Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,410
- 31,395
Na mfano kama huu ndio wengi mnakosea sana sana. Yaani una pick up siku moja au mwaka mmoja na unaacha miaka 20.Huwezi kusifia utawala wa Nyerere wakati vitu vidogo vidogo vya matumizi ya binadamu vilikuwa hakuna..
Wakati wa Nyerere watu tulikosa sabauni za kuongea na kufuria, dawa za meno, vyakula vibovu binadamu wanapewa..
Maduka ya ushirika unapangiwa vitu vya kununua unapewa maharage mabovu pamoja na magadi kwa ajili ya kuivisha wakati unayapika..
Unalazimishwa ununue vitu ambavyo utaki, lazima ununue panga, tube za baiskeli, sigara aina mbili Zakuchuja na Zaraha, mkuki, jembe, spoku za baiskeli za Swala..
Watu wanakwenda shule bila viatu, ukitaka radio mpaka ukanunue RTC..
Ukikutwa na dola 50 utajuta ukiweka akiba ndani ya chakula unaitwa muhujumu uchumi...ukitaka kupiga simu mpaka uende posta upange foleni..
Tumekula chakula cha farasi wa Texas, mahindi ya njano..
Watu walikuwa wanatembea nguo zimetoboka kwenye makalio, viraka kila sehemu..
Ngoja kwanza niishie apa kwanza...
Wakati wewe unasema hayo mwingine aliyeishi nyakati za mwalimu haswa na si kusimuliwa atasema hivi
1. Alikuwa tunakwenda shule bila ada na huko tunapewa vitabu na madaftari
2. Alikuwa tunasafiri kwenda shule kwa warrant na kama haukuchukuliwa akifika shule anadai nauli yake na inarudishwa.
3. Atakwambia mfanyakazi alikuwa anapewa warrant ya usafiri wa yeye na familia yake popote nchini kwa gharama yoyote
4 Atakwambia ukiumwa unaenda hospitali mambo yote unawaachia wao kuanzia vipimo hadi dawa
5. Atakwambia kama mlikuwa mahindi ya Texas, siku hizi mnakula kuku zilziooza kutoka South Africa na si kila mmoja ana afford
6 Zamani ulikuwa ukimaliza shule unapata ajira, ahh hayo ni mambo ya Nyerere na ujamaa. Siku hizi mambo safi unamaliza shule unatafuta bahasha za khaki 100 unaweka CV unaanza kuzunguka mtaani hadi soli iishe. Si tuna viatu bwana na si kama zamani!!
7. Atakwambia kutembea na dola 50 ilikuwa kosa lakini hiyo sh 10 ilikuwa inanua unga, sabuni, sukari na kitoweo.
Je sasa hivi kuna wangapi wana dola 1 mfukoni. Kama mtu hawezi kununua dozi ya peniciline ya sh 1200 yaani senti 90 dollar inamsaidia nini kumruhusu atembee na dola 2000. Huoni hapa ni akina fisadi wanaopaswa kushangilia na si Kibambara, Ng'onda au Zainabu.
8. Ukitaka radio lazima uende RTC, sasa siku hizi unapata kutoka china kesho unatupa. Tulikuwa na Matshusita iliyokuwa inatoa ajira na bidhaa bora sana , siku hizi ni faster faster unanunua sub standard haraka bila kwenda RTC. Hebu rejea post ya Mkandara hapo juu
Watu waangalie mambo in broad spectrum na si kutafuta kitu kimoja na kukifanya kama ndio mada. Mwaka 1974 kulikuwa na njaa kali sana iliyotokana na ukame. Sijui hapa mwalimu alaumiwe nini na ujamaa ulaumiwe vipi. Mbona nchi zote zinakumbwa na njaa kama tunavyoona Somalia na Kenya kwasasa. Mwaka 2006 watu wamekufa kwa kula ming'oko kule Rufiji, hapo je!
Ukiangalia kazi ya mwalimu kwa sabuni, tv na internet utapata shida kweli kumwelewa. Ukiangalia kazi ya mwalimu in terms of vision, execution and long term sustainable projects unaweza kukosa cha kumsumanga hata kwa bahati mbya tu.