Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Ji habari reeeefu halisomeki, wala sina muda wa kulisoma, kwa kifupi:

Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga

Niliposema kwenye thread moja kuwa huyu mwanamke ana "pepo jeshi" wengine walinibeza na kusema nina matatizo yangu...kauli kama hii,ikitoka kwa mtanzania ni kama kuwatukana watanzania...Huyu sio mtanzania ni kikundi cha Al-shabaab aliyeajiriwa na magamba kupinga mema ya watu makini kama Nyerere...kama unapinga kuwa Nyerere hakuwa kiongozi makini,haya nipe hao viongozi wako...au unataka kuwaleta viongozi wako wa BAKWATA? Huyu mwanamke anapepo wakuu...na kama tusipochukua hatua kumkabili ataleta maafa makubwa kwa mume wake na familia yake...nimepata taarifa kuwa ni mwanachama wa Al-shaabab na anampango mkubwa sana huyu..........
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Kwa hiyo Yat -Sen wa China, Carlos Cespedes wa Cuba na Mahatma Ghandi wa India wote wameitwa mama Baba wa Taifa kwa ajili ya Ukatoliki?
Chuki ya kidini ikikukaa sana moyoni hugeuka sumu na kukutafuna mwenyewe ndani kwa ndani kama mtu aliyekunywa acid.
Kwa kiwango chako cha uelewa FF hungeweza kushindwa kuliona hili ila udini umekutia upofu na unakumaliza kidogokidogo maana ni sumu hiyo bibie!
 
Mchambuzi!
Naunga mkono hoja ila next time jaribu kufupisha hii ni ndeefu sana!

Wasi wasi wangu ni kwamba umeunga hoja mkono pasipo kuisoma, na kama umeisoma basi utakuwa umeishia kwenye para ya kwanza. Jitahidi kuisoma hadi mwisho ili uone hoja za mchambuzi, zimekaa kisomi sana.

Hata hivyo mchambuzi alianza kwa kututaka tuwe wavumilivu lakini naona wewe uzalendo umekushinda.

Back to the topic, ninachoweza kusema ni kimoja tu mkuu, kama kuna watu ama mtu alikuwa anabebwa na mafuriko ya kumkejeli ama kumkashifu Nyerere akilisoma hili andiko with open mind atajifunza vitu vingi na hawezi kubaki kwenye msimamo wa kumbeza mwalimu.
Lakini kwakuwa kuna watu wako kazini kumchafua mwalimu ili kujaribu kuficha madhaifu yao, usishangae watazidi kushupaza shingo zao.
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.

Ninachopenda ni kuwa HUKUBALIANI ila kila sehemu na kwenye maofisi hata biashara yako (kama ni kubwa) PICHA yake iliyoandikwa baba wa Taifa ipo.

Mchambuzi,

Mie sina tatizo na Ubaba wa Taifa na nadhani ni wachache tena wadini kama huyo hapo juu ndo wana matatizo.

Naomba andaa article nyingine ya UTENDAJI wake kazi, zingatia pamoja na mengine yafuatayo:

- Kutowajibisha watumishi wabadhirifu na kuwahamishia pengine (mifano ipo mengi sana, ukiharibu NMC unaenda BIT ukiharibu unaenda BET au ATC)

- Kuunganisha CHAMA na mashirika ya umma na serikali hivyo kuweka vyeo mara mbili mbili kwenye kuendesha UCHUMI na Biashara.

- Kutotaka kupingwa, Mtei, Kambona etc na ukimpinga labda uhame nchi au Kizuizini (kuwa Dicteta) na baada ya miaka 25 ya kukataa mawazo anagundua yeye ndo alikuwa wrong.

- Kuweka Usalama wa Taifa wenye nguvu sana na kuchunguza mpaka unywaji wa bia wa mtu (misuse of public funds) YET, NARUDIA YET kutowatambua akina BWM na wenzake kuwa sio vijana wake (hawafuati itikadi yake).

- Kuweka Vijiji vya Ujamaa (1972?)(kurudisha watu nyuma kimaendeleo), angalia uchagani hamna vijiji na angalia wapo wapi kimajengo etc.

- Azimio la Arusha.

- Vita vya Kagera ambavyo vimeirudisha taifa nyuma kiuchumi mpaka tukawa tunapanga foleni ya unga wa YANGA, wakati essence ni kumweka rafiki yake madarakani. Kutumia resources za taifa.

