Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

1. Kulipa deni la chama cha ushirika Nyanza 5 billion
2. Uwanja wa ndege wa kimataifa Mbeya (Songwe)
3. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigoma
4. Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam
 
Kulipa madeni ya vyama vya Ushirika vyote na akatoa mfano wa Nyanza, Corecu..... etc,
 
7. Njia ya mkato kawe junction ifunguliwe na JWTZ - Imefuguliwa
8. Meneja Mtibwa Sugar Afukuzwe - Kafukuzwa
9. Sumaye apokwe shamba la ekari 320 Mororgoro
10. ....
11. ...
 
7. Njia ya mkato kawe junction ifunguliwe na JWTZ - Imefuguliwa
8. Meneja Mtibwa Sugar Afukuzwe - Kafukuzwa
9. Sumaye apokwe shamba la ekari 320 Mororgoro
10. ....
11. ...
Watanzania wote waamue kupima UKIMYA......yeye kapima na majibu yake tumeambiwa ila mimi Mzitto SIYAAMINI. Yatakuwa ni KINYUME cha ukweli!
 
Kwa kuanzia mimi nakumbuka AHADI hizi hapa chini
  1. Meli kubwa ya usafiri- Ziwa Victoria
  2. Maboti ya Usalama Ziwa Victoria na Tanganyika
  3. Daraja la Kigamboni
  4. Barabara za juu kwa jiji la Darisalama
  5. Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa- Bukoba
  6. Ununuzi wa Ambulance Bajaj (400)
  7. ...
  8. ...
  9. ...
Na orodha hii iendelee... karibuni sana wanajamvi

Kama kweli wapiga kura wake wako satisfied na watapigia kula hayo mambo hapo juu,basi Tanzania yangu na yako itabaki masikini hata kama kutapatikana mafuta sehemu yoyote ya nchi,na kikazalishwa kiwango sawa na kile kinachozalishwa na nchi ya Kuwait.
Huyu mtu "atajenga" barabara za juu kwa juu, hili nadhani atalifanikisha kwa sababu barabara anazozizungumzia yeye ni kama ile ya pale Manzese ambayo watu wanapita juu na magali yanapita chini.
Aliahidi ajira lukuki,kumbe aina ya ajira anazo zungumzia ni kama vile NG'OTI amefungua saluni ya kutengeneza nywele, na akaweka wasusi wawili hii anasema ni moja ya ajira alizotengeneza kutekeleza ilani ya chama.....!!! Jamani nyie easily satisfied jaribuni kuchanganua mambo,huo uwanja wa ndege mpya anaoahidi kuujenga utawezekanaje wakati hata ule wa pale Songwe unasuasua tu...........!!!!
 
Taifa Stars kuingia fainali za kombe la dunia 2018 - dalili zinaonyesha
kutokana na Uranium umeme kuwa bure 2020
 
Wadau, nimeikuta hii Mwananchi....nimeileta ili tujadili maoni ya wasomaji hapo chini kabisa....


JK: Nikipata urais kero ya maji kukoma Send to a friend
Friday, 10 September 2010 08:39




Jakaya Mrisho Kikwete
Hussein Semdoe Handeni
MGOMBEA wa Urais kupitia CCM Jakaya Kikwete, juzi aliwaahidi wakazi wa Wilaya ya Handeni kwamba akipata urais atahakikisha kero ya maji inakoma.

Wilaya ya Handeni ni moja ya wilaya ambazo wakazi wake wanapoteza muda mwingi kusaka maji hususani katika miji ya Handeni, Mkata na Chanika ambako kwa miaka zaidi ya 10 iliyopita haina maji ya uhakika.

Kikwete ambaye anasaka kipindi cha kumalizia miaka 10 inayoruhusu kikatiba rais kuongoza nchi, alisema akipata uongozi nawamu ya bpili ana uhakika kumaliza matatizo hayo.

Hata hivyo hakufafanua kama atarekebisha vipi kasoro hiyo ambayo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita aliiona.

