Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Kumezuka tabia ya baadhi ya Watanzania kukebehi heshima aliyopewa Mwalimu Nyerere, kama Baba wa Taifa la Tanzania.

Kuna wanaodai Mwalimu Nyerere hastahili kuitwa Baba wa Taifa kwasababu hajalifanyia taifa hili lolote la maana ukifananisha na viongozi waliomfuatia baadae; Wengine wanakujenga hoja kwamba Nyerere ni Baba wa Taifa wa Tanzania Bara, na sio Tanzania Visiwani. Wapo wanaoenda mbali zaidi, wanapandikiza mbegu za chuki na kutugawanya kwa kejeli kwamba ‘watanzania wanaomheshimu Nyerere kama baba wa taifa wamerithishwa ulimbukeni kwasababu Nyerere sio Msahafu wa Taifa la Tanzania. Huu ni upotoshaji na upindishaji wa ukweli wa makusudi. Pia ni matusi na kejeli kwa Mwalimu, na ni juhudi za makusudi za kutugawa kama taifa. Tabia hii haiwezi kuachwa iendelee ikiwa bado tunataka kuendeleza matunda ya uhuru ambayo ni pamoja na udugu, amani, na mshikamano wetu kama taifa. Wafitini hawa lazima wajibiwe kwa hoja, sio malumbano, kwani yawezekana kabisa kwamba kuna mambo ambayo hawayafahamu au wanapotoshwa juu ya ukweli kwanini Nyerere ni Baba wa Taifa. Hilo ndilo lengo kuu la makala yangu leo. Ni ndefu kidogo, Kwahiyo naomba uvumilivu kwa wale watakaopenda kuisoma. Nitaanza mjadala kwa kuangalia tofauti kati ya heshima ya Rais kuitwa BABA WA TAIFA na heshima ya Rais kuitwa 'RAIS BORA WA TAIFA'.

MAANA HALISI YA BABA WA TAIFA KI-ULIMWENGU:

Baba wa Taifa, katika nchi zote ulimwenguni, ni Tunu au Heshima anayopewa mtu/binadamu (mwanaharakati) kutokana na mchango wake katika uongozi wa harakati za kulikomboa taifa kutoka kwenye utawala wa wachache, usio shirikisha wengi katika maamuzi kupitia demokrasia (aidha ya chama kimoja au vyama vingi), na wenye sera zisizotoa fursa na haki sawa za kijamii, kisiasa na kiuchumi (zinazotambulika rasmi kikatiba) kwa walio wengi, hivyo kupelekea uwepo wa jamii iliyojaa dhuluma, uonevu, unyonyaji, na ubaguzi wa aina mbalimbali. Utawala wa namna hii unaweza ni kuwa wa taifa moja kwa taifa jingine (mfano enzi za ukoloni wa mwingereza, mreno, na mfaransa Bara la Africa); lakini pia hali hii inaweza kujitokeza ndani ya taifa moja (mfano Afrika ya kusini wakati wa ubaguzi wa rangi). Mifano ya aina hizi za utawala ni pamoja na:

  • Mahatma Ghandi – India: Aliongoza harakati dhidi ya utawala wa kikoloni wa Mwingereza.
  • Nelson Mandela – Afrika ya Kusini: Aliongoza harakati dhidi ya utawala wa dhuluma wa watu wachache (makaburu) kwa walio wengi (weusi) ndani ya Afrika.
Heshima ya Baba wa taifa inatambulika na bunge la nchi husika kwa mujibu wa Sheria, kwa kuzingatia kwamba bunge ndio chombo cha kuwakilisha maoni ya wengi. Heshima ya Baba wa taifa haina mahusiano yoyote na kitabu chochote kitakatifu (Quran au Biblia) hasa ukizingatia kwamba serikali nyingi, kikatiba, hazina dini. Ni muhimu tutambue kwamba, katika historia ya dunia, haijawahi kutokea hali ya kwa taifa lolote huru kuingia katika mzozo juu ya nani anastahili heshima ya kuwa Baba wa Taifa, kwa sababu, kama tulivyokwisha ona asili ya heshima hii ni hali ya mwananchi mmoja kujitoa mhanga kuongoza wengi katika harakati za ukombozi. Vilevile, hakujawahi kutokea mjadala unahusu Baba wa Taifa, katika taifa lolote huru duniani, unaligawa taifa kwa misingi ya kidini, kikabila, au itikadi ya siasa, pia kwa sababu, kama tulivyoona, ubaguzi wa aina yoyote ndicho kiini cha mapambano ya uhuru au ukombozi. Mjadala wa namna hii umejitokeza Tanzania, ambapo hata wenzetu wa Kenya ambao, kihistoria wamegawanyika sana kama taifa kikabila, bado hawatofautiani juu ya Baba wao wa Taifa Mzee Kenyatta.

Watanzania tuliishangza dunia kwa mshikamano chini ya makabila 120, lakini sasa tunaanza kuishangaza dunia kwa sisi wenyewe kuanza hoji kiini cha nguvu ya mshikamano huo.

Ebu sasa tutazame maana ya Heshima ya Rais kuitwa ‘Rais Bora wa Taifa'.

Ø MAANA HALISI YA RAIS BORA WA TAIFA KI-ULIMWENGU

Tofauti na Heshima ya Baba wa Taifa ambayoe inatambulika kisheria, heshima Rais Bora huwa ni maoni ya wananchi walio wengi ambayo hupitia mchakato wa tafiti/vipima joto mbali mbali zinazolenga kukusanya maoni ya wananchi. Tutaliangalia kwa undani zaidi suala hili, lakini vigezo vikubwa vinavyotumiwa katika tafiti hizi ni pamoja na kuhoji wananchi juu ya ubora, usimamizi na utekelezaji wa sera mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi, na kuangalia mchango wake katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na yanayopelekea wananchi ‘walio wengi' (sio wachache), kujisikia kama taifa, kwamba uongozi uliopo unaelewa matatizo yao na hivyo unajitahidi kuboresha maisha yao. Kipimo kingine pia ni juu ya ubora, usimamizi, na utekelezaji wa sera zinazodumisha Amani, Mshikamano, Utulivu na Maelewano, sio baina ya wananchi wa taifa husika pekee, bali hataa baina ya taifa hilo na mataifa mengine.

Kwa mataifa machanga, ni kawaida wananchi kuwa na maoni kwamba Baba wa Taifa pia ni Rais Bora; Ingawa sio katika mataifa yote, mataifa mengi huanza historia zake kwa namna hiyo (tutaona mfano wa Marekani Baadae). Ila kofia hizi sio lazima zibakie chini ya mtu mmoja milele. Kuna sababu kuu mbili kofia hizi kujitenga. Moja, ni kutokana na Rais wa Kwanza wan chi husika kubadilika na kuwasaliti wananchi wake na kuwa dikteta au fisadi. Na pili, hutokana na ukweli kwamba historia ni dynamic (hayasimami), sio static (iliyosimama). Dynamism hii katika historia hupelekea au hambatana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia (mfano jamii zote zilianza na kilimo kabla ya viwanda); lakini muhimu vilevile ni kwamba dynamism hii huambatana au hupelekea madaliko ya ‘taste and preference' ya bidhaa na huduma katika jamii, kutokana na modernity - mfano, katika jamii inayitegemea kilimo, kuna baadhi ya bidhaa au huduma zinaweza kuonekana ni anasa, tofauti na jamii inayotegemea viwanda.

