Ole Sendeka afutiwa mashitaka

Na huyo mkuu wa mkoa kununuliwa na Mafisadi kumrubuni Millya kwenda kituo kwa case fake,hii ni ajabu kwa kiongozi wa Serikali kujihusisha na siasa wanasahau kuwa wanawahudumia wananchi wote wao bdo wanakuwa wabunge ndani ya mkoa wanaoongoza.
 
hahahaha

jama alikuwa analalmika ile mbaya

ohh kaniweka bastola kichwan, kanipiga , himmhhhmh
 
zamu kwa sendeka kuomba fidia kubwa ya kuchafuluwa jina.

Aachane nao hao hakuna haja ya kuwekeeana kinyongo yeye sendeka aangalie mambo ya jimboni sasa na nijinsi gani atawatatulia wananchi wake shida zinazowakabili kwa jimbo lake na kuhakikisha Mererani isikaliwe na watu wachache na wenye maslahi yao binafsi pia na Aridhi kwa watu wa jimbo lake ni muhimu sana maaana nasikia chanzo kilikuwa hicho kuwa aridhi watu wanaipola na wananchi wa jimbo lile hawapati kitu

Millya bado ni kijana mdogo sana na anamwanga mzuri sana wa kimaendeleo navyo tarajiwa kwani nakumbuka hapa hapa mlituambia ni mwanasheria sasa kwa elimu yake hiyo sasa apime mambo yake na ajiweke sawa kwa 2015 najua atakuwa amepikika vyema na kawiva kisiasa sasa

hahahaha

jama alikuwa analalmika ile mbaya

ohh kaniweka bastola kichwan, kanipiga , himmhhhmh
 
Hongera Sendeka...hii inaonyesha hata jimbo lako utatetea bila wasiwasi.
 
Natuwe madeep thinker.hayo ndo matokeo ya kufutiliwa kwa mbali kwa richmonduli. Ilikuwa ni lazima wapambanaji wasamehe hilo ili nao walindwe kiaina.so MUNGU WABARIKI WADANGANYIKA ni upuuzi mtupu wandugu but natuombe MUNGU takukuru na posho mbili hilo nalo ni kichefuchefu tupu maana mtuhumiwa na kesi yake ubaoni ghafla anamshitaki mlalamikaji then mahakama inaacha kesi ya msingi inasikiliza kesi mpya HII NI NINI LAKiNI? Inakera sana
 
Ushindi wa mpiganaji Ole Sendeka ni pigo kubwa kwa Lowassa. Na bado! Mungu daima huwa upande wa wenye haki.
 
..sasa hivi hakuna "wapiganaji" na mafisadi tena, wote wamekuwa kitu kimoja.
 
Kwanza nampongeza Mbunge wa simanjiro Mhe Ole sendeka kwa kushinda kesi dhidi ya wale waliokuwa wanataka kumchafulia .kulingana na hukumu ni kwamba ushahidi uluotolewa dhidi yake umeonekana ni wa kupikwa na mashahidi walitumika na kupeleka ushahidi wa uongo sasa jamani mtumishi wa umma mwenye maadili na cheo kama cha RC kwa sababu ya uchu ulikosa ubunge na 2005 ulishindwa na sendeka na ni kibaraka umetumiwa na ukatumika hivi huyu si anaweza akauza ardhi ya wananchi ilimradi akitumiwa kama alivyotumiwa kwenye kesi? na hafai kuwa kiongozi mimi namuomba kabla mkuu wa kaya hajamtoa atoke mwenyewe sijui bado yupo singida najua ni kone,atuachie tubaki na wakuu wa mikoa waadilifu.
 
Haa, Mkuu nilivyosoma Heading nilidhani amejiuzuru Tayari.

Anyway, hao jamaa hawajiuzuru hata watu wafe, sembuse kusema Uongo...

Well, appreciated your opinions
 
Kwanza nampongeza Mbunge wa simanjiro Mhe Ole sendeka kwa kushinda kesi dhidi ya wale waliokuwa wanataka kumchafulia .kulingana na hukumu ni kwamba ushahidi uluotolewa dhidi yake umeonekana ni wa kupikwa na mashahidi walitumika na kupeleka ushahidi wa uongo sasa jamani mtumishi wa umma mwenye maadili na cheo kama cha RC kwa sababu ya uchu ulikosa ubunge na 2005 ulishindwa na sendeka na ni kibaraka umetumiwa na ukatumika hivi huyu si anaweza akauza ardhi ya wananchi ilimradi akitumiwa kama alivyotumiwa kwenye kesi? na hafai kuwa kiongozi mimi namuomba kabla mkuu wa kaya hajamtoa atoke mwenyewe sijui bado yupo singida najua ni kone,atuachie tubaki na wakuu wa mikoa waadilifu.
Hilo haliwezi kutokea. Nchi hii hakuna neno kujiuzulu kwa kuwajibika. Msamiatihuo umeshafutika siku nyingi.
Mambo yanatokea,yanasemwa kisha kimya. Juzi tuu yametokea Rukwa kuhusu wizi wa mabilioni ya fedha za pembejeo na kwa namna fulani RC alipaswa ajiwajibishe. Nani anazungumza tena?kwisha. Mifano ni mingi mpaka inachosha kuitaja. SERA NI KWAMBA, HAWAJIBIKI MTU. MAMBO NI MBELE KWA MBELE. Mkipiga kelele sana mtaishia kuambiwa mna wivu wa kike.
 
hajajiuzuru ila angekuwa ana busara,hekima na akajua nafasi yake kuwa alikuwa vetted then anasema uongo kwa makusudi angeachia nafasi ili akajiandae tena na mikakati maana kumshinda sendeka kwa fitna kumeshindikana lakini tatizo hawana utamaduni huo kama ulivyosema sasa waanze wakati ndio huu
 
Utamaduni ya kuwajibika kwa matendo yako hapo kwa viongozi na watendaji wetu wa sasa serikalini
 
Huyu RC tangu ashindwe ubunge ana usongo na Mheshimiwa Ole Sendeka.

Tena ni wa Singida na alipewa hiyo nafasi na EL wakati huo baada ya kubwagwa chini jimboni simanjiro sasa akawa anamrubuni kijana wa watu maskini wanamwaribia CV yake ya kisiasa, Sasa sijui hao vijana wa arusha walikuwa hawa mshauri kijana mwenzao kuhusiana na hili sakata najuu fika kuna vijana wengine wa UVCCM waliliona hili ni pandikizo ili kuchafuana na wengine waka muhusisha na mumiliki wa ITV kuwa ana m'support Ole, yaaani sasa nimeamini siasa ya Kitanzania ni ya kufanyiziana ubaya na unyama na haija tulia kuwatuliza wananchi wake kabisa

Najua huko simanjiro ndipo patakuwa shika nguo kuchanika sasa maana itakuwa CCM wenyewe wakichuana vikali.

Ni wakati mwafaka kuchambua na kuchagua viongozi wetu kwa kuangalia historia, Kabla Millya hajapewa uenyekiti wa mkoa kupitia UVCCM alipaswa kuulizwa alifanya nini alipokua Rais wa jumuiya ya wanafunzi pale Tumaini mahali nilipofahamiana nae kwa kukaa nae darasa moja. Alipopewa tu madaraka aliyatumia kwa kutafuta umaarufu ndivyo anavyotumia uenyekiti wake,leo hii ametumia kesi kujipambanua hata huku Ughaibuni kila mtu ananiuliza millya ni nani,si ajabu nyumbani kila mtu sasa anamfahamu. He is not a person who can deliver, he graduated a Masters Degree in SA but he is not practising amebaki akiombaomba pesa kwa kisingizio cha kugombea jimbo la simanjiro, vijana tunapaswa kuangalia upya malengo yetu tusiwe watu wa kutumika na kutumiwa. Ni imani yangu EL hayuko nyuma ya kesi hii ila kwasababu tu Milya hana kazi rasmi na ni kijana Mmasai,anawapa nafasi watu kufikiri wanayofikiri.
 
Hongera mzee, tulijua utawaahibisha wabakaji wa demokrasia. Endelea kuchanua hadi jimboni. Hongera laigwanani.
ole.jpg
 
Hii tamu zaidi

Ole Sendeka ambwaga mshirika wa Lowassa

Na Charles Ngereza

headline_bullet.jpg
Ashinda kesi aliyopakaziwa ya kushambulia
headline_bullet.jpg
Pia alidaiwa kutishia kuua kwa bastola
headline_bullet.jpg
Iliibuliwa wakati wa mkutano alioandaa Lowassa

ole(2).jpg

Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akipongezwa na baadhi ya wananchi wa jimbo lake baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumshambulia Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Millya mwaka jana wilayani Monduli.

