ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Probabilitiy ya Dr. Slaa kushinda ubunge katika jimbo lake ni 95%. Na probability ya Dr. Slaa kushinda urais wa Tanzania 5%. Probability ya Zitto Kabwe kushinda uchaguzi wa ubunge ni 98% na probability ya kushinda urais ni 10%. Hivyo basi kwa maendeleo yalivyo sasa, Kabwe na Slaa wanategemewa kugombea tena nafasi zao za ubunge. Na kama Zitto na Slaa watagombea ubunge, basi wanasiasa wenye ngazi kubwa ndani ya CHADEMA akiwemo ndugu Mbowe watategemewa kugombea nafasi hiyo. Hivyo kum-project ndugu Mbowe kama rais mtarajiwa sio makosa, na kama ni makosa je matarajio gani watu wategemee kutoka kwake?
Zakumi, umeongea mambo mazuri "kiujumla" ila hizi probability zako zinahitaji uhakiki. Je unafahamu kuwa mwaka 2005 Zitto hakupata hata asilimia 52 ya kura? Sasa hizo alimia 98 zinatoka wapi? The fact kwamba Zitto mwenyewe ametangaza kutokugombea tena ubunge wakati hakuna mission yoyote aliyoiaccomplish kwa kupitia ubunge wake zaidi ya kuandikwa na magazeti inadhihirisha kuwa anatambua ugumu wa kunyakua tena jimbo hilo, ambalo ukweli ni kwamba ana nafasi kubwa ya kulishinda tena ila sio kwa asilimia ulizozitaja hapo juu.