JE, INAWEZEKANA HESHIMA YA BABA WA TAIFA KUPEWA RAIS MWINGINE?

Jibu ni hapana ingawa sio la moja kwa moja. Kama tulivyokwisha ona, heshima ya baba wa taifa haitengani sio tu na historia ya taifa husika bali pia harakati za ukombozi/uhuru unaopelekea taifa husika kuunda jamhuri huru, inayotoa fursa na haki kwa raia wote kisiasa, kijamii na kiuchumi, kwa mujibu wa katiba. Kiongozi akishapewa tu heshima hiyo, historia haiweza kujirudia tena kupelekea kiongozi huyo kuipoteza. Kwahiyo, heshima hii hubakia kwa mtu mmoja katika maisha yote ya taifa husika. Hivyo mjadala wowote juu ya ulakini wa Baba wa Taifa katika nchi yoyote lazima uangaliwe kwa jicho la tahadhari kwani unalenga kuikana Historia ya taifa na wananchi husika na kutaka kuiandika upya. Duniani kote, hakuna historia inayowezwa kuandikwa upya.

Mpaka hapa, nadhani wafitini wa Baba wa Taifa wameshaelewa vigezo na sifa za baba wa taifa, na pia kwanini haziwezi tenganishwa na historia ya taifa husika. Bila shaka, wanaomkejeli Mwalimu Nyerere wakiulizwa baba wa taifa wa Cuba au China ni nani? Hawatakuwa na jibu kabla ya kufanya utafiti. Bila ya utafiti, watatoa jina la Rais Bora, badala ya Baba wa Taifa.

Wengi wa wanaomkejeli Mwalimu juu ya heshima yake ya Baba wa Taifa ni watu wasioelewa nini maana ya heshima hii, na pia kuwa na tabia ya kuchanganya mjadala wa baba wa Taifa na Rais Bora. Ni kawaida kwa wafitini hawa kuhoji mara kwa mara: Je Nyerere kalifanyia nini taifa hili mpaka aitwe baba wa taifa? Kwa watu wa namna hii, vigezo au sifa za kiongozi kuitwa baba wa taifa ni kuona Maendeleo ya aina fulani fulani chini ya Rais husika, mfano - Magorofa marefu ya vioo (sio vijijini, mijini), barabara za lami zinazojengwa kwa nia ya kurahisha usafirishaji wa Mazao na madini toka mikoani (sio zinazorahisisha biashara na mawasiliano kati ya Kijiji A na Kijiji B), wingi wa vitu madukani kutoka China (sio kutoka katika viwanda vyetu na bila ya kujali iwapo kuna uwiano kati ya wingi wa vitu madukani na wingi wa watanzania wenye uwezo kuvinunua, hasa hasa vijijini), na Televisheni majumbani (asilimia 15% ya watanzania wenye umeme, takwimu iliyobakia hivyo hivyo kwa miaka mingi sana). Haya yote hayamvunjii Baba wa Taifa aliyepo heshima yake, kwani yeye ndiye muasisi wa Taifa ambalo ndilo limekuja zaa yote hayo kwani bila yeye, aidha taifa lisingekuwepo au lingekuwa na historia tofauti kabisa iliyotokana na makabila na lugha zaidi ya 120 zilizogawanyika nusu kwa nusu katika uumini wa dini (50/50 Uislam na Ukristo).

- Tutazame nchi za wenzetu, baba wa mataifa yao ni nani na kwanini:

  1. Marekani – George Washington kwa kuongoza wamarekani kama kamanda mkuu wa majeshi katika vita dhidi ya ukoloni wa Mwingereza, na yeye kuwa Rais wa kwanza wa marekani huru mwaka 1789 - 1797;
  2. China – Yat – Sen kwa kuongoza mapambano ya kupindua ufalme wa Qing mwaka 1912, ufalme uliodumu kwa miaka 2,000, na baadae kuwa Rais wa kwanza wa wa China; Mao Tse Sung alikuja kuwa rais wa China mwaka 1943, miaka 18 baada ya Yat – Sen kufariki; bila shaka kwa wengi wanaomkejeli Mwalimu Nyerere, ufahamu wao ni kwamba Baba wa Taifa la China ni Mao Tse Sung.
  3. Cuba – Carlos Cespedes - Mwaka 1868, aliwaongoza watu wa Cuba katika mapambano ya ukombozi dhidi ya ukoloni wa Kispaniola, na hatimaye kuwa Rais wa Kwanza wa Cuba huru; Ni dhahiri uelewa wa wafitini wa Mwalimu ni kwamba Fidel Castro ndiye baba wa taifa la Cuba; Castro alikuja kuwa Rais wa Cuba miaka 81 baada ya Cespedes kuuwawa (Castro Urais wake ulianzia mwaka 1949);
  4. Kenya – Jommo Kenyatta – natumaini sote tupo pamoja katika hili;
  5. Namibia – Sam Nujoma – Pia kwa hili natumaini sote tupo pamoja;
  6. Msumbiji – Samora Machel - Pia kwa hili natumaini sote tupo pamoja;
  7. Zaire (DRC) - Patrice Lumumba - Pia kwa hili natumaini sote tupo pamoja;
  8. Afrika ya Kusini – Nelson Mandela - Pia kwa hili natumaini sote tupo pamoja;
  9. Tanzania – Julius Kambaraga Nyerere - Tofauti kubwa aliyonayo Mwalimu na wenzake ni kwamba katika nchi za Angola, Msumbiji, Namibia, Afrika Ya Kusini, kuna watu pia wanasema wanamheshimu kama mmoja wa waasisi wa mataifa yao (sio baba wa taifa), huku baba zao wa taifa wakiwa ni wale wale (Agustino Neto – Angola, Samora Machel – Msumbiji, Sam Nujoma – Namibia, na Nelson Mandela – Afrika Kusini). Wengi wa wafitini wa Mwalimu hawaoni umuhimu wa harakati za Mwalimu kusini. Inawezekana sababu kubwa hapa ni kwamba, wafitini hawaoni kitu in common kati yao na watu wa kusini, 'kiutamaduni'.
- HOJA ZA WAFITINI WA MWALIMU NA UBABA WA TAIFA.

Wafitini wa Mwalimu huwa wanahoja kuu mbili:

(a) Je, Mwalimu Nyerere kalifanyia nini Taifa hili kitakwimu mpaka aitwe baba wa taifa?
(b) Mwalimu ana uhalali gani wa kuwa baba wa taifa kwenye muungano?