Ile kesi ya jinai dhidi ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ambayo chimbuko lake ni mkutano wa wazee wa Kimasai ulioitishwa na Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, imetupwa na mahakama.
Kesi hiyo ilitupiliwa mbali jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Devota Minja, baada ya kuthibitika kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi wa upande wa mashitaka ulikuwa dhaifu na wa kujichanganya hivyo kukosa nguvu ya kisheria kumfanya Sendeka awe na kesi ya kujibu katika kesi hiyo, Sendeka alikuwa akishitakiwa kwa tuhuma za kutishia kwa bastola na shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Millya.
Millya kada kijana wa CCM, wakati kesi hiyo ikiendeshwa alidaiwa kuwa anaishi kwenye moja ya nyumba za Lowassa iliyoko mkoani Arusha.
Wakati usikilizaji wa kesi hiyo ukiendelea, jopo la mawakili watano wa upande wa utetezi wakiongozwa na wakili Mpaya Kamala, uliwasilisha hoja za kutupwa kwa kesi dhidi ya mteja wao kwa hoja kuwa mashahidi wa upande wa mashitaka walijichanganya na kupingana katika ushahidi wao mahakamani.
Aidha, Mahakama hiyo ilieleza kuwa ushahidi uliotolewa na mtu aliyemjazia fomu mlalamikaji haukuwa na hoja ya msingi kwa kuwa hakuwa na sifa za kuwa daktari.
Baada ya Hakimu Minja kusoma uamuzi huo, umati mkubwa wa wafuasi wa Sendeka kutoka maeneo ya Simanjiro, Longido na Arusha walianza kupiga mayowe mahakamani wakiashiria kufurahia maamuzi hayo.
Wananchi hao walikuwa wamevaa mavazi ya Kimasai huku baadhi yao wakiwa wameshika mabango mbalimbali moja likisomeka “Hata Yusufu alisingiziwa kubaka na baadaye kuonekana hana hatia.”
Wananchi hao walijazana katika eneo la mahakama wakipongezana kufuatia uamuzi huo wa mahakama.
Shamrashamra za wafuasi wa Sendeka zilisababisha shughuli za mahakama kusimama kwa muda huku watumishi wakitoka nje kushuhudia umati wa watu waliokuwa mahakamani kujua hatma ya mbunge huyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wananchi wa jamii ya Kimasai waliokuwepo mahakamani wanaokadiriwa kufikia 500 walikuwa wakiruka na wengine kupandwa na mori wakati wakimpa mkono wa hongera Sendeka, ambaye ni mbunge wao.
Mara baada ya kuondoka katika eneo la mahakama, Wamasai hao waliendelea na maandamano yao ya amani wakimzunguka mbunge wao huku wakiwa na silaha zao za jadi hadi eneo la Makao Mapya ambapo walianza maandalizi ya tafrija kubwa ya kupongezana iliyotarajiwa kufanyika jana jioni. Akizungumza mara baada ya kufika katika eneo la Makao Mapya, Sendeka aliishukuru mahakama kwa kumtendea haki katika kesi hiyo aliyodai ilipikwa na kutungiwa uongo na maadui zake katika ulingo wa kisiasa mkoani Arusha na Manyara. Hata hivyo, hakuwataja kwa majina. “Binafsi nilikuwa radhi kupokea uamuzi wowote, kama nilivyowaahidi wenzangu wakati kesi hiyo ikianza Januari mwaka jana, niliwaambia waende kuendelea na kazi za kujenga Taifa kwa kuwa niliamini kuwa mahakama zetu zina hadhi ya kuaminiwa na zinatenda haki,” alisema Sendeka.
Alidai kuwa hata kama angeambiwa ajitetee angeweza kusaidia umma kupata ukweli wa upande wa pili wa shilingi katika sakata hilo.
