Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

pamoja na udhaifu aliouonyesha Nundu,
bado kuna swali: naibu waziri alipata wapi nguvu yakufanya hayo? Ya kumzunguka waziri wake?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
pamoja na udhaifu aliouonyesha Nundu,
bado kuna swali: naibu waziri alipata wapi nguvu yakufanya hayo? Ya kumzunguka waziri wake?

Usishangae mkuu....kumbuka hotuba ya JK wakati wa Mgogoro wa Madaktari aliposema kuwa Kuna Mawaziri na Manaibu wao hawaaminiania kabisa.... Mambo yameshaenda kombo.

Nina experience na Wachina...hiyo ndio tabia yao. Niko industry ya ambayo wanaitawala Tz na Africa...wakiona Bosi mmoja hatoi support wanaenda kwa wachini yake. Hapo watakuja na style nyingine. Utapewa hata demu wa kichina ilimradi wapewe kazi. Na mambo ya kusafirishwa China... hiyo ndio kawaida yao.
 
Binafsi nimeshangazwa na alichokifanya mh Nundu kuwaita wanahabari na kutoa tuhuma dhidi ya naibu wake.Kimsingi pale si mahala pake.Ulikua wapi muda wote usilifikishe mahali husika?
yani yote unayatoa kwakua unapaswa kuwajika!
Yote ni kukosa uwajibikaji.Yupo mh waziri mkuu,yupo pia Mh rais na hizi ndio sehemu ambazo unapaswa kufikisha haya,sasa kama hata haya pia mnataka wananchi tuwaelekeze mnatutia shaka hata katika utendaji wenu!

Kwa kweli nimeshangazwa sana na kitendo hiki japo naukubali weledi wa Mh. Nundu
 
Binafsi nimeshangazwa na alichokifanya mh Nundu kuwaita wanahabari na kutoa tuhuma dhidi ya naibu wake.Kimsingi pale si mahala pake.Ulikua wapi muda wote usilifikishe mahali husika?
yani yote unayatoa kwakua unapaswa kuwajika!
Yote ni kukosa uwajibikaji.Yupo mh waziri mkuu,yupo pia Mh rais na hizi ndio sehemu ambazo unapaswa kufikisha haya,sasa kama hata haya pia mnataka wananchi tuwaelekeze mnatutia shaka hata katika utendaji wenu!

Mkuu unamjua kikwete na pinda au unaongelea kutoka bar. Kumbuka hata EPA ilivyoongelewa serikali ya ccm ilipinga sana. Malima alishalala hotelini kwa kujiita jina tofauti hatua gani ilichukuliwa dhidi yake na Vasco Dagama? Ngeleja alivurunda hatua gani zimechukuliwa? Mponda na Blandina wamefanywa nini? Pinda aliahidi nini na akafanya nini? Jairo na Luhanjo walifanywa nini pamoja na ukweli kuwa wazi? Shimbo mwenye minoti ya kuendesha serikali si yupo anatesa mtaani, amefanywa nini? Kagoda pamoja na mwizi husika kujulikana, nani kakamatwa? Achilia mbali richmond, deep green, meremeta?

Mi nadhani umeandika hii thread kutokea choo cha bar wakati pee wewe sio bure. Na unapoona jamaa ameamua kupasukia hadharani ujue kuna makubwa yalomfanya aweke mambo hadharani. Na hapo usikute hata Ikulu ina maslahi na hiyo move ya mfutakamba. Kwa kiongozi mwenye akili timamu, mwenye kujua hali ya mambo na ufisadi unaoendelea ndani ya CCM, hawezi kutia shaka kwamba Mfutakamba analindwa na mtu ambaye lazima ana-connection na 'ikulu'. Sio rahisi kwa hali ya kisiasa tuliyonayo mtu kama mfutkamba aka-engineer dili nzito na kutaka kufanya hilo.

