Ole Medeye jiandae kuachia jimbo

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
baada ya kazi nzito iliyofanywa na nguvu ya umma huko arumeru mashariki dalili zinaonyesha wakati umefika kwa gharika hili kuhamia jimbo pacha la arumeru magharibi.

Kijografia majimbo haya mawili yako chini ya wilaya moja inayojulikana kama arumeru.wilaya hii pia imegawanyika katika halmashauri mbili za meru DC na arusha DC.
Kimaendeleo halmashauri ya meru(jimbo la arumeru mashariki) linaonekana kuwa mbele kimaendeleo kulinganisha na halmashauri ya arusha(jimbo la arumeru magharibi)
wakazi wengi wa arumeru magharibi ni wa kabila la waarusha huku wakazi wengi wa arumeru mashariki ni kutoka kabila la wameru.

matatizo ya wananchi wa majimbo haya yanalingana sana.
1.Ukosefu wa maji safi na salama licha ya kuwa na chanzo muhimu cha maji(mlima meru).maji haya yanaanzia arumeru kwenda monduli bila kutumiwa na wakazi wa arumeru.

2.wananchi kudhulumiwa ardhi na mafisadi pamoja na mabeberu ya kizungu.
Kama mnakumbuka halmashauri ya arusha iliuza mashamba ya burka katika hali iliyoacha manunguniko kwa wananchi(wafanyakazi wa kipato cha kati,wakulima na wafugaji wadogo).Ardhi hii ilienda kwa vigogo mfano chaz kimey,rizwani,ole medey(mbunge na naibu waziri wa ardhi)
pia ukienda maeneo ya selian estate utakutana na makaburu walioigeuza Tanzania kama sehemu ya south afrika.

Kwa upande wa arumeru mashariki mengi yalisemwa na mbunge Nassari.

Kuna matatizo mengine mengi yanayofanana na sehemu nyingi za Tanzania kama vile kwenye sekta ya afya,elimu na miundo mbinu.

Baada ya wakazi wa meru kushtuka sasa ni zamu ya wananchi wa jimbo la arumeru magharibi kufanya maamuzi ya kiukombozi.
Ni wakati wa chadema ku-organize nguvu ya umma iliyoko jimbo la ole medey.

Siku za ole medei na ccm kuwakilisha waarusha zinaelekea ukingoni.

Siku za ole medey kuwasalimia wananchi wa jimbo lako kwa kutumia mkia wa ng'ombe zinahesabika.nguvu ya umma inakuja..

Naomba kuwasilisha kwa niaba ya NGUVU YA UMMA(PEOPLES POWER)

UPDATES:uamuzi wa ole millya kujivua gamba na kuamia chadema ni sehemu muhimu ya kumuondoa ole medey arumeru magharibi.kada huyu aliyetoka ccm anaungwa mkono na wakazi wa arumeru magharibi hivyo kazi ya uhamasishaji kwa cdm itakuwa rahisi kuliko maelezo.
 
Ni kweli kamanda.Kwa ujumla kazi ilishaanza yani propaganda za kule kwisha habari yake.Kikubwa tunachokifanya hasa ni kukijenga chama kuanzia ngazi ya chini.Ni dhahiri Chama kikiwa na mizizi na kuwa na wakazi wanaotambulika kama ofisi na matawi hasa maeneo yetu ya umasaini hasa Oldonyosambu, Seliani,Siwandeeti,Kisongo,Sanawari,Ilboru Orgilai na kwingine hasa maeneo ya vijijini ni dhahiri CDM tutafanikiwa.Matatizo ya Ar Mashariki na Magharibi yote yanafanana hilo halina ubishi..Kinachohitajika ni kuweka mizizi ya kutosha hasa kikubwa hapa ni kukijenga chama kwanza kwa kuwa jimbo lile lina mbunge wake mpaka 2015.
 
OLe Medeye yeye ni pandikizi la Lowassa wakati alipogombana na Elisa Mollel, sasa mfadhili wake kadondoka ajue kuwa na yeye ndio anakwenda na maji!
 
Bila kutaka kujifunza na kurekebisha makosa, we are preparing our own downfall. CCM wana masikio...naamini wameanza kusikia kuchoka kwa watu na haya mambo yanayoendelea
 
Eti walifikiri karata ya Rais kurudisha ekari 5000 za ardhi kule Arumeru magharibi ingewasidia! hahahahaha
 
Huyu lazima atoke, maana ndo anauza ardhi kwa wageni kwa fujo. hana msaada kwa wananchi wake, kwanza anawachakachua ardhi

Wa arusha ni tofauti na wameru. Waarusha ni wagumu kubadilika ila vijana wao ndo wataleta mageuzi, so inatakiwa elimu ya uraia na pia vijana waandikishwe katika dftari la wapiga kura.
 
