota unakojoa

Ni ishara kuwa kibofu cha mkojo kimejaa na hivyo unapata ishara uamke ukakojoe hivyo ukishindwa kutofautisha kati ya ndoto na reality lazima uachie mzigo palepale kitandani.

30. Kuota kinyesi

Endapo umejipaka au kuona au kuguswa na kinyesi katika ndoto ni ishara njema kidunia kuwa utapata fedha.

Lakini ikitokea umezungukwa na mazingira machafu yenye vinyesi na hali inayokera ni ishara ya kuchafuliwa nyota na wanaokuonea kijicho.

31. Kuota umeokota pesa

Ni ishara ya kupoteza hela zako au kufilisika.

32. Kuota umeng'atwa

Ni ishara ya kurogwa au kurushiwa uchawi

33. Kuota unakimbizwa

Ni kukimbia kivuli chako mwenyewe, ni ishara ya kujikataa na kuyakimbia matatizo yako mwenyewe ambayo unapaswa kuyatatua kwa maana popote utakapoenda yatakufuata tu.

34. Kuota umefukuzwa kazi

Ni ishara kuwa tegemea habari njema kazini kwako.

35. Kuota umefeli mtihani

Ni ishara kuwa tegemea habari njema.

36. Kuota maji

Ni ishara ya utulivu wa nafsi na mood yako, yakiwa matulivu ni ishara njema ila yakiwa na mawimbi makali ni ishara ya kukumbwa na hali ya hasira kali au moody

37. Kuota unasali

Ni ishara njema ya kuendelea kukomaa kiroho nakuzishinda roho ovu.

38. Kuota unapita kwenye msitu wakutisha au hifadhi yenye wanyama wakali

Ni ishara kuwa roho yako inawindwa na roho za mauti na ikiwa unawapita wanyama hao pasipo kudhurika basi tambua kuwa unakinga imara ya kiroho inayokuponya dhidi yao.

39. Kuota unacheka

Ni ishara mbaya na kinyume chake inamaana utalia na kujuta.

40. Kuota unaomboleza au kuzika

Ni ishara kuwa utasahau mateso yote na kufurahia maisha.

41. Kuota unapanda mlima mrefu kwa shida na kufika kileleni

Ni ishara kuwa utapitia njia ndefu na ngumu kuelekea yalipo mafanikio yako ila ukishayafikia utokaa ushuke tena kimaisha.

42. Kuota umedumbukia kwenye shimo refu lenye kiza kinene na huwezi kutoka

Ni ishara ya kujihisi kukwama katika kila jambo lako na uoni wapi pa kujishkiza.

43. Kuota unagombezwa

Ni ishara kuwa unakanywa au unatakiwa ujirekebishe na kuacha kufanya jambo fulani maishani mwako ambalo si sahihi.

44. Kuota umeachwa na usafiri

Usafiri ni maisha na wewe ndiye msafiri, hii ni ishara kuwa soma majira ya nyakati na ujipambanie mapema kabla haujaachwa na muda.
Mods washauunganisha huu uzi.. dah!
 
Mods wakati mwingine wanasababisha usumbufu usio wa lazima, wafuatiliaji wengi wa uzi wa tafsiri za ndoto wananiijia PM kuuliza kulikoni uzi nimeufuta kumbe mods washafanya yao.
 
Mods wakati mwingine wanasababisha usumbufu usio wa lazima, wafuatiliaji wengi wa uzi wa tafsiri za ndoto wananiijia PM kuuliza kulikoni uzi nimeufuta kumbe mods washafanya yao.
Msaada tutani, mtu ameota ndoto kua aliyekua mwanaume wake ameuawa kwa kunyongwa, kastuka usingizini analia vibaya kwa sababu ya ndoto hiyo, nini tafsiri ya ndoto hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada tutani, mtu ameota ndoto kua aliyekua mwanaume wake ameuawa kwa kunyongwa, kastuka usingizini analia vibaya kwa sababu ya ndoto hiyo, nini tafsiri ya ndoto hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndoto inajaribu kuongelea uhalisia wa hisia zake za ndani juu ya mahusiano yaliyopita na muhusika kwa kuwa kuna kiashiria cha haja ya mapenzi hayo kukoma na kusauliwa (kuuawa/kunyongwa) lakini hisia ya kujali (kilio cha uchungu) bado inaonesha kuwa mwotaji bado ajaamua ku-move on completely.

Jawabu;
1. Kumzika moyoni na kumsahau kabisa na uanze maisha yako mapya ya kimahusiano pasipo yeye.
2.Kuufata moyo na kutafuta uwezekano wa kuyajenga upya au kuamua kutengeneza ukaribu nae wa kirafiki, chaguo ni lako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom