Oneni huyu mzungu anavyoichafua Tanzania.Hii ni email aliyomwandikia mwenzake

kama ni kweli,safi sana...............hivi anajua ni kiasi gani babu yake alichukua kwa chifu Mangungo???
Yaani nimecheeeka mpaka basi. Sasa Mdau, tukianza kulipizana visasi kwa mambo ya enzi zileee, tutafika kweli?
 
Airport Bongo nuksi sana, Ukisahau kuweka kofuli sanduku lako, Hesabu maumivu kama kwa vitu vidogovidogo kama Camera, Simu, Ipod n.k.

Wageni wangu mwaka jana walilizwa hapa hapa Bongo ilikua aibu sana.

ukweli mtupu, the guy is right, mambo yanayofanyika tanzania huwezi kuyaona nchi nyingine dunian, ni aibu sana
 
Sikubaliani naye, huyu alikuja kuvuna Tanzania bahati mbaya wamemstukia akakasirika, mzungu gani ana msaada na mswahili na aende asirudi akipenda awaambie na familia yake wasije kuibia nchi yetu
 
Eti kuna watu wanatetea na wengine hata kumshuku huyu mzungu! Labda kama hayajakukuta huwezi kujua. Au kwa vile aslan unaishi katika nchi ya kisirani kwa hiyo umezoea the status quo?
Mimi yamenikuta kama hayo na zaidi. Niliingia mpaka wa Horohoro kutokea Mombasa. 'Bahati mbaya' nilikuwa naendesha gari lililosajiliwa Kenya. Nasema bahati mbaya maana kwa maafisa wa Tanzania kila kitu kigeni ni sababu ya kupata pesa za bure. Nadhani wana mentality kila asiye Mtanzania ana fedha nyingi. Kwa maana nyingine: Tanzania ni ya mwisho duniani.
Kwa kukata stori, nilibambikwa makosa ya kitoto na kuamriwa kulipa zaidi ya laki 2 ! Moja ya makosa hayo ni kupaki vibaya niliposimamishwa na polisi, kutokuwa na triangle, fire extinguisher, spare tyre ambayo wanadhani haina upepo mzuri, tinted mirror kioo cha nyuma, na kukata insurance ya COMESA ya wiki (badala ya mwezi). Imagine kama sikukata kabisa! Tanzania hata haimo katika nchi za Comesa, lakini wajinga hawa hawajui wala hawasomi!
Hapo mpakani nililazimisha kuchanjwa yellow fever kwa dola 50! Hakuna chanjo, watoa dola, wapewa kikadi! etc etc....

Wakati mmoja nilirogwa kuingiza gari kutoka Japan. Huko niliinunua kwa dola elfu tatu. Nilichargiwa zaidi dola elfu 4 hadi naitoa. Given, ni gari ya mwaka 2004, lakini hata ile thamani yake kama walivyoandika Wajapani wenyewe eti ilikuwa na makosa na wao huko Darisalama wanajua zaidi thamani ya gari hiyo!
Vitu kama hivi kwa wakaazi wa Tanzania wanaona ni vya kawaida na pengine haviwadhuru tena. lakini kwa sisi tunaokuja kwa kutembea tu, vinatufanya tusiwe hata na hamu ya kurudi, lau si familia zetu.
Mzungu ana haki na kama nisingekuwa na familia TZ hata mimi 'I would not have set my foot in that cursed country' Tanzania inahitajia revolution. Kwa kweli imefikia mwisho wa uvundo. Hakuna zaidi ya hapo.
 
