Oneni huyu mzungu anavyoichafua Tanzania.Hii ni email aliyomwandikia mwenzake

labda hayajakukuta, umewahi kusikia wale trafik police wa himo moshi wana mashine ya kucheki pesa feki barabarani ulishasikia wamekamata pesa ngapi feki
Hiyo ya Moshi iliniacha hoi...yaani baada ya polisi kugundua kuwa wanepewa hela bandia ya rushwa wakaamua kutafuta kifaa cha kutambua kama fedha ni halali au la ili wasipigwe bao na watoa rushwa. Bongo haiishi vituko.
 
hii email nahisi kuna kuua utalii tz. Airport ya Kenya mayo inaaminika kuwa na wizi uliokithiri kuliko JKNIA.

Ili kuepuka ukiritimba TRA nadhani kungekuwa na sehemu mmoja tu ya kulipia ukifika pale unatoa makaratasi yako yahusuyo mzigo wanafanya ukaguzi wao then unapewa taarifa kiasi gain ulipe ukishalipa wanakupa mzigo wko
 
Ni kweli aliyosema, lakini kama suala la wizi hata kwao upo pia viwanja vya ndege, huyu alikuwa na jambo zaidi ya hilo! UTALII.
 
wakuu sasa napata uhakika kwamba hakuna system inayofanya kazi ipasavyo nchini Tanzania..labda hii system ya hawa madereva wa daladala kurudisha hesabu kwa owners hii haina rushwa wala longo longo kabisa, akicheza kazi hana. Pamoja na hii system ya vinyozi na saloon's zao. - Hii system ya misosi mahotelini pia unaweza kuwekewa wali wa juzi ukalipa 60,000/- kesho yake tumbo mvurugano mnakimbizana kwenda Toilet na familia yako. duh bongo aibu.

No any system that is working 100% perfect in this country!!! mzungu upo sahihi -- pole sana hii ndiyo bongo daresalama ishi kwa ubongo, usiogope mvua inayonyesha mara moja kwa msimu kisha inasepa unakimbia pango - kuwa kidume wa shida starehe ni ulaya tu.
 
Mizigo kupotea airport ni issue ya airliner ambao ndege ikitua wanaiweka ktk baggage carousel (ule mkanda wa mabegi unaozunguka) na wanakuwepo abiria wote kusubiri mizigo yao, usipouona ni issue ya airliner ambao hulipa fidia. Huyo mzungu ni mwongo alitaka kuchakachua insurance ili alipwe.
 
Back
Top Bottom