On Star TV: Gharama za Kuendesha Vyama vya Siasa na Rushwa katika Siasa Nchini Tanzania

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Habari za Asubuhi Wakuu,

Jumapili ya leo tutaangazia kuhusu GHARAMA ZA KUENDESHA VYAMA VYA SIASA NA RUSHWA KATIKA SIASA NCHINI TANZANIA. Mswaada huu uliwasilishwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba katika Kongamano la vyama vya Siasa Oktoba 16, 2008.

Tutajadili maaudhui katika waraka huo sambamba na matumiziya rushwa katika chaguzi ndani ya vyama vya siasa na majaaliwa ya Demokrasia Nchini Tanzania.

Wageni:
Prof Ibrahim Lipumba - MKITI CUF
Bw.James Mbatia - MKITI NCCR Mageuzi

Mwanza atakuwepo Mzee Emmanuel Rutalaka
Karibuni Katika Mjadala

NB: Tutahadhari na maswali yanayokinzana na shughuli za Uchaguzi leo
 
Nafurahi kusikia tena toka Yahya Mohamed.

Langu moja tu, ruzuku kwa vyama vya siasa isitishwe, vyama vijiendeshe kwa michango ya wanachama hii itasaidia kuleta uwajibikaji lakini pia pesa yetu ya kodi itaendelea kufanya mambo ya maendeleo.

Watu wanatumia pesa nyingi kushinda chaguzi kwa sababu siasa imegeuka deal, na hii ni kwa sababu ya ruzuku zisizo na sababu, zaidi ya 1.2 bilioni kila mwezi vinalipwa vyama vya siasa kama ruzuku.

Fikiria kama pesa hii tungeiwekeza kwenye vyanzo mbadala vya umeme, leo tusingekuwa na matatizo ya umeme
 
Rushwa huchagizwa na mfumo wa chaguzi zetu zisizo huru, kama mtu amenunua kura kutakuwa na ugum gani kuifilisi nchi?
 
CCM kama chama dola hakiwezi kukwepa kuwa mlezi na mdau mkuu katika kulea rushwa. Mfano ni chaguzi za CCM, chama kimebariki, mwenyekiti kabariki rohoni ila mdomoni analalamika, mamlaka kiserikali anayo kichama anayo,madaraka yananunuliwa.

Leo hii ndani ya CCM kuwa mjumbe wa NEC unazungumza na wakongwe ndani ya chama unaweka dau mezani wanakushauri ni sh ngapi zinaweza kukupa ujmbe. Tuache kuzunguka dawa ni kuiondoa CCM madarakani.

Asante Yahaya.
 
Mzee Rutalaka, CCM ndiye muasisi wa rushwa hapa Tanzania, Baada ya Nyerere kuacha uongozi CCM imehalalisha rushwa, Vyama vingine havina pesa za kuhonga, ila CCM wanatumia rasilimali zetu kutuhonga.

Mzee Rutalaka nakuomba hama Chama nenda kwenye chama kingine cha siasa upeleke mafundisho mazuri uliyonayo Mungu atakubariki kung'ang'ania CCM ambayo rushwa ni sera Mungu atakulaani kwa ubinafsi fanya maamuzi magumu kwa faida ya taifa.
 
Rushwa inatokana na mfumo wa uongozi uliopo hapa nchini, mmojawapo upeanaji wa nyadhifa mbalimbali katika nchi kwa vigezo vya urafiki na ujamaa, hii imekuwa inachangia sana kuunda makundi ya walio nacho na wasio nacho, na hapo ndipo lushwa inaanza tumika kwa walionacho kuwapoteza wasiokuwa nacho, mfano ni yanayotokea chama cha mapinduzi.
 
YAHYA,

Mimi nipo Mwanza, naomba waambie hao wazee, na watanzania wengine kua kwa hapa Africa na especially hapa Tanzania tutegeuza na kubadilisha kila kauli mbiu ya kulaani rushwa, lakini itakua ni kama kuchota maji kwenye ndoo iliyotoboka au kumeza sindano na kutegemea utajisaidia mtarimbo!

China waliliona hilo ndiyo wakawa na mrejesho wa rushwa kwa risasi ya kichwa .
 
manoah

Mzee Rutaraka anafanya siasa tu. Anashindwa kusema waziwazi kuwa CCM imekithiri kwa rushwa. Anatumia blanket statement eti "rushwa iko vyama vyote."

Anaonekana kabisa amekata tamaa. Atuambie ni hatua gani imechukuliwa kwa waliotoa rushwa?
 
Last edited by a moderator:
Rushwa na gharama za uendeshaji vyma inatokana na;-

1. Katika vyama hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kukemea kama ilivykuiwa kwa hayati Mwl. Nyerere

2. Viongozi wanaotakiwa kukemea rushwa uongozi wao ulitonana na rushwa kama inavyoendelea kwenye chaguzi zinazoendelea leo hii....mfano chaguzi za CCM.

3. Hakuna aliye msafi mwenye uwezo wa kukemea mwenzie.

4. PCCB haina meno na haipo huru, inakuwa kama kibaraka na alama ya kuwaonyesha wahisani kuwa tuna utawala bora ili tukizi vigezo vyao vya kusaidiwa.