Ni kweli kamanda.Kwa ujumla kazi ilishaanza yani propaganda za kule kwisha habari yake.Kikubwa tunachokifanya hasa ni kukijenga chama kuanzia ngazi ya chini.Ni dhahiri Chama kikiwa na mizizi na kuwa na wakazi wanaotambulika kama ofisi na matawi hasa maeneo yetu ya umasaini hasa Oldonyosambu, Seliani,Siwandeeti,Kisongo,Sanawari,Ilboru Orgilai na kwingine hasa maeneo ya vijijini ni dhahiri CDM tutafanikiwa.Matatizo ya Ar Mashariki na Magharibi yote yanafanana hilo halina ubishi..Kinachohitajika ni kuweka mizizi ya kutosha hasa kikubwa hapa ni kukijenga chama kwanza kwa kuwa jimbo lile lina mbunge wake mpaka 2015.
naamini maeneo ya engare olmotonyi,kibaoni,kwa iddi,kibao cha dodoma ni maeneo muhimu ya ukombozi kama ilivyokua Usa,tengeru,maji ya chai na kikatiti
 
Upo sahihi mkuu. Pia natoa tahadhari kwa Salome Mwambu wa Iramba mashariki na Mwigulu Nchemba wa Iramba magharibi wafungashe virago vyao mapema kwa sababu 2015 hawataambulia kitu. M4C FOREVER.
 
Huyo jamaa alishindwa uchaguzi uliopita na mgombea wa cdm anayeitwa Olekishambuu! Nec wakaamua kumtangaza Medeye, EL akiwa nyuma ya mkurugenzi wakati website ya nec ikiwa imeshajazwa jina la mgombea wa cdm kama mshindi! Kimsingi ni mbunge wa Nec na sio wa wana Arumeru West!
 
Kwa taarifa yako ni kwamba Ole Medeye alipigwa chini 2010,wakachakachua! Sema CDM uchaguzi ujao wajiandae kulinda kura zao!
 
Huyu gamba aitwaye Ole Medeye ni pandikizi la EL lakini hakika kwa hali tunayoenenda nayo ni kwmb huyu ni Ole ni JANGA kwa wanainchi wa Arumeru Magharibi ila ni juzi tu nimebahatika kukutana na wenyeji wa Kata mbili tofauti na wakiwa na hoja nyingi tata waliahidiwa na MB waliyompa kura na akawasahau tangu wampe kura hajatia mguu kuwasalimu katu katu!

Na kwa dalili hii nibora aachie jimbo tu hana maana yeyote ya kuwepo kwake jimbo kwa wanainchi na waliompa kura.
 
Kwa taarifa yako ni kwamba Ole Medeye alipigwa chini 2010,wakachakachua! Sema CDM uchaguzi ujao wajiandae kulinda kura zao!
mkuu chadema wajiandae ku-organise nguvu ya umma.piga kura linda kura ndio mpango wenyewe!
 
Matokeo ya 2010 yalikuwa ni upepo wa kaskazi kwa CDM hivyo kubeba kenge na mamba.2015 wapo watakao toswa katika uchaguzi wa ndani na changamoto itakuwa kubwa kwa wangombea wapya wenye tamaa ya uongozi na wenye nia ya dhati.

Kujipanga kwa CDM ni muhimu kwani magamba huwa wananguvu katika chaguzi za jumla kwani ushambuliaji (team ya CDM kama ya Arumeru,Igunga na Uzini) unakuwa haupo, kila mgombea anakufa kivyake katika jimbo.
 
najiandaa kuchukua jimbo hili mnipe sapoti wakuu. Nimezaliwa Kijiji cha Manyire Kata Mlangarifni nina uwezo na elimu ya degree 2. Matatizo ya Arumeru mgrb ndio profession yangu niliosomea.
 
ki ukweli medeye hana mashiko arumeru, ujanja wake upo knye kuchangia misiba tu na kuketi karibu na mafisadi, ila kimkakati waarusha wameanza kubadilika, ilboru, mula, siwandeti, sakina, snawari, sekei kote jamaaa hakubaliki kabisa na vijana wapo tayari muda wowote kumtoa jamaa 2015, ishu iliyopo ni kuanza mkakati mapema tukijenge chama mapema na kuhamasisha vijana wengi wajiandikishe kupiga kura ili 2015 idadi ya vijana iwafunike wazee na wasiotaka mabadiliko.
mwisho wanaharakati kuanza kujuana ili kujipa moyo na kutengeneza network ya ushawishi kwa umma na kugawana majukumu. medeye mwepesi kabisa
 
Back
Top Bottom