nywele

Tafuta mafuta ya T444 check website yao .. mafuta mazuri sana tu .. kopo ni Tshs 40,000/-

ila kakopo ni kadogo kweli kweli kulingana na thamani ya pesa yenyewe. Ili upate matokeo mazuri yakupasa kutumia si chini ya miezi 6 na kuendelea. Sukia weaving ila make sure msusi hazikamati za usoni, ili aziache zikue kwanza.
 
usipende kuretouch kila baada ya week 6.....dawa za siku hizi zinakata sana nywele.....hakikisha nywele zako zinapata growth ya kutosha then ndio uretouch.....na huyo anayekuretouch awe makini sana kuretouch growth tu....kukushauri tafuta Venus Relaxer regular ya kwenye box inaweza kukusaidia
 
kama ulishaamua hapana usingeweka kwenye post yako.....uamuzi ni wako kwa kuwa pia kichwa ni chako sisi tunakushauri hatukuambii fanya hivi!!
yamekuwa hayo jmn bac sorry, me naomba tuu ushauri, suala la kunyoa labda ni uamuzi wa mwisho coz cjapenda hili
 
Tafuta full package ya profectiv.
Inauzwa laki na.
Nenda s h amon.
Halafu nasikia tabata kuna madaktari wana vipimo maalum vya nywele.
Sina details zaidi ila kama utahitaji nipm nikutaftie details zaidi kuhusu dokta.
Ushauri mwingine ni kunyoa ingawa ushaukataa ila nywele nazo zina kikomo cha kukua kwahyo bora uanze upya.
 
nyoa afu tafuta mawigi yako mawili mazuri uwe unavaa,zikianza kukua suka za mkono huku unaendelea kuvaa wigi,kama unaogopa kunyoa na kuacha kichwa wazi.
mawigi mazuri nitayapata wapi dada angu? labda nishauri hilo kwanza, coz nikifikiria kunyoa nafikiria na kuacha kichwa waz
 
wifi yangu bana!kaka kakuchunia maana unarukaruka mno ila haachi kukupenda maana ndo kafika hivyo!mie mzima kaa mkao wa wk end,,,,,,hebu assume ikatokea hakuna mawig,weaving,relaxer,au hata rasta za kusuka kitatokea nini kwa wanawake?
hapo itakuwa hakuna kuchekana, tutasuka tuu za mkono
 
Pole sana mpendwa kwa lililokusibu wengi hukutwa na hali kama yako pindi wanaposuka mtindo huo wa kimasai,ila kwasababu umesema hutaki kunyoa japo kuna mitindo mbalimbali ya kunyoa ambayo ungependeza sana ,na hata kama ukinyoa basi unaweza kuvaa wigi kama ulivyopendekeza mwenyewe,kama hutaki kufunga lemba, sijajua upo mkoa gani lakini unapoishi unaweza kupata weaving la gharama utakayomudu endapo utapita kwenye maduka ya urembo/vipodozi.
Na pia unaweza kutumia vitu vya asili kama parachichi,,samli kama steaming pia.
Kingine kuna shampoo nyingi ambazo zinatumika kwenye saloon zipo chini ya viwango na huchangia pia kuharibika kwa nywele hivyo uwe makini na hilo.
Uzuri unao ila tayari umeshajitia kasoro mwenyewe kuwa una kichogo,kichogo si kasoro bali ni jinsi Mungu alivyokuumba
niko dar kwa sasa, mawigi nilinunua ya elfu20 hayakuwa mazuri , labda nitafute mengine ila yasifike laki moja ndio uwezo wangu
 
Tafuta full package ya profectiv.
Inauzwa laki na.
Nenda s h amon.
Halafu nasikia tabata kuna madaktari wana vipimo maalum vya nywele.
Sina details zaidi ila kama utahitaji nipm nikutaftie details zaidi kuhusu dokta.
Ushauri mwingine ni kunyoa ingawa ushaukataa ila nywele nazo zina kikomo cha kukua kwahyo bora uanze upya.
nimekusoma dada angu , nitatembelea hizo dawa s h amon kwanza
 
Pole sana ndugu....

Nahc unasumbuliwa na na maradhi ya fulani ya "unwyemwi" ambayo yanakusababishia Upungufu wa nywele mwilini.

Nakushauri utumie matunda sana mf. Parachichi, Ndizi, na Matango. Pia usisahau kufanya mazoezi hasa asubuhi na jioni.

Kumbuka kuvaa kofia muda wote... pia usiku uwe unapaka asali ya nyuki wakali sana sana wa kutoka Mto wa Mbu..

By... Dr. Mohan L. Ndesamburo
Mawasiliano:
Fika Zahanati ya Kimandoro Clinic Centre
Arusha , Mwanza, Morogoro au DSM mwembechai
 
Sorry nilikuwa napita tu ila nimecheka sana hapo kwenye kisogo. Ungekuwa wakiume hicho kisogo ungekifichaje?
 
Sikushauri utumie sana wig, kwa kuwa ule mpira wa kwenye wig unasababisha nywele za usoni na za nyuma kutokuota kutokana na kubanwa sana na ile eleastic
 
My dear ushari wangu ni suka wevi. .
maana utakuwa unasuka nywele zako binafsi
na zitakuwa haraka
kuliko kuchanganya na rasta ..
usiweke dawa utazikata zaidi acha zijae kwanza..
 
Mie natumia african proud au optimum care..
unaweza kununua kwenye internet..
 
Back
Top Bottom