Ofisi ya "directorate of post graduate studies udsm" kuna nini?????

Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,238
324
Wadau kuna tatizo gani ndani ya hiyo ofisi, hasa sehemu ambako transcripts zinatolewa! Kumekwepo na urasimu usiokuwa na maana sana kwa hawa wahusika: Wako wadada watatu (3), na hawako makini sana kwani wanapochapisha transcripts kuna makosa ya kizembe sana-inaonekana hawafanyi proof reading wao ni kufyatua makaratasi tu, mbaya zaidi: Pale ambapo makosa yao wenyewe wanayageuza kuwa adhabu kwako mteja- maake utaambiwa njoo baada ya wiki tatu, pia wanasahau kuwa kuna watu wanatoka mikoani kwenda kufatilia transcripts-lakini bado utaingizwa kwenye urasimu wa ajabu. Inasikitisha sana mtu unapofatilia transcrip kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi!
Wahusika watambue kuwa ofisi hii hapo udsm inachafua sura ya chuo hasa wakati huu tunapohadhimisha miaka 50 toka chuo kianze! Tunaomba wahusika wajirekebishe na kutoa huduma hii kwa wakati!
Kwani usumbufu huu unatukosesha amani ktk maeneo yetu ya kazi-pale mwajiri anapotaka uthibitisho kuwa umegraduate na aone matokeo yako! Mnaboa sana!
 
mkuu hiyo case hata tumaini iringa ni hivyo hivyo! Sijui wanakuwaje hawa watu! Au wanataka rushwa???!
 
ingekuwa vzuri kama wangepewa habari hii live manake nahofia ujembe wako huu mzito hautafikia walengwa
 
ni kweli kabisa nafikiri muda mwingine tunawapa kidogo, lakini hao watu wanachonga hata Konda haoni ndani eti!:dance::dance:
 
... Wako wadada watatu (3), na hawako makini sana kwani wanapochapisha transcripts kuna makosa ya kizembe sana-inaonekana hawafanyi proof reading wao ni kufyatua makaratasi tu,

Mimi transcipt yangu niliwarudishia mara tatu warudie kuchapisha kutokana na makosa yao, na nikawaambia waziwazi kwamba wasipojirekebisha nitawaripoti kwa DVC Academic. Niliwaambia wanipishe mezani nichapishe mwenyewe, wakakataa. Hata hiyo ya nne ikatoka na makosa, ila nikaamua niichukue tu. Sasa kama hawajajirekebisha nitajitolea kwenda kuwaonyesha thread hii, naombeni wote mlioathirika muandike hapa ili niende na ushahidi wa kutosha, wasije wakasema ni chuki zangu binafsi. Wanakiaibisha chuo sana wale, hata format ya transcipt ni mbaya kwa mtu wa hadhi ya postgraduate.
 
sio tu post graduate hata under graduate ni tabu vile vile,
mi sikusumbuka sana ila pale pia pana rushwa wakati wewe unaambiwa njoo baada
ya 7 days hv km sikosei wakati mwingine anakuja asbh anatoa buku 10 kwa wale wadada pale
ground floor mchana anachukua copy yake......panakera sana
 
nakubaliana sana bwana SINKALA- kwa kweli hiyo hali inakera sana wafunge kengele!
 
Back
Top Bottom