[A] Tuanze na hoja yao ya kwanza: Je, Mwalimu kalifanyia taifa hili hadi aitwe baba wa taifa?


  1. Baba wa Taifa wa Zaire (DRC), Patrice Lumumba, ambae alifariki miaka michache sana baada ya kuikomboa Zaire, na ambae alikuwa mshirika mkubwa wa Nyerere, Je amelifanyia nini Taifa la Zaire kitakwimu mpaka aitwe baba wa taifa? Tusisahau kwamba aliuwawa kikatili na mabepari wa nje wakati anajaribu kufanya uchumi wa Zaire uwe wa wote kama Nyerere.

  1. Baba wa Taifa wa Msumbiji, Samora Machel, ambae aliuwawa na makaburu sio zaidi ya miaka kumi tangia aikomboe nchi yake, na ambae alikuwa mshirika mkubwa wa Nyerere, Je amelifanyia nini Taifa la Msumbiji kitakwimu mpaka aitwe baba wa taifa?

  1. Baba wa Taifa wa China, Yat – Sen, Je, amelifanyia nini Taifa la China kitakwimu mpaka aitwe baba wa taifa? Sen alifariki mwaka 1925 wakati huo China ikiwa moja na nchi maskini duniani.

  1. Baba wa Taifa wa Marekani, George Washington, Je amelifanyia nini taifa la Marekani kitakwimu? Washington alifariki marekani ikiwa ni nchi inayotegemea kilimo; mpaka anafariki, Marekani haikuwa nchi ya viwanda bali watumwa na kilimo; na ilikuwa nyuma kimaendeleo kwa nchi kama Japan, Uingereza, Ufaransa, Ubejgiji, Ujerumani, Denmark na nyingine nyingi.

  • Mifano hii inadhihirisha kwenu kwamba kipimo cha baba wa taifa sio magorofa, wingi wa bidhaa madukani, wingi wa madaraja na barabara za kisasa na wingi televisheni majumbani, mchango wake uliotoa mwamko kwa wananchi wa ya "self-determination", iliyopelekea nchi husika kuingia katika harakazi za kujikomboa ili kuwa na huru na yenye uongozi unaotoa fursa na haki sawa kwa wote (kikatiba) kijamii, kisiasa, na kiuchumi. Viongozi wa magorofa, bidhaa madukani, barabara na madaraja, wao ni matokeo tu ya harakati hizo ambazo zinaweza wapelekea kuwa Ma-Rais Bora, ila iwapo asilimia kubwa ya wananchi wanahisi wanafaidika moja kwa moja na Maendeleo hayo.
· Moja ya sifa kubwa anayopewa Mwalimu kimataifa ni uwezo wake wa kuwaunganisha wananchi wa jamii yenye lugha na makabila zaidi ya 120 na iliyogawanyika karibia nusu kwa nusu kwa imani za kidini (Uislam na Ukristo), na kuweza kuwaongoza na kufanikisha ukombozi wa taifa lao na wakabakia katika amani, mshikamano na utulivu wakati wote wa utawala wake.

Kwahivyo, tukubaliane kwamba mjadala unaotumia takwimu kama sifa au kigezo cha heshima ya mtu kuwa baba wa taifa ni kinyume na desturi hata kimataifa. Mjadala wa namna hii huwa unaelekezwa kutafuta maoni ya wananchi juu ya nani ni Rais Bora, Sio Nani ni Baba wa Taifa. Ni sahihi wananchi kujadili nani ni Rais bora kwani kila mmoja ana uhuru wa kutoa mawazo yake kutokana na maisha yake binafsi, lakini suala la Baba wa Taifa sio suala la mtu binafsi au la mapenzi pekee yake juu ya kiongozi fulani. Kwangu binafsi, kwa Tanzania ya sasa, Mwalimu Nyerere ana kofia zote mbili za: Baba wa Taifa na Rais Bora wa Tanzania, lakini nipo tayari kukosolewa juu ya Nyerere na Rais Bora.

Vinginevyo Mjadala unaohoji kwa kebehi, dharau, matusi, kejeli juu Baba wa Taifa lolote lile ni suala linalokaribiana na uhaini kwa sababu ambazo tumekwishaziona, Kwahiyo, hata hapa Tanzania, tabia hii inatakiwa ikemewe kwa ukali na viongozi wa kitaifa kutoka vyama vyote vya siasa, kila mara inapojitokeza. Vinginevyo, mjadala wa Rais bora katika taifa ni suala huru wa kila mwananchi kutoa maoni au mawazo yake, ili mradi halivunji heshima ya baba wa taifa.

Tuingie kwenye hoja ya pili inayohoji uhalali wa Mwalimu Nyerere kuwa Baba wa Taifa katika Muungano:

Hoja hii ni dhaifu sana. Marekani (USA) ya leo ni matokea ya Muungano wa majimbo 50. Miaka ya nyuma, majimbo haya hayakuwa pamoja bali yalikuwa kama vile Kenya, Tanzania, Ugana n.k. Muungano wa majimbo 50 ndio umezaa jina la nchi kama United States of America – kwa maana ya Umoja wa Mataifa ya Marekani. Ni muhimu nikasema kwamba Serikali tatu Tanzania ni suala ambalo halikwepeki, na kwamba litatupelekea kuiga mfumo mzima wa Marekani huko mbeleni, mfumo ambao ni wa mafanikio makubwa kuliko yote duniani. Kwa kuanzia, hata mapendekezo ya tume ya bomani yaliyopelekea utaratibu wa mgombea mwenza kutoka Zanzibar yaliazimwa kutoka mfumo wa Marekani.

Kwa wale wanaomfitini Mwalimu ni muhimu wakatambua kwamba, majimbo haya 50 ya Marekani hayakujiunga kwa mkupuo mmoja, bali katika vipindi mbali mbali tofauti. Wakati wa ukoloni wa mwingereza, majimbo haya yalikuwa kivayo vyao, kama vile Kenya, Tanzania, Zambia n.k wakati wa ukoloni. Safari ya George Washington kuelekea kuwa baba wa Taifa ilianza na nia na uwezo wake wa kuyaunganisha majimbo 13 (sio majimbo 50 ya leo), ili yaweze kuwa na nguvu ya pamoja kupambana na mkoloni. Juhudi hizo zilifanikiwa, marekani ikapata uhuru wake mwaka 1776, na baadae Washingoton kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Marekani iliyo huru.

Ni muhimu tufahamu kwamba katiba ya marekani ambayo kwa viwango vyote ni moja ya katiba bora duniani haikuandikwa kwa njia za kidemokrasia bali watu wachache chini ya Rais Washington. Isitoshe, chini ya Washington, hapakuwa demokrasia ya vyama vya siasa, vilikuwa havijazaliwa bado, hivyo kupelekea Rais Washington kuwa Rais wa taifa lisilo na chama chochote cha siasa. Wakati wa Urais wake, Washington alifanikiwa kuongeza majimbo mengine matatu katika muungano ule na hivyo kupelekea Marekani kuwa nchi yenye jumla ya majimbo 16 (sio 50 ya leo) mpaka anastaafu na kufariki.

