Ole Medeye jiandae kuachia jimbo

Huyo jamaa alishindwa uchaguzi uliopita na mgombea wa cdm anayeitwa Olekishambuu! Nec wakaamua kumtangaza Medeye, EL akiwa nyuma ya mkurugenzi wakati website ya nec ikiwa imeshajazwa jina la mgombea wa cdm kama mshindi! Kimsingi ni mbunge wa Nec na sio wa wana Arumeru West!

Mathias Ole Kisambu alitangazwa mshindi, lakini cha ajabu kesho yake Olemedeye akatangazwa mshindi.
Inasemekana Ole Kisambu aliupiga bei ushindi wake.
Kwakuwa CDM wana madiwani wengi Arumeru Magharibi, kinachotakiwa ni kumsimamisha mtu mwingine anayekubalika kwa wananchi wa Arumeru tofauti na Ole Kisambu.
Kwa mfano yule diwani wa Olturoto, anajituma sana kufanya kazi za maendeleo. Hata Kendo wa Kata ya Sokon two.
 
Ole kisambu wala hakuibiwa, aliuza jimbo. Alisaidiwa sana na jamaa yangu kwenye kampeni, na aliposhinda gafla akashindwa, jamaa akapigiwa sim kulizwa ni nini kimetokea, akajib nitakuambia... Ndo kimoja hata akipigiwa sim hapokei mpaka leo. Jamaa INASADIKIKA alikula hela ya EL.
 
najiandaa kuchukua jimbo hili mnipe sapoti wakuu. Nimezaliwa Kijiji cha Manyire Kata Mlangarifni nina uwezo na elimu ya degree 2. Matatizo ya Arumeru mgrb ndio profession yangu niliosomea.

uko chama kipi?arusha wameshaizika ccm makaburi ya ngarasero!
 
baada ya kazi nzito iliyofanywa na nguvu ya umma huko arumeru mashariki dalili zinaonyesha wakati umefika kwa gharika hili kuhamia jimbo pacha la arumeru magharibi.

Kijografia majimbo haya mawili yako chini ya wilaya moja inayojulikana kama arumeru.wilaya hii pia imegawanyika katika halmashauri mbili za meru DC na arusha DC.
Kimaendeleo halmashauri ya meru(jimbo la arumeru mashariki) linaonekana kuwa mbele kimaendeleo kulinganisha na halmashauri ya arusha(jimbo la arumeru magharibi)
wakazi wengi wa arumeru magharibi ni wa kabila la waarusha huku wakazi wengi wa arumeru mashariki ni kutoka kabila la wameru.

matatizo ya wananchi wa majimbo haya yanalingana sana.
1.Ukosefu wa maji safi na salama licha ya kuwa na chanzo muhimu cha maji(mlima meru).maji haya yanaanzia arumeru kwenda monduli bila kutumiwa na wakazi wa arumeru.

2.wananchi kudhulumiwa ardhi na mafisadi pamoja na mabeberu ya kizungu.
Kama mnakumbuka halmashauri ya arusha iliuza mashamba ya burka katika hali iliyoacha manunguniko kwa wananchi(wafanyakazi wa kipato cha kati,wakulima na wafugaji wadogo).Ardhi hii ilienda kwa vigogo mfano chaz kimey,rizwani,ole medey(mbunge na naibu waziri wa ardhi)
pia ukienda maeneo ya selian estate utakutana na makaburu walioigeuza Tanzania kama sehemu ya south afrika.

Kwa upande wa arumeru mashariki mengi yalisemwa na mbunge Nassari.

Kuna matatizo mengine mengi yanayofanana na sehemu nyingi za Tanzania kama vile kwenye sekta ya afya,elimu na miundo mbinu.

Baada ya wakazi wa meru kushtuka sasa ni zamu ya wananchi wa jimbo la arumeru magharibi kufanya maamuzi ya kiukombozi.
Ni wakati wa chadema ku-organize nguvu ya umma iliyoko jimbo la ole medey.

