On Mbowe: Man, Family Life and Politics

Status
Not open for further replies.
GT nadhani title yako ingekuwa nzuri kama ungeandika ''Freeman Mbowe, the man,politician and Nyerere's son. Off course we know than he is a man!

waberoya
 
.... Leo tunazungumiza chama pekee chenye wenyeviti wa tatu wa kitaifa tangu kuanzishwa kwake, Mtei, Makani na sasa Mbowe. Kwa hiyo chama kina awamu tatu za uongozi....

Hii ni tamu, hebu tufanye hesabu rahisi kwa Vyama vikuu:

CCM 1977-2008: Wenyeviti 4
CUF 1995-2008: Wenyeviti 2
CHADEMA: 1995-2008: Wenyeviti 3

CHADEMA kinaonekana ni Chama cha Kidemokrasia zaidi kuliko vingine na ukweli ni kuwa kinavyojionyesha ni kuwa hakitegemei Umaarufu wa Mtu kupata Kiti which is good kama Chama mbadala.

Nani alimjua Mh. Arfi, Mbunge wa Mpanda Magharibi? Naamini hata mimi nisiye maarufu na mapesa kama wengine nikigombe Ububge kwa tiketi ya CHADEMA naweza kuukwaa.
 
Hivi kweli serious watu wanataka Mbowe awe Rais? ama kweli tumekuwa kichwa cha mwendawazimu
 
Chadema ni ma centrist, social democrats. Interresting whatever that mean in the Tanzanian context. Kichekesho ni CCM. Are they really communists as their constitution proclaim.

CCM are rather the ultra conservatives (in action) further to the right a million times the GOP of the US. Au ni mabepari uchwara (pseudo capitalist)! Kuielewa CCM kwa hali ilivyo sasa inahitaji doctoral thesis za mapolitical scientists kama mia hivi!
 
Mtu Huru anaogopwa tu, kati viongozi zaidi wa vyama 15 nchini anaejadiliwa mara kwa mara ni yeye, hii inakupa picha kuwa anajadiliwa kwa msukumo ni hofu na wanajua anachokaribia kufanya. Ikiwa Kikwete anazungukwa na kuvutia watu kama kina makamba,ngeleja,chiligati n.k na bado aonekana anafaa na kwamba ana uwezo wa kuongoza ila tu anaangushwa na wasaidizi wake(aliowachagua) halafu Mtuhuru anawavutia na kuwaongoza watu wenye weledi kama kina slaa,zito,lissu,mnyika n.k anaonekana yeye hafi ila wanaomzunguka ndio wazuri! Wanapuuzi kanuni ya asili kwamba ili uwezo kuvutia lazima uwe na mvutu na ili uwezo kuvutia watu waenye weledi mkubwa lazima uwe na weledi mkubwa! Ukishasikiliza sarakasi hizi unalewa kuwa mijadala mingi juu ya mtuu huru ni kilelezo cha hofu na kutambua nafasi yake adimu katika siasa za Tanzania.

Hoja ya uchaga ni moja ya hoja ya kizembe mno, wakati Marekani wanachagua kiongozi wa kwanza katika historia ya taifa hilo mwenye asili ya Afrika huku tumekazana kumshambulia mtu kwa kuwa ni mchaga! Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawakuwa wachaga lakini tumeona na tunaendekea kuona namna tawala zao zilivyoangamiza taifa!

Mwalimu Nyerere ambae wengi tunamtazama kama kilelelezo cha uadilifu katia uongozi alimemtua Ndugu Edwin Mtei(Badae muasisi wa CHADEMA) kuwa gavana wa kwanza mzalendo Tanzania ambae ni mchaga na badae wizara nyeti ya fedha! Ipo imani zaidi ya hii?

Sehemu kubwa ya mijadala inayomhusu Mtuhuru ni mitupu mno, watu wanapagawa wakisikia jina lake limetajwa hawasikii raha wakiona jina lake halijataswa wanawasilisha mapenzi yao kwake katika mtazamo hasi kwa lengo la kusikia taarifa zake zaidi ili wapate majibu ya ziada kuridhisha hisia zao juu ya uchaguzi walioufanya wa kumuunga mkono. Ndicho nakiona hapa.
 
Hivi kweli serious watu wanataka Mbowe awe Rais? ama kweli tumekuwa kichwa cha mwendawazimu

Tulishakuwa kichwa cha mwendawazimu toka tulipomchagua(au tulichaguliwa?) Mwinyi kuwa raisi.