-Kupenda kukwezwa kama kiongozi, akienda sehemu shughuli za kiuchumi zinasimama kwa hata siku nzima akiimbwa na kutukuzwa kama miungu na wananchi na wanafunzi. (A smart leader cannot do this)

Sio kwamba hakuna mazuri aliyofanya. LA HASHA. Ila kama kiongozi alikuwa dhaifu sana, hakuwa visionary leader, hakuwa flexible wala dynamic.

Kwa leo tuachie hapo. NASUBIRI majibu/uchambuzi
 
hakika wewe ni great thinker!
sasa ngoja tusubiri mitazamo ya kina FF,RITZ,MS,REJAO ili tujue nao wana maoni gani

Mkuu hao ni ze-uaharo funs.......hawawezi kuchangia threads makini kama hii,watachafua tu thrads...
 
Mimi uwa nawashangaa watu wanaomzungumzia mwalimu Nyerere kwa mabaya..ni kweli alikuwa na mapungufu tena makubwa,lakini alifanya makubwa sana kwa nchi hii....alikuwa tayari kufa kwa Taifa hili.
Ukichunguza sana na kwa makini,wanaombeza na kusambaza chuki kwa Hayati baba wa Taifa hapa JF ni wale wapenzi wakubwa na watetezi wa CCM na utawala wa Awamu ya nne. Tujiulize kwa nini ni hivyo?
Lazima iko namna au ni mkakati maalum ambao haukuanzia JF ila una baraka toka juu.
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.

Dada Faiza,
Mtazamo wako ni dhahiri unasukumwa na imani ya dini, wenye kuishi (angalau kimawazo) katika taifa lenye dini moja, lisilowapa wenye imani nyingine haki na fursa sawa kisiasa, kiuchumi, na kijamii, huku suala la jinsia ya kike katika mazingira hayo likipewa nafasi jikoni, chumbanii na sebuleni peke yake. Pili, hoja zako zipo informed zaidi na experience ya mataifa ya kifalme za kiarabu ambapo watawala hukaa kwa maisha yote, na wakifa wanawarithishwa watoto wao. Kwa mtazamo uliokuwa informed namna hii, mjadala wa baba wa taifa ambao kiini chake ni ukombozi wa taifa kutoka katika makucha ya udini, ukabila, na rangi, ili kuunda taifa kwa njia ya kidemokrasia, taifa lisilo na dini kikatiba, mjadala wa namna hiyo utakuchanganya tu dada yangu Faiza Foxy.

Swali juu ya ridhaa ya nani ilimpa mwalimu heshima ya baba wa taifa, inaonekana haujasoma makala yangu vizuri - hiyo ni heshima kwa mujibu wa katiba inayopitishwa na bunge la nchi husika, kwani hicho ndicho chombo cha kuwakilisha maoni, hisia, na mtazamo wa wengi. Jina la Nyerere /heshima kama baba wa taifa lilipitishwa kwa asilimia mia na wabunge wa dini zote Tanzania.

Vinginevyo fanya utafiti kwenye google juu ya maana ya baba wa taifa; inawezekana unadhania ni utunzi wa wakatoliki kwa sababu unaitafuta kwenye google kama "baba wa taifa" na kutorudisha majibu ya maana; google "father of the nation", na upesi utabaini kwamba hiyo ni heshima ya kidunia bila kujali kama taifa ni la kikomunisti au kibepari, kinachoangaliwa hapo ni taifa lililozaliwa kwa njia ya mapinduzi yaliyotokana na kiu ya watu wa dini, rangi, na makabila mbalimbali kutaka kuondoa tofuuti zao na kujitawala kwa njia ya ki demokrasia, inayotoa fursa na haki sawa kwa watu wa dini, rangi, na makabila mbalimbali, ndani ya taifa moja;
 
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.

PELEKA HUO UDINI KWA MAMA AKO! bila nyerere vilevile BABA yako asingesoma bure...,Tanzania haikuwa nnchi ya Kiislamu kama unavyotaka kupotosha! Mbona alivyokuwa Hai Hamkusema huo UHARO wenu! Paka amekufa ndio mnajifanya Mnajua Kuongea sana! WANAFIKI WAKUBWA NYIE
 
Ji habari reeeefu halisomeki, wala sina muda wa kulisoma, kwa kifupi:

Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.

Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?

Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga

Ha ha haaa, hii kali ya leo.

Kama habari ni ndefu na hujaisoma, umejuaje kwamba Nyerere katajwa kama baba wa taifa?

Ujumbe umekufikia, na wewe waambie wenzako waje kupata ujumbe hapa.

Kazi nzuri mchambuzi.
 
Wasi wasi wangu ni kwamba umeunga hoja mkono pasipo kuisoma, na kama umeisoma basi utakuwa umeishia kwenye para ya kwanza. Jitahidi kuisoma hadi mwisho ili uone hoja za mchambuzi, zimekaa kisomi sana.

Hata hivyo mchambuzi alianza kwa kututaka tuwe wavumilivu lakini naona wewe uzalendo umekushinda.

Back to the topic, ninachoweza kusema ni kimoja tu mkuu, kama kuna watu ama mtu alikuwa anabebwa na mafuriko ya kumkejeli ama kumkashifu Nyerere akilisoma hili andiko with open mind atajifunza vitu vingi na hawezi kubaki kwenye msimamo wa kumbeza mwalimu.
Lakini kwakuwa kuna watu wako kazini kumchafua mwalimu ili kujaribu kuficha madhaifu yao, usishangae watazidi kushupaza shingo zao.

MKUU,

Nadhani article inaongelea UBABA WA TAIFA wa Mwalimu JKN. Kama ni kujadili (nakanusha kuhusu kutumia neno kebehi) kuhusu utendaji wake kuna mapungufu mengi sana tu. Machache nimeyaweka hapo juu. Naomba yajadili.
 
Kuna mtu aliwahi kusema JK hamuiti mwalimu BABA WA TAIFA. Kuna kaukweli? (of coz sioni kosa kama hamuiti hivyo)
 
Kuna mtu aliwahi kusema JK hamuiti mwalimu BABA WA TAIFA. Kuna kaukweli? (of coz sioni kosa kama hamuiti hivyo)

Hilo nimepata kulisikia pia toka kwa mwana ubalozi wetu mmoja.

Mimi nadhani kuna tatizo la binafsi zaidi kuliko kiuongozi kwa yeye kufanya hivyo.
Na hoja za kuhoji ubaba wa taifa wa Nyerere zimekuwepo kipindi cha Dr. JK kuliko wakati wowote.
Kiongozi wa nchi ni mhamisishaji namba moja ktk yale anayoyaamini....... 2006 Dr. JK aliipa support sana Taifa Stars na kwa mshangao wa wengi tulijikuta mahaba kwa timu yetu ama taifa letu yameongezeka. Tukavaa jezi, skafu na vilemba venye rangi ya bendera yetu.

Vivyo hivyo kwa vile Dr. JK haoni kwa nini Nyerere aitwe baba wa taifa sumu hiyo inamwagikia kwa baadhi yetu pia. Ktk hao wanaoitwa wafitini na Mchambuzi (mtoa hoja) nashawishika kuamini Dr. JK ni mmoja wao.

Nyerere kama binadamu ama kiongozi alikuwa na madhaifu mengi tu, lakini pia kipindi walichoongoza wao kilikuwa kigumu zaidi.
Kwa kung'ang'ania serikali mbili (kuua ya Tanganyika) kwangu mimi Nyerere alifeli LAKINI hilo na jingine lolote haliondoi heshima yake ya Baba wa Taifa.

Nyerere, a man and a leader!
 
Wahenga walishawahi kunena ''SHUKRANI ZA PUNDA SIKU ZOTE NI MATEKE''
''FANYA WEMA NENDA ZAKO USINGOJE SHUKRANI''

Hayati Baba wa Taifa JULIUS K.NYERERE siku zote ataendelea kukumbukwa Kama Baba wa Taifa Bora Tanzania na Hata Kiongozi Bora Afrika
Kutokana na Misingi Imara,Uadilifu na Kuweka Nnchi Katika Umoja,Amani,Ushikamano na Upendo!
Hivi leo TANZANIA ndio nchi pekee ambayo hakuna Ukabila,Watu wanaishi kwa Amani bila Ubaguzi Na hata Udini Tanzania Hakuna ila Kuna Kikundi cha watu WANAONZA KUPANDIKIZA MBEGU ZA UDINI amnao wanapata ufadhili kutoka nnje kutuharibia Amani Yetu Watanzania..,Amani ambayo Baba wa Taifa aliipigania...leo hii kikundi cha watu wachache wanataka kuharibu misingi ambayo baba wa taifa aliijenga kwa miaka 24 katika utawala wake