Ni muhimu pia tukatambua kwamba Muungano wa Marekani haukuwa mrahisi kama wengi wanavyofikiri kwani ulikumbwa na misukosuko mikubwa sana kuliko hata huu wa kwetu Tanzania. Hivyo, sio kwamba George Washington alipofariki aliacha Muungano SalamaSalmini kwani miaka 62 baada ya Washington kufariki, Muungano huo ulijikuta katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopelekea kupotea maisha ya watu wengi, wakati huo Marekani ikiwa chini ya Utawala wa Rais wa 16 wa nchi hiyo - Abraham Lincoln. Rais Lincoln alipokea nchi yenye Muungano wa jumla ya majimbo 36 (sio 50 ya leo), ikiwa na maana kwamba Marais waliomfuatia Washington waliongeza majimbo mengine 20 zaidi.

Sababu kuu ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe 1861 – 1865, ilikuwa ni mifarakano ya mara kwa mara ambayo ni ya kawaida katika muungano wowote wa nchi changa. Lakini sababu iliyowasha kibiriti cha moto wa vita ilikuwa ni sera ya Rais Lincoln ya kutokomeza Utumwa. Nchi ikagawanyika kati ya kusini na kaskazini, kusini wakitaka biashara iendelee, huku kaskazini wakimuunga Rais Lincoln kuitokomeza. Muungano ukavunjika na kuzaa mataifa mawili - Taifa la kwanza lilijitenga na majimbo yake 11 chini ya rais wake mpya na kujiita a confederation. Taifa la pili likabakia na majimbo 25 (na kujiita a union), chini ya Rais Lincoln. Pamoja na tofauti zote hizi, miaka mitano baadae, rais Lincoln alifanikiwa kuvimaliza vita vile, kutokomeza utumwa na kuirudisha Marekani kuwa mungano wa majimbo 36 kama awali. George Washington na wengine tuliowaona ni baba wa mataifa yao kutokana na kuongoza na kushinda vita dhidi ya ukoloni.

- JE WENYE HOJA ZA KUMKEJELI BABA WA TAIFA WANAJIFUNZA NINI?

1. George Washington aliongoza na kuunda marekani yenye majimbo au mataifa 16 tu. Pamoja na kwamba Marais waliomfuata wameongeza majimbo mengine 36 katika nyakaii tofauti, hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

2. George Washington aliongoza mchakato wa katiba ya kwanza ya marekani katika mazingira yasiyokuwa na demokrasia, katiba iliyohusu majimbo 16 tu (sio 50 ya leo), lakini hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

3. George Washington hakuwa Rais alietokana na demokrasia ya chama kimoja wala vyama vingi kwani hakuanzisha utaratibu huo, na kupelekea yeye kuwa Rais waa nchi isiyokuwa na chama hata kimoja cha Siasa, bali muungano tu wa majimbo 16, lakini hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

4. George Washington aliwaachia Wamarekani muungano uliojaa kero na tofauti nyingi za ki mfumo, muundo, mtazamo, na sera, kiasi cha kupelekea nchi kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenywe miaka 64 baada ya Washington kufariki, lakini hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

5. Rais alipelekea muungano wa Marekani kuvunjia alikuwa Abraham Lincoln na ndiye yeye alieurudisha na kujenga mazingira yaliyovutia majimbo mengine 14 kujiunga baadae na kukamilisha taifa lenye jumla ya majimbo 50, lakini hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

6. George Washington aliacha nyuma Marekani kama taifa lisilo na Maendeleo makubwa kiuchumi; lilikuwa taifa linalotegemea kilimo, lililo nyuma sana kimaendeleo ikifananishwa na nchi za Uingereza, Japan, Ufaransa, Italy, Ubelgiji, Denmark, Sweden, Ujerumani, lakini hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

7. George Washington hakujenga barabara zozote, wala madaraja yoyote, wana uwanja wa ndege, wala magorofa yoyote ya glasi mijini; ni Marais waliomfuatia, waliojenga hayo katika maeneo mbali mbali ya muungano ule, na pia ni wao walioleta mapinduzi ya viwanda, na baadae kuwa taifa kubwa kuliko yote duniani kiuchumi na kijeshi, lakini hilo halijamvunjia heshima George Washington kama Baba wa taifa la marekani.

8. George Washington ameacha taifa lenye muungano ambao pamoja na tofauti kubwa ambazo bado zipo, wamarekani huwa wanayatatua bila ya mifarakano kwani Baba wao wa Taifa aliwafundisha kwamba Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Vinginevyo wamarekani wamegawanyika sana kimtazamo, kimsimamo juu ya jamii yao na ile ya kimataifa; ni muungano wenye mchanganyiko wa makabila makubwa matatu (weupe, weusi, latino/mexico); tofauti hizi huwa zinajitokeza wakati wa chaguzi kuu kwani kwa miaka zaidi ya 50, hakuna chama cha siasa (kati ya viwili vikubwa vilivyopo – Democrats na Republicans) kilicho weza kushinda chaguzi za Urais kwa zaidi ya asilimia 51; lakini pamoja na tofauti zao kubwa, Marekani, taifa lililoasisiwa na baba wake wa taifa, George Washington halijatetereka, na halijarudi nyuma; na adui mkubwa wa Muungano huu amebakia wa nje ya marekani, sio wa kutoka ndani ya muungano ule. Marekani imebaki kuwa role model kwa watu wengi sana duniani, pamoja na wale wanaomkejeli Mwalimu.

- USHAURI KWA WAFITINI WA BABA WA TAIFA

· Ubaba wa taifa sio Mapenzi ya mtu mmoja mmoja aidha kwa kutumwa au kwa juhudi binafsi bali ni heshima kwa mujibu wa sheria kama tulivyokwisha ona. Ili kuacha legacy kwa nchi, sio lazima kwa rais mwingine nchi apewe tena heshima ya baba wa taifa; Kuna njia nyingine nyingi sana ambazo zikitumika katika jina la Maendeleo ya watanzania walio vijijini, inawezekana kabisa kumpokonya Mwalimu Nyerere kofia ya Rais Bora wa Tanzania, na kumwachia ile ya Baba wa taifa ambayo hata nyinyi wafitini sasa mmeelewa kwanini haipokonyeki; na njia pekee ya kuipokonya ni ya nyinyi kutugawa, na kutafuta taifa jipya litakalozaa baba wenu mwingine mpya wa taifa. Hilo, watanzania hawatalikubali.