Siku za ole medei na ccm kuwakilisha waarusha zinaelekea ukingoni.

Siku za ole medey kuwasalimia wananchi wa jimbo lako kwa kutumia mkia wa ng'ombe zinahesabika.nguvu ya umma inakuja..

Naomba kuwasilisha kwa niaba ya NGUVU YA UMMA(PEOPLES POWER)

Arumeru magharibi ni jimbo la CDM uchaguzi wa 2010 ole kisambu alishinda ila alivyokuwa boya akapewa 60mil na medeye ili akubali kushindwa naye akakubali akalamba mshiko kisha akakimbia jimbo kwa miezi 2 ndo akarudi.
Medeye akubaliki kabisa recent event wananchi wa sekei walijichangisha wakajenga kisima cha maji wakamuomba Medeye aje kuzingua akawambia wananchi kuwa eti hawana ushirikiano hivyo akawatosa unaambiwa kwa hasira wale wananchi wakaapa kumuwajibisha medeye 2015
Mytake: CDM tafuteni kamanda wa ukweli ambaye ataongoza mapambano ya ukombizi tusifanye kosa kumrudisha Ole kisambu coz alishatusaliti uchaguzi uliopita
 
Ajiandaaje sasa, ina`maaana akusanye sanaaa, adui unamsuprise. ukimpa muda wa kujiandaaa ni sawa na muuza duka wako umuambie jiandae nataka kukufukuza manake unamuhimiza akufufanyie nn hapo?
 
Ajiandaaje sasa, ina`maaana akusanye sanaaa, adui unamsuprise. ukimpa muda wa kujiandaaa ni sawa na muuza duka wako umuambie jiandae nataka kukufukuza manake unamuhimiza akufufanyie nn hapo?
ajiandae kuachia jimbo!jaribu kuelewa thread kabla ya kupost.
 
najiandaa kuchukua jimbo hili mnipe sapoti wakuu. Nimezaliwa Kijiji cha Manyire Kata Mlangarifni nina uwezo na elimu ya degree 2. Matatizo ya Arumeru mgrb ndio profession yangu niliosomea.

1.Unakadi ya CDM?upo due?
2. Umejiandikisha Arumeru magharibi?
3.Unarudigi kwenu?
4. Unaweza kujenga hoja au ndo mambo ya sioi?
5. Kilugha unajua?
Jipe hapo kama ukipita screan nyingine itafuata
 
baada ya kazi nzito iliyofanywa na nguvu ya umma huko arumeru mashariki dalili zinaonyesha wakati umefika kwa gharika hili kuhamia jimbo pacha la arumeru magharibi.

Kijografia majimbo haya mawili yako chini ya wilaya moja inayojulikana kama arumeru.wilaya hii pia imegawanyika katika halmashauri mbili za meru DC na arusha DC.
Kimaendeleo halmashauri ya meru(jimbo la arumeru mashariki) linaonekana kuwa mbele kimaendeleo kulinganisha na halmashauri ya arusha(jimbo la arumeru magharibi)
wakazi wengi wa arumeru magharibi ni wa kabila la waarusha huku wakazi wengi wa arumeru mashariki ni kutoka kabila la wameru.

matatizo ya wananchi wa majimbo haya yanalingana sana.
1.Ukosefu wa maji safi na salama licha ya kuwa na chanzo muhimu cha maji(mlima meru).maji haya yanaanzia arumeru kwenda monduli bila kutumiwa na wakazi wa arumeru.

2.wananchi kudhulumiwa ardhi na mafisadi pamoja na mabeberu ya kizungu.
Kama mnakumbuka halmashauri ya arusha iliuza mashamba ya burka katika hali iliyoacha manunguniko kwa wananchi(wafanyakazi wa kipato cha kati,wakulima na wafugaji wadogo).Ardhi hii ilienda kwa vigogo mfano chaz kimey,rizwani,ole medey(mbunge na naibu waziri wa ardhi)
pia ukienda maeneo ya selian estate utakutana na makaburu walioigeuza Tanzania kama sehemu ya south afrika.