Kama Nyerere Angekuwa Raisi Mbovu basi

+Hata ile vita ya Kagera Tungeshindwa...,mimi naamini Ushupavu wa Raisi ni uimara wa kusimamia matatizo na majanga ya Kimataifa kama vita,njaa na matatizo mengine! hivi leo umeme tu unaihenyesha serikali..,tafakari
+Tanzania Kusingekuwa na Umoja wa Makabila zaidi 150,,.nnchi Kama kenya leo hii ni tatizo kubwa..,rwanda wenzetu walichinjana
+Kusingekuwa na Umoja kati ya Wakristo na Waislamu...Hivi leo Nigeria hawa kuwa na Bahati ya Kupata Kiongozi aliweza

kuunganisha umoja kati ya wakristo na waislamu paka leo ni Kiama kwao
Mimi naamini kama Nyerere angekuwa kiongozi mbovu hata jeshi lingempindua kama Nkurumah,Azikiwe,obote kwani ukiangaliia kiini cha mapinduzi mengi ya afrika tatizo kubwa ilikuwa ni umaskini pamoja na utwala mbovu na w a upendelo..,ila kutokana utawala imara! Nyerere aliweza kusimama thabiti..

Kama nyerere angekuwa mdini basi asingeziamuru seminari kuwa shule za serikali,au ahata hospitali kuwa za serikali,...au hata asingewateua akina Rashid Kawawa,Salim A.Salim kuwa viongozi..,aliweka kila kitu kwa usawa...,tatizo wenzetu waislamu waliathiriwa na tatizo la wakoloni ambao hawakuwezesha sana huduma za jamii pamoja na elimu katika maeneo wanaotoka kama Mtwara,Lindi na Tabora!

Na kama Nyerere Angekuwa mdini na Hata Muungano na Zanzibar asingekubali...,
Jamani sitaki kuongea mengi sana! Ila Wanaompinga Nyerere wanaajenda yao YA KUTUVURUGA SISI WATANZANIA WANATAKA KUANZISHA AL SHABAAB YAO AU BOKO HARAM ILI WATIMIZE HAJA ZAO! na vilevile ni wanafiki kwanini hawakuwasilisha hoja zao wakati yupo hai...,TAFAKARI
 
A Master piece...of Master class!!
God bless you Mchambuzi! Laiti Mungu angetupa Mawazo Huru,..Uelewa wazi...Upendo wa Kweli na Kuipenda Kweli...Laiti pia Mungu angetuondolea UVIVU wa KUSOMA makala ndefu kidogo...

Ningekua mod,ningeistikisha hii sredi.

Tutafika tuu!:poa
 
FP,

Mwalimu alikuwa na mapungufu yake. Mengine aliyakiri hadharani mara kadhaa na pale ilipowezekana aliyarekebisha tafauti na viongozi wa sasa ambao kukiri wamekosea ni nadra sana na mara nyingi wanapasiana makosa kama wacheza mpira. Chukua mfano wa Richmond ambao nafahamu unamgusa mmoja wa watu wako wa karibu.

Hili la kuhamisha wabadhirifu sio kweli. Mwalimu alichukia sana vitendo hivi kwa kauli na matendo. Akina Mzee Mwapachu kuhama toka shirika moja kwenda jingine haikuwa sababu ya ubadhirifu. Kumbuka pia idadi ya wasomi na managers tuliokuwa nao wakati ule ilivyokuwa ndogo.

Hili la kuweka makada wa CHAMA kwenye taasisi za UMMA liliamriwa na vikao vya TANU/CCM. Linaweza kuwa halikuhitajika lakini lilimzuia nani kufanya nini. Makada hawa walikuwepo hadi kwenye vyombo vya DOLA. Hii waliita chama kushika hatamu.

Mwalimu alipingwa na wengi tu. Mtei hakukimbilia nje. Alikwenda kwa baraka za Mwalimu. Kambona ni hadithi ndefu. Hata Kambona mwenyewe alipata taabu kulisemea hilo hadi anafariki.