Tumeona jinsi gani viongozi kama Abraham Lincoln, Mao Tse Sung, Tony Blair, Joachim Chisano, Ronald Reagan, Margaret Thatcher ambao sio baba wala mama wa mataifa yao, bali wamejipatia heshima kubwa sana kimataifa kutokana na utawala wao, kiasi cha kupelekea baadhi yao kupokonya hadhi za Urais bora kutoka kwa waliowatangulia na kuwaachia ile ya baba wa taifa – mfano Abraham Lincoln (Marekani), na Joachim Chisano (Msumbiji) ambao sasa wametuzwa na wananchi wao kama Marais bora.

Jambo la kumvua heshima baba wa taifa aliyepo na kumpa mtu mwingine haliwezekani. Lakini msife moyo kwani, jambo la kumpokonya baba wa taifa kofia ya Rais Bora katika jina la Maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watanzania wengi (vijijini) linawezekana kabisa, na hii ndio iwe changamoto kwa watu watakaofanikiwa kuwa Marais wetu. Tukumbuke kwamba, kabla ya ujio wa Abraham Lincol, kwa miaka 60, George Washington alikuwa na kofia zote mbili – baba wa taifa na Rais bora wa taifa. Kofia hii ilikuja kuvuliwa na Rais was 16, Abraham Lincoln. Huu ni utafiti/vipima joto huko marekani. Washington kwa sasa ni Rais wa pili kwa ubora, na nafasi ya tatu ipo kwa Thomas Jefferson ambae alikuwa Rais wa tatu wa marekani. Angalizo: Rais wa 16 wa nchi (Lincoln) ni Rais wa kwanza kwa uBora, huku Rais wa Kwanza wa nchi (na baba wa taifa) akiwa wa pili kwa ubora; na Rais wa tatu wa nchi (Jefferson), pia ni Rais wa tatu kwa ubora. Rais Obama ambae ni Rais was Rais wa 44 wa nchi, ambae hajamaliza hata muhula wake wa kwanza, tayari baadhi ya tafiti zinamuweka nafasi ya 14 katika ubora wa marais wa marekani (kati ya jumla ya marais 44),akiwa nyuma ya Clinton aliyepo nafasi ya 13. Hii ina maana hata Tanzania, haya yanawezekana.

· Wafitini wa Mwalimu, kwanini msielekeze juhudi zenu binafsi kuisaida jamii yetu ipate kina Abraham Lincoln, Thomas Jefferson, Tony Blair, Joachim Chisano, Winston Churchill, Mao Tse Sung, Fidel Castrol, au Margaret Thatcher wa Tanzania?

Juhudi zenu binafsi zinatupa watu wasiwasi kwamba pengine nia yenu ni kuturudisha nyuma kama taifa, na kutuingiza katika katika machafuko ili mjipatie taifa jipya (hatujui kwa vigezo vipi), na hatimaye baba wenu mpya wa taifa.

Ni muhimu mtambue kwamba Viongozi kama Abraham Lincoln, Joachim Chisano, Mao – Tse Sung, na Fidel Castro hawakufanikiwa kupokonya kofia ya URAIS BORA kwa njia za fitina na chuki kwa baba wa taifa aliyepo bali wamejipatia sifa hizo kutokana na sababu kuu kumi:
(1) Kulinda heshima kwa baba zao wa taifa;
(2) Kufuata misingi iliyowekwa na baba wa mataifa yao;
(3) Kulipa taifa a Self – determination kisiasa na kiuchumi;
(4) Uzalendo kwa nchi zao;
(5) Uadilifu;
(6) Uongozi unaofuata haki na sheria na usiowagawa wananchi kwa namna yoyote ile;
(7) Sera zenye matokeo yanayobadili hali za maisha ya walio wengi
(8) Uongozi bora (sio bora uongozi);
(9) Misimamo na kutokubali kuingiliwa au kuendeshwa na mataifa mengine au taasisi za kimataifa kuhusu sera na mwelekeo wa nchi zao, kwa mfano kuwa na ujasiri wa kuwaambia WorldBank, IMF, WTO, kwamba, tunawahitaji sana mtusaidie lakini sera au masharti yenu katika uwekezaji n.k HAPANA, hayaendani na mipango yetu ya kutokomeza umaskini vijijini.
(10) Ambae ataongoza kwa mfano, ili kuwapa vijana moyo na ari ya kufanya kazi kwa bidii, kujenga kwa vijana nidhamu ya kazi, kuwatengeneza mazingira ya kutokimbilia nje kutafuta maisha (brain drain), kuwafunza waadilifu, uzalendo, na kuwahamasishwa vijana kwamba kulipa KODI ni sifa moja wapo ya Uzalendo, Utaifa na uraia wa kweli;

· Kipimo cha kiongozi huyo kupewa heshima ya kuwa Rais bora na watanzania atakuwa yule ambae atawaletea mabadiliko na uhuru wa kiuchumi ya kweli asilimia 70 ya Watanzania ambao kwa sasa wapo vijijini wakihangaika; sio kuletea mabadilio wachache walio mijini, au wale watakaokuwa wanajipendekeza kwa uongozi husika. Tanzania kama taifa ni vijijini, sio Dar-es-salaam kwani asilimia 70 (watu milioni zaidi ya 30 kati ya jumla ya milioni karibia 45) ndio wanaishi huko;

· Ndugu zangu wafitini wa Mwalimu, ukiachilia mbali heshima ya baba wa taifa au Rais bora, pia zipo heshima nyingi sana za kuzitafuta, mfano tuzo za Mo – Ibrahim ya Good Governance in Africa, na ile ya Nobel Peace. Juhudi binafsi za kutafuta ubaba wa taifa unaweza pelekea viongozi mnaowapenda kukosa kila kitu na kuishia ICC kwa Ocampo.

· Ubaba wa taifa sio mwisho, ilichukua miaka zaidi ya 60 kumpokonya George Washington kofia ya Urais bora na kumshusha kuwa namba mbili na Lincoln kupanda kuwa namba moja. Kwahiyo, hata kama itatuchukua miaka 100, hata Tanzania inawezekana! Muhimu pia ni kusema kwamba, Lincoln, Chisano, Castro, au Mao wa Tanzania anaweza kutokea chama chochote cha siasa kitakachopata madaraka, sio CCM pekee, bali hata CHADEMA, CCK, CUF, au vingine vingi kati ya karibia 17 vilivyopo Tanzania ya sasa. Kwani hata marekani, viongozi toka vyama vyote viwili vikubwa– Republicans na Democrats vimezaa viongozi mbalimbali wenye heshima;