Lakini alidokeza kwamba atauboresha mradi wa maji wa Handeni Trank Men (HTM), unaosambaza maji kutoka katika mto Pangani maarufu kwa jina la Ruvu na kusambazwa maeneo mbalimbali hadi katika kijiji cha Manga mpakani mwa Mikoa ya Tanga na Pwani.

Ahadi hiyo aliitoa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara alipokuwa akijinadi kwa wananchi akiwaomba kumchagua pamoja na mbunge na madiwani wa CCM, uliofanyika katika uwanja wa Azimio mjini Chanika wilayani Handeni.

"Chagueni mafiga matatu, uraisi, wabunge na madiwani wote kutoka CCM. Ahadi zetu mmeona zinatekelezwa, tuliahidi barabara za lami katika kampeni zilizopita. Sasa kero kubwa iliyobaki Handeni ni maji, lakini itatoweka. Tutafumua na kuujenga upya mradi wa maji wa HTM, ili maji yasambazwe sehemu nyingi, mjini Chanika, mkata hadi katika Kijiji cha Manga" alisema Kikwete na kuongeza kuwa.

Mradi ule utajengwa upya kwa kuweka mabomba mapya. Huyu mbunge wenu Dk Kigoda amekuwa akinisumbua kila mara akihimiza ujenzi wa barabara za Handeni kwa kiwango cha lami. Baadaye kukawa na maneno maneo wakamsumbua kutaka kumkwamisha, nikawaambia hapana haiwezekani pitisheni" alisema huku wananchi wakimshangilia kufurahia ahadi hizo na mafanikio hayo.

Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho taifa alisema kuwa upembuzi yakinifu unafanywa ili barabara ya Handeni kwenda Kibirashi, Wilayani Kiteto, Kondoa hadi Singida kujengwa kwa kiwango cha lami ili kuimarisha mawasiliano yatakayoinua uchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.



Add this page to your favorite Social Bookmarking websites



Comments
12

+1
#17 HAJI 2010-09-10 17:34

Watanzania tumesituka na ahadi za uongo na sasa kila anayeomba tutampa miaka mitano tu ya kumjaribu akiboronga tunampiga chini. Hata Dr Slaa tunampa miaka mitano kama wewe akileta usanii mpira anapasiwa Lipumba.CCM pumzikeni na muende shule mjifunze hakuna nchi inaendeshwa bila viwanda.
Quote


+3
#16 Mjengaji 2010-09-10 15:12

JE KIKWETE HAKUFIKA HANDENI KATIKA KAMPENI ZA AWAMU ILIYOPITA? MBONA AMEJISAHAU SANA KIASI KWAMBA ANAJINADI KANA KWAMBA NDO ANAOMBA RIDHAA YA WATU WA HANDENI MARA YA KWANZA KUINGIA IKULU?

KUMBE WAONGO MAKINI - WASIOSAHAU WANACHODANGANYA - HAWAJAZALIWA!!! CONFIDENCE YA WAO-M NI MAZOEA NA UVUMILIVU WA WATZ WA KUKUBALI LONGOLONGO ZA WAO-M KUWA NI UKWELI KILA AWAMU. UGONJWA HUU NDIYO KIKWAZO KIKUBWA CHA MAGEUZI HASA KWA WALE WANAOLISHWA "CHANGARAWE" MCHANA MWEUPEEEE.

WATZ, TUTIBU MASIKIO YETU NA FAHAMU ZETU ZILIZOZOEZWA USANII ILI TUPONYWE NA JINAMIZI LA WAO-M. TIBA PEKEE NI, AWAMU HII HATUDANYIKIIIII IIII! LAZIMA WAO-M WAPIGWE CHINI ILI TAIFA LIPONE. TUKO SERIOUS NA HATUTAFANYA KOSA TENA!
Quote