MY NIGHTMARE IN TANZANIA

From: Ray Bergen

To: Lisana Koliskowski

Hello Lisa

I am glad to be back in America after such a disastrous trip to Tanzania . The most important thing was getting back home safely and seeing my family. The only thing I can assure you is that, I will never set my foot in that country, and will advice anybody planning to visit Tanzania to refrain from doing so. The nightmare started at the airport, when my luggage checked in from Amsterdam disappeared mysteriously in Dar es Salaam . And my inquiry with the airport authorities was forwarded to the police. At the police station (Central) I was told that I could not get help unless I bribe them $500, because they needed the money for fuel and other necessary needs to investigate the theft.Supposedly the police officer did not open the case and turned me to be the criminal, constantly coming to my Hotel room, asking me for money. In short all my four year work was lost with the laptop at the Airport.
Came clearing the vehicle we were supposed to use in the research, from the agents to the customs authorities, the vehicle exceeded the actual cost. I would have paid $38,000 for a $16,000 vehicle. I could not bear being in such a corrupt country and decided to terminate my research, and left the vehicle uncleared after one month of struggle with the customs, who needed money after money and bogus letters. Supposedly these exuberant fees were not supposed to be there in the first place, because all registered NGO’s are supposed to be exempted from paying these taxes and fees, but then the deal had been cooked to rip Muzungu off. Being a Muzungu is being a cash cow in Tanzania . They don’t even ****en know that we are trying to help them. I pity the African continent and her people, I am glad they did not confuse me with Albino.

Please advise any potential traveler to Tanzania to look for alternative country to visit, and if possible pass the message to the State Department as a warning to other Americans intending to visit this poor and corrupt country. I visited Botswana with my family in 2006. I tell you, could not be more satisfied with their politeness and straightforwardness, the same was in
Mozambique where we received utmost hospitality.

Please, be careful and only travel to Tanzania when there is need and not to visit and do not carry any valuable. As soon as you arrive, register with the American Embassy.

Sincerely,


Ray Bergen.

I am not convinced kwamba hii sio story ya kutunga. Sijawahi kuona mtu ambaye amepotelewa na mzigo wake through check in/out likafanywa suala la Polisi hata siku moja. Ukipanda ndege unapewa copy ya namba ya mzigo wako. Ukifika mwisho wa safari yako na mzigo hauonekani anayodaiwa ni airline na wala suala hilo haliwezi kupelekwa polisi. Hivi kuna sababu gani ya kuleta story za kutunga hapa? Na huyu aliyeleta hii thread yeye hayo mawasiliano ameyapata wapi wakati yeye sio mlengwa?

Lets be serious!!!!!

Tiba
 
I am not convinced kwamba hii sio story ya kutunga. Sijawahi kuona mtu ambaye amepotelewa na mzigo wake through check in/out likafanywa suala la Polisi hata siku moja. Ukipanda ndege unapewa copy ya namba ya mzigo wako. Ukifika mwisho wa safari yako na mzigo hauonekani anayodaiwa ni airline na wala suala hilo haliwezi kupelekwa polisi. Hivi kuna sababu gani ya kuleta story za kutunga hapa? Na huyu aliyeleta hii thread yeye hayo mawasiliano ameyapata wapi wakati yeye sio mlengwa?

Lets be serious!!!!!

Tiba
labda hayajakukuta, umewahi kusikia wale trafik police wa himo moshi wana mashine ya kucheki pesa feki barabarani ulishasikia wamekamata pesa ngapi feki
 
labda hayajakukuta, umewahi kusikia wale trafik police wa himo moshi wana mashine ya kucheki pesa feki barabarani ulishasikia wamekamata pesa ngapi feki

Mkuu mimi ni mtanzania na ninaijua vizuri Tanzania. Kuna mengi mabaya yanayofanywa na wafanyakazi wa serikali kuanzia UWT, Polisi, Customs na kwingineko. Mengine yamenikuta mimi mwenyewe na nimewahi kuripoti maovu kadhaa humu JF. Yapo mengi machafu yanafanyika lakini kwa case hii hapa aliyoileta mwenzetu ni story feki na mimi nasema haiwezekani mzigo uliopotea mikononi mwa airline suala lake lipelekwe polisi. Airline wenyewe wanatafuta jinsi ya kumaliza masuala yanayohusu upotevu wa mizigo, period!!!!