Kwa taarifa yako, safari ya Mfutakamba kwenda Uchina na kwingine kuliko tajwa kuna mkono kama sio wa Ikulu basi Ofisi ya PM maana ni hao pekee ndiyo wenye uwezo wa kumpa ruhusa Waziri/naibu waziri kutoka nje ya kituo chake cha kazi achilia mbali kusafiri nje ya nchi!

Safi sana Nundu, heri umetuweka wazi kuliko 'kufa' na kinyongo moyoni kama anavyofanya Mwakyembe!
 
Binafsi nimeshangazwa na alichokifanya mh Nundu kuwaita wanahabari na kutoa tuhuma dhidi ya naibu wake.Kimsingi pale si mahala pake.Ulikua wapi muda wote usilifikishe mahali husika?
yani yote unayatoa kwakua unapaswa kuwajika!
Yote ni kukosa uwajibikaji.Yupo mh waziri mkuu,yupo pia Mh rais na hizi ndio sehemu ambazo unapaswa kufikisha haya,sasa kama hata haya pia mnataka wananchi tuwaelekeze mnatutia shaka hata katika utendaji wenu!

Labda alishafikisha bila mafanikio?
 
nundu cjamkubali na utetezi wake, af anaonekana hana mahusiano mazuri na naibu wake, nimemchek luningani full kumkandia naibu, hapo ni kwamba km cyo kujiuzulu yy bas naibu atoke au wote, akibisha kutoka itabidi wasiwe ofisi moja tena.
 
Nimeanza kuogopa kwa kuwa yanatimia maneno yaliyonenwa na manabii kwamba ukisikia ukiona ndugu kwa ndugu wanainuka na kupigana basi ujue Mwana wa Adam yu karibu. Nimeona ndugu kwa ndugu wanaumbuana ya kwamba wewe ulikula Rushwa ya safari lakini simuoni Mwana wa Adam.
 
pamoja na udhaifu aliouonyesha Nundu,
bado kuna swali: naibu waziri alipata wapi nguvu yakufanya hayo? Ya kumzunguka waziri wake?
Inawezekana Nundu ana hoja na jana aling'aka Bungeni! Kama ni kweli Naibu Waziri wake alifanya hivyo yaani alipelekwa huko kutembea kwa pesa za hao CCC (NASHINDWA KUTOMUAMINI NUNDU) basi kesho PCCB waanze uchunguzi rasmi dhidi ya Naibu Waziri tena akiwa nje ya Ofisi manake hii tuhuma ni kubwa mno tena toka kwa Waziri wake. Hii tuhuma inaipaka matope serikali inaonekana kana kwamba viongozi kwa maana ya mawaziri na manaibu waziri wanaliana timing katika kula Rushwa. Mwenzio akikuwahi hupati kitu hivyo inabidi uzibe eneo fulani. Hii hali haieteteki kwa kuwa si majungu ya magazeti bali ni maneno yaliyotoka kwenye kinywa cha Waziri wa Serikali ambaye ni moja ya wasaidizi wakuu wa Rais.

Ikiwa si hivyo ni bora Rais kesho akaanzia hata hiyo Wizara kwanza akawatenganisha manake hapo sisi watanzania hatuna imani kama viongozi wetu hawa wanafanya kazi kwa maslahi yetu. Kama hawaelewani watatutumikiaje hao? Ndio maana si ajabu kila kitu chini ya hii Wizara ni shaghilabaghla!Hakuna cha reli, meli wala ndege!
 
Huyo nundu kashindwa kazi lazima ajiuzulu kwanza hajui hata kupanga hoja. Jk inabidi awe makini sana kuchagua wasaidizi wake adha wise ataonekana pia hafai kutokana na wasaidizi wake kumuangusha.
 
Siku moja jamaa walikua wakibishana, kila mmoja anamtetea mwanasiasa anayempenda, mmoja alimwambia mwenzake, "we unashabikia sana huyu ... Amekupa ngapi?".... Mwenzake akamjibu, "kumbe wewe unashabikia kwa sababu ya kulipwa! Ndio maana hujengi hoja wala husikilizi hoja zangu, unabishana sana na wala hutoi ushahidi, sasa nimekuelewa umelipwa kwa kazi hiyo, lakini ujue mimi sijalipwa nasema ukweli na ungekuwa mkweli ningebadilika kama ungenipa hoja." Sasa na katika suala hili, Nundu amekula rushwa na ndio maana anaamini Naibu wake kala fedha na ndio maana anapambana naye hadi povu linamtoka na busara zinapotea. Nundu aliamini kwamba wenzake wote kuanzia mtangulizi wake Dr Kawambwa, Chambo, (Katibu Mkuu toka enzi za Kawambwa), Wizara ya Fedha, Bodi ya TPA, Menejimenti ya TPA na sasa wajumbe wote wa Kamati ya Miundombinu. Haingii akilini mradi wa 2008 ambao hata Mfutakamba hakuwa Mbunge, alikuwa DC tu, useme amekula rushwa, ili afanye nini? Kama yeye alienda China akitegemea CCCC wampe mshiko, akaambiwa wenzako walishachukua, aseme ndio maana sasa anawaka... Kesho akiondoka JK akiteua mwingine naye akaombe rushwa akinyimwa asimamishe miradi yote aliyoianzisha. Haingii akilini na watu na akili zetu tunatetea na kushabikia. Hii ni aibu. Kama Naibu wake kaiba, haihalalishi yeye kuwa ni safi, kila mtu atahukumiwa kwa nafasi yake. Kabla ya yeye kusulubiwa mbona hakuwahi kuita waandishi na kusema hayo leo. Ni sawa na mafisadi kuanza kutoa siri ama kuzusha ufisadi wa wengine, ili ionekana wote ni wachafu, lakini wezi wakigombana polisi makini atakamata wote, wa kwanza ni yule anayetaja wenzake kwamba "sikuiba peke yangu hata na huyu pia!!", mwaka huu, tutaona mengi!!! Tubadilike, tuache kufikiri kwa tumbo!!!
 
wana JF mnanishangaza sana

hivi tangu lini kazi za serikali hufanywa bila tenda kutangazwa? kikawaida ni lazima tenda itangazwe na wahusika washindanishwe nipo apatikane mwenye vigezo

lakini chakushangaza cccc wao wanatakiwa kupewa mamlaka ya kufanya kazi hiyo pasi hata tenda kutangazwa hii inashangaza sana.

kwa upande wa china

hii kampuni ya cccc kama kweli imejihusisha na rushwa mpaka sasa wamiliki wao wanatafuta njia ya kukimbilia,kwani uchina haitaji kampuni itakayo itia doa,hakika nawaeleza labda haya yasemwayo yasiwafikie viongozi wa uchina kampuni hii ipo mashakani

soma hapa

Wen Jiabao promises crackdown on corruption in China

Premier's announcement of action against abuse of office follows Bo Xilai's suspension from party over Neil Heywood murder caseChinese premier Wen Jiabao has promised tougher curbs on corruption and abuse of power, state media reported on Sunday

img_2027381.jpg

Someni hapa, ndio muanze kuhukumu. Nundu anatetea ulaji, anaamini wenzake wamekula!! Sasa anapiga mkwara.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/255443-nyaraka-omar-nundu-ni-msafi.html#post3759251
 
....Mzalendo yoyote hawezi kukubali wala kuuunga mkono makataba kama huu, hakika Nundu anastahili pongezi na wala sio kejeli kwa kuupiga stop mwelekeo wa mkataba wa muktadha huu...

...Ili tutoke hapa tulipo kama taifa, tunahitaji viongozi wengi zaidi wasioweza kuulembalemba uozo wa wazi kama huu eti kwa jina la "mwendelezo wa makubaliano yaliyokwisha fanyika", no way, ujinga kama huu haukubaliki kwa viwango vyovyote....

