DOKEZO Mabucha ya Nyama Kanda ya Ziwa yachunguzwe kuhusu dawa wanazopuliza buchani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na viashiria vya wauzaji wa nyama wengi mkoani Kagera hususani Manispaa ya Bukoba kutumia dawa mbalimbali kupulizia nyama ili kuepusha nzi wasisogelee pamoja na nyama kutoharibika haraka.

Hali hiyo Ilianzia kwenye mabucha kadhaa siku za nyuma kidogo lakini kwa sasa sehemu nyingi zinaonekana kutumia utaratibu huo na imekuwa kama ni mazoea.

Kuna jamaa zangu ambao wana bucha nilijaribu kutumia mbinu zangu ninazozijua kutaka kujua wanaepukaje nzi na nyama kutokuwa na harufu ya kuoza kwa haraka, wadai kuna dawa wamekuwa wakizitumia kupuliza nyama (sitozitaja dawa hizo kwa sasa).

Dawa hizo zinadaiwa kusaidia kuepusha nzi na kufanya nyama kukauka na kukaa siku nyingi buchani, ambapo leo hii ikitokea mtu akaenda kwenye bucha za Rwamishenye, Kashai, Amgembe na maeneo mengine hali ni ileile.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakinong’ona chinichini juu ya nyama siku hizi kukosa ladha, katika ufatiliaji wangu madai hayo yana ukweli na dawa hizo uenda ni kati ya visababishi vikuu ambapo Wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mbinu hiyo kujinufaisha kimaslahi bila kuzingatia umuhimu wa afya za watumiaji.

Jamaa wengi nilioongea nao walinitonya wazi kuwa jambo hilo linafanyika kwenye maeneo mengi ya Kanda ya Ziwa hususani maeneo ya miji ikiwemo Jijini Mwanza.

Nashauri mamlaka za juu zifuatilie kwa kina jambo hili kwa lengo la kubaini watu wanaojihusisha vitendo hivyo wachukuliwe hatu sambamba na kubaini athari za dawa hizo kwa watumiaji ili uwajibikaji uwepo.

Inavyoonekana uenda mamlaka za ndani ya Manispaa au Halmashauri husika ambapo jambo hilo linadaiwa kutendeka wamekosa nguvu ya kulithibi suala hilo, nasema hivi kwa kuwa wauzaji wa nyama wengi wanakuwa na vibali vinavyohitajika unajiuliza wanavipataje wakati kuna mchezo mchafu wanaucheza.

Tunaweza kukumbuka Mwaka 2021 Bodi ya Nyama ilitangaza kupiga marufuku matumizi dawa ya kuua nzi na kuua wadudu wengine zilizodaiwa kupulizwa kwenye mabucha wakati nyama ikiwemo ndani.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa wa Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kurwa alisema kuwa baadhi ya mabucha ya nyama wamekuwa wakitumia dawa za kuua nzi wakati nyama ikiwemo ndani ya bucha jambo ambalo alidai kuwa ni hatari kwa afya ya watumiaji wa nyama hiyo.

Uenda hali hiyo isipotafutiwa tiba kwa sasa mbeleni yanaweza kutokea madhara makubwa ambayo tutabakia kunyoosheana vidole na kutumia nguvu na rasilimali kubwa kutafuta suluhu kuliko uwajibikaji unaoweza kuwepo kwa sasa japokuwa tumechelewa kwa kiwango fulani.

MICHEZO YA KUUZA DAWA ZA KUPULIZIA
Utafiti wangu umeonesha kuwa mara nyingi dawa hizo wanazipata kutoka kwa Maafisa walipewa jukumu na wanaosimamia zoezi la usambazaji dawa nchini.

Maafisa hao hawakuuzii dawa kama hawakujui au kama hauna connection ya mtu wao, lazima uwe kwenye 'system' yao, hii inafanyika kwa siri na Wamiliki au wauzaji wa bucha hawatakiwi kusema popote.

Pia wanaojua kuhusu hilo ni baadhi ya maafisa wa hospitali hasa Madaktari wachache mbao wanahusika na uuzaji wa dawa hizo inapotokea zimefikishwa kwenye vituo vyao kwa ajili ya matumizi mengine ya kitabibu.
 
Ndio maana huwa nashangaa unapita mahala butcher ilipo na unaona katundika utumbo nje lakn hamna inzi hata mmoja anaeonekana kutua pale tena syo mara moja tofauti na zamani kidogo hali haikuwa hivyo
 
Sasa hizo.dawa hata ukificha wakati shule za kata zimetudaidia kusoma biology na tumefanya mtihani wa paper 2?
 
Mwanzo ilikuwa wanatumia formaline ikapigwa marufuku sasa hivi sijui wamekuja na gia gani.
 
Back
Top Bottom