“Ninachoweza kusema nikiwa Mkristo nawasamehe wote walionitendea haya kwa dhamira ovu wakiwa na nia mbaya, lakini kwa kuwa wananchi wa Simanjiro na Watanzania wenzangu wamekuwa wakifika katika mahakama hii toka siku ya kwanza kwa gharama zao kunisindikiza kwa nia ya kuweka kumbukumbu sawa na kulinda hadhi yetu dhidi ya wale waliokusudia kuharibu hadhi na heshima yetu, nitazungumza nao kama watanikubalia niwasamehe, wakikataa tutawataka watuombe radhi na kusafisha majina yetu,” alisema Sendeka.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Minja alisema kuwa anakubaliana na hoja za upande wa utetezi kuwa mtuhumiwa hana kesi ya kujibu na mahakama imetupilia mbali kesi hiyo.
Alieleza kuwa mahakama imeziangalia kwa makini hoja za pande zote na misingi ya kisheria ya makosa ya jinai na kubaini kuwa Mbunge huyo hana kesi ya kujibu.
Nipashe ilijaribu kuwasiliana na upande wa Jamhuri kupata maoni yake kama unakusudia kukata rufani na wakili wa serikali, Hashim Ngole, alisema kuwa unajipanga kujua la kufanya baada ya uamuzi huo wa mahakama.
Awali mawakili wa utetezi wakiongozwa na Kamala waliiambia mahakama kuwa madai ya upande wa mashitaka hayakuwa na msingi wowote na hayana nguvu ya kisheria wa kuifanya mahakama kutamka kuwa mteja wao ana kesi ya kujibu.
Alisema kuwa mashahidi wote waliotoa ushahidi walipingana wao kwa wao huku wengine wakitoa ushahidi wa kusikia ukiwa na mapungufu makubwa ya kisheria ya kuweza kuisadia mahakama kumtendea Sendeka haki.
Aidha, mawakili katika hoja zao walisema kuwa mahakama kuendelea na kesi hiyo ingekuwa ni kupoteza muda wa mahakama na mawakili wa pande zote kutokana na kila jambo kuwa wazi kisheria kuwa mashahidi waliotoa utetezi hawana sifa ya kuisaidia mahakama kutenda haki.
Walidai kuwa katika ushahidi wa shitaka la pili, mashahidi wa upande wa mashitaka namba 6 na 7 waliiambia mahakama kuwa shahidi namba mbili, Parseko Kone, hakuwa katika eneo la tukio na kwamba shahidi huyo aliiambia mahakama kuwa alimwona mshitakiwa akishika bastola na kumwelekezea Millya.
Aliendelea kuiambia mahakama kuwa katika shitaka la kwanza la shambulio la kudhuru mwili, shahidi namba 2, 6 na 7 waliiambia mahakama kuwa shahidi namba 5 hakuwa katika eneo la tukio na alitoa ushahidi wa kumwona Sendeka akimpiga Millya.
Kuhusu ushahidi wa tabibu kutoka hospitali ya Wilaya ya Monduli kujaza fomu namba tatu, wakili mwingine wa utetezi, Michael Ngalo, alidai kuwa upande wa mashitaka ulisisitiza kuwa ushahidi huo ulikuwa na upungufu kutokana na kujazwa na mtu asiyeruhusiwa kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa sheria.
Mbunge huyo alikuwa akituhumiwa kutenda makosa hayo yaliyotupiliwa mbali Januari 9, mwaka jana majira ya saa 10 jioni katika Chuo cha Ualimu Monduli wakati wa mkutano huo.
Ilidaiwa katika maelezo ya awali mahakamani hapo kuwa siku ya tukio
mtuhumiwa alikuwa anahudhuria mkutano ulioandaliwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, uliokuwa na lengo la kuzungumzia suala la elimu kwa watoto wa kike wa jamii za wafugaji wa Kimasai ambapo baadhi ya wajumbe walitofautiana wakati wa uchangiaji wa mada zilizowasilishwa. Ilidaiwa kuwa baada ya kutoka mapumziko ya chakula cha mchana ndipo Sendeka alimshambulia Millya na kumsababishia maumivu na kumtishia kwa bastola yake.

