Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
Jamaa walichakachua Cement wakaweka mchanga nini :biggrin1:
Faculty of social sciences and Humanities ya chuo kikuu cha Dodoma, ina nyufa kubwa sana zinazohatarisha maisha ya wanafunzi wa chuo hicho. Pia mifumo ya majitaka ni mibovu kiasi cha kusababisha harufu mbaya kwenye ma bweni na kuna muda hata maji hayapandi kwenye vyoo na baadhi ya vyoo vimefungwa kiasi cha kuwafanya wanafunzi wahamie facult nyingine kwa ajili ya kupata huduma hiyo muhimu.
Hayo yote yameshuhudiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape baada ya msafara wake uliokuwa umetoka kwa Mkuu wa Chuo Pro. Kikula kusimamishwa na wanafunzi na kumwambia aende akaone hali halisi na kumuomba aongee na Rais ili serikali itatue hili haraka iwezekanavyo.
Nape alijionea mwenyewe na kuwa ahidi vijana wa UDOM kuwa suala hili atalishughulikia kwani lengo la CCM ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu katika mazingira mazuri na pia alisisitiza mifumo hiyo mibovu ya maji taka ni hatari kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
Vijana wa UDOM wamekuwa na imani sana na huyo kiongozi kijana anayekuja kwa kasi katika kuisimamia serikali kutekeleza wajibu wake.
Hivi hiki chuo kimejengwa kwa pesa za ccm. Mbona Nape anafuatilia vitu ambavyo havimhusu. Yeye angeenda kufungua tawi la chama na kutafuta wanachama sio kutuzuga eti anakagua majengo for what then what next, yaani ccm inatapatapa.
Who is Nape?
wana ccm nape anatuangushe he pretends to know everything sasa itabidi uandikiwe kazi za kufunyaHivi hiki chuo kimejengwa kwa pesa za ccm. Mbona Nape anafuatilia vitu ambavyo havimhusu. Yeye angeenda kufungua tawi la chama na kutafuta wanachama sio kutuzuga eti anakagua majengo for what then what next, yaani ccm inatapatapa.
Labda kuna matetemeko ya ardhi; hivi likipiga tetemeko la ardhi hapo wamejiandaa; na majengo hayo yamejengwa na nani?