Ok Pinda... here is the deal..

Pinda is nothing but a big joke ambaye hata wenzake kina Mkapa,JK,Lowassa they dont even respect him nina uhakika kina Rostam na Mgonja wana nguvu kuliko this lazy a$$....huyu mtu anafanya office ya katibu kata ionekane ina nguvu kuliko ya Waziri mkuu....tuandike maumivu tuu.


Nafikiri tunaelekea kuwafikia mafisadi.

Pinda inatakiwa aondoke hili asiingizwe kwenye kundi moja kwa moja.

Please Pinda Ondoka ondoka tu. Kuwa mwananchi mtiifu wa Tanzania.
 
Nafikiri tunaelekea kuwafikia mafisadi.

Pinda inatakiwa aondoke hili asiingizwe kwenye kundi moja kwa moja.

Please Pinda Ondoka ondoka tu. Kuwa mwananchi mtiifu wa Tanzania.

He is no longer mtiifu any more kwa Tanzania ,bali kwa Mafisadi wa Meremeta,Tangold,Deepgreen finance, Mwananchi Gold ltd. .....unaweza kuendeleza mpaka mwisho wa siku.
 
Nafikiri tunaelekea kuwafikia mafisadi.

Pinda inatakiwa aondoke hili asiingizwe kwenye kundi moja kwa moja.

Please Pinda Ondoka ondoka tu. Kuwa mwananchi mtiifu wa Tanzania.

Yani kwa maelezo yake bungeni leo asiwekwe moja kwa moja?
Ama na yeye apewe nafasi kama wengine mliokuwa mkiwapa nafasi!?
MH!
Ila this time around huyu unataka kumpa nafasi ya kuja na kukanusha kuwa hakukanusha KWAMBA MKAPA NI FISADI...MEREMETA NI YAKE NA SI YA JESHI!
Duh!
 
Nilianzisha thread na kumtaka Killango atoke ccm kwasababu kikao walichokaa na MKAPA...SAMBAMBA NA FAMILIA YA MWALIMU KUAMUA KUMKUMBATIA WAZI WAZI NA KUMWACHA HATA KWENYE FAMILIA YAO....NI KITENDO CHA HUZUNI KILICHOPELEKEA MIMI KUKIRI WAZI KUWA...MWALIMU ALIPOKUFA NA ccm ILIKUFA NAYE!
 
"Jumatano, mbingu zitafunguka na sauti itasikika ya kwamba "mafisadi mmekwisha"! Mna siku tano kujisahihisha kuhusu uzugaji huu! "

Mwanakijiji

Nasubiri kwa hamu siku hiyo ya jumatano, maana wengi tutafufuka.
 
Katiba yetu ina vipengele vifuatavyo ambaavyo naamini vinaweza kutumika kutota katika hii time warp ya ufisadi. Pinda anakuwa kama Q wa Star Trek!

Katiba inasema kuwa Rais anaweza kulivunja Bunge endapo baadhi ya mambo yatatokea, miongoni mwa hayo ni:


Ibara 90:2
(b) kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti
iliyopendekezwa na Serikali;

na:

(d) kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni ya
msingi katika sera za Serikali, na Rais anaona
kwamba njia ya kuendelea kutoka hapo si kumteua
Waziri Mkuu mwingine bali ni kuitisha Uchaguzi Mkuu;

Mimi naamini wabunge wakatae kupitisha mojawapo ya bajeti hizi zas serikali au hoja ya Waziri Mkuu ili hatimaye Rais alazimike kuvunja Bunge na turudi kwa wananchi na kuanza moja.

Kuhusu Majeshi yetu Katiba inasema hivi:

MAJESHI YA ULINZI

147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au
kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au
kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu
wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina
mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi
wa Tanzania.
(3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na
chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki
ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
(4) Kwa madhumuni ya ibara hii, "mwanajeshi" maana yake
ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu
katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi
la Kujenga Taifa.