+1
#15 Mbunge Mtarajiwa 2010-09-10 15:02

Sizani kama kuna ukweli juu ya hili... Alafu si ajabu wakati anayasema hayo watu walimshangilia kama ndivyo bas walikuwa wanakung'ong'a. Tumechoka ahadi zisizotekelezek a iko wapi kauli ya maisha bora kwa kila Mtanzania si mlituahidi ivyo miaka 5 iliyopita... tunataka mabadiliko na ahadi zinazotekelezek a sio ntawajengea kiwanja cha ndege kipya wakati vilivyopo vmewashinda kuvirekebisha au Ntawaletea Meli mpya ziwa viktoria wakati ata fidia za wahanga waliopata ajali na Mv bukoba hawajalipwa
Quote


+6
#14 Mac d 2010-09-10 14:5
5
heeey mr president you cant be sirious by promising thing which you failed to fulfill before, so what do you think of us?stupid, fools or what?plizzz give us a break and start parking your staff and get out of IKULU....
Quote


+5
#13 Joseph 2010-09-10 14:43

Tumechoka kusikia marudio! Mheshimiwa angalia bana usije ukasema ukiwa Raisi utageuza IKULU hospitali! We gave you the chance but you have failed to show us mishemishe! Hatudanganyiki
Quote


+5
#12 Michael Zunzu 2010-09-10 14:17

Hazina haikuwa na pesa za kutosha kuongezea mishahara ya wafanya kazi wa kima cha chini hata kwa miaka 8, mabilioni hayo yatatoka wapi kusaiodia utekelezaji wa miradi mikubwa yote hiyo? Kusema ukweli ni kuhadaa watu, nitasikitika kama kunawatu wanaweka matumaini yao kwa hayo yanayosemwa.
Ni heri ya kusema ukweli kulingana na uwezo wa serikali, jamani mbona Mwalimu Nyererer alikuwa akisemaukweli tu, Mkuu wetu kajaa uswahili wa Pwani, hatuutaki sisi!
Quote


+3
#11 ASNATH 2010-09-10 13:39

ACHA KUTUFANYA SISI WATOTO KIKWETE, HIVI HUONI AIBU KURUDIA MAKOSA YA 2005. AHADI KIBAO BILA UTEKELEZAJI. WANAOKUPIGIA MAKOFI UNAPOTOA AHADI ZA UONGO NI WANAFIKI KWANI HATA WAO WANAJUA KUWA HUWEZI KUTIMIZA AHADI UNAZOTOA.
Quote


+6
#10 Ninawi 2010-09-10 12:55

ASANTE JK KWA KUTUONA VICHAA.INAWEZEKANA UNA TATIZO LA AKILI.Unbeliavable!
Quote


+7
#9 Riches 2010-09-10 12:12

WAKATI UMEFIKA HUYU MTU JK APIMWE AKILI TUSIJEKUA TUNAMLAUMU BURE KUMBE HIZO MIELEKA AMEKUA AKIZIPATA ZIMESHAATHIRI NA UBONGO JAMANI. HUU UONGO NA USANII UMEZIDI KWA HUYU MWENZETU. INAWEZEKANA KABISA KAMA WAVYOSEMA NI AWAMU YAKE YA MWISHO HAKUNA ATAKAYEMUULIZA TENA, YE ATAKUA HAYUKOOOOOOOO
Quote


+8
#8 hamisi 2010-09-10 11:37

kwanini usianze [NENO BAYA]liza tatizo la maji dsm unapokaa kabla ya kutatua tatizo la maji kijijini??, huo ni UONGO wa wazi.
Quote


-2
#7 hussein mazila 2010-09-10 11:35

Quoting haiba:
I think JK is either nuts or completely crazy

kwanini utukane?kuwa na nidhamu na jenga hoja na si [NENO BAYA].
Quote


+6
#6 M7 2010-09-10 11:34

WIZI MTUPU
Kwa pesa gani atafanya hayo?
Safari za kwenda ulaya na amerika labda zikiisha.....
JK Acha uongo Jamani.... haya utaanguka hadharani hadi huko Ulaya.
Quote