Kwa upande wa arumeru mashariki mengi yalisemwa na mbunge Nassari.

Kuna matatizo mengine mengi yanayofanana na sehemu nyingi za Tanzania kama vile kwenye sekta ya afya,elimu na miundo mbinu.

Baada ya wakazi wa meru kushtuka sasa ni zamu ya wananchi wa jimbo la arumeru magharibi kufanya maamuzi ya kiukombozi.
Ni wakati wa chadema ku-organize nguvu ya umma iliyoko jimbo la ole medey.

Siku za ole medei na ccm kuwakilisha waarusha zinaelekea ukingoni.

Siku za ole medey kuwasalimia wananchi wa jimbo lako kwa kutumia mkia wa ng'ombe zinahesabika.nguvu ya umma inakuja..

Naomba kuwasilisha kwa niaba ya NGUVU YA UMMA(PEOPLES POWER)

Naunga mkono 100% elmedeye asulubiwe
 
Asome alama za nyakati tu kuliko kupoteza pesa kwa kuhonga
Mwache ahonge ili atakapopigwa chini awe ameshafilisika na hela zote alizoiba kwa kujitengenezea safari za mara kwa mara alipokuwa Mkurugenzi wa fedha pale TCRA!
 
lingine lipo mbeya vijijini japo aliyeliuza kipindi kile(bwn shitambala) anajipanga kuleta upinzani mbeya mjini 2015 kupitia magamba,yote hiyo ni tamaa tuu,hata iweje 2015 mbeya vijijini lazima likombolewe
 
chadema hana nafasi arumeru magharibi

Hata wengine walidiriki kusema watajinyonga kama itakuwa kweli CDM ingechukua Arumeru Mashariki.

Lakini baadae hawajaonekana hata walitorokea na kurudi wajuako hakika hawajaaga hata mafisadi wenzio waliokuwa nao ktk ufisadi wao!
 
Pia 2010 Ole Madeye alishinda kwa tabu sana kuliko wabunge wengine wa Arusha. CHADEMA wakati ni huu mikati ya kukomboa hili jibo ifanyike sasa
 
Ngaramtoni kuna shida ya maji safi ya bomba watu wanatumia maji ya visima maji ya bomba yapo kwa mbunge wa zamani wa CCM ndo anawapa watu maji safi ya kunywa tena si zaidi ya ndoo mbili hata hayatoshi.
 
kipuyo,elisa mollel na sasa ole medey hawajaitendea haki arumeru magharibi.pamoja na kwamba jimbo hili liko mpakani mwa kenya na tanzania na pia kupakana na manispaa ya arusha bado tunaendelea kushuhudia wakazi wake wakiwa maskini na ombaomba mijini.
Wakazi wa jimbo hili hawajui kusoma na kuandika.
Watoto wa ki-arusha wanakufa kwa utapiamlo na magonjwa ya kuambukiza.

Pesa iliyopatikana wakati wa mchakato wa uuzaji wa viwanja vya burka haieleweki imetumika vipi.

Mbunge wake hajawahi kusimama bungeni na kuuliza kwa nini barabara namanga-arusha iliyokuwa ikamilike na kukabidhiwa august mwaka jana haijakamilika mpaka leo.

Ol medey jiandae
 
2010 mgombea wa CDM Ole Kisambu alimpeleka sana Ole Medeye tatizo hakuwa na comitted mawakala ktk maeneo ya Oljoro na Mirongine ambao by saa 7 wengi wao walikuwa washalewa na kama sikosei CDM arumeru Magh ina madiwani 6 means inatawala kata 6 kuanzia kiranyi na tayari CDM ina nguvu huu ukanda wa Nairobi road nguvu ielekezwe upande wa chini wa barabara ya BAbati huko ndo bado ila 2015 hadi Longido CDM inabeba wana hasira na CCM haijawalipa fidia ya mifugo yao ilyokufa ingawa inatangaza imelipa
 
Back
Top Bottom