  • Mafanikio ya Rais wa namna hiyo yatakuja iwapo tu kama kiongozi huyo atakuja na programu na mikakati mipya na tofauti kabisa ya maendeleo, na mengi yapo kwenye Azimio la Arusha.Kiongozi anaetetemeka akisikia Azimio la Arusha hastahili kuwa Rais Bora wa Tanzania.
Vinginevyo CCM ya sasa imechanganyikiwa (upande mmoja Azimio La Arusha kwa maneno, Upande Mwingine Azimio La Zanzibar kwa vitendo). Kama ilivyo CCM, CHADEMA nao hawana jipya, kwani sera zao ni za kushirikiana na Worldbank, IMF, WTO bila ya kuwahoji, na badala yake kuendeleza ukoloni mamboleo ambao kwa miaka 26 (1986 – 2011), takwimu zinaonyesha mwanakijiji amekuwa fukara zaidi kuliko kipindi cha (1967 – 1986) – rejea social development indicators, mtabainihili. Tunawahitaji sana IMF, WTO, Worldbank katika mipango ya uchumi wetu, lakini sio kwa wao kutupangia Maendeleo yetu wenyewe; wao ni nani kupangia Maendeleo ya wengine? Kwanini wasituheshimu kama wnavyoheshimu mataifa mengine? Rais Bora atakuwa yule atayeweza establish a dialogue na wakubwa hawa, yenye common interest kwa mwanakijiji. Vinginevyo, sio CCM, wala CHADEMA ambao wanaonyesha kwamba wana uthubutu wa kukaa na wakubwa hawa across the table na kuwaambia "hapana, hilo hatuliafiki kwani halipo katika dira yetu na mipango yetu ya maendeleo ya mkulima kijijini". Aliyeweza alikwa Waziri wa fedha wa zamani, Amir Jamal aliyeikataa hotuba aliyoandaliwa na IMF kwenye mkutano huko Washington kwani mawaziri wetu wa Fedha wakienda kule wanapewa hotuba zilizoandikwa na IMF wawasomee wajumbe wa mikutano husiku.

Hata ukiangalia ilani za chaguzi za vyama vya CCM na CHADEMA ambavyo ndio vikubwa, havina tofauti za msingi, kilicho bayana ni ushindani wa kukimbilia Ikulu kwenda kuwa watekelezaji bora (kuliko chama kingine) wa matakwa ya IMF, WorldBank na wakubwa wa nchi za OECD bila ya kuyahoji, matakwa ambayo Mwalimu alipingana nayo kwa miaka karibia mitano (1980 – 1985). Baada ya miaka 26 ya soko huria ambalo Mtanzania hakuandaliwa kushiriki kikamilifu na badala yake kushtukizwa mwaka 1986, tumeshaona hofu ya Mwalimu juu ya hilo ilikuwa ni ipi. Ni ile ya uchumi kukua kwa wastani wa asilimia 7 kwa miaka kumi mfululizo kama sasa, kutokana tu na uzalishaji wa Dhahabu ambayo haina faida yoyote kwa wakulima vijijini. Kwa mfano, ukitoa Gold Exports katika equation ya GDP yetu, uchumi wetu ni uchumi duni na usio na tofauti na ule wa Mwalimu kabla ya miaka ya 80.

Tujiulize: Inakuwaje kwa miaka karibia kumi (2000 – 2011), kasi ya kukua kwa uchumi Tanzania ya asilimia 7 kwa wastani kwa mwaka, inayopelekea Tanzania kuwa katika nchi 40 bora duniani (kati ya nchi 187) kwa kasi ya GDP growth, lakini wakati huo huo, kwa kipindi chote hicho ni Human Development Index (HDI) inatuweka nafasi ya 150 kati ya nchi 187 permanently? HDI inaangalia impact ya GDP kwenye life expectancy, literacy levels, educational outcome, and standard of living.

Tumetimiza miaka 50 uhuru; ndani ya miaka hiyo, Tanzania iliongozwa na sera za Ujamaa kwa miaka 18 na na imekuwa chini ya sera za soko huria holela kwa miaka miaka 26 ambayo ni mingi zaidi ya ile ya Ujamaa. Wapo wanaoleta hoja kwamba Tanzania isingefuata Ujamaa ingekuwa mbali. Majibu kwa watu waliopotoka namna hii ni kwamba, HDI inagawanywa nchi 187 katika makundi manne ya Maendeleo:


  1. Very High Development
  2. High Development
  3. Medium Development
  4. Low Development
Kinachopimwa katika maendeleo ya nchi kabla haijawekwa katika kundi husika kati ya hayo manne hapo juu ni outcome ya ukuaji wa kasi wa uchumi – GDP growth rate kwenye Maendeleo ya Jamii - life expectancy, literacy, educational outcome, and standard of living. Kama tulivyokwisha ona, Tanzania daima imekuwa katika nafasi ya 150 kati ya nchi 187. Lakini kujibu hoja za wafitini wa Mwalimu kwamba tungekuwa mbali bila Ujamaa, kwanini basi hata zile nchi zilizoamua kufuata soko huria hazijatuacha kimaendelea? Mfano:


  1. Very High Development
Hakuna nchi kutoka Africa.
  1. High Development
Libya pekee - Hii ni nchi yenye wananchi walioendelea kimaisha kuliko taifa lolote Afrika.!
  1. Medium Development
Nchi 7 tu za Africa zipo kwenye ligi hii: South Africa, Namibia, Botswana, Morocco, Gabon, Egypt, Algeria,
  1. Low Development
Kenya, Tanzania, Nigeria, Cameroon, Uganda, Zambia, Angola, Cameroon, Rwanda, Ivory Coast, Sudan, Malawi, Burundi, na nyingine nyingi za Africa. Pamoja na Nigeria kufuata soko huru miaka yote tangia uhuru, na kuwa nchi ya 7 duniani kwa kuzalisha mafuta, Tanzania ipo juu ya Nigeria kimaendeleo kufuatana na HDI indicators.

Ndugu zetu mnaomkejeli Mwalimu, hoja zenu kwamba Ujamaa umetupotezea muda, Je wenzetu hapo juu wameutumiaje muda huo? Je, hii haitoshi kuwaonyesha kwamba kuna mdudu hapa ambae ni common kwetu sote ambae anatufana, bila ya kujali Ujamaa au Soko Huru? Ndio maana Mwalimu anabakia kuwa Rais Bora wa Tanzania mbali ya kuwa baba wa taifa kwa sababu alithubutu kujaribu geuza madudu haya, kwa kulipa taifa letu a self determination chini ya Ujamaa na Kujitegemea. Kilichomshinda Mwalimu ni uchanga wan chi kuweza kuzalisha kwa wingi na wakati huo huo kutimiza ahadi za uhuru – ajira kwa wote, huduma bora kwa wote. Angalau alishindwa lakini hakuwasaliti na ahadi zake za wakati wa uhuru. Mbali ya hili na pia utekelezaji mbaya wa sera, sababu za kushindwa pia ni kutokana na unduminakwili wa baadhi ya watendaji wake ambao walikuwa wanashirikiana na mabepari wa nje, na hatimaye kumshinda nguvu. Nyerere bado ni Rais bora kutokana na ukweli kwamba alishindwa kwa sababu za maadui (ukiachilia utekelezaji mbovu wa sera); Bado Nyerere ni Rais bora kwani hata nchi za nje zilimpa heshima ya kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kusini – South Commision, hata baada ya Ujamaa kushindwa, kwa kutambua kwamba ana uwezo wa kuziletea nchi zote maskini mwongozo wa jinsi gani ya kupambana na mfumo wa uchumi wa kimataifa usio wa haki.