+4
#5 hamisi 2010-09-10 11:28

WATZ NI WATU WA AJABU SANA, KUNA WATU WANASEMA SIWEZI KUMPIGIA KURA SLAA KWA SABABU YA SWALA LA NDOA KWAMBA SIYO MWAMINIFU LAKINI WAKATI HUO HUO YUKO TAYARI KUWAPIGIA KURA MAFISADI WANAOIBA MATRILIONI YA SHILLINGI AMBAYO YANGENUNUA MADAWA HOSPITALINI,JEN GA SHULE NA BARABARA. WATZ AMKENI NYIE MFUMBUE MACHO MTAKUWA HAMNA MTU WA KUMLAUMU BAADA YA HILI.
Quote


+3
#4 haiba 2010-09-10 11:01

I think JK is either nuts or completely crazy
Quote


+3
#3 Msaudia 2010-09-10 10:46
Wananchi wa TZ, zipokeeni ahadi za JK kwa tahadhari kubwa sana. JK hipi ni kipindi chake cha mwisho anaweza kuahidi hata kujenga barabara angani, ana uhakika hakuna atayemuuliza kipindi kinachokuja. Hivyo yuko tayari kumwaga ahadi nyingi za uongo ambazo hakuna atakayemuuliza baadaye. Ninawahurumia sana kama mtaziamini hizo ahadi hewa za JK. Ni vizuri tukajiuliza kwamba alikuwa wapi kutekeleza hizo ahadi katika miaka mitano yote ya mwanzo aliyokuwa ikulu? DANGANYA TOTO!
Quote

source: JK: Nikipata urais kero ya maji kukoma
 
Wananchi wa TZ, zipokeeni ahadi za JK kwa tahadhari kubwa sana. JK hipi ni kipindi chake cha mwisho anaweza kuahidi hata kujenga barabara angani, ana uhakika hakuna atayemuuliza kipindi kinachokuja. Hivyo yuko tayari kumwaga ahadi nyingi za uongo ambazo hakuna atakayemuuliza baadaye. Ninawahurumia sana kama mtaziamini hizo ahadi hewa za JK. Ni vizuri tukajiuliza kwamba alikuwa wapi kutekeleza hizo ahadi katika miaka mitano yote ya mwanzo aliyokuwa ikulu? DANGANYA TOTO!

Nimecheka kusoma hayo maoni, mwandishi naona kishasau kuwa JK kaahidi kujenga barabara za angani. Ameahidi kubadili Kigoma iwe dubai, amesema kigamboni itakuwa ulaya, na kisha kali kabisa ili kuvuruga kila alichosema - akaaahidi kuwapatia bajaji 400 kinamama wajawazito ... yaaaaakyhi
 
Mwangalieni kwa makini JK akitaka kutoa ahadi anacheka then anatoa, maana yake anapiga changa la macho. Mi nilishamshitukia mapema. Anaahidi harafu anatoa stori huku akimalizia na kicheko akijua kuwa kapiga changa la macho.
 
Hiyo Dar mji mkuu hadi leo maji ni shida tena sii kidogo na ameshindwa kabisa...
Kifupi ktk maswala muhimu ya kijamii yakitanguliwa na ELIMU na AFYA - ameshindwa, Maswala ya kiuchumi yakitanguliwa na - MAJI na UMEME ameshindwa, hivyo mikakati yoyote ile iwe kilimo kwanza au ile ya MKUKUTA haiwezi fanikiwa ikiwa msingi wake tumeshindwa kuujenga..
 
Adanganyiki mtu wala mie situmi upuuzi huu kwa mtu. Acha waendelee kudanganyana wana sisi m wenyewe, maana wao kila analosema kikwete wao huwa wanakenua meno kushangilia. Hawajui saa ngapi kawadanganya.
 
we need changes ,this guy cannot accomplish anything ,he is surrounded by incompetent people
 
Sasa, mgombea wa kiti cha Urais kwa kupitia chama fulani anapoahidi kuleta maji kwenye kijiji fulani, mgombea ubunge wa eneo hilo kupitia chama hicho hicho ataahidi nini? Kuleta ndoo za kuteka maji au?
 
Back
Top Bottom