Dar es Salaam ni kama 'Converter', lazima ikubadilishe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
DAR ES SALAAM NI KAMA CONVERTER LAZIMA IKUBADILISHE

Anaandika, Robert Heriel

Mimi Kule kwetu ukiwatajia Jina Taikon watakuambia hawamjui, ndio ni Kule kwetu Makanya nilipozaliwa Mnyamwezi, Taikon Master, wananijua Kwa Majina na uhusika mwingine kabisaa! Ukiwaletea Mimi Taikon wa Mjini alafu wao wakakuletea Mimi Taikon wa Makanya ni Watu wawili Tofauti.

Nilipofika Dsm Kwa mara ya Kwanza nilikuwa nimefubaa, nimezorota, ngozi yangu ilikuwa nyeusi, nilikuwa na kiharufu cha shamba ambacho ni kawaida kukaa siku mbilitatu bila ya kuoga. Sisemi nilikuwa nanuka. Hasha! Ila sikuwa na harufu ya kunukia, ningejulia wapi kupaka manukato na marashi Mimi, sisemi kwetu kijijini hakuna manukato au Marashi Hasha, Ila Hakukuwa na ulazima wa kufanya hayo yote. Ingawaje kimwonekano na haiba ni kijana barubaru ambaye ni nadra Sana kukataliwa na Warembo waliowengi lakini haifichi ukweli kuwa nilikuwa nimefubaa.

Taikon wa DAR sio Yule wa Kijijini. Amekuwa na rutuba na Hali yangu imetengemaa. Rangi yangu imenawiri. Nimejipa majukumu ya kimjini mpaka wanaonijua wakiniona wananishangaa.

Ukifika Mjini utajijuta unasombwa na upepo wa Mjini, mambo mengi yanabadilika kuendana na Kasi ya michezo ya mjini.

Huku mjini Zuhura atajiita Zuchu
Amina atajiita Minah
Juma atajiita Jux
Jafari atajiita Jeffy
Fatuma atajiita Fetty
Paulina, Prisca, Priscilla na wote wenye Majina yenye Herufi P hujiita P.
Zubeda atajiita Zuu
Muhammad/Mohamed atajiita MOO
Ramadhan atajiita Ramso
Joseph atajiita Jay
Wababa watu wazima huitwa Daddy,

Mimi kabla ya kubadilisha jina langu, nilipitia kipindi kigumu Sana. Mambo yangu yalikuwa hayaendi. Kama unavyojua mambo ya ujana. Vitoto virembo vilikuwa vinanitolea nje, vinapiga KO Kama ya mandonga, AAA! Nikawa najiuliza shida nini. Wakati huo ninaitwa ROBAπŸ˜€πŸ˜€ Kama Abbreviation ya Robert, siku moja nikiwa Maeneo ya Walatozo nikasikia mtu mwenye jina Kama langu akiitwa BOB na mrembo mmoja hivi. Nikasema anhaa! Kumbe!

Basi nikiporudi nyumbani nikawa nahangaika kutafuta jina la kujiita lenye Swagger 😊 nikasema nikizubaa hapa nitabaki kuwa msindikizaji kwenye huu mji, nitabaki kuwamezea mate hizi pisikali wakati hata Mimi nazitaka. Nikasema subiri, lazima nifanye Jambo.

Kimsingi nina Majina matatu Hivi, TAIKON likiwa jina la kazi zangu Ila hata mengine mawili na yakazi maalumu za kimjini mjiniπŸ˜€πŸ˜€.

Wanasema huwezi kuwa Mjini ukawa na jina moja kama Mbwa! AKA ni muhimu Sana Kwa mishemishe za Jijini.

Basi mbinu ya kubadilisha jina ikafanikiwa kunipa matokeo niliyokuwa nayataka. Ikiwa ni pamoja na watoto wakali wakawa hawanipi shida.

