On Star TV: Gharama za Kuendesha Vyama vya Siasa na Rushwa katika Siasa Nchini Tanzania

Mzee Rutalaka nini tathimini yako katika chaguzi za ndani za CCM zilizotawaliwa na rushwa vurugu na makundi?

Ni kwa kiasi gani katika chaguzi hizi CCM imeweza kutekeleza dhana ya kujivua gamba? Nini nafasi ya TAKUKURU?
 
Mbatia anadai PCCB haiko huru kwakua iko chini ya ofisi ya rais, ok fine!

Tunamuuliza yeye aligombea ubunge akamwagwa chini, JK akamuonea huruma akamtupia nyama ya salala! Yuko mjengoni kwa hisani ya baba mwenye kaya! Je, Anatuthibitishae kua nae yuko huru? Atathubutu kukipa challenge chama cha aliyempa salala?

wanasema adui yako mweke karibu nawe, mbatia hawezi kuipa challenge ccm kwasasa imebak blah blah tu!
 
CCM bila rushwa haitaweza tena kuongoza kwani ndio sera yao kuu katika chaguzi zote hapa nchini
 
CCM haitoi haki kwa kila mwanachama kugombea uongozi kwa sifa zake.

Mfano, hivi ni raia gani wa Tanzania anaweza kugombea uongozi na mke au mtoto wa rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama? Lazima mwenyekiti aoneshe njia kwanza kwa kutoa haki kwa wanachama
 
Asante Yahya,

Wenyeviti wa baadhi ya vyama,hasa vyama vikuu vya siasa kwa maana ya vyama vyenye wabunge na madiwani wengi wasiishie kulalamika tu wachukue hatua ili kutokomeza mdudu huyu rushwa anayetafuna vyama vya siasa kwa sasa na hasa CCM.

Ni hayo tu.
 
Rushwa kuondoka au kupungua ni ndoto kwani maslahi na umaskini kwa mtz ni janga la taifa.
 
Bwana Misoji ameongea pointi sana, ni kweli ili uweze kuwatawala ni lazima uwajengee mfumo utakaoweza kuwatawala utakavyo!
 
Tafadhari Yahaya unapowakilisha hoja tuwekee na namba ya simu.Kweni kwenye runinga kwa sisi tuliopo nje ya nchi tunawafatilia kupitia mtandao namba haionekani natoa pongezi kwa kazi nzuri.
 
Bwana Yahya Mohamed anasema Jumapili ndani ya nyumba atakuwepo mwenyekiti wa CDM na Mwenyekiti wa CCM au mwenye hadhi hiyo!
 
Ccm ndio chama pekee chenye kugawa rushwa na kuvuruga tartatibu na kanuni za chaguzi na hata kuhatarisha usalama wa nchi pale wanapo shindwa ktk chaguzi mbalimbali za kitaifa,kikwete ameilea rushwa na ufisadi ahasa anapotoa msamaha kwa wezi wa epa.nchi imeoza hata wageni hapo ofisini kwenu simuoni anae nena kwa dhati kuhusu kukemea rushwa hata mwenendo wa vyama vyao na mapatano yao na ccm ni rushwa tupu.hote wezi hao
 
manoah

Mzee Rutaraka anafanya siasa tu. Anashindwa kusema waziwazi kuwa CCM imekithiri kwa rushwa. Anatumia blanket statement eti "rushwa iko vyama vyote."

Anaonekana kabisa amekata tamaa. Atuambie ni hatua gani imechukuliwa kwa waliotoa rushwa?
Usipoteze kubishana na asie na manufaa katika maisha ya mtanzania, hukumu ya machungu ya maisha wanayosababisha inawahukumu.
 
Back
Top Bottom