Ofisi ya Mfamasia Mkuu inawanyanyasa sana wamiliki wa Maduka ya Dawa Nchini

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Ndugu zangu kuna hili janga linalowakumba wamiliki wa Maduka ya Dawa Nchini, kuna ukiritimba na unyanyasaji wa hali ya juu kwa Wafanyabiashara za Dawa! Hawa watu wanafanya biashara kama wakimbizi, ukaguzi kila siku kwa nia ya kujipatia rushwa!

Madawa yote hata yale ya kawaida ambayo tulizoea kuyakuta madukani kwa sasa yamepigwa marufuku, wanaoruhusiwa kuuza ni wamiliki wa Pharmacy kubwa tu.

Mfano dawa kama Erythromacn, Ciproxacin, Flaggy, dawa za Malaria aina zote, Doxaclin, Muvera Plus, na nyingine kibao kwa sasa haziruhusiwi kuuzwa madukani mpaka uitafute pharmacy iliko.

Kwa sisi ambao tunaishi vijijini haya maduka ndio salama yetu, pharmacy tutazikuta wapi? Ukienda hospitali hupewi dawa unaambiwa kanunue, ukienda kununua tumekatazwa kuuza dawa zote za Antibiotic.

Akina mama wanakimbizana na wakaguzi kama Traffic wa barabarani na madereva, ukaguzi umekuwa wa holela na hongo imetawala hasa mikoani kila wiki ni ukaguzi.

Ofisi ya Mfamasia Mkuu iache kunyanyasa Wafanyabiashara kwa maslahi binafsi, mnawalinda mapapa na kutafuna vidagaa, Waziri wa Afya, Waziri Ummy unataka maduka ya dawa tuuze maandazi?

Nilichogundua hapo ni Wamiliki wa pharmacy kulindwa na sio usalama wa watumiaji, pili hizo ndio dawa zinazohitajika kila siku ni watumiaji wa kawaida kwa sasa mmiliki wa Duka la Dawa hana dawa za kuuza maana zote zimepigwa marufuku.
 
Kwani lazima uzianike kwenye shelfu mkuu ? Tia hata darini wakija wakute pritoni tu.
 
Si majuzi tumeambiwa hao Famasia wameondolewa sifa ya kusimamia hayo maduka ya Dawa badala yake kazi wamepewa TMDA. Sasa labda twambie aliyeleta hayo masharti ni huyu msimamizi mpya TMDA au yule wa Zamani?
Lakini maelezo yalikuwa wazi kwamba ugumu wa kupata dawa ulizotaja umewekwa ili kupunguza Usugu wa Virusi maaana kwa maelezo yao hizo dawa inapaswa zitoke kwa cheti cha Daktari sio wewe ukiskia mkojo unauma unakimbia dukani kubeba Doxy mbili tatu unameza. Hiii ndio sababu wamepiga kufuri ili kunusuru afya yako mkuu.
 
Kimsingi hayo maduka AKA DLDM yalitakiwa yasiwepo kabisa !!! Kutoka Maduka ya Dawa Baridi kwenda DLDM hakuna cha maana kilichoonekana katika kumlinda mlengwa. Serikali ijikite katika kuongeza na kuimarisha huduma za msingi kwa ngazi ya Zahanati na Vituo vya Afya (na hata Hospitali) ili kuendana na ukuaji wa mahitaji.
 
Ndugu zangu kuna hili janga linalowakumba wamiliki wa maduka ya dawa nchini, kuna ukiritimba na unyanyasaji wa hali ya juu kwa wafanyabiashara za dawa! Hawa watu wanafanya biashara kama wakimbizi, ukaguzi kila siku kwa nia ya kujipatia rushwa!

Madawa yote hata yale ya kawaida ambayo tulizoea kuyakuta madukani kwa sasa yamepigwa marufuku, wanaoruhusiwa kuuza ni wamiliki wa pharmacy kubwa tu.

Mfano dawa kama Erythromacn, Ciproxacin, Flagyl, dawa za Malaria aina zote, Doxaclin, Muvera Plus, na nyingine kibao kwa sasa haziruhusiwi kuuzwa madukani mpaka uitafute pharmacy iliko.

Kwa sisi ambao tunaishi vijijini haya maduka ndio salama yetu, phamarcy tutazikuta wapi? Ukienda hospital hupewi dawa unaambiwa kanunue, ukienda kununua tumekatazwa kuuza dawa zote za Antibiotic.

Nilichogundua hapo ni wamiliki wa pharmacy kulindwa na sio usalama wa watumiaji, pili hizo ndio dawa zinazohitajika kila siku ni watumiaji wa kawaida kwa sasa mmiliki wa duka la dawa hana dawa za kuuza maana zote zimepigwa marufuku.

Akina mama wanakimbizana na wakaguzi kama traffic wa barabarani na madereva, ukaguzi umekuwa wa holela na hongo imetawala hasa mikoani kila wiki ni ukaguzi.

Ofisi ya Mfamasia Mkuu iache kunyanyasa wafanyabiashara kwa maslahi binafsi, mnawalinda mapapa na kutafuna vidagaa, Waziri Ummy unataka maduka ya dawa tuuze maandazi?
Peleka haya malalamiko yako kwa Eliza shakalage na Mitango Fimbo
 
Madawa yote hata yale ya kawaida ambayo tulizoea kuyakuta madukani kwa sasa yamepigwa marufuku, wanaoruhusiwa kuuza ni wamiliki wa Pharmacy kubwa tu.

Mfano dawa kama Erythromacn, Ciproxacin, Flaggy, dawa za Malaria aina zote, Doxaclin, Muvera Plus, na nyingine kibao kwa sasa haziruhusiwi kuuzwa madukani mpaka uitafute pharmacy iliko.
Ipo sababu ya kufanya baraza la famasi likishirikiana na TMDA kuweka kanuni na sheria zinazotaka dawa kubwakubwa ziuzwe famasi tu.

Katika pharmacy kuna mfamasia pamoja na mteknolojia wa dawa, au zamani fundi sanifu wa dawa na mteknolojia wa dawa msaidizi. Hawa ndio waliofundishwa utaalamu wa kusimamia ugawaji wa dawa 'hatarishi'

Ni tofauti na maduka ya dawa muhimu ambapo masharti yamelegezwa kuhusiana na wataalamu wanaopaswa kuhusika. Ni lazima wawe wa afya lakini si lazima ku'specialize' kama walioko famasi. Cheti tu kinatosha.

Dawa hazipaswi kugawiwa kimazoea kama ulivyotamka.

Na kuthibitisha pointi yangu nitafanya marekebisho kiasi tu katika majina ya dawa uliyoandika;

Ciproxacin - Usahihi ni ciprofloxacin 500mg ni dawa ambayo haifai kutolewa kwa watoto ambao hawajakamilika kubalehe, kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza katika mishipa/kamba inayoshikilia misuli na mifupa yaani 'tendoni'. Dawa hii inaweza kupelekea kufunga kwa ukuaji mifupa kulikowahishwa hivyo kuathiri umbile na afya ya mtoto kiujumla. Tahadhari ichukuliwe kutofanya kazi jua kali sana. Na apate chakula cha kutosha anapoitumia dawa hii. Dawa hii inapaswa kutolewa na daktari na haitolewi kwa wenye umri mdogo isipokuwa kwa sababu maalumu ambapo hatari haijaizidi faida. Sasa maelezo yote haya kwa asiyesomea madawa kikamilifu anayafahamu?
Flaggy - Kiusahihi ni flagyl au kikamilifu kabisa ni metronidazole 200mg. Dawa hii ikitolewa kiholela bila tahadhari ya kutochanganya na kilevi huweza kuleta hali mbaya kabisa ya 'disulfiram reaction' ni hatari.
Doxaclin - Kiusahihi dawa hii inaitwa doxycycline 100mg, ni dawa jamii ya tetracycline, haiwafai wajawazito(inaweza kusababisha madhara kwa mimba), haiwafai watoto, haiwafai ambao mifupa yao bado inakua. Huharibu uimara na rangi mifupa ikuayo, mfano meno kuwa na rangi isiyokwisha maisha yake yote. Nayo ni dawa yenye nguvu inayohitaji lishe
Muvera Plus - Sawa na kikamilifu inaitwa meloxicam 15/7.5mg dawa ya maumivu hasa ya kudumu ya mwili, mgongo, mifupa etc. Inapaswa kutolewa pale ambapo mgonjwa atahitaji hiyo lakini sio kwa vimaumivu vya kawaida vya kichwa na tumbo.

Kwa dawa za malaria na Erythromacin - (Usahihi ni erythromycin) zenyewe ziko na usalama zaidi sina hakika kuhusu sababu za kuchukuliwa kuwa sio 'dawa baridi' .

Lakini serikali inaweza kuwa imeweka sera ili kudhibiti usugu wa vimelea kwa madawa. Na zaidi kwa dawa za malaria huwa na sera mbalimbali mfano;
Kuna dawa ni kwa ajili ya kingatiba kwa wajawazito tu (IPT) hizi ni kundi la SP.

Lakini pia inawezekana dozi ya dawa mseto ikachanganya watoa huduma. Inaanza na masaa nane kisha kila baada ya masaa 12.

Na la mwisho labda ni kuzuia tabia ya kila mgonjwa kupewa dawa za malaria kwa kila homa bila ya kupima

Cha kumalizia tu ni kwamba dawa hazipaswi kuendelea kutolewa kwa mazoea. Ni lazima tujali afya za walaji na kuzingatia elimu na sayansi ya kisasa zaidi 'up-to-date evidence based practice' na wataalamu wenye ujuzi huo. Ahsante
 
Back
Top Bottom