Mji ni Converter lazima ukubali kubadilishwa na Kujibadilisha,
Miongoni mwa Religious Figure zilizobadilisha Majina ni pamoja na Ibrahimu aliyekuwa akiitwa Abrahamu, Sarai aliyekuwa akiitwa Sarah,
Israel aliyekuwa akiitwa Yakobo,

Yesu Kristo alipokuwa akifika Mijini mpaka Jerusalem alikuwa anapenda kujiita AKA zaidi kuliko Jina lake halisi, alikuwa ana-swaggars za kimjini mjini, alikuwa anapenda kujiita Simba wa Yuda, Kama vile unavyowaona Wasanii Kama kina Diamond Platinum akijiita Simba, Yesu alikuwa akijiita pia Mwana wa Adamu, Maji ya Uhai Kama vile Baadhi ya watu wakijiita Sukari ya Warembo. Hayo ni Mambo ya Mjini.

Hujajua nazungumzia nini bado? 😊😊
Tuliza akili Yako wee!

Sikuwahu kufikiri siku moja nywele zangu nitapaka Sijui Black, sijui Wave na makorokoro mengine. Niliwaona wapakaji wa hivyo vitu ni washamba au pengine wanamambo ya ajabu Kama sio ya hovyo.

Lakini siku moja isiyo na jina mtazamo wangu ulibadilishwa.
Nilikuwa nimeenda kwenye sherehe moja ya Walamba Asali ya nchi, Huko wenzangu wote walikuwa wamependeza, sio Vijana sio wazee, nywele zao zilikuwa nyeusi zinawakawaka, Mimi pekee ndiye niliyekuwa na kipilipili mule ndani, alafu nywele zangu zilikuwa na Rangi ya ugoro. Kwa kweli hata hamu ya sherehe iliisha nilileta mambo ya Kijijini Mjini, Moto niliuona. Hakuna aliyekuwa na habari na MimiπŸ˜€.

Nilizikimbia Kamera Kama sina akili nzuri, Kwa nini wanichukue Rekodi wakati sikuwa nimependeza, au wanataka nini kwenye kipilipili changu cha Rangi ya ugoro.

Tangu siku hiyo nikasema sitorudia tenaπŸ˜‚. Kesho yake nikajipeleka Saluni moja matata. Huko ndio nilikwisha kabisa, Huduma za Saluni za Mjini sio zakispot spot.

Mimi nilizoea Saluni za Kule kwetu kijini, ambapo nitakuta Vioo viwili au vitatu, picha za mitindo ya kunyoa na kinyozi, lakini huku Dar Ile saluni ilivunja Rekodi.

Kwanza nilipokelewa na Mwanamke Mrembo sijapata kuona Kwa wakati ule mpaka pale rekodi ya urembo wake ilipovunjwa na Mpenzi wangu😊.

Nikakaribishwa, nikaingia hapo Yule Mdada mrembo akaniletea juisi ya Embe, akiwa kavaa Sketi yake Fupi nyeusi iliyokuwa inaning'inia kwenye mapaja yake manene mazito laini yaliyokuwa.

yanawakawaka Kama ngozi ya chatu. Juu alikuwa kavalia kiblauzi kifupi cha Rangi ya Yakuti Samawi kilichokuwa kinapanda na kushuka huku wakati mwingine kikiacha kitovu chake wazi. Taikon taabani muda wowote mtego utamnasa.

Baada ya kupewa juisi Yule Dada akaondoka kuufuta mlango wa ndani, Mimi nikawa namsindikiza Kwa uchu nikiyatazama mashindano ya Matako yake mawili yaliyokuwa yanapimana nguvu na uzito, chini juu, chini juu, juu chini, juu chini. Chini chini, juu juu! Yanagongana kisha yanatikisika tindindindindi! Doooh! Shetani mbaya nilijikuta nageuka Refa wa mapambano Yale mpaka pale Yule Dada alipopotea kwenye mlango na kuniacha nikiachia pumzi nzito mithili ya Bata Dume! Cheki ulivyo tulia Kwa Kupenda Stori πŸ˜‚πŸ˜‚.

Mambo ya Mjini hayo. Nikameza fumba la Juisi ya embe kulainishi koo langu lililokuwa limekauka, hisia zangu zikiwa zimesafiri Maili nyingi na sasa huenda zilikuwa zinakaribia kufika Kasulu, Kigoma mwisho wa Reli.