...Ni mtu aliyekula 10% tu au asiye mzalendo ndiye anayeweza kuutetea ujinga kama huu, atleast kwa hili hongera sana Nundu...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/255443-nyaraka-omar-nundu-ni-msafi.html#post3759251
 
Jana usiku katika taarifa ya habari vituo vingi vilirusha maelezo ya waziri Nundu aliyoyatoa mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwake Dodoma.
Mantiki ya maelezo yake hayo ni tuhuma alizozitoa moja kwa moja kwa naibu waziri wake Ndg. Mfutakamba na baadhi ya watendaji walio wizarani pale miundo mbinu. Si huyo tu, hata Nyalandu kafanya hivyo kwa Waziri wake Chami.
Shutuma ni rushwa na ujambazi wa wazi wazi unaofanywa na wateule hawa wa pale magogoni katika rasimali za taifa maskini Tanzania
Mwenzenu nimepigwa na bumbuwazi kubwa mno na kuanza kuililia nchi yangu inayotia huruma;
Kwanza, kwa Mkuu wa nchi kuendelea kuwavumilia mawaziri wanaovuana nguo hadharani mfano wa hawa niliowataja.
At least ingekuwa ni vitu ambavyo ni majungu ya ndoa zao tungepuuza, lakini kuvuana nguo na sarakasi zao ni zina ushenzi, kuvimbiwa matumbo na madaraka, ujambazi wa mchana kweupe unaombatana na dili za kimafia ndani ya serikali
Pili,
Majambazi hawa wa rasilimali zetu wanaendelea kutamalaki na kutumia ovyo majukwaa ya siasa as if Watanzania wamelala usingizi wa pono!
Tatu,
Majambazi hawa kuendelea kujigamba kwa kauli za kebehi zenye dharau kwa wananchi kwamba hawajiuzulu hata kama wamefanya ushenzi wa wazi mfano wa madudu waliyoyafanya.
Nne,
Kimya cha serikali kuhusu ushenzi huo, kinaonyesha imebariki na kuyashadidia. Huu ni ujumbe tosha kwetu Watanzania tuanze kuchukua hatua kwa mmoja pale alipo kwa uwezo wake wote!
Hakika tupo gulioni tumeuzwa! akili mukichwa!
Nawasilisha.
 
katika mkutano wa waziri Nundu na waandishi wa habari ilionyesha ni namna gani mawaziri wasivyofanya kazi kwa kushirikiana hata pale wanapokuwa kwenye wizara moja (Nundu alimtuhumu naibu wake kwa kwenda kinyume na yeye) Hali hii imekuwa inajitokeza sana (mtakumbuka wakati wa sakata la Richmond ambapo mawaziri walionekana kuwa na makundi)

Lakini pia kumekuwa na tuhuma za mawaziri na makatibu wakuu kutofautiana kwa mambo mengi kiasi cha wakati mwingine makatibu wakuu kujiona wababe sana. Hivi hali hii itatufikisha wapi? What kind of cabinet do we have and is this the way we are gonna go forward?

Mi sidhani.............
 
Hivi Tanzania kuita "press conference" ni kitu rahisi mno! Nahisi hata vichaa hapo baadaye wanaweza kufanya hivyo. Mhe. Nundu analalamika kuwa amezidiwa kete na naibu wake. Hiyo ni sababu tosha kuwa hajui majukumu yake kama Waziri mwenye dhamana na hiyo ni sababu tosha kwake kuachia ngazi.
 
Kutofautiana kwa Mfutarope na Omar Nundu ni JANGA KWA TAIFA
Ukiliangalia hili suala critically unaweza kugundua harufu ya rushwa humu! Halafu naanza kupata hofu na kamati katika suala hili wanaonekana kama walipotoshwa au nao.............
 
Back
Top Bottom