Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, kuwasaka Wavuta Shisha kila sehemu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), imetangaza kuanza operesheni maalumu katika kumbi za starehe na mahoteli zenye shisha ili kubaini wanaochanganya kiburudisho hicho na dawa za kulevya.

Taarifa ya operesheni hiyo imetolewa leo, Alhamisi Januari 25, 2024 na Kamishna Mkuu wa DCEA, Aretas Lyimo alipozungumza na waandishi wa habari.

Amesema watatembelea katika kumbi hizo na kupima mitungi kubaini kama kuna mchanganyiko na dawa za kulevya.

"Tutatembelea kumbi hizo tutapima mitungi ya shisha ili kubaini kama kuna uchanganyaji na dawa za kulevya na tukigundua tunawakamata wahusika," amesema. Amesema operesheni hiyo itahusisha ufuatiliaji wa matumizi na uzalishaji wa dawa za kulevya nchi kavu na majini.

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

TAARIFA KWA UMMA

UKAMATAJI WA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA AINA YA COCAINE


Dar es Salaam, 25 Januari, 2024
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imefanikiwa kumkamata kinara
wa mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina cocaine nchini pamoja na kukamata jumla ya gramu 692.336 za cocaine zinazowahusisha watuhumiwa wanne (4), katika operasheni maalum zinazoendelea Nchini.

Mfanyabishara huyo wa mtandao wa cocaine ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu
alikamatwa katika eneo la Boko wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na washirika wake watatu ambapo kati yao wawili walikamatwa jijini Dar es Salaam na mmoja alikamatwa katika kijiji cha Shamwengo wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani Mbeya.

Pia, Mamlaka imebaini kuwa, wafanyabiashara wa matandao wa cocaine wamekuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia watu ambao humeza dawa hizo tumboni au kuweka kwenye maungo mengine ya mwili. Mfanyabiashara aliyekamatwa ana mtandao mkubwa wa wabebaji (punda) kutoka nchi mbalimbali ambao huwatumia kusafirisha dawa hizo kwa njia ya kumeza.

Hivyo, makosa yake yanaangukia katika uhalifu wa kupangwa unaovuka mipaka.

Dawa ya kulevya aina ya cocaine ni dawa inayozalishwa kutoka kwenye mmea wa Coca unaojulikana kitaalam kama Erythroxylum coca (coca Plant) ambao hulimwa zaidi
katika nchi za Bolivia, Peru, na Colombia zilizopo Amerika ya Kusini. Dawa hii ipo katika kundi la vichangamshi kama zilivyo dawa za kulevya aina ya amphetamine,
methamphetamine na mirungi.

Wabebaji wa dawa hizi huzimeza zikiwa katika mfumo wa pipi ambapo mtu mmoja huweza kubeba kuanzia gramu 300 hadi gramu 2000 kwa wakati mmoja.

Dawa hii ni hatari kwa afya ya mtumiaji, kwani huathiri utendaji wa mfumo wa fahamu, husababisha kukosa usingizi, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, kiharusi na vifo vya ghafla.

Aidha cocaine huweza kusababisha matatizo ya afya ya akili na husababisha hasira, ukatili, vurugu, kukosa utulivu na hata mtumiaji kutaka kujiua. Dawa hii
husababisha uraibu wa haraka na utegemezi na hivyo, kuwa vigumu kwa mtumiaji kuiacha.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya itafanya operesheni kali za
nchi kavu na baharini kwa mwaka huu 2024. Operasheni za nchi kavu zitahusisha mashamba ya dawa za kulevya, kwenye mipaka, maeneo ya mijini kwenye vijiwe vya
usambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya.

Kwa upande na baharini, operesheni zitahusisha fukwe na katikati ya bahari. Aidha operasheni hizo zitahusisha maeneo yote wanayouza shisha ili kubaini matumizi ya dawa za kulevya ambapo wale wote watakaobainika kutumia dawa za kulevya kupitia shisha watachukuliwa hatua kali za kisheria. Vilevile, operasheni hii itahusisha wauzaji wanaokiuka taratibu za uuzaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya na kemikali bashirifu.

Aidha, Mamlaka inatoa onyo kwa wote watakaoendelea kujihusisha na uzalishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini kuacha kwani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuiwezesha Mamlaka kwa kununua vifaa vya kisasa na mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka na hivyo kuwajengea ujasiri na weledi katika kutekeleza operasheni kwa ufanisi mkubwa.

Hivyo, kwa wale wote watakaoendelea na kilimo cha bangi, mirungi na biashara
ya dawa za kulevya za viwandani watashughuliwa ipasavyo.

Mamlaka inawaomba wananchi kuendelea kutoa kutoa taarifa za watu wote wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa salama kwa kupiga simu kwenye namba ya bure 119 na taarifa zitapokelewa kwa usiri mkubwa na kufanyiwa kazi.

Imetolewa na,

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini, imemkamata kigogo wa biashara za dawa za kulevya alyekuwa anatafutwa kwa miaka 23 na kumkuta akiwa na kokeini zenye uzito wa gramu 692.336 na alikuwa anasafirisha dawa kutoka America ya Kusini kwenda nchi mbalimbali kupitia vijana wa kike na kiume.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo wakati anaongea na waandishi wa habari Leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa madawa hayo yalikuwa yanasafirishwa kwa njia ya kumezwa tumboni.

“Mfanyabiashara huyo alikamatwa eneo la Boko huku washirika wake watatu, wawili wamekamatwa Dar es Salaam na mmoja mkoa wa Mbeya na madawa haya walikuwa wanasafirisha kupitia vijana maarufu kwa jina la Punda ambapo walikuwa wanawamezesha tumboni na uwezo wa mtu mmoja kumeza ni pipi gramu 300 mpaka 1000, kwa mwanamke mwenye tumbo kubwa ana uwezo wa kumeza mpaka gramu 2000," amesema kamishna.

#EastAfricaTV
 
Hao wameshindwa kazi, kwahiyo wameanza kuhangaika na watumiaji?
 
Back
Top Bottom