Yule Dada akarudi akiwa amebeba Kishikwambi, sitaki kukumbuka tembea yake ya madoido ya kumnasa mwanaume yeyote, nikawa namuangalia Kama mtu ambaye sina ujanja. Akafika na Kuketi karibu yangu. Mapigo yangu ya Moyo yalikuwa yakidunda Kwa nguvu sana. Nikawa najizuia asijue akanipa Kishikwambia akiwa tayari kanifungulia picha nyingi za style ya kunyoa na gharama zake, kisha akaondoka. Akaniambia baada ya dakika tano zamu yangu ya kunyoa itakuwa imefika hivyo nijiandae.

Nikamsindikiza Kwa macho tena, raundi hii alitembea Kwa haraka Hali iliyofanya matako yake yatikisike maradufu, Doooh! Iiiiih!ni Kama alikuwa akitaka kuichomoa roho yangu. Alafu alipofika mlangoni akanigeukia paap! Almanusuru niangushe kishikwambi cha watu. Aisee! Taikon Kwisha! Akatabasamu kisha akazama ndani.

Kumbe ndio maana! Anhaa! Sasa nimejua! Vijana wakifika mjini hawataki Kurudi vijijini kulima, kumbe ndio maana! Oooh! Okay! Now I know! Kama mambo yenyewe ndio haya Taikon atarudi kweli Makanya, lakini Mimi lazima nirudi. Wengine mpaka warudishwe na Machela au Jeneza Kabisa.

Mjini kuna mambo mengi yanayovuta macho, yanayoweza kukupumbaza mpaka ukasahau ulipotoka, mjini yahitaji utulivu wa Hali ya juu Sana.
Mji ni converter inabadilisha tabia za watu.

Muda wa kunyolewa ukafika, Yule Dada akaniita akiwa mlangoni. Nikamfuata, nikaingia katika Ukumbi uliokuwa na viti vinne vya saluni. Kwa kweli Mule ndani kulikuwa kuzuri Sana. Kulikuwa kunavutia Sana. Fundi aliyepadizaini alistahili kulipwa vizuri Kwa kazi yake. Rangi pamoja na mpangilio wa mule ndani iliyafanya macho yangu yajawe na uhondo.

Walikuwepo watu watatu waliokuwa wananyolewa. Kiti kimoja hakikuwa na mtu, Yule Dada mrembo akanikaribisha kwenye Kile kiti kisichokuwa na mtu. Nikakaa. Kisha akanivalisha Ile Aproni na kunifunika kotekote huku akiacha sehemu ya kichwa changu nje. Muda wote nilikuwa namtazama kwenye Kioo jinsi alivyokuwa ananihudumia Kwa upendo wa Hali ya juu. Alikuwa yupo serious na kazi yake, Kwa harakaharaka nilimuona Mdada anayeipenda kazi yake hiyo.

Akaniuliza mtindo gani niliochagua nikamuambia namba ya mtindo. Kisha akaondoka.

Nikashusha pumzi, na kabla sijavuta pumzi nyingine akatokea kijana mmoja akaja, tukasalimiana, kisha akachukua vifaa vya kunyolea akaninyoa. Alipomaliza kuninyoa, akaviweka vile vifaa alivyotumia kuninyolea kwenye kifaa Fulani cha kiteknolojia kisha akaniambia nisubiri dakika moja alafu akaondoka, nikawa najitazama nilivyokuwa nimependeza. Kwa kweli alininyoa vizuri Sana.

Alikuwa kaniwekea kokoto/black kisha baada ya dakika moja yuleyule Dada mrembo akarudi akiwa amestaajabu kuniona vile nilivyokuwa nimebadilika.

Akaniambia umependeza, nikawa Kama nababaika Kama mtu niliyekuwa siamini nilichokuwa nimekisikia. Akawa anacheka, huku tukitazamana kwenye Kilo kikubwa. Akanivua Ile Apron ya saluni kisha akaniambia nimfuate. Hapo akawa mbele yangu Mimi nyuma yake.

Kwa kweli niseme wazi nilihisi degedege inataka kunipata, umbo la Yule Dada mrembo WA saluni lilinishinda uvumilivu wangu. Nilitamani nilishike lakini nikajionya. Msinione Taikon ninatabia mbaya, Mimi nimeamua tuu kuwasimulia ilivyokuwa.

Au Kama sivyo Mimi naacha kusimulia maana naona mnaanza kunisengenya kimoyomoyo. Ooh! Huyu jamaa mroho Sana! Mara ooh! Anatutia aibu anasimulia mambo yake ya SiriπŸ˜€. Sasa Mimi nifanyaje. Mimi nasimulia Washikaji zangu. Lakini naona mshaanza kujifanya Watakatifu. Siendelei sasa.

Mjini kunabadilisha sio tuu majina Bali hata miondoko ya kutembea. Kuna Miondoko ya mjini na miondoko ya vijijini. Mjini lazima utembee Kwa Swagger, utafune na umeze chakula au maji Kwa swagger, Ucheke na kuongea Kwa Swagger, mjini kuna namna yake ya kutabasamu na kuchezesha Sura wakati wa mazungumzo.

Mambo ya Mjini yangenishinda lakini nikikumbuka Jembe la kijijini wengi wetu tunaona Bora tukomae hukuhuku.

Basi Bhana! Yule Dada mrembo akaniambia nikae kwenye kiti ambacho juu yake kulikuwa na kitu mfano wa Dryer Yale ya wanawake. Nilipoketi akaingiza Ile Dryer kwenye kichwa changu, kisha akabonyeza bonyeza muda huo kichwa changu kikiwa kimevalishwa Dryer mfano wa Helmet ya pikipiki. Alafu akaondoka.

Ilikuwa ni mashine ya kukaushia Ile Black/kokoto niliyokuwa nimepakwa kichwani. Nikaanza kusikia Moto ukipenya kwenye ngozi ya kichwa changu. Kisha baada ya dakika Kama Saba hivi Yule Dada Mrembo akarudi. Akatoa ile Dryer kisha akanipa Pole, akanichukua mpaka Chumba kingine kisha akagonga mlango. Hapo mlango ukafunguliwa na Mdada mwingine ambaye huyu sasa ndiye alinichanganya kabisa.

Nikazama ndani, kisha nikaamrishwa niingie chumba cha pili kilichodizainiwa na mapazia kwaajili ya kubadilisha nguo, nikabadilisha nguo nikarudi nikiwa nimevaa Taulo kiunoni nikiwa kifua wazi. Muda huo Yule Dada mrembo WA awali alikuwa ameshaondoka, nimebaki na Dada mrembo mpya ambaye alikuwa kavaa Kwa namna ya ajabu yenye kutamanisha Mno. Nilishindwa kuelewa nipo Dar au nipo wapi, nilikuwa kwenye Chumba cha kubadilisha akili, tabia na muonekano niwe wa kimjini mjini.

Baada ya kulala kwenye kile kiti, Yule Dada mrembo bila ya kuongea chochote akanipaka Mafuta Fulani kichwani kisha akachanganya na Mafuta mengi Kama sabuni hivi. Kisha akasugua kichwa changu mpaka alipoona inafaa, akachukua maji ya Moto kiasi akaosha kichwa changu, kisha akaja usoni hapo akawa anaushika USO Kama tabibu wa Misuli ya USO. Nilikuwa nasikia Raha Sana. Nikiwa nimefumba macho nilianza kuona mafaili ya kijijini yakifutika moja baada ya jingine. Ingawaje kuna mafaili yalikuwa magumu kufutika na yaliandika Unsupported files check the administrator".

Yule Dada akaendelea kuufanyia USO wangu Skrabu mpaka pale aliporidhika. Baada ya kuukausha na kuupaka Mafuta USO wangu akaniamuru nilalie tumbo, kisha akahamia kwenye mgongo.

Mgongo kufuga uchafu ubongoni. Sijui alikuwa anamaanisha nini. Kwamba ubongo wangu ulikuwa na virus hivyo lazima aviondoe. Ilikuwa kisanga sitaki kukumbuka. Yale mafaili yote yaliyokuwa yanaandika unsupported file raundi hii hatakufua dafu, yote yalifutwa. Kumbe Administrator Yule kwenye mgongo huko wanasema ilipo Spinal cord.
Mimi ningejuaje sasa mambo hayo.

