Ok Pinda... here is the deal..

"kama mtu mwenye akili akikupa wazo la kijinga akijua na wewe una akili nawe ukalikubali (wazo hilo) atakudharau" - Nyerere (Mei Mosi 1995, Mbeya)[/QUOTE

Mzee Mwanakijiji,

Asante sana nilighafilika kidogo kwenye hiyo quote. Sasa kweli MAFISADI wanaonyesha kutudharau. Let's not let them get away with it this time. Naamini kabisa huyo MWEZA YOTE yuko pamoja nasi na hatatutupa.
 
ni kitu gani kilichowapa viongozi wa ccm jeuri ya kufikia hata kudharau waliowachagua kiasi hiki?
 
Nasikia kuwa baada ya mzee Mandela kushika uongozi S/A kulionekana tatizo la usalama wa bahari yetu ya Hindi kuingiliwa hovyo bila serikali kugundua, hivyo Mzee Mandela akasema Watanzania mlinisaidia sana nami sipendi kuona usalama wenu ukiwa hatarini hivyo natoa mapesa muone mtayatumia jinsi gani kuimarisha ulinzi wenu pamoja na bahari yenu, mipesa hiyo ikaingia mikononi mwa BWM na watalaam wake wakupindisha mambo ndipo ikabuniwa Buhemba,Meremeta,Tangold,etc alimradi fujo ilianzia hapo kwani wote waliokuwa wanajua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Madiba walinufaika mpaka Buhemba ilipokufa, kitamu kingine katika ze comedy hii ni kwamba kwa maisha yote ya marehemu BUhemba mpaka ilipokufa na kuzikwa hakuna hata senti tano iliyoingia si Buhemba, serekalini, wala Nyumbu-TATC pale Kibaha. waliuza sana lakini pesa-0000....

Kwa hilo ndugu zanguni Pinda atasema nini zaidi ya kusema Meremeta ni siri ya serikali? (story hii ni habari niliyopewa na jamaa yangu aliyekuwa karibu nao katika kwapuakwapua)
 
Ndugu zanguni,
Kazi moja ya Waziri Mkuu ni kutetea kwa nguvu zote shughuli zote za Serikali yake. Kwa maana nyingine Pinda hana alternative bali kutetea ama kutafuta mbinu za kutoidhalilisha Serikali aliyoitumikia na anayoendelea kutumikia. Kwa hiyo, tusitarajie Waziri Mkuu wa Serikali ya CCM kwenda kinyume na maamuzi ama vitendo vya Serikali yake. Vivyo hivyo Wabunge wa CCM, wanadhani wana wajibu wa kutetea Serikali yao ndio maana wengi wanapata kigugumizi ama kukosa ujasiri wa kusimama na kukosoa Serikali ya chama chao. Na hao wachache wanaozungumza kuikosoa Serikali moja kwa moja wanafanya hivyo wakijua wanajitafutia maadui ndani ya Serikali na miongoni mwa Wabunge ambao hawapendi kuunga mkono ukweli wakidhani kwa kufanya hivyo wanaikosea Serikali. Ndio maana tumesikia Wabunge wenye ujasiri wa kuikosoa Serikali wanatoa matamshi kwamba hawaogopi vitisho n.k..

Mie nadhani tumefika mahali viongozi wa Serikali na Wabunge wanasahau kwamba wao ni wawakilishi/watumwa wa wananchi, na wanajenga dhana kwamba wananchi ndio watumwa wao kwa maana hiyo wanaweza kuwaamulia lolote lile bila kutilia maanani utashi wa wananchi. Wanachotaka wananchi ni majibu ama maelezo sahihi juu ya masuala ama vitendo vya Serikali vyenye utata. Majibu yakitolewa ambayo yana mashaka, wananchi wataendelea kudai. Kuna tatizo gani ku-down grade hiyo Siri ikawa Wazi ili wananchi waridhike kwamba hakukuwa na makosa yaliyofanyika ndani ya Siri hiyo? Na kama makosa yalikuwepo yabainike ili wananchi wajiridhishe kwamba hayatafanyika tena?

Kwa mwenendo huu wa kuamini kwamba kuna mambo hayapaswi wananchi kuyajua kuhusu hoja zenye utata, hata kama watafikia uamuzi wa Bunge kukaa wakafunga milango yote na madirisha, wakazima kamera zote kujadili Meremeta na mengine yanayosemwa kuwa yanahusu 'Ulinzi na Usalama' na midhali shughuli za Ulinzi na Usalama zinafanywa na vyombo vya Serikali bado yatajaribu kutolewa maelezo ‘matamu’ kwa Serikali ya CCM kutetea maamuzi ya Serikali. Pia, midhali Wabunge wa CCM ndio wengi, utetezi wa Serikali utaungwa mkono na hao wengi wa CCM. Na kama itapigwa kura ya siri, wapo wengine watakaoogopa kupinga utetezi wa Serikali wakidhani kwa kuwa kama masuala ya Usalama ni ya usiri mkubwa basi huenda jicho la siri la 'Usalama' limo Bungeni linawamulika! Pamoja na hayo, hata kama Waziri Mkuu Pinda yeye kama Pinda amegundua na anayachukia sana maamuzi yale kwa kuwa yameifikisha pabaya Serikali anayoitumikia, kwa cheo alichonacho tayari mdomo wake umeishawekewa 'gavana' ya kutotamka anachoamini bali atawajibika kutetea maamuzi ya Serikali anayoiongoza. Kwa hiyo, bado kuna kazi kubwa ya kubadilisha fikra za kulinda Tawala.

