Operation Chaos: Lowassa, Chenge, Rostam et al; Don't Quit CCM!

Viongozi ni viziwi, vipofu na wajinga. Zaidi ya yote hao wanaojiita usalama wa Taifa wameoza kwani ndio wanaowalinda hao viongozi vipofu, viziwi na wajinga ili waendelee kutawala
 
Kweli Kikwete na hiyo timu yako tunaomba mlaaniwe maana mliamua kumtosa mzee Sita kisa eti alikuwa akiruhusu mijadala ambayo ilikuwa ikiwagusa ninyi, sasa mkaamua kutuwekea PILATO wa kike anayetoa maamuzi sawa na PILATO aliyetoa hukumu ya kucharazwa viboko kwa Yesu, huyu speaker anawatumikia na kuwalinda Mafisadi wa nchi hii akiwemo kinara wao Lowasa.
 
na mwandishi wetu


23rd june 2011


email.png

b-pepe



printer.png

chapa



comment_bubble.png

maoni




hosea e(10).jpg

mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru), dk. Edward hoseah


vijana wanaojiita wazalendo wa umoja wa vijana wa ccm (uvccm) wanaosoma katika chuo kikuu cha dar es salaam wamemuandikia barua mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru), dk. Edward hoseah, na kumpa siku 14 kuhakikisha watuhumiwa wa kashfa za ununuzi wa rada, richmond na kagoda agriculture limited wanafikishwa mahakamani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana sinza, jijini dar es salaam kwa niaba ya vijana hao, mjumbe wa mkutano mkuu wa uvccm mkoa wa dar es salaam, agustino matefu, alisema kuwa wameamua kumuandikia dk. Hoseah barua kwa kuwa wameona watuhumiwa hao hawajafikishwa mahakamani mpaka sasa.
Matefu alisema, katika barua waliyomwandikia mkurugenzi juni 21, juni mwaka huu, walimtaka amchukulie hatua waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya richmond, edward lowassa, na mbunge wa igunga, rostam aziz ambaye anahusishwa na dowans na kagoda.
Alisema kuwa yeye na vijana wenzake wazalendo wa uvccm, wanataka ufafanuzi pia kuhusu mbunge wa bariadi magharibi, andrew chenge, anayehusishwa na tuhuma za ununuzi wa rada ya kijeshi kwa bei kubwa kuliko thamani halisi na kuhoji kwa nini hajafikishwa mahakamani wakati takukuru ina taarifa zote.
"kwa nini hawa watuhumiwa hawafikishwi mahakamani, au takukuru inawaogopa?" sisi, kama vijana wazalendo wa uvccm tunampa mkurugenzi wa takukuru siku 14 za kushughulikia suala hilo na kuhakikisha kuwa watuhumiwa hao wanafikishwa mahakamani," alisema matefu akiwa ameongozana na mmoja wa wajumbe wa umoja wa wazalendo wa uvccm aliyetambulishwa kwa jina moja la lawrence.
Aliendelea kusema kuwa kama hatua hiyo haitakuwa imechukuliwa baada ya siku hizo, watafanya maandamano nchi nzima wao kama umoja wa vijana wazalendo wa uvccm kuwaambia watanzania kwamba naye (dk. Hoseah) anashirikiana na mafisadi kuwakandamiza watanzania.
"kama ofisi yako itashindwa kutekeleza jambo hili, tunafanya maandamano nchi nzima lengo kuu ni kuwaambia watanzania kuwa na wewe si mtu safi na unashirikiana na mafisadi na tutaishinikiza serikali iifute takukuru, " alisema matefu.
Aidha, matefu alisema kama takukuru itashindwa kutekeleza hayo baada ya siku 14 walizopewa maandamano yataazia chuo kikuu cha dar es salaam hadi ofisi za takukuru.
Nipashe ilipomtafuta dk. Hoseah kuthibitisha kama ameipata barua ya vijana hao, hakupatikana na katibu muhtasi wake alisema kuwa alikuwa nje ya ofisi. Hata alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani, ilikuwa imefungwa.
Kwa upande wake msemaji wa takukuru, doreen kapwaya, alikataa kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kuwa hakuwa na taarifa kama dk. Hoseah amepata barua hiyo.
Kumekuwa na tuhuma dhidi ya viongozi hao watatu wakihusishwa na kupotea kwa umaarufu wa ccm, wakielezwa kuwa katika mabadiliko yaliyopewa jina la kujivua gamba wanatakiwa waache nafasi zao ndani ya chama. Wote ni wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa (nec) ya ccm.
Sababu kuu wanazotuhumiwa nazo ni kwamba wamekuwa na tuhuma za ufisadi, juu ya richmond, wizi wa fedha za akaunti ya madeni ya nje (epa) ndani ya benki kuu ya tanzania kupitia kampuni ya kagoda na rada ya bei mbaya.
Lowassa na chenge walijiuzulu nafasi zao serikalini kutokana na tuhuma hizo. Chenge alijiuzulu aprili mwaka 2008 kutokana na kashfa hiyo wakati huo akiwa waziri wa miundombinu (sasa ujenzi) baada ya kubainika kuwa na akaunti nene ughaibuni visiwa vya jersey. Alikuwa na akiba ya dola milioni moja, fedha zilizodaiwa kuwa huenda ni mgawo wa rushwa ya rada.
Alikana tuhuma hizo. Rostam amekuwa akihusishwa na kagoda ambayo ilichota sh. Bilioni 40 za epa lakini hadi leo wahusika wake hawajafikishwa mahakamani. Rostam naye amekana kuijua kagoda licha ya kutumia anuani ya kampuni yake.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa arusha, james ole millya, amesema hajamwomba radhi katibu wa ccm wa mkoa, mary chatanda, kwa kuwa hajapata taarifa rasmi ya kufanya hivyo.
Alisema taarifa za kutakiwa kumwomba radhi katibu huyo kwa madai ya kumtolea kauli za matusi, kashfa na lugha za udhalilishaji amezisoma kwenye vyombo vya habari.
"hayo nimeyasoma kwenye vyombo vya habari, lakini mpaka sasa sijapata barua rasmi inayonielekeza nifanye hivyo," alisema.
" lakini hata kama ningepata maelekezo ya kumuomba msamaha, hayupo hapa mkoani, yupo dodoma kwenye vikao vya bunge," alisema.
Chatanda ambaye ni mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa tanga, alithibitisha kuwa hajaombwa radhi na millya.
Alisema kuna njia mbili ambazo mtu anaweza kufanya ili kuomba radhi, moja ikiwa ni kuandika barua na nyingine kwenda kuonana naye uso kwa uso.
Katika kikao cha dharura cha halmashauri kuu ya ccm mkoa wa arusha, kilichofanyika juni 6, mwaka huu, kuzungumzia mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya siasa ya mkoa ya kuwavua uanachama wa ccm wanachama wanane akiwemo millya na mjumbe wa baraza kuu la uvccm, mrisho gambo, kwa madai ya kufanya maandamano haramu yaliyokuwa yakishinikiza kung'olewa kwa chatanda, kilimtaka millya kumwomba radhi chatanda.
" mimi niliondoka siku ya pili baada ya kikao kile, nipo dodoma…bado hajaomba radhi," alisema.
Aidha maamuzi ya kikao hicho, pia yalimtaka gambo kumwomba radhi aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la arusha mjini, dk batilda burian, kwa madai ya kumtolea matusi, kashfa na udhalilishaji wa kijinsia.
Akizungumza na nipashe kwa njia ya simu, gambo alisema kuwa yupo mjini dodoma kwa mambo ya kifamilia.
Alisema kuwa : "binafsi bado sijapata barua yoyote kuhusu maamuzi ya halmashauri kuu ya ccm mkoa, yanayomtaka kufanya hivyo…hayo maneno nayasoma tu kwenye magazeti, nikipata barua labda nitakuwa na cha kusema."



chanzo: Nipashe

uraisi 2015 hadi watanzania tubaguane wenyewe kwa wenyewe, kama hawa ni wazalendo kna wenzao ndani ya uvccm sio wazalendo kwanini bado wapo ndani ya jumuia hiyo? Unafiki wa kutafuta urais
 
Hao wamekosa cha kufanya, tokea lini mwizi akampeleka mwizi mwenzake Mahakamani huku wote ni wahusika na ushahidi upo, fanyeji mambo mengine tu UVCCM
 
LOwassa alishasema ikifika wakati akachoka na kelele zinazopigwa juu yake juu ya yeye kuitwa Fisadi, sasa atalazimika kusema hata yale ambayo alikuwa hataki kuyasema, mnataka kumuumbua mpaka Raisi wenu wa nchi sasa,
 
LOwassa alishasema ikifika wakati akachoka na kelele zinazopigwa juu yake juu ya yeye kuitwa Fisadi, sasa atalazimika kusema hata yale ambayo alikuwa hataki kuyasema, mnataka kumuumbua mpaka Raisi wenu wa nchi sasa,
Sasa hivi ndiyo serikali inajifanya inataka chenji ya rada wakati wa kesi walikuwa hawaonekani. Hivi kwa nini wabunge wa ccm + Cheyo nao wamejiingiza kwenye huu mkenge. Hivi ni hela za nani zimewapeleka huko uingereza wakati BAE ilishatoa tamko kuwa hizo hela tutazipata thru NGO. Nashindwa kuelewa kwa nini watanzania ni mbumbum hivi. Wanatafuta hizi hela wazichakachue tena. I am tired of illusions!
 
Sasa hivi ndiyo serikali inajifanya inataka chenji ya rada wakati wa kesi walikuwa hawaonekani. Hivi kwa nini wabunge wa ccm + Cheyo nao wamejiingiza kwenye huu mkenge. Hivi ni hela za nani zimewapeleka huko uingereza wakati BAE ilishatoa tamko kuwa hizo hela tutazipata thru NGO. Nashindwa kuelewa kwa nini watanzania ni mbumbum hivi. Wanatafuta hizi hela wazichakachue tena. I am tired of illusions!

Wewe hujui wakisafiri hivi wanalipwa posho ya usafiri - perdiem?. Kimsingi kilichowapeleka UK ni posho waliyolipwa kwa ajili ya safari na siyo kufuatilia pesa za Rada. Bila shaka pesa wanayotumia ni za walipa kodi wa Tanzania.
 
Hao wamekosa cha kufanya, tokea lini mwizi akampeleka mwizi mwenzake Mahakamani huku wote ni wahusika na ushahidi upo, fanyeji mambo mengine tu UVCCM

Tatizo lao hawasomi alama za nyakati, hawajui CCM imefika ukingoni. Hawa vijana ni ma oportunist, wamekula chaka.
 
LOwassa alishasema ikifika wakati akachoka na kelele zinazopigwa juu yake juu ya yeye kuitwa Fisadi, sasa atalazimika kusema hata yale ambayo alikuwa hataki kuyasema, mnataka kumuumbua mpaka Raisi wenu wa nchi sasa,

Ametishia nyau siku nyingi akidhani kwamba kauli hiyo itakuwa kinga kwake. Aliposhtukiwa na Mwalimu miaka ile, aliiba na JK? Hivi unadhani anampenda huyo Rais kiasi cha kumstahi kama anavyodai? Kama anaweza kumsingizia mtoto wa Rais mauongo yote hayo, angeshindwaje kusema yale ya ukweli kuhusu rais kama yapo? Jamaa yuko kwenye kona, anataka kujiokoa na anadhani kauli hiyo itatusahaulisha dhambi zake. Kamwe hatutamsamehe!
 
I hate to pat myself on the back. Hawa jamaa wamefuata ushauri vizuri. Na Rostam akafuata ushauri wangu vizuri. So... operation chaos is still on. The best thing fo EL na AC to do is to go back kwenye majimbo yao kufanya mikutano ya hadhara kuzungumzia mafanikio ya CCM as if nothing is going on..
 
I hate to pat myself on the back. Hawa jamaa wamefuata ushauri vizuri. Na Rostam akafuata ushauri wangu vizuri. So... operation chaos is still on. The best thing fo EL na AC to do is to go back kwenye majimbo yao kufanya mikutano ya hadhara kuzungumzia mafanikio ya CCM as if nothing is going on..

I was looking for this one maana baada ya kusoma ile thread ya yaliyotokana na CC nikajikuta naikumbuka sana hii thread! Thanks.
 
I was looking for this one maana baada ya kusoma ile thread ya yaliyotokana na CC nikajikuta naikumbuka sana hii thread! Thanks.

yeah nilikusoma ikabidi niende kuitafuta. Ila CCM imejionesha kuwa iko dhaifu sana. Yaani, kama RA asingejiuzulu kwa ajili ya biashara zake wote wangekuwa bado wamo...
 
yeah nilikusoma ikabidi niende kuitafuta. Ila CCM imejionesha kuwa iko dhaifu sana. Yaani, kama RA asingejiuzulu kwa ajili ya biashara zake wote wangekuwa bado wamo...

Tena kuliko wakati wowote ule, lakini yote hii inatokana na kufanya mambo kutegemea busara za mwenyekiti ambaye in today's CCM terms ni mwenyekiti is alwayz right, lazima aungwe mkono no matter what. Yaani hilo tamko lao ni full vague statements, hakuna specifics hata mahala pamoja. Maybe ni just kutimiza wajibu anyways tusioipenda hiyo GOP ni furaha yetu.
 
So.. stay put, enjoy your position, work like ever before and don't mind the new CCM leadership. They can't do a damn thing.

And this is exactly what is happening, kweli bongo tambarare!!!!!!!!!
 
this is great!! maana vinginevyo wataonekana wanawaonea tu. Unless walete specific charges against them, la kusema kuwa waachie ngazi kwa maslahi ya chama haingii akilini.
 
this is great!! maana vinginevyo wataonekana wanawaonea tu. Unless walete specific charges against them, la kusema kuwa waachie ngazi kwa maslahi ya chama haingii akilini.

Wanawaogopa na sababu kubwa pengine ni ushirika wao na wale ambao CCM hiyohiyo inataka tuamini ni wasafi! Kubwa kuliko ni JK na Mkapa, maana how do you accuse Chenge ukamwacha Mkapa au do the same to EL ukamwacha JK?
 
Je wanajamvi mnadhani EL & AC wanaweza kujiondoa gamba chamani pasipo kumwaga mboga? Nijuavyo mimi, unless wameahidiwa mambo mazuri kwenye business zao au post nyingine (may be nje ya nchi), ni vigumu kuondoka kwa shinikizo la kitoto namna hii. Kimsingi kama alivyosema Mwanakijiji, labda waje na specific charges against them. Hii ina maana charges hizo, lazima ziwalenge hao EL& AC peke yake, lakini endapo in the process mzee wa kaya na magwiji wengine watakuwa implicated, jitihada hizo zitafutika na kuonekana ni uzushi mtupu.
 
Kuondoka kwao ni mwiba kwa CCM,kutokuondoka ni mwiba kwa CCM.
Wao kwa nafasi zao wapime tu ukubwa wa tatizo.
Ama CCM ife wakiwemo ama waiache ife yenyewe.
 
Back
Top Bottom