Kihisia nilikuwa mbali, akili zikiwa zimesafishwa zote sikubaki hata na akili moja mwenyewe akasema mpaka ani-Restore na afanye Backup baadhi ya mafaili.
Nilitamani kumwambia chochote tuu lakini sikujua nitumie lugha gani.

Lugha ya mjini sio Sawa na Lugha ya Kule kwetu Makanya.
Wakati nakuja mjini nilikuwa naulimi mzito Sana, lakini tangu nifike saluni
Ile ulimi wangu ni laini na mwepesi. Maneno yananitoka Kama MC wa Harusi.
Mji ni Converter inayobadilisha watu.

Zipo converter kuu zilizopo Mjini
1. Club, Pub, Casino Converters.
2. PDF converters
Mjini kuna vijarida, vijitabu na magazeti ya udaku yaliyokafika mfumo wa maandishi au picha yanayobadilisha watu tabia.
3. Saluni Converters
Hapa kuna saluni za kike na saluni za kiume.

4. Madhabahu Converters
Mjini ndio sehemu pekee ambayo Kuna makanisa mengi ambayo hubadilisha baadhi ya watu tabia hasahasa Wanawake aidha wawe jeuri au maamuma au wawe watu Bora.

5. Fasheni Converters
Mavazi, urembo, simu ni moja ya converters kuu zinazobadilisha watu.

6. Car Converters
Magari ni sehemu ya converters muhimu Kwa watu wengi hasa wanawake. Mwanamke anaweza akakubadilikia kisa kapata mwanaume mwenye Gari.

7. Vikoba Converters
Mtu wawatu kabla hajajiingiza kwenye vikoba alikuwa mtu mzuri kabisa lakini alipoingia kwenye Vikoba akaanza kuwa mtu wa Madeni, kudanga, n.k

8. Media Converters
Mitandao ya kijamii, vyombo vya habari Kama Luninga na redio ni sehemu ya vitu vinavyobadilisha watu mitazamo, tabia na Uelewa.

Nikasema hawa Wadada wanataka kuniingiza mkenge hawa. Kwani tamaa yangu ilikuwa IPO juu Sana.
Kimsingi Yule Dada naye alikuwa amenielewa, si nilishasema kuwa ni nadra Sana warembo kunikatalia. Basi tukabadilishana mawasiliano Kwa minajili ya kufahamiana vizuri.
Nini kilitokea? Hiyo ni habari ya siku nyingine.

Taikon Kwa sasa ni mweupe ingawaje nilikuwa Mweusi. Taikon Kwa sasa ananywele za singasinga wakati nilikuja na kipilipili. Taikon Kwa sasa naongea kimjini mjini wakati nilikuja ulimi mzito Kama MSUKULE. Taikon Kwa sasa navaa mikato ya kijanja wakati nilikuha sijui kupigilia pamba.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
40fb683dedec6678895f83ccd1704027d2-06-baby-beer.rsquare.w700.jpg
ngoja nivuteee fundo na chaliii nitarudiiii kumaliziaaa
 
Mm binfs nilimebadili jina na nineshakuwa maarufu kwa kujita engineer deo mtaa mzima unanifahamu kwa jina hilo nikaacha jina langu la halis la nyanguzi Dsm inakubsiliksha kbsa had muonekano wangu sas nimebadili hata nguo zangu nimebadili sas HV navaa modo tu shat la leo nililolifah kanisani ni modo kbsa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nje ya mada...mkuu upo vizuri sana sana...hongera sana...ila nimesoma upareni...miaka 4 aisee waparee wana akil nzito sana...na ni wajuaji haswa....

Siku moja same sec pale nipo na mbaga simu yake imeisha chaji...na simu hazirusiwi shuleni...jamaa main switch katoa viwaya vyake afu kaunganisha na chaji yake...mara paap kanyukwa shot...sasa vitanda ni double...wenge lile kutoka juu mpaka chin kaanguka....

Afu ni kama hajitambui...kalala chin anasema anasikia baridi...tumpepeee...sasa kwa joto la Same lile baridi inatoka wapi...??

Akanyanyuka akaanza kukimbia anasema moto unawaka..wenge ilo...
 
Back
Top Bottom