Waziri Mkuu wa Zamani wa Malaysia wa Dr. Mahatir Bin Mohamad,ambae hata wafitini wa Mwalimu wanamwona ni mmoja wa viongozi bora aliyepata kutokea katika nchi za Kusini (mimi nikiwa mmoja wa anaekubaliana na hilo), ndiye aliewashawishi wenzake kuunda Tume Ya Kusini, na baadae wote kwa pamoja kumchagua Nyerere kuwa Mwenyekiti wa Kwanza bila kupingwa. Nchi wanachama walikuwa ni pamoja na: India, Egypt, Kuwait, Phillipines, Msumbiji, Brazil, Sri Lanka, India, Zimbabwe, Jamaica, Mexico, Nigeria, Venezuela, Pakistan, Senegal, Malaysia, Samoa, Indonesia, na Algeria. Nia ya kuja na umoja huu ilikuwa ufahamu kwamba muundo wa kimataifa wa uchumi sio wa haki na ndio sababu ya umaskini, Kwahiyo umoja wa ungewapa nguvu, kwani hata wakubwa wana umoja wa kupitia G8 na OECD; ni humu ndipo WorldBank, IMF, na WTO wanaelekezwa jinsi ya kuendeleza ukoloni mamboleo katika nchi maskini. South Commission ilifanikiwa sana kuyafanya mataifa makubwa yaanze kusamehe madeni kwa nchi maskini na vilevile kuwalegezea masharti ya biashara.

Lincoln wa Tanzania atatokana na kazi ya kuyaendeleza haya. Kwa Tanzania, awali Mwalimu alianza na Ujamaa na Kujitegemea. Vinginevyo tabia ya wanasiasa kuwaadaa wananchi kwamba tupo imara na uchumi wetu unakuwa kwa kasi ya wastani wa aslimia 7 kwa mwaka tangia mwaka 2000 hazimsaidii maskini wa kijijini. Uchumi huu ni wa wachache, ni uchumi wa kufukua Dhahabu bila faida yoyote kwa wakulima, kwani asilimia 70 ya watanzania wanaduwa kuona magorofa ya mavioo, ambayo hawajawahi kuingia na hawathubutu kusogelea kwani wakiingia wanaweza onekana vibaka kutokana na mavazi na miili yao duni; wanaduwaa kusikia siku hizi kila mtu ana TV wakati asilimia 85 hawajui umeme ni nini; wanaduwaa kuona wingi wa bidhaa madukani ambao haupo sambamba na wingi wa fedha mifukoni mwao. Zote hizi ni changamoto kwa Marais wetu kwani haya yakigeuzwa, tutampata Abraham Lincoln Wa Tanzania.

Vinginevyo, Wafitini wa Mwalimu, nafasi ya George Washington wa Tanzania imeshajaa, na vilevile bado hakuna anaetosha katika nafasi ya Abraham Lincoln, Chisano, Mao, Castro wa Tanzania kwa tarehe ya leo: 14/12/2011. Vinginevyo mpaka wakati huo uwadie, tuache kumkejeli Baba wa Taifa na Rais bora kuliko wote wa Tanzania, badala yake tumtafute Lincoln Watanzania, Kwani hilo inawezekana.

Mungu amrehemu Baba Wetu wa Taifa, Mwalimu Julius Kambaraga Nyerere.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
hakika wewe ni great thinker!
sasa ngoja tusubiri mitazamo ya kina FF,RITZ,MS,REJAO ili tujue nao wana maoni gani
 
Watanzania wachache wanaombeza baba wa Taifa wajue kuwa wao sio kila kitu. Tuko tunaothamini mchango wake tena kwa data kama ulivyomwaga hapo juu. Vile vile hata mawe iko siku yatasema!
 
Kiukweli naweza kusema Nyerere siyo kila kitu kwani na yeye alikuwa na mapungufu yake na wanaombeza ni wana ccm walio kubuhu kwa rushwa!!!kama unataka kumaliza hii hali inatakiwa misingi ya kumabdu Nyerere ianzie oale ccm mtaacha kumbeza siyo kumbeza kwa maneno ila wanambeza kwa vitendo nikiwa na maana yale aliyoyaacha ccm imeshindwa kuyatekeleza na walakuyaendeleza leo hii mnasema mnunue mitumba??kwa ajili yakuendeleza Taifa??kama ni hivyo basi wakina mataka waachiwe huru kwa kosa lao lakununua magari ya yaliyotumika na kuyatumia kama asset za ATCL!!CCM wezi na hawataki kusikia neno Nyerere tusidanganyane hapa!!!
 
Hivi kama patrice Lumbumba angechukua nchi na kuweka misingi ya kikomunisti nchini Zaire, kweli Lwambo na Lipua Lipua wangetamba barani africa?SI unajua wakomunistoi huondoa hati miliki za wanamuziki nakuwadhoofisha wanamuziki? Je zaire ingecheza world cup 1974 na kuchukua AFCON mwaka huo huo? Tazama nchi za kikomunisti zilivyo dolola kisoka mara baada ya kuuingiza ukomunisti nchini mwao. Ulaya mashariki yote, hamna hata nchi moja inayoweza kuifunga Ivory Cost, Ghana, Cameroon na Zambia.

Wazaire walijua kabisaa tokea zamani kuwa ukomunisti ni Unyama. Hivyo walimchinja Lumumba na kumtia mwili wake katika pipa la acid ayeyuke mpaka mifupa. halafu mpaka leo kaburi lake halijaonekana. Hapo waliwakomboa sana watu wenye vipaji vyao na kuajilika navyo kama vile kina Lwambo, DR Nico, Verkyis, Josky Kiambukuta, shaba kahamba na wengine wengi.

Nchi kama guine, ilikuwa taifa bora kwa soka hapa africa. Lakini mara baada ya kuingiza ukomunisti tuu, klabu yake ya Hafia iliyowahi kutwaa ubingwa wa africa mara nne iliporomoka vibaya sana. Soka la guine likafa na kukabakia makwaya na magwaride tuu.

Halafu lazima ukumbuke kuwa ukomunisti hapa africa, umeuwa watu wengi sana kuliko vita vya uhuru. Tazama walivyouana Angola, Msumbiji, Congo Brazavile na Ethiopia. ni ukweli kabisaa kuwa , shetani alitaka kuitawala dunia kwa kupitia sera za kinyama za kikomunisti. wazaire usiwalaumu kwa kumyonga Lumumba, hakuwa na tofauti na kina Boris Pugo-wa Urussi.

sasa hivi zaire ni taifa la tatu duniani , kwa kupeleka viaja wake kucheza soka la kulipwa ulaya mashariki na magharibi mpaka bara la america. Ya kwanza ni Brazil, na ya pili ni algentina.

Ukomunisti haujui kabisaa kulea vijana . Huwatumia viajan kuimba kwaya, kucheza gwaride na kuwapeleka mashambani kulima.
 