Haya ya Usalama wa Taifa ni mapokeo tu. Tulipokezana wenyewe woga huu. Enzi hizo pesa ya kunywa pombe mtumishi wa kawaida wa UMMA haikuwepo. Wizi, ubadhirifu, ufisadi ulikuwepo kwa viwango vidogo sana. Ulionekana wa ajabu kupitisha raundi ya bia kwenye meza ya watu watano! Sasa hivi kuna wizi uliohalalishwa kama posho, mafao, marupurupu,...

Vijiji vya Ujamaa vimetusaidia wengi kuziona shule na huduma nyingine za kijamii. Kilimanjaro wakati vijiji vinaanza ardhi ilishakwisha. Vjiji hivi sasa ndio miji midogo. Kulikuwa na mapungufu kwenye utekelezaji wa sera hii. Haya hayakuwa makubwa kiasi cha kuathiri manufaa ya vijiji hivi. Mikoa mingine watu hawakuwa tofauti na wanyama huko maporini.

Azimio la Arusha ndilo linalokosekana sasa tunateswa na UFISADI. Hakuna aliye madarakani analitaka hili. Jiulize ni kwa nini!

Vita ya Kagera haikuleta unga wa Yanga. Labda umri wako ni mdogo hauyafahamu haya. Pengine pia haufahamu kuwa Idd Amin aliichora upya mipaka ya Tanzania. Tulipata shida za kiuchumi na kijamii baada ya vita hii ni kweli. Idd Amin hakuwepo tangu wakati huo na Obote aliondoka tena mapema tu kenda kufia Zambia.

Mwalimu alikuwa mtu simple sana. Misafara yake mikoani hakuiratibu yeye. Mara nyingi aliikemea misafara hii mirefu. Shida ilikuwa ni kwa Watanzania wenyewe kutaka kumwona Mwalimu. Alikuwa na mvuto wa aina yake kwa Watanzania. Tv hazikuwepo kwamba tungemwona kwenye picha kila siku kama tunavyowaona viongozi wa sasa. Mwalimu alipendwa sana tu.
 
Mchambuzi; salute! I don't get emotional easily this one just moved me. I thought tumebakia wachache sana wenye heshima isiyotisikwa kwa Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere. Its a classic piece of such an intellectual caliber, thought-provoking, and jaw-dropping proposition. Tatizo ni kuwa vita dhidi ya Nyerere inaendeshwa kwa makusudi na makusudi ni kuhalalisha uhalifu na ufisadi unaofanywa sasa hivi. Wao wanaamini Nyerere anasimama kama Mleta mashtaka dhidi yao na njia pekee ni kujaribu kumdestroy Nyerere and his legacy.

Mwanakijiji kula mpunga wako utulie heshima ya Mwl. Nyerere itaendelea na idumu miaka yote, hao wapiga porojo wanapoteza muda wao watanzania wanamkumbuka Mwl. Nyerere kwa mapana na marefu.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Ndugu yangu!!!!wengi wetu humu jf hatukupata wasaa mzuri wa kuuona utawala wa Nyerere!!lakin yumkini kwamba malezi yetu yakijumuisha formal na informal education yametupatia wasaa mzuri wa kutafakari utawala wake!!!hoja yako hiyo ama kwa hakika ndio msingi wa wote wanaombeza!!!

ni Udini na Unafiki!!!na lazima tuwe wawazi!
! WAISLAMU NA BAADHI YA WANAFIKI WA KIKIRSTO ndo wanaompinga Nyerere!!! swali muhimu baada ya Nyerere ni yupi aliisaidia kidogo nchi hii!!!tuache unafiki tuwe wahalisia!!!
 
ETI BABA WA TAIFA !!!!!!!! kuna mijitu inapenda kutukuza mtu eti wanampa heshima huko aliko hana heshima hata kidogo heshima yake iliisha siku alipo pigiwa mizinga 12 baada ya hapo hana heshima tena na ndio maana wana sema watu wakatoe heshima zao za mwisho lakini kwa upande mwingine nisiwalaumu kwasababu hata yesu mulimpa heshima kuwa yeye ni mungu kwahiyo huu ni muendelezo
 
Pamoja na kazi yoooote ya uchambuzi alofanya Mchambuzi haya ndio majibu.

Sasa naelewa kwa nini walimu wetu wakati mwingine wanatembeza bakora.........
 
Back
Top Bottom