Nyerere Alijua Mapinduzi Yanakuja; Akaamua Kuachia Ngazi Mwenyewe

Haki

JF-Expert Member
Jan 14, 2009
356
17
Kila siku najiuliza kama Nyerere angekuwa "madarakani" mpaka sasa hivi angetolewa kama Gaddafi, Mubarak, Shah, or Zine el Abidine Ben Ali???

Naomba munisaidie wana JF
 
Saa ingine kama huna la maana kuchangia kwenye ukumbi huu wa great thinkers heri ukae kimya!
 
Kila siku najiuliza kama Nyerere angekuwa "madarakani" mpaka sasa hivi angetolewa kama Gaddafi, Mubarak, Shah, or Zine el Abidine Ben Ali???