Ndo ninachowapendea watz sasa hivi tuko bega kwa bega kwa propaganda zinatengenezwa kila siku. Mwaka huu ni "kolikoli" na idara ya Tambwe Hiza tutabanana mpk kieleweke. Sasa hivi kila mmoja anajua wajibu wake kwa nchi yake. Elimu ya uraia hoyee! Cdm hoyee.
 
hakika wewe ni great thinker!
sasa ngoja tusubiri mitazamo ya kina FF,RITZ,MS,REJAO ili tujue nao wana maoni gani
Unachafua sredi kwa kutaja taja watu. Ungetoa maoni yako, na kama wao wana yao wangekuja nayo hapa.
 
Mchambuzi; salute! I don't get emotional easily this one just moved me. I thought tumebakia wachache sana wenye heshima isiyotisikwa kwa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere. Its a classic piece of such an intellectual caliber, thought-provoking, and jaw-dropping proposition. Tatizo ni kuwa vita dhidi ya Nyerere inaendeshwa kwa makusudi na makusudi ni kuhalalisha uhalifu na ufisadi unaofanywa sasa hivi. Wao wanaamini Nyerere anasimama kama Mleta mashtaka dhidi yao na njia pekee ni kujaribu kumdestroy Nyerere and his legacy.
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.

hayo ni mawazo yako na wenzio wachache. Na si ya dini yako uwe mkweli.
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Tayari anaitwa hivo na historia ya Taifa hili inalikubali. Hata hivyo anayo majina mengine mazuri tu. Unachagua umuiteje ili kichwa kisikuwange. Muite Mwalimu, Kambarage, Julius au hata Nyerre sio Nyerere kwa kuwa jina hilo kwa Kizanaki halipo.
 
Deep down my heart I know there is no human being with ability to meddle with the truth. Nyerere, whether we like or not, is on different political sphere.
Na waswahili husema, wa mbili havai moja....ngoja tuone kama usemi huu wa wahenga hauna maana tena....the game is over....leo kubadilisha mambo ni ngumu!!!
Nyerere stands alone as the single most effect leader so far in this country. Wenye wivu wajinyonge. Kuna watu hapa baada ya kumaliza madaraka watatafuta pa kuingilia, maana madudu waliyoyatengeneza yatawaandama kama nyuki wenye hasira, ambao hata ukijitupa ndani ya maji marefu, wao huwa wanakaa nje wakisubiri uchomoze kichwa chako kutafuta hewa. Time will tell!!!
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
hapo sasa.....kwa hiyo hata Baba faizah ni mkatoliki?
 
Mimi uwa nawashangaa watu wanaomzungumzia mwalimu Nyerere kwa mabaya..ni kweli alikuwa na mapungufu tena makubwa,lakini alifanya makubwa sana kwa nchi hii....alikuwa tayari kufa kwa Taifa hili.
 
Hivi kama patrice Lumbumba angechukua nchi na kuweka misingi ya kikomunisti nchini Zaire, kweli Lwambo na Lipua Lipua wangetamba barani africa?SI unajua wakomunistoi huondoa hati miliki za wanamuziki nakuwadhoofisha wanamuziki? Je zaire ingecheza world cup 1974 na kuchukua AFCON mwaka huo huo? Tazama nchi za kikomunisti zilivyo dolola kisoka mara baada ya kuuingiza ukomunisti nchini mwao. Ulaya mashariki yote, hamna hata nchi moja inayoweza kuifunga Ivory Cost, Ghana, Cameroon na Zambia.

Wazaire walijua kabisaa tokea zamani kuwa ukomunisti ni Unyama. Hivyo walimchinja Lumumba na kumtia mwili wake katika pipa la acid ayeyuke mpaka mifupa. halafu mpaka leo kaburi lake halijaonekana. Hapo waliwakomboa sana watu wenye vipaji vyao na kuajilika navyo kama vile kina Lwambo, DR Nico, Verkyis, Josky Kiambukuta, shaba kahamba na wengine wengi.

Nchi kama guine, ilikuwa taifa bora kwa soka hapa africa. Lakini mara baada ya kuingiza ukomunisti tuu, klabu yake ya Hafia iliyowahi kutwaa ubingwa wa africa mara nne iliporomoka vibaya sana. Soka la guine likafa na kukabakia makwaya na magwaride tuu.

Halafu lazima ukumbuke kuwa ukomunisti hapa africa, umeuwa watu wengi sana kuliko vita vya uhuru. Tazama walivyouana Angola, Msumbiji, Congo Brazavile na Ethiopia. ni ukweli kabisaa kuwa , shetani alitaka kuitawala dunia kwa kupitia sera za kinyama za kikomunisti. wazaire usiwalaumu kwa kumyonga Lumumba, hakuwa na tofauti na kina Boris Pugo-wa Urussi.

sasa hivi zaire ni taifa la tatu duniani , kwa kupeleka viaja wake kucheza soka la kulipwa ulaya mashariki na magharibi mpaka bara la america. Ya kwanza ni Brazil, na ya pili ni algentina.

Ukomunisti haujui kabisaa kulea vijana . Huwatumia viajan kuimba kwaya, kucheza gwaride na kuwapeleka mashambani kulima.

Na zaire (DRC) hiyo hiyo kwa miaka mingi, na hata 2011, ni nchi ya 187 kati ya nchi 187 (ya mwisho duniani) kimaendeleo in kwa vigezo vya UNDP Human Development Index life expectancy, educational outcome, literacy rate, and quality of life, ingawa ni nchi ya kumi kati ya nchi 187 duniani kwa impressive GDP growth rate 9.1% per annum, (GDP ya kufukua na kupeleka madini nje); Hodi Hodi Tanzania, hayo yaja;
 
Mchambuzi; salute! I don't get emotional easily this one just moved me. I thought tumebakia wachache sana wenye heshima isiyotisikwa kwa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere. Its a classic piece of such an intellectual caliber, thought-provoking, and jaw-dropping proposition. Tatizo ni kuwa vita dhidi ya Nyerere inaendeshwa kwa makusudi na makusudi ni kuhalalisha uhalifu na ufisadi unaofanywa sasa hivi. Wao wanaamini Nyerere anasimama kama Mleta mashtaka dhidi yao na njia pekee ni kujaribu kumdestroy Nyerere and his legacy.
Katika watu wanaopata taabu kumwita Mwalimu Baba wa Taifa ni JK. Inasemekana huwa analitamka hilo jina kwenye hotuba anazoandikiwa tu au kiajaliajali! Sielewi ni kwa nini. Hata ile orodha yake ya watu 17 juzi pale uwanja wa Uhuru ni katika kutaka kuwaambia watu kuwa "avumae baharini ni papa, kumbe na wengine wapo!" Nawahurumia sana watu wanaojaribu kupambana na HISTORIA au kujaribu kuiandika upya.
 
Back
Top Bottom