Yaliyojiri kesi ya Sendeka Jan.2009 - Machi 2010
Nipashe Januari 10, 2009: Mkutano wa Lowassa wazua balaa Monduli
Mkutano wa viongozi wa jadi wa kabila la Kimasai ulioitishwa na kiongozi wake aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, umezua balaa baada ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, James Ole Millya, kurushiana makonde mazito hadharani.
Nipashe Januari 13, 2009: Polisi bado kuamua kumshtaki Sendeka.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limesema halina mamlaka juu ya hatma ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, kufikishwa mahakamani au la, kufuatia tuhuma za kumpiga ngumi na kutishia kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Ole Millya.
Nipashe Januari 17, 2009: Kesi ya Sendeka yatikisa Arusha
Wamasai wengi wajitokeza kumuunga mkono
Wataka kuandamana jimboni Simanjiro
Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, kujibu shtaka la kumshambulia na kumdhuru mwili Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Ole Millya.
Nipashe Machi 13, 2009: Kesi ya Sendeka kunguruma Aprili 20
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha itaanza kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ya kumshambulia Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha, James Ole Millya, Aprili 20, mwaka huu.
Nipashe Aprili 21, 2009: Kesi ya Sendeka yaanza kunguruma
Hatimaye kesi inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, imeanza kunguruma.
Nipashe Mei 28, 2009: Mbunge Sendeka augua, kesi yapigwa kalenda
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imeahirisha kesi ya shambulio la kudhuru mwili na kutishia kuua kwa silaha inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, hadi Julai 29, mwaka huu, baada ya mshtakiwa huyo kudaiwa kuwa mgonjwa.
Nipashe Agosti 20, 2009: Mshtaki wa Sendeka aishi nyumba ya Lowassa
Kesi inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ya kumshambulia James Ole Millya, jana ilianza kusikilizwa huku mlalamikaji akielezwa kwamba anaishi nyumba ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Nipashe Agosti 21, 2009: Lowassa atajwa tena kesi ya Sendeka
Uhalali wa cheo cha mwenyekiti wa viongozi wa kimila wa kabila la Wamasai (Ilaigwanani) ambacho kinadaiwa ni cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kimehojiwa mahakamani katika kesi inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ya kumshambulia James Ole Millya.
Nipashe Agosti 22, 2009: Wakili wa serikali kesi ya Sendeka akwama
Wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha ikikubali kupokea waraka uliozua utata wa maelezo ya shahidi wa pili, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Ole Kone, katika kesi ya kumshambulia James Ole Millya, inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, shahidi wa tatu katika kesi hiyo, Ngisayo Majuka, amesema hakuona mshtakiwa akimnyooshea bastola mshtakiwa.
Nipashe Novemba 24, 2009: Shahidi upande wa mashtaka ampa ahueni Sendeka
Mpelelezi katika kesi ya kutishia kuua inayomkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ambaye ni shahidi wa nane wa upande wa mashtaka, amekana mahakamani kuwapo kwa maelezo ya awali ya kutishia kuua kwa bastola katika jalada la kesi hiyo na kwamba hayo yalikuja baadaye.
Nipashe Machi 5, 2010: Hatma ya kesi ya Sendeka leo
Uamuzi wa kesi inayomkabili Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, ikiwa ana kesi ya kujibu au la, utatolewa leo.
 