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano,
mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
(2) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
iliyotungwa na Bunge, madaraka juu ya mambo yafuatayo
yatakuwa mikononi mwa Amiri Jeshi Mkuu, yaani-
(a) madaraka ya kuwateua viongozi katika majeshi ya
ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(b) madaraka ya kuwateua watu watakaojiunga na
majeshi ya ulinzi na madaraka ya kuwaondoa jeshini
wanajeshi;
(c) madaraka ya kuwateua wanajeshi watakaoongoza
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
105
vikosi mbali mbali vya majeshi ya ulinzi; na
(d) madaraka ya kumwamuru mwanajeshi yeyote
asitumie madaraka yoyote aliyokabidhiwa na
ambayo yanaambatana na kuwa kwake mwanajeshi.
(3) Jambo lolote atakalotenda mwanajeshi yoyote kinyume
cha amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu kwa mujibu wa
masharti ya ibara ndogo ya (1) na (2) ya ibara hii litakuwa
batilifu.

Sijaona mahali popote pale ambapo panampa madaraka Rais kuliamuru Jeshi letu lolote kufanya biashara ya aina yoyote isipokuwa iwe inahusiana na Vita na ulinzi wa nchi. NI lazima serikali ioneshe ni jinsi gani Meremeta na makampuni mengine yamehusishwa na masuala ya vita au ulinzi wa nchi. Yaani, hiyo vita iliyosababisha kuundwa kwa Meremeta na kuchotwa mabilioni ilikuwa inapiganwa wapi?
 
Na Sasa Nimeamini Option Ni Mbili...

Option 1...

Ccm Walikomboe Taifa Kwa Kuyatema Maslahi Ya Chama Na Makubaliano Yao Na Mkapa Kwene Kikao Chao Cha Siri!

Option...wapinzani Na Mkongozwa Na Dk Slaa Pamoja Na Wengine Kama Kina Mwakyembe Simamieni Haki Na Muhakikishe Mchele Na Chuya Vinabainishwa...hili Litasaidia Kuuza Issue Kwa Taifa Ambalo Limeshaanza Kusikia Harufu Mbaya!

Mungu Atuongoze Na Atuangazie Ili Mwanga Wake Uwamulike Waovu Wote Waliomtenda Yeye Na Watu Wake Mabaya Yasiyothimilka!

God Willing....we Will Be Victorious!
 
We need a new government with a new Mandate.. turudi kwa wapiga kura. Let me look at the constitution...

Nimekuwa nikisema kila siku kuwa kuna haja ya kuwahamasisha wapiga kura ili kufanikisha regime change kwa uhalali. Wapiga kura wahamasishwe waone mapungufu ya serikali waliyoichagua, ili wakati wa kura ujao waweze kufanya uamuzi wa manufaa kwao.

POWER TO THE PEOPLE!
VENCEREMOS!
PATRIA O MUERTE!
 
He is no longer mtiifu any more kwa Tanzania ,bali kwa Mafisadi wa Meremeta,Tangold,Deepgreen finance, Mwananchi Gold ltd. .....unaweza kuendeleza mpaka mwisho wa siku.

Pinda ameishapinda kabisa. Lakini kuna msemo kuwa jina huwa lina mahusiano na matendo. Kwa hiyo sishangai
 
katiba Yetu Ina Vipengele Vifuatavyo Ambaavyo Naamini Vinaweza Kutumika Kutota Katika Hii Time Warp Ya Ufisadi. Pinda Anakuwa Kama Q Wa Star Trek!

Katiba Inasema Kuwa Rais Anaweza Kulivunja Bunge Endapo Baadhi Ya Mambo Yatatokea, Miongoni Mwa Hayo Ni:




Mimi Naamini Wabunge Wakatae Kupitisha Mojawapo Ya Bajeti Hizi Zas Serikali Au Hoja Ya Waziri Mkuu Ili Hatimaye Rais Alazimike Kuvunja Bunge Na Turudi Kwa Wananchi Na Kuanza Moja.

Kuhusu Majeshi Yetu Katiba Inasema Hivi:



Sijaona Mahali Popote Pale Ambapo Panampa Madaraka Rais Kuliamuru Jeshi Letu Lolote Kufanya Biashara Ya Aina Yoyote Isipokuwa Iwe Inahusiana Na Vita Na Ulinzi Wa Nchi. Ni Lazima Serikali Ioneshe Ni Jinsi Gani Meremeta Na Makampuni Mengine Yamehusishwa Na Masuala Ya Vita Au Ulinzi Wa Nchi. Yaani, Hiyo Vita Iliyosababisha Kuundwa Kwa Meremeta Na Kuchotwa Mabilioni Ilikuwa Inapiganwa Wapi?

Hivi Nilivyosema Niko Mbioni Kuifungulia Serikali Mashitaka Ulifikiri Nacheza?
Nilimpa Kikwete Wiki Hadi Ijumaa!
Amekataa!
Na Mimi Nilijua Hawawezi Kuuficha Huu Ukweli Bila Kukiuka Katiba Yetu Ya Jamhuri Wa Muungano Waliyoigeuza Kuwa Katiba Ya Mafioso Mafisadi!

Na TRUST ME...Baada ya OPTION A KILLANGO...HII NI OPTION P PINDA!
MIMI NILIWAAMBIA WAJE NA OPTION B.
SASA WAMEPITILIZA NA KWENDA HADI P...WAMEPTILIZA ALPHABETI TAKRIBAN 16 HIVI!(A-P=16)
WAO WANABAKIA KUSEMA JMUSHI KICHAA...AMA HATA KUAMINI!

NILIWAANZISHIA THREAD NA KUWAPA USHAURI WA KUTOIPIGIA KURA BAJETI YA MAFISADI ILI BUNGE LIVUNJWE TURUDISHIWE WATU WETU!
WAPINZANI WOTE WALISIKILIZA USHAURI KASORO CHEYO AMBAYE NAYE SASA AMEKURUPUKA KWANI ANAJUA MAISHA YAKE YA KISIASA YAKO DTERMINED DEPENDING NA PERFORMANCE YAKE KWENYE BUNGE HILI LA KIHISTORIA KABISA TZ KULIKO ILIVYOWHI KUWA WAKATI WOWOTE ULE KWENYE HISTORIA YA TAIFA LETU TUNALOLIPENDA KUPITA KIASI!
 
Hawa jamaa wanatuzuga kwa kutulazimisha tukubaliane nao kwamba wanajeshi wanaruhusiwa na katiba ya nchi kufanya biashara za siri, hata kama si biashara halali. Kama ni biashara halali basi si wangetuonyesha balance sheet.... Sisi si wadanganyika kiasi hiki.

Wakati murua umefika kwa Pinda kujiuzuru... Si vyema kukubali kudanganywa milele na watu waliopata publicity kubwa siku chache baada ya kuapishwa kutumikia Taifa kuwa wao ni watu wa Mungu kumbe ni wazugaji tu. Mtu huyu ana-deserve kuzomewa kanisani kwamba yeye ni fisadi kila mara anapokwenda kupokea sakramenti. Akiwa analishwa tu sakramenti my two year old daughter will say it loud kwa sauti ya kitoto "FISADIIIII"... Ebu nipeni address ya kanisa analosali ili mi na familia yangu tukajipange humo na kuanzisha huu moto. Si vyema kukubali kuongozwa na watu wanafiki.
 
Hawa jamaa wanatuzuga kwa kutulazimisha tukubaliane nao kwamba wanajeshi wanaruhusiwa na katiba ya nchi kufanya biashara za siri, hata kama si biashara halali. Kama ni biashara halali basi si wangetuonyesha balance sheet.... Sisi si wadanganyika kiasi hiki.

Wakati murua umefika kwa Pinda kujiuzuru... Si vyema kukubali kudanganywa milele na watu waliopata publicity kubwa siku chache baada ya kuapishwa kutumikia Taifa kuwa wao ni watu wa Mungu kumbe ni wazugaji tu. Mtu huyu ana-deserve kuzomewa kanisani kwamba yeye ni fisadi kila mara anapokwenda kupokea sakramenti. Ebu nipeni address ya kanisa analosali ili mi na familia yangu tukajipange humo na kuanzisha huu moto. Si vyema kukubali kuongozwa na watu wanafiki.

Huyo PADRI atakaye mpa hiyo sacramenti apigwe mawe kama hiyo biblia yao inavyosema!
Kwamba kama MUNGU mwenyewe keshatuonyesha wazi wazi hivi halafu kuna wanaotaka ku PINDA haki yetu...Washirika wao nao watakuwa ni majambazi sambamba na PINDA,MKAPA,ROSTAMA AZIZI,IDDI SIMBA,CHENGE,KIKWETE,KARAMAGI,LUKAZA,MALEGESI,BALALI..THE LIST GOES ON AND ON!
 
Tangu kuteuliwa kwake nilikataa kusema lolote juu ya Pinda na nakumbuka niliandika kuwa nampa benefit of the doubt ili aniconvince yeye si mmoja wao. Niliamini kwamba kila mtu ahukumiwe kwa vitendo vyake na maamuzi yake; niliamini kuwa kila mtu apewe nafasi ya kuonesha uongozi ili ijulikane anaongoza.

Ni kwa sababu hiyo tangu kuteuliwa kwa Pinda sijasema lolote dhidi yake, kauli zake, maamuzi yake n.k Nikimpa nafasi ya kufanya makosa mwanzoni na kujisahihisha kwani ndio anaanza. Miezi zaidi ya minne baadaye, uendelezo wa sera za kizugaji, na maamuzi ya kubabaisha unanilazimu nikiwa nadhamira safi kujikuta natumwa kuwapinga tena, na kuwapinga vikali.

Ni jukumu la raia kuikatalia serikali yake pake inapofanya jambo ambalo halina msingi, manufaa au uwazi kwa wananchi. Niliandika huko nyuma kuwa "lazima tuwakatalie" nikiamini kuwa msingi wa utawala wa demokrasia na unaofuata sheria umejengwa katika nguzo za wananchi kuihoji serikali yao na kutaka maelezo ya kuridhisha na serikali hiyo inaposhindwa kufanya hivyo basi inatakiwa kujiuzulu.

Kwa vile Waziri Mkuu Pinda ameamua kutokuwa mkweli kwa wananchi, na kwa makusudi kutoa taarifa za kupotosha umma, kulipigisha magoti Bunge, natoa ushauri wa bure asahihishe kauli yake Bungeni, na kutoa maelezo mara moja kuhusu kampuni ya Meremeta na ushiriki wa Jeshi letu kwenye biashara ya madini. Afafanue ni sheria gani, maamuzi gani, na kipengele gani cha Katiba yetu kimelipa JWTZ jukumu la kufanya biashara ya madini bila Bunge au wawakilishi wa wananchi kujulishwa. Zaidi ya yote, awaeleze wananchi ni kikao gani cha Baraza la Mawaziri ambacho kiliamuru kuanzishwa kwa kampuni ya Meremeta na kilibariki makampuni ya Mwananchi Gold, Deep Green, Tangold n.k ambayo yote kwa namna moja au nyingine yamehusishwa na uchotaji wa mabilioni ya fedha zetu toka benki kuu.

Kwa vile suala la usalama linahusu usalama wa Taifa letu na wanaoohoji ni wabunge wa Taifa hilo ambao ni wawakilishi wetu, basi hata kama suala la Meremeta haliwezi kuwekwa hadharani (kwa kurushwa kwenye Luninga) basi Bunge lifunge macho na masikio ya nje na Wabunge wote wawe briefed wazi na moja kwa moja kuhusu Meremeta, umiliki wake na uhusiano wake na JWTZ na usalama wa TAifa. Na endapo wabunge wataridhika basi tutapenda kusikia kuwa wameridhika na maelezo hayo na kama wabunge wapige kura kama wasimamizi wa serikali kuamua kama habari hizo kweli zinatishia usalama wa Taifa na kama wananchi wanapaswa kuziona.

Endapo wabunge wataona kuwa suala la Meremeta halitishii Usalama wa Taifa na hakuna jambo lolote ambalo linahatarisha usalama huo isipokuwa linaweza kuaibisha na kuumbua watu wachache basi habari hizo ziwekwe hadharani kwa kila mwananchi kuona.

Kama Bw. Pinda hayuko tayari kufanya hivyo, basi na yeye aamue kujiuzulu maramoja kwani ameamua kwa makusudi kabisa kuwaficha wananchi habari kuhusu Taifa lao na mojawapo ya chombo chao muhimu na kwa maneno yake mwenyewe ameamua kuwazuga Watanzania. Hili halikubaliki.

Tumedanganywa kiasi cha kutosha,
Tumezugwa kiasi cha kutosha,
Tumeburuzwa kiasi cha kutosha!

Na sasa tunadai haki yetu ya kuheshimiwa na kuthaminiwa kama raia!

Tunataka kutambuliwa kama ndiyo chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Tunataka kuheshimiwa kama ndio waajiri halali wa serikali iliyoko madarakani na ya kuwa wao wanafanya kazi kwa niaba yetu na hakuna jambo lolote wanaloweza kufanya ambalo ni "siri yao" na sisi wananchi au wawakilishi wetu wasijulishwe.

Kama kuna kanuni ya Bunge ambayo inazuia kujadiliwa kwa masuala ya Usalama basi Bunge litengue kanuni hiyo kwani liko ndani ya uwezo wake. Hatukubali tena kuburuzwa kama mkokoteni uliovunjika, na hatuko tayari tena kubebwa mzoba mzomba kama lumbesa!

Kuweni wa kweli sasa kwani saa ya mjaribu inakuja na imefika, siku ya Jumatano ijayo kama nilivyofanya mwaka jana nitaongoza sala ya "baraka na laana" na Mungu aliye mbinguni mwenye kutawala nyakati na nyakati, mmiliki wa nyota na sayari na muumbaji wa muda, kina, umbali na mwendo! na Mfadhili wa uhai wote atasikia. Kwa yeye peke yake najisalimisha na uhai wangu uko mikononi mwake! Kwake yeye peke hofu yangu ipo na kwa mwanadamu awaye yote sitomhofia na simhofu yeyote mwenye kuudhuru mwili na asiiguse roho yangu! Jumatano, mbingu zitafunguka na sauti itasikika ya kwamba "mafisadi mmekwisha"! Mna siku tano kujisahihisha kuhusu uzugaji huu!

Kila jambo lina wakati wake, muda wao kutuzuga umepita na haurudi tena... huu ni muda wetu! Ni muda wetu kutaka serikali yenye uwazi, ni muda wetu kutaka serikali inayowajibika, na kwa hakika ni muda wetu kutaka viongozi wa kweli siyo wanafurahia kupigiwa saluti na kumulikwa na vimuli muli! Huu ni muda wa Watanzania, na watanzania hatimaye watashinda! Si kwa nguvu, si kwa jeshi, si umwagaji damu, si kwa ngumi.. bali kwa hoja zenye nguvu zibadilishazo fikira za wana na wana wa wana!

Huu ni wakati wetu, wa kwenu umefikia 11:59PM

Nachukulia haya kama amri kutoka JF, kama mtumishi wenu nitasema! Nitahoji! Nitatoa ushahidi kuwa PM hajasema ukweli wote kuhusu Meremeta! Jumatatu
 
Nachukulia haya kama amri kutoka JF, kama mtumishi wenu nitasema! Nitahoji! Nitatoa ushahidi kuwa PM hajasema ukweli wote kuhusu Meremeta! Jumatatu

Shukrani bwana Zitto kwa kuona uzito wa suala hili aliloanzisha mwanakijiji kwamba linahitaji kuchukuliwa seriously.

Tunaamini uyasemayo, na kwa jinsi tunavyokufahamu upangaji hoja wako ulivyo makini tunategemea spika atakuelewa na kutekeleza inavyotakiwa.

Asante sana na Mungu akubariki milele. Tuko pamoja nawe.
 
Nachukulia haya kama amri kutoka JF, kama mtumishi wenu nitasema! Nitahoji! Nitatoa ushahidi kuwa PM hajasema ukweli wote kuhusu Meremeta! Jumatatu

Hivi hata PM akilidanganya bunge inatakiwa achukuliwe hatua zipi? Lakini nafikiri cha maana ajiuzulu tu.
 
Go on Zitto.. this is the right moment for the truth.
Wengine tayari tumeanza novena na mafungo kwa ajili ya taifa letu lililopo katika hatari ya kuangamizwa na mafisadi.
 
Go on Zitto.. this is the right moment for the truth.
Wengine tayari tumeanza novena na mafungo kwa ajili ya taifa letu lililopo katika hatari ya kuangamizwa na mafisadi.

Kama Pinda akiwa succesfull kwenye issue ya Meremeta what do you expect him to say kwenye issue ya KIWIRA na Mkapa? We should stop this nonsense now. To him, this is like litmus test ... maana akifanikiwa kwenye hili ndio ataona kwamba "Yote Yanawezekana" na ataendeleza kauli mbiu zake kutetea ufisadi wa aina zote ambao utapitia kwenye anga zake.

Tusikubali kulelea tabia za aina hii kwani akiwa sugu itakua ni vigumu kumrekebisha. "Samaki hupindwa akiwa mbichi". This is the right time kumpinda ndugu Pinda. He deserve to go...
 
Shukrani bwana Zitto kwa kuona uzito wa suala hili aliloanzisha mwanakijiji kwamba linahitaji kuchukuliwa seriously.

Tunaamini uyasemayo, na kwa jinsi tunavyokufahamu upangaji hoja wako ulivyo makini tunategemea spika atakuelewa na kutekeleza inavyotakiwa.

Asante sana na Mungu akubariki milele. Tuko pamoja nawe.

Kanuni zitatumika ipasavyo.......... niachie!
 
kuna wakati ambapo mistari tuliyoichora isikubali kuvukwa. Si na Kikwete, si na Pinda wala si na mtu yeyote yule. Kuheshimu wananchi unaowatawala ni mstari ambao hauvukwi na mtu yeyote yule. Kitendo cha Pinda na serikali kutuzungusha kuhusu Meremeta ni dharau ya hali ya juu kwa taifa letu, na hili hatuwezi kuwakubalia.

Hivi ninyi ni mabingwa wa kusahau???
mnakumbuka wakati jina lake limepelekwa bungeni mara ya kwanza ili awe waziri mkuu wabunge walipata nafasi ya kuchangia?? Kuna mbunge mmoja wa monduli alisimama akasema HUYU JAMAA NI KAMA MIMI.... na akaendelea kumwagia misifa mpaka nikahisi luninga yangu inanuka shombo....

Basi mwenye sikio na aone na mwenye macho asikie kwani nchi hii imejaa miujiza kila kukicha. Kuna siku bakora zitajishusha zenyewe ktk matawi ya miti na kuanza kuwacharaza hawa walumendago
 
Last edited:
Back
Top Bottom