Hata hivyo, naamini kwamba kutokana na juhudi zinazoendelea kupitia majukwaa mbalimbali za kuwaelimisha wananchi juu haki yao ya msingi ya kutaka maelezo unapotokea utata wowote juu ya mwenendo wa Serikali yao na kelele zinazopigwa dhidi ya viongozi wasio waadilifu, yapo matumaini kwamba viongozi watapata “upako” utakaogeuza fikra zao ili wapate fikra mpya ama warejeshe “Fikra Sahihi ….” za kujali kwa dhati na kuweka mbele maslahi ya wananchi na maslahi ya taifa letu kwa ujumla!
 
Bibi Ntilie.. umesema maneno mazito na kimsingi umetupa ile ethos inayoongoza mjadala ndani ya CCM na serikali yake. Lakini huu mtindo wa kuitetea serikali yao ndio uliotufikisha kwenye matukio ya Februari. Wasipoangalia na Pinda naye anaweza kujikuta analazimishwa kujiuzulu kwa kulidanganya Bunge.

Haitakuwa mara ya kwanza duniani kwa waziri mkuu kulazimika kuondolewa madarakani muda si mrefu tangu aingie. Haiwezekani mtu atawale nchi kwa geresha na aongoze kwa hadaa. Ukweli utajulikana tu.
 
Kuweni wa kweli sasa kwani saa ya mjaribu inakuja na imefika, siku ya Jumatano ijayo kama nilivyofanya mwaka jana nitaongoza sala ya "baraka na laana" na Mungu aliye mbinguni mwenye kutawala nyakati na nyakati, mmiliki wa nyota na sayari na muumbaji wa muda, kina, umbali na mwendo! na Mfadhili wa uhai wote atasikia.

Mwanakijiji,

Ngoja nikukumbushe kidogo sala yako ulioahidi kuiswali juzi jumatano, maana mawio ya Ijumaa hapa bongo yanakaribia kuanza na sala hatujaisikia. Tunakua na wasiwasi kidogo labda umeamua kuachana na uchungaji bila kutustua watoa sadaka.
 
Nasikia kuwa baada ya mzee Mandela kushika uongozi S/A kulionekana tatizo la usalama wa bahari yetu ya Hindi kuingiliwa hovyo bila serikali kugundua, hivyo Mzee Mandela akasema Watanzania mlinisaidia sana nami sipendi kuona usalama wenu ukiwa hatarini hivyo natoa mapesa muone mtayatumia jinsi gani kuimarisha ulinzi wenu pamoja na bahari yenu, mipesa hiyo ikaingia mikononi mwa BWM na watalaam wake wakupindisha mambo ndipo ikabuniwa Buhemba,Meremeta,Tangold,etc alimradi fujo ilianzia hapo kwani wote waliokuwa wanajua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Madiba walinufaika mpaka Buhemba ilipokufa, kitamu kingine katika ze comedy hii ni kwamba kwa maisha yote ya marehemu BUhemba mpaka ilipokufa na kuzikwa hakuna hata senti tano iliyoingia si Buhemba, serekalini, wala Nyumbu-TATC pale Kibaha. waliuza sana lakini pesa-0000....

Kwa hilo ndugu zanguni Pinda atasema nini zaidi ya kusema Meremeta ni siri ya serikali? (story hii ni habari niliyopewa na jamaa yangu aliyekuwa karibu nao katika kwapuakwapua)

Halafu kuna waliolalamika eti kwanini MANDELA hakuja kwenye msiba wa mwalimu!
Hao watu hawakujuwa kuwa msiba wa taifa ni kuuzwa kwa taifa?
 
Sijaona ubavu wa bunge kumuambia Pinda ajiuzuru kwa kusema uwongo may be saa imefika and I stand corrected!
 
Sasa imefika wakati..watu wawe wanaogopa cheo hiki..Uwaziri Mkuu'' sio waone kuchaguliwa ni dili..kwanini msiwe kama Sokoine????!!

R.I.P Sokoine... Tanzanians Miss U a Lot
 
nyota njema huonekana asubuhi lakini kwa pinda alishaanza kupinda toka mwanzo bora aondoke mapema tupate wa kumalizia hii miaka 2 kabla 2010 hatujaing'oa ccm.
 
Bibi Ntilie.. umesema maneno mazito na kimsingi umetupa ile ethos inayoongoza mjadala ndani ya CCM na serikali yake. Lakini huu mtindo wa kuitetea serikali yao ndio uliotufikisha kwenye matukio ya Februari. Wasipoangalia na Pinda naye anaweza kujikuta analazimishwa kujiuzulu kwa kulidanganya Bunge.

Haitakuwa mara ya kwanza duniani kwa waziri mkuu kulazimika kuondolewa madarakani muda si mrefu tangu aingie. Haiwezekani mtu atawale nchi kwa geresha na aongoze kwa hadaa. Ukweli utajulikana tu
.

Mzee Mwanakijiji, naomba nikuite Mzee wa Kijiji kutokana na michango yako kwenye kijiji hiki. Nakubaliana nawe. Iwapo kelele za wananchi zitaendelea kudai maelezo katika masuala mengi tata ambayo yanaikabili Serikali hivi sasa na iwapo Pinda hatakuwa makini na kuelewa kwamba anawajibika zaidi kwa wananchi na maslahi sahihi ya taifa letu, atafikishwa mahali ambapo hatapapenda na sisi ambao tuna imani naye tangu ateuliwa tutabaki kumsikitikia.

Waziri Mkuu Pinda amekuwa akisifiwa sana katika uwezo wake wa kujibu maswali ya papo kwa papo Bungeni. Hili ni jambo jema sana inaonyesha anajua Serikali anayoiongoza inafanya nini. Lakini pamoja na hayo lazima wakati wote azingatie kwamba majibu anayotoa yanapaswa yawe na maslahi ama utetezi kwa wananchi kuliko kuitetea Serikali. Suala zima la uongozi mahiri linazunguka kwenye namna ya kuwaangalia wananchi, kujua shida zao, na kutafuta njia za dhati za kuwasaidia kutatua matatizo waliyonayo. Kwa yale tunayoyashuhudia hivi sasa, ni wazi bado hakuna utashi wa dhati wa viongozi watu kuangalia kwa jicho makini shida walizonazo wananchi na kuwasaidia bali kinachoendelea katika kujibu hoja mbalimbali ni kutetea Serikali kwa kuficha ukweli wa mambo muhimu.
 
Katiba yetu ina vipengele vifuatavyo ambaavyo naamini vinaweza kutumika kutota katika hii time warp ya ufisadi. Pinda anakuwa kama Q wa Star Trek!

Katiba inasema kuwa Rais anaweza kulivunja Bunge endapo baadhi ya mambo yatatokea, miongoni mwa hayo ni:




Mimi naamini wabunge wakatae kupitisha mojawapo ya bajeti hizi zas serikali au hoja ya Waziri Mkuu ili hatimaye Rais alazimike kuvunja Bunge na turudi kwa wananchi na kuanza moja.

Kuhusu Majeshi yetu Katiba inasema hivi:



Sijaona mahali popote pale ambapo panampa madaraka Rais kuliamuru Jeshi letu lolote kufanya biashara ya aina yoyote isipokuwa iwe inahusiana na Vita na ulinzi wa nchi. NI lazima serikali ioneshe ni jinsi gani Meremeta na makampuni mengine yamehusishwa na masuala ya vita au ulinzi wa nchi. Yaani, hiyo vita iliyosababisha kuundwa kwa Meremeta na kuchotwa mabilioni ilikuwa inapiganwa wapi?

Kwa hiyo tusubirie bajeti ya 2010-2011 tena?!! What an unfortunate nation!
 
Samahani kwa kuchelewa kuwajibu; taarifa yote itakuwa tayari kesho ya jinsi ya kupreorder ripoti hiyo. Tunatengeneza nakala 100 tu (each serialized and individually password protected).

Ripoti yenyewe ina kurasa karibu 40 na references zaidi ya 50 na viambatanishi vyenye kurasa nyingine nyingi; picha na vielelezo vingine vinakuja na ripoti hiyo (zikiwemo za ndege za usafirishaji wa silaha haramu zikiwa Mwanza!)

Ripoti itapatikana kwa mchango wa dola 30/sawa na 30,000 kwa mtindo wa first come, first serve.

Tutakuwa na aina mbili ya kulipia: Kwa kutumia Credit Cards kwa wale wenye nazo na kwa kutumia Western Union. Kwa Western Union kutakuwa na sehemu mbili (kwa taasisi na public officials) na nyingine for the rest of us.

More details tomorrow. All I can say is that it will be "entertainingly shocking!"..

Thanks

M. M. Mwanakijiji

Consortium of Concerned Tanzanians Intl
"Nothing and no one else, but the country first!"
 
....Mwkjj, i would bet my last penny on this...however much the TRUTH will be NAKED,not only will Kingunge & Yusufu be the first ones to feel Sorry4it but they will also try to cover it up!!!,at least a little bit...you will see.
 
Back
Top Bottom