ole%282%29.jpg

CHANZO: NIPASHE
 
lC.gif
Mwandishi Wetu, Arusha​
Machi 10, 2010
rC.jpg

bul2.gif
Wazee wa Kimasai ? Lagwanani watoa msimamo wao

bul2.gif
Millya asema ni wapambe wa Sendeka

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya sasa yuko katika "mazingira magumu kisiasa" baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa kuifuta kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, kwa maelezo kuwa mbunge huyo hakuwa na kesi ya kujibu.
Kesi hiyo ilifunguliwa mapema mwaka jana na Jamhuri baada ya Millya kulalamika kupigwa ngumi na kutishiwa kwa bastola na mbunge huyo wa Simanjiro wakati wakiwa wilayani Monduli katika mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kuhusu masuala ya elimu kwa jamii ya wafugaji.
millya_1.jpg

MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya
Sendeka anadaiwa kumpiga ngumi Millya, na kisha kumtolea bastola baada ya kutokea malumbano baina yao wakati wa kipindi cha mapumziko cha mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Monduli, Januari 9, 2009.
Baada ya mapambano makali ya kisheria mahakamani, yaliyodumu kwa mwaka mzima kati ya upande wa mashitaka, ukioongozwa na Wakili wa Serikali, Hashim Ngole na utetezi ukiongozwa na wakili Mpaya Kamara na jopo la mawakili watano, hatimaye mahakama ilikubaliana na upande wa utetezi kuwa mbunge huyo hakuwa na kesi ya kujibu katika hukumu iliyosomwa Machi 5 mwaka huu.
Mawakili wengine waliokuwa wanamtetea Sendeka ni Ezra Mwaluko, Michael Ngalo na Modest Akida.
Hukumu hiyo ilisomwa na Hakimu Devotha Msoffe akimwakilisha hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha ambaye, hata hivyo, alihamishiwa kikazi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kabla ya kuhitimisha kesi hiyo.
Katika hukumu yake, hakimu huyo alieleza kuwa mahakama haioni sababu ya Sendeka kujitetea kwa kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani ulikuwa na mapungufu mengi ya kisheria; huku shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri, ambaye ni Millya mwenyewe, akitoa maelezo tofauti mahakamani kuhusu alipigwa sehemu gani ya mwili wake.
Alisema katika maelezo yake polisi, Millya alieleza kupigwa kofi la kushoto lakini wakati akitoa ushahidi wake mahakamani alieleza kuwa mshitakiwa Sendeka alimpiga ngumi upande wa kulia; huku akisahau maelezo mengine kuwa alimtishia kwa bastola.
sendeka_1.jpg

Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka
“Kwa mazingira hayo, ni vigumu kwa mahakama kufahamu mlalamikaji alipigwa sehemu gani ya mwili wake; hivyo ushahidi wake unakosa nguvu ya kisheria”, alisema.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, wazee wa kimila (Lagwanani) kutoka jamii ya Kimasai ambao walikuwepo mahakamani kufuatilia kesi hiyo, walizungumza na waandishi na kutoa maoni yao; huku wakimtuhumu Millya kwa kuvunja miiko ya asili ya jamii hiyo kwa kuamua kupeleka malalamiko yake mahakamani badala ya kusuluhishwa kimila.
Kiongozi wa kwanza wa kimila kuzungumzia suala hilo alikuwa Yohana ole Tiamongoi ambaye pia ni katibu wa baraza la wazee hao wa kimila wa Kimasai mkoani Arusha. Tiamongoi alieleza wazi kuwa hawakufurahishwa na hatua ya Millya kukataa kusuluhishwa kimila baada ya kutofautiana na Sendeka.
Alisema jamii ya Kimasai imejiwekea utaratibu wa kumaliza tofauti zinazojitokeza katika makundi mbalimbali ya kijamii kama vijana, watu wa rika la kati, wanawake na wazee, na utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa karne nyingi; hivyo Wamasai kujenga jamii ambayo imeweza kudumumisha mila na desturi zake hadi leo.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa kimila, wakati mgogoro huo ulipotokea, wazee wa kimila kutoka wilaya za Monduli, Simanjiro, Ngorongoro na Longido, viongozi wa dini (maaskofu Thomas Laizer na Askofu Mameo wa Dayosisi ya Morogoro ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT) walijaribu kuwasuluhisha nje ya mahakama lakini Millya aligoma.
Alisema Millya hakupaswa kupeleka shauri hilo katika vyombo vya sheria; hasa katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Simanjiro katika uchaguzi wa mwaka huu.
“Kama kiongozi wa vijana, alipaswa kuonyesha mfano kwa vitendo kwa kusikiliza ushauri wa wazee na kumaliza shauri hilo nje ya mahakama……sasa kama hawezi kusamehe wenzake atakuwa kiongozi wa aina gani?”, alihoji mzee huyo wa kimila.
Tiamongoi aliongeza: “Hata viongozi wa vijana wa rika lake la Korianga walijitahidi sana kuzungumza naye ili suala hilo limalizwe kimila, lakini bado aligoma na hiyo inaonyesha wazi kuwa kijana huyo amepuuza mila na desturi zetu za watu kuheshimiana”, alisema.
Kiongozi mwingine aliyezungumzia suala hilo ni Joel Lesongoyo aliyesema kuwa jamii ya Wamasai imejijengea utamaduni wa watu kupendana, kuheshimiana na kushikamana na linapotokea tatizo lolote huchukuliwa kama changamoto kwa jamii na watu wote kwa rika zao hushirikiana kumaliza tatizo hilo.
“Kwangu mimi itakuwa vigumu sana kwa Millya kuwashawishi watu wa Simanjiro kuwa yeye ni moja wetu na anataka kuwa kiongozi wa umma wakati ameshindwa kutoa ushirikiano wa kumaliza tatizo dogo kama lililotokea”, alisema.
Lesongoyo alisema kimsingi suala hilo litamgharimu Millya katika harakati zake za kuwani ubunge wa jimbo la Simanjiro na kuongeza kuwa watu wengi hawakufurahishwa na uamuzi wake wa kumpeleka Sendeka mahakamani.
“Siwezi kulisemea suala hili kuwa kuna shinikizo la kisiasa kutoka kwa makundi hasimu, lakini ukweli unabaki kuwa ni Millya binafsi ndiye aliyekuwa na maamuzi ya mwisho kuhusu mgogoro baina yake na Mbunge Sendeka”, alisema.
Hata hivyo, akizungumza na Raia Mwema kwa njia ya simu, Millya alipuuza madai yanayotolewa kuwa kesi hiyo itamgharimu kisiasa na kueleza kuwa alifikia uamuzi wa yeye kugombea ubunge kabla hata ya kutokea ugomvi baina yake na Sendeka.
“Madai hayo hayana msingi wowote na nia yangu ya kuwania ubunge wa jimbo la Simanjiro kwa tiketi ya CCM ni ya muda mrefu kabla hata ya kesi iliyotokea. Kwa hiyo nia yangu iko palepale, na wala hukumu ya kesi hii haiwezi kunizuia katika malengo yangu ya kisiasa”, alisema.
Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya UV-CCM aliongeza kuwa hata wazee wanaozungumza kuwa nitakuwa nimejiweka katika mazingira magumu kisiasa ni wale ambao wanamuunga mkono mbunge wa sasa (Sendeka) na wote hao walikuwa wanahudhuria mahakamani kufuatilia kesi hiyo si kama wazee wa kimila bali marafiki wa mbunge huyo.
Alisema mpaka kufikia uamuzi na kutangaza nia ya kugombea ubunge, alifanya utafiti wa kutosha kuwa anakubalika miongoni mwa rika tofauti kwa wananchi wa jimbo la Simanjiro ambao kimsingi ndiyo wenye uamuzi wa mwisho kuhusu nani awe mbunge wao mwaka 2010.
“Tuwape wananchi wa jimbo la Simanjiro nafasi ya kumchagua mtu wanayeona anafaa kuwa mwakilishi wao….wananchi ndiyo mahakimu wazuri kidemokrasia badala wapambe kulumbana katika masuala yasiyo na msingi”, alisema Millya.
Kwa upande wake, akizungumza muda mfupi baada ya kuachiwa huru na mahakama, Sendeka aliwaeleza waandishi wa habari kuwa anashukuru mahakama imetoa maamuzi ya haki katika kesi hiyo hiyo lakini binafsi alikuwa tayari kupokea maamuzi yoyote.
“Binafsi nilikuwa radhi kupokea maamuzi yoyote yatakayotolewa na mahakama kama nilivyowaambia wenzangu tangu Januari mwaka jana kuwa waendelee na kazi zao kama kawaida kwa kuwa mahakama zetu zina hadhi ya kuaminiwa”, alisema Sendeka.
Sendeka aliongeza: “Binafsi kama Mkiristo nimewasamehe kwa nia moja wale wote waliohusika katika kutaka kunichafulia jina langu na hadhi yangu miongoni mwa wanajamii, lakini napenda kuweka wazi kuwa nitashauriana na wenzangu tuone jinsi waliohusika watakavyosafisha jina langu”, alisema.
Mbunge huyo jana Jumanne alitarajiwa kupokelewa kishujaa katika mji wa Orkesmet ambako ni makao makuu ya wilaya hiyo katika mkutano mkubwa wa hadhara ulioandaliwa na wafuasi wake.

My comments are: Ole sendeka usikubali, chapa kazi yako na wananchi wamejua jema na baya na kibaraka ni nani.
 
Back
Top Bottom