Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa Demokrasia tarehe 04 Januari 2024

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,696
59,856
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyopewa, alitoa maagizo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kuandaa mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa.

Lengo la maagizo hayo lilikuwa kutoa fursa kwa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi kilichojikita katika kufanyia kazi masuala yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa Nchini Tanzania

View: https://www.youtube.com/live/x3LQPRi8598?si=Um8CK-rCUseVWIEw

1704352709177.png
 
Ni kuhusu Sheria ya tume ya uchaguzi. Mwongoza mada anaeleza kuwa mswada unakuja kuiweka tume ya uchaguzi kuwa huru.

Sheria hii imekuja moja ya dhamira yake ni upekee siyo kutajwa kwenye katiba tu bali kuwa na sheria iliyoainisha vitu mbalimbali.

Ukitaka kujua sheria lazima usome preamble ili ujue dhamira ya sheria. Sheria hii imekuja kubainisha
1. Muundo
2. Majukumu
Utaratibu wa upatikanaji wa wajumbe watume ya uchaguzi nk
 
Mtoa Mada Bwana Alex.
Kikubwa zaidi kuwa na sheria ya tume ya uchaguzi siyo tu kutajwa kwenye katiba. Kupoteza nafasi hii ya kutunga sheria ni muhimu sana.

Machakato wa katiba ni mchakato mrefu.
Wakati huu ukitazama mabadiliko yanahitajika sana kuwa na sheria.

Majukumu ya tume sitaongea maana yameelezwa na vikao vya tume sitavieleza
 
Majukumu ya mkurugenzi wa tume ya uchaguzi namna anavyopatikana na majukumu yake. Kwa kutazama majukumu yake tunataka awe mtu wa namna gani. Ninawaomba muweze kutoa mawazo yenu.
 
Sehemu ya nne ni masharti ya kifedha sitayazungumzia maana yameelezwa.
Sheria hii imetoa mwanya wa kuweza kutunga kanuni katika sehemu ya tano. Utekelezaji wa sheria hii utaonekana kwenye kanuni.

Pamoja na kwamba mapendekezo yametolewa na tume lakini ni muhimu kuwa na kanuni.

Kuitamka sheria pekee kwenye katiba inakuwa ni ngumu kuifanyia mabadiliko.
Kwakuwa sasa hivi kutakuwa na sheria huru. tunaweza kuifanyia marekebisho.

Hatua hii ni muhimu
Bwana Alex Anamaliza kuwasilisha
 
Wachangiaji
Dr. Idda
Mwasilishaji ameweza kutoa maelezo yote. Nina mshukuru na naipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia. Kwa kutuletea mswada huu. Tunaamini utaenda kuongza kiwango cha demokrasia.


Naenda haraka kwenye kifungu cha nane.
8(f) na 9(d) Kifungu kinaeleza kuongeza kwa jinsia. Tafiti zinaonesha kadiri tunapokuwa na usawa wa kijinsia tunapata mawazo kutoka kwenye makundi yote. Kifungu hiki nakipongeza. Hatuangalii tu idadi bali tuweke watu wenye uwezo.

Nimefanya utafiti kwenye upande wa madiwani. Kweli kuna wanawake lakini mazingira wanayofanyia kazi wanakuwa hawawezi. Ni muhimu tuweke watu wenye uwezo.

Kifungu cha 9 sehemu ya tano.
Nafikiri Tangazo liweze kuwafikiwa watanzania wote wenye uono hafifu na wale wenyematatizo ya usikivu.
Tangazo hili tunaamini litaongeza idadi ya watu kuwemo kwenye hizi kamati.

Kifungu 21, 22. Inatakiwa kuwa na watendaji na rasilmali fedha. Tume hii itakapokuwa na watenda na kuwa na raslmali fedha itakuwa inaweze kutenda kazi kwa uhuru.

Wajumbe watano kutafanyika usaili. Naomba kuwe na usawa na kijinsia. Ikitokea watu wote wanafanana basi waangalie jinsia. Siyo kuongeza tu mwanamke kwa sababu ya jinsia.

Kifungu 13. Hili pendekezo linaweza kuwekwa kwenye kanuni na siyo kwenye sheria. Mapema kwa muda gani siku masaa au nini.

Sheria hii tunayoenda kuitunga ya tume ya uchanguzi. Hatjawahi kuwa na sheria hii. Ikitumika vizuri itakuza demokrasia.
 
Dr. Mrisho
Kama alivyosema mwasilishaji wa kwanza na mchangiaji wa kwanza.
Sheria yote inakuwa na madhumuni. Sheria hii ina madhumuni ya kutengeneza sheria moja inayozungumzia tume ya uchaguzi. Kutoka kwenye kutajwa kwenye katiba na kuwa sheria. Ni mwelekeo mzuri.

Je, kuna mambo yanayotakiwa kuongezwa jibu ni ndio. ndio maana tupo hapa.
Eneo nitakalopenda kuchangia, ni dhana nzima ya kuongeza uwazi na kupunguza mamalaka ya rasi katika kupata wajumbe.

Kuwepo usaili wa wajumbe. Nafikiri huu ni mwanzo mzuri wa demokrasia. Tunaweza kujadili njia gani usaili uwe au tunaweza kujadili sifa. Kupunguza mamlaka ya rais ni moja ya kuimarisha demokrasia.

Dhana nzima hii ya kupunguza mamlaka ya rais nadhani ni heri. Kwa kuanzia imeonesha nia njema.

Lakini pia ilisemwa na wakili msomi. Dhana ya kushindanisha watu. Sasa hivi tuna watu wengi wenye uwezo tofauti na zamani.

Huu ni mwazo wa fursa wa kuwa natume iliyo bora zaidi ya hii iliyopo.
 
Mwangoza manda: Mswada huu ni wetu tunauwezo wakutoa mawazo na kupendekeza. Ili tupate sheria iliyo bora na itamaliza kiu ya kila mmoja wetu.
 
Mchangiaji wa kwanza:
Mwenyekit UWT
Uteuzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti. Sheria itamke wazi kuwa mwenyekiti akiwa jinsi moja makamu mwenye kiti awe jinsia tofauti.

Wajumbe wa kambati ya usaili watakuwa watano. Kuwa mmoja atateuliwa na rais kuzingatia jinsia. Ni muhimu kuongeza mmoja kwa kuzingatia jinsia.

Naomba kuongeza ibara mpya. Sheria iongeze uzingatio wa jinsia kwenye uchaguzi.
Tunapendekeza tume isimamie matumizi ya fedha.
 
Yasin Mohame Mwenyekiti wa ngome ya wazee ACT
Makundi maaalum yanayoshiriki uchaguzi.
Sijaona kundi la wazee. Sijawazikia wazee. Sheria zote zimeongea makundi mengine.
Wazee katika nchi hii kimewapa kipaumbele gani. Kwenye sensa wazee tupo 5.7%

Mnafahamu tumezaliwa na wazazi wetu. Bila kuwatendea haki wazee wetu tutaelekea kubaya. Wazee wamefanya kazi kubwa sana katika nchi hii.
Ombi langu ili wazee waonekane wanashiriki kwenye mambo ya kisheria, wapewe kipaumbele.
Mambo mengi yanafanyika katika nchi hii hayawahusishi wazee.
 
Masalamakali Singo Naibu Chadema Bara
Nianze na mapendekezo, Napendekeza kwamba kikao tunapongeza baraza.

Baada ya maoni ya wadau, baraza tukutane tuweze kupitia nyaraka za Warioba na nyaraka zingine. Tuweze kuenda kwenye bunge kama baraza. Tusikubali kuenda kwa kuwakilishwa na sekretaliet.

Mimi jana nilifurahi sana kuona tunajadili R4. Nilitegemea tunajadili ili kutandika jamvi.
Nilitegemea utendaji wa serikali uta reflect 4R.
Nilitegemea hivyo na sioni. kwa sababu yapo matatizo ta tume hayajaguswa.
Yapo mambo ambayo ni kikwazo chatume

1. Tume ina mikia miwili. Mkiwa wa kwanza ni hapo juu na wapili ni TAMISEMI ambayo haiongelewi.
Uchaguzi unafanyika kwenye vituo na unatangazwa huko. Je, wale kule chini wamesemwaje kwenye sheria.
Uhuru wa tume ni mambo makuu manne au matano.
Tume inapatikanaje.

2. Tume inawajibika kwa nani.
3. Mambo ya fedha
4. Security ya tume
Hiyo kamati ya usaili ni kamati ya rais.
 
Hashimu Juma MWenyekiti wa wazee Chadema
Mjumbe mmoja alisema kwenye 4R kuwa tuwe wajasili katika kusikiliza.

Mambo yote tunayoyafanya katika nchi hii hatupo serious. Kama hapa tupo katika kutafuta katiba. Katiba ya warioba ipo. Mtoa mada anamwelekeza tujielekeze kwenye mada.

Taarifa kutoka kwa Maganya kwenda kwa mchangiaji. Seriousness ya Rais ni pamoja na huu mchakato huu tulionao.
Mwongozaji anaeleza kuwa hata kuwepo hapa ni seriousness ya Rais.

Hashim Juma anaendelea.
Kwakuwa hakuna sheria. Namtaka mwenyekiti mtungi atuoneshe barua ya wale wanawake 19 wa CHADEMA.

Maelewano yanapotea kwenye mkutano.
Mwangozaji anasema mchangiaji hakuwa anaongelea mada alikuwa anaongelea mambo mengine.
Anaeleza mawazo hayo tunayaheshimu sana. Anaombwa bwana Hashimu atulie.
 
Mchangiaji mwingine. Selasini
Hapa tumeitwa kujadili miswada siyo kitu kingine. Kama tungekuwa makini tungeenda kifungu kwa kifungu. Hakuna sehemu kwenye sheria Samia ametajwa. Sisi tunataka mswada huu ujadiliwe kwa undani.

Naomba mwenyekiti uweze kudhibiti mjadala.
Tunaomba tujadili mswada
 
Katherine Baraza la wanake Chadema
Namuunga mkono mwenyekiti wa UWT. Kuhusu wanawake kwa kuzingatia jinsia. Tunaomba nafasi ya mwanke katika wajumbe hawa lizingatiwe.

Liongozewe kuwa tume isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa. Uchaguzi ujao
Tunaomba sana. Aliyekuwa anawasilisha jioni alione sexual abuse.
Tunaomba mtupe heshima kama wanawake.
 
Mtoa Mada Bwana Alex.
Kikubwa zaidi kuwa na sheria ya tume ya uchaguzi siyo tu kutajwa kwenye katiba. Kupoteza nafasi hii ya kutunga sheria ni muhimu sana.

Machakato wa katiba ni mchakato mrefu.
Wakati huu ukitazama mabadiliko yanahitajika sana kuwa na sheria.

Majukumu ya tume sitaongea maana yameelezwa na vikao vya tume sitavieleza
Jifunze kuandika, unaandika sehemu moja siyo post kibao
 
Katherine Baraza la wanake Chadema
Namuunga mkono mwenyekiti wa UWT. Kuhusu wanawake kwa kuzingatia jinsia. Tunaomba nafasi ya mwanke katika wajumbe hawa lizingatiwe.

Liongozewe kuwa tume isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa. Uchaguzi ujao
Tunaomba sana. Aliyekuwa anawasilisha jioni alione sexual abuse.
Tunaomba mtupe heshima kama wanawake.
Issue siyo kujaza jinsia, issue ni mchango wa mtu na uwezo
 
Jaji Mtungi:
Nilitaka ile taharuki iliyojitokeza. Mimi kanitaja ndio maana nataka nitoe ufafanuzi.
Alivyo sugest bwana Kigaila, wengine waliopo hapa siyo wajumbe. Tusipotoshe kuingiza mambo mengine.
Tutakapoitisha baraza hilo jambo tutaliweka kwenye ajenda.

Umma wanategemea tusijadili mambo mengine
 
Back
Top Bottom