Kwakuwa wote waliupata uongozi kwa kutoa rushwa, hivyo lazima warudishe gharama zao, faida na kujilimbikizia kwa kufisdi kila jambo.

Kibanga Msese
 
Wananchi haswa sisi wa kawaida tusipoamka, tukapambana iwe kwa maandamano, makelele kwenye vyombo vya habari na kila kona hii rushwa itatuangamiza, tutakosa huduma muhimu katika huduma za kijamii kama vile elimu, afya n.k

hata katika nyadhifa za mbalimbali kwetu ndo itakuwa ni ndoto kabisaa, hv mimi mkulima nisiye na kipato leo hii nikienda kugombea ccm leo nitapata nafasi gani kama sitaishia kuwa mjumbe wa nyumba 10 tu ambaye nawatengenezea watu ulaji?

Vyama vya siasa haswa upinzani hamna dhamira ya dhati ya kutukomboa isipokuwa maslahi yenu binafsi..

Mfano ni kwako mheshimwa Prof. Lipumba; kwanini hutaki kupisha watu wengine waongoze CUF? Hebu ng'atuka useme kwamba unapisha mwingine ajaribu uone kama atakosekana mtu hapo! Binafsi mimi siamini eti wewe tu ndo mwenye vigezo vya kuongoza chama na kugombea urais toka 1995
 
Mwalimu alikemea rushwa kipindi kifupi kabla ya uchaguzi mwaka 1995. Hivyo basi, tuna haki ya kukemea rushwa wakati wa uchaguzi wa madiwani leo.
 
Naomba muulizeni mzee Rutalaka hapo Mwanza kuwa aina ya wakuu wa wilaya tulionao, ambao wengine wanafahamika kuwa walikuwa wanahabari na waliipigia debe CCM na sasa wamepewa ukuu wa wilaya...

Hiyo ni rushwa kwa kwa wanahabari ili waseme CCM na serekali yake vizuri ili waweze kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya. Kwa hivyo, najumuisha kwa kusema 'CCM ndio rushwa"
 
Naomba Prof Lipumba atuambie, ule msafara wa CUF wa kupeleka watu Arusha kwa mabasi kwaajili ya mkutano wa siku moja waliwalipa nini hao watu? Nahisi kulikuwa na rushwa
 
Rushwa ni kansa iliyojikita kwe mfumo wa uongozi uliopo hapa nchini,

Lakini yote haya ni matokeo ya serikali iliyopo madarakani kuwa muumini mkuu wa rushwa! Hata kama tungekuwa na sheria nzuri za kuzuia rushwa kama za babeli ya kale, kama dola iliyopo si adilifu ni kazi bure tu! Chaguzi za Tanzania sasa zinabadili maana ya uchaguzi na kuwa mwenye pesa ndie mshindi!

Rushwa haitaisha mpaka watz kwaujumla tuamue kubadilika, na haitatokea tu bali atatokea mzalendo mmoja tu na kulikomboa taifa na watu wake hata kwa damu, Mtu huyo si mwingine ni CHADEMA tu!
 
Misingi ya Azimio la Arusha naamini bado ipo, ni kiasi cha kuifukua na kusimamisha ukuta mwingine juu ya msingi ule, tukileta ya China hapa tutakuja kukosa viongozi kabisa, kila siku tutapiga risasi viongozi wasiopungua kumi.

Ila ukweli ni kuwa CCM ndiye mama wa Rushwa.
 
Wa SONGEA.

RUSHWA HAPA TANZANIA IPO KATIKA MIFUMO YOTE HAPA TANZANIA SI KWENYE VYAMA VYA SIASA TU,HII INASABABISHWA NA WATU WALIOPEWA DHAMANA YA KUTUONGOZA NA KUPAMBANA NA RUSHWA KUTO KUWA MAKINI,TUNAPINGA RUSHWA KINADHARIA ZAIDI TU HAKUNA JIPYA RUSHWA IMEOTA MIZIZI KWA KUWALINDA WALA RUSHWA.

Asante STARTV.
 
Mbatia anadai PCCB haiko huru kwakua iko chini ya ofisi ya rais, ok fine!

Tunamuuliza yeye aligombea ubunge akamwagwa chini, JK akamuonea huruma akamtupia nyama ya salala! Yuko mjengoni kwa hisani ya baba mwenye kaya! Je, Anatuthibitishae kua nae yuko huru? Atathubutu kukipa challenge chama cha aliyempa salala?
 
Hakuna rushwa mbona hawatajwi? Nanyi hapo studio mnaongea tu kama wapo watajeni
 
Rais analia na rushwa sasa sijui ni ameshindwa kuishughulikia au na yeye ni mmoja wao?

Ninapata wasiwasi na kilio cha rais amirijeshi mkuu kulia kuwa rushwa imekithiri sasa kama yeye ndie mkuu wa nchi na analalamika na tunamuona unafikiri vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla tutaiga vipi?
 
Back
Top Bottom