Na sasa hivi ndio tumekuwa mataahira kabisa kwa kumchagua Kikwete, akiwa na baraza la mawaziri wa aina ya Stephen Wasira.
 
jamani naomba nimzungumze Mbowe kibinaadamu na kijamii na sio kisiasa. Freeman Mbowe ninayemjua mimi ni mtu wa msaada hata bila kukujua. Natao ushuhuda binafsi wakati najiandaa kwa harusi yangu, Freeman alijitolea bure kutumia ukumbi wake wa Bilicanas bila gharama yoyote. Huu ni ushahidi tosha anajitolea kusaidia anapoweza.

Kuna wakati nilikutana naye Washington DC mimi nikibeba maboksi. Akaniuliza kama nina taaluma yoyote ama naweza kufaanya kazi gani kkati ya decent jobs. Alinichukua na kunipeleka mpaka nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Voice of America, Emmanuel Muganda, maeneo ya Maryland. Akanitambulisha akaniiombea kusaidiwa kupata kazi VOA. Muganda alinielekeza taratibu za kufuata kujoin VOA, sio siri nikachemsha mwenyewe nikaendelea na kubeba mabox- toka jimbo moja hadi jingine.

Kunawakati tulikutana tena mjini Boston yeye akiwa na rafikiye kwa jina la Makundi. Kama kawaida watanzania tukikutana ugenini tunachangamkiana sana. Wakaniuliza kama ninaprogram yoyote, japo nilikuwa na ka program kangu mshenzi, nikajibu niko free. Akaniuliza sehemu gani kuna bia na nyama choma ilikuwa aibu maana wao walifurahi wakajua wana mwenyeji, kumbe mie mwisho wangu ni kwa junk food za -
Kentuck au Tennesee. Akampigia simu jamaa mmoja akiitwa Asante Nsilo Swai yeye mwenyeji Boston akatuelekesa mahali. Akawapigia wabongo wengine wawili kundi likawa kubwa sie hao tukaenda kula nyama choma na bia.

Tulipofika hapo mahali unalipa dola 20 unaingia ndani unakula nyama unavyotaka. Freeman mbowe alitulipia wote, dola zaidi ya mia. Sio siri watanzania tu wakarimu tukikutana bar tunazungusha lakini kukutana na mbongo tena katoka bongo anazungusha Marekani sio kawaida huyu jamaa ana wema wa asili

Hayo yote yalitokea kipindi cha nyuma kabla Freeman hajaingia kwenye siasa. Sasa hivi sijui kama bado anatoa ukumbi wa bills bure na kama bado anamwagaa offers.
 
hee, kumbe kumwaga offer ndo wema tena ya nyama choma, ya dola ishirini.

Inaelekea kwa alivyomwema kila wiki harusi inayofanyika pale bills ukumbi ni wa bure. Huu ndio Utanzania, ukarimu usio na mfano. Duh....
 
Migomo left and right serikali iko bize na mafisadi kila kukicha na hakuna kinachoeleweka...lakini in the light of all these scandals the so called President in waiting bwana FREEMAN (The silentman) MBOWE yuko kimya. Maana ukweli usiopingika kuwa MAALIM SEFU nadhani bado kupiga msumari wa mwisho kwenye sanduku lake la career yake ya siasa so he/ or CUF cannot qualify as the real alternative.

Maana haya mambo ya kumwachia ZITO kuwa mouth piece ya CHADEMA yanaboa

There is just much one man can do, tena kwa vijisent vya Ubunge. Sasa kama Mbowe kashindwa kutia neno wakati wa hili vugu vugu kwa nini ZITO asipewe hicho cheo cha FREEMAN halafu huyu the SILENT MAN akaendelea na biashara yake(nasikia mpaka leo Bilicanas club bado haijafunguliwa) sasa sijui ndicho kinachomtia ubize au vipi

CHADEMA amueni kiongozi wenu ni ZITTO au MBOWE na kama mbowe then I,m sorry to say kuwa kimya chake wakati huu kinatisha.Imagine angekuwa Ikulu nani angekuwa ana run nchi...please dont tell me Mzee Mtei
 
-Hiyo kelele ampigie nani asiyesikia makelele ya WANAOGOMA.
-Mangapi yamepigiwa kelele.
-Mangapi yametatuliwa kwa kelele za wapinzani.
-Malele mangapi yamepigwa na kusikika kuhusu Mgonja,Mramba,Hosea and the like
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom