Nyota na masuala ya kidini (UDINI)

Magical power

JF-Expert Member
Sep 27, 2022
356
1,605
NYOTA NA MASUALA YA KIDINI ( UDINI )

1. Hawa kiukweli ni watu wanaoegemea upande wa dini yao tu. Yaani hufuata sana dini yao tu. Na wapo tayari kuilinda dini hio ILA SASA kinachofanya waheshimu dini na mila za imani zingine ni maslahi yao binafsi. Hawa wamegundua ukiweka sana misimamo utawapoteza watu kwenye Mzunguko wako wa maisha na rizki kiujumla.
Ndio ndio unakuta mtu anavaa nikabu au hijabu ILA anafundisha shule ya Mtakatifu Yohana. Na ANAISHI vizuri tu.

Wenye Nyota:
PUNDA ( A. M. Y )
MIZANI ( G. S )
MBUZI ( J. V )
KAA ( D. P )

Au waliozaliwa tarehe:
1. 13. 25. 7. 19. 10. 22. 31. 4. 16.

2. Hawa dini yao wanaipenda sana na tena wanaimani sana tena wabobezi sana. Ila wanapenda watu wamkubali MUNGU kuliko kuweka vita za KIDINI. Huamini binadamu wote muhimu duniani. Kama ni mkristo siku akivurugwa unaweza kumkuta kahuzuria darasa msikitini au kama muislamu usishangae unamkuta kwenye kongamano la mlima wa moto. Kikubwa watu wanapata kumjua Mungu. Kikubwa watu wanamuamini Mungu. Hawa sio wabaguzi maana wao wenyewe hupenda watu waishi vizuri. Hata wakristo hupiga kanzu kama waislamu. Hata ukiwa mkristo mwenzao na ukautukana uislamu hawapendi au UKIWA muislamu na unatoa matusi KWA wakristo hawapendi.

Wenye Nyota:
NG'OMBE ( B. N. Z )
NG'E ( H. T )
MSHALE ( I. U )
MAPACHA ( C. O )

Au waliozaliwa tarehe:
2. 14. 26. 8. 20. 9. 21. 3. 15. 29.

3. Hawa bhana kiukweli wamegawanyika. Wapo ambao hawaamini Mungu Yaani wanaamini nguvu zingine tu za kiulimwengu. Na kweli hufanikiwa kupitia imani hizo.
Wapo ambao huamini dini tu lakini matendo mtihani.
Ndio unasikia mtu anakashfa ILA asubuhi misa ya KWANZA.

Wengi wanaamini uchawi tu. AKISEMA mvua nyesha. Kweli inashuka. Hata magwiji huku mitaani kwenu wanatokea nyota hizi.

Wengi watu wema wapo kiimani wapo na utu.

Kiufupi hawa jamaa wametawaliwa na miujiza miujiza tu.

Wenye Nyota:
SAMAKI ( L. X )
MASHUKE ( F. R )
NDOO ( K. W )
SIMBA ( E. Q )

Au waliozaliwa tarehe:
12. 24. 6. 18. 11. 23.5.17.30
By magical power
 
Huo muda wa kutunga na kuandika vitu vya kufukirika si ungeutumia kujifunza namna bora ya ufugaji bata
 
Back
Top Bottom