Kwa kifupi sipendi story za kutunga kwani zinawapotezea watu muda kuchangia wakati ni kitu cha kupikwa tu!!!!

Tiba
 
Tanzania ndivyo tulivyo wala hajakosea kabisa. Tope mgongoni tumelibeba wanaoliona na kutuambia tu wachafu migongoni mwetu hawakosei.
 
Hiyo barua inaonekana kwangu mimi kama vile imeandikwa na Mwafrika,Mtanzania labda. Hakiandikwa na mtu ambaye Kiingereza ni lugha yake ya kwanza. T

hata mimi sikutaka kuamini kuwa ni mzungu kweli kaandika. Hiyo inglish iko straight sana kwa mzungu kuandika. Pia iko formal sana kwa watu wawili kutumiana email
 
acheni kubeza hivi hayaja wakuta? Si wageni tu, hata na hasa watanzania hunyanyasika sana airports hapa bongo.
Hii nchi ni corrupt na msifunike maovu kwa kufananisha na nchi zingine.
Mbona Kenya na SA ni wastaarabu?
 
Jamani tuseme tu ukweli Bongo wanaiba Airport, wanaiba mahotelini ila tukubali tu waswahili ukweli ukiwekwa wazi hatupendi haka ni kakasoro ketu.Pili kwa upande wa lugha kuongea pia kiswahili sio kuwa kila mtu anakijua hasa kwenye uandishi na hii nimeona ni kwa kila lugha wengi wanakosea kama huamini upewe paper ya kiswahili sidhani kuwa wabongo wote mtapata mia kwa mia kubali usikubali.
 
acheni kubeza hivi hayaja wakuta? Si wageni tu, hata na hasa watanzania hunyanyasika sana airports hapa bongo.
Hii nchi ni corrupt na msifunike maovu kwa kufananisha na nchi zingine.
Mbona Kenya na SA ni wastaarabu?

Hata nchi zote alizozitaja za Botswana, South Africa na Kenya zina corruption index inayofanana tu Na Tanzania. Hii ni cooked story tu ambayo imelenga kuchafua nchi yetu
 
Umekosea spelling, hilo neno huwa halianzi na "U", huwa linaanza na "L". However, nakushauri uende ukaishi Pristina, Kosovo.

Negative affixation is added to a root to change the meaning of a word sa we unataka aanze na L wakati mwenzio lengo lake kukanusha?
 
Thanx Muzungu ushawahi tembelea Caracas!! au anachuki binasfi na Tz lol baba tembea uone halafu utoe mikasfa kama hiyo!!!!
haya ndo mawazo potofu yanayoendeleza ulegelege na ushenzi wa wabongo. nani kakamwambia kwamba kwa vile caracas wanaishi kama wanyama basi ni sawa tu na sisi tukiishi kama wao? ya huko carcas yanatuhusu ni sisi? acha uswahili bana
 
Mzungu yupo sawa. Hapa bongo bana ukiingia kama wewe umetoka nchi ambayo rushwa ni zero degree utadhani ndio umetia mguu jehanamu inayozungumzwa kwenye vitabu vya dini. Mtu unaripoti kuibiwa bado unatakiwa kugharimia upotevu wa mali zako.??
We acha tu..! Kuna siku nimeshawahi kuombwa dollar 10 na mwanausalama humohumo ndani ya uwanja wa ndege! Ila huyo mzungu naye ni wakuja tu....hauwezi kuwa na kazi ya research ya miaka minne ukaihifadhi ndani ya laptop tu bila kuwa na backup..! Na mizigo huwa inapotea hata kwenye viwanja vyao..! Tuseme yeye amepata experience mbaya hapa TZ na inawezekana wapo wengine kama yeye ila wapo wengine wengi tu wanaoisifu sana TZ na baadhi yao wanarudi bongo mara kwa mara na wengine wanaishi kabisa bongo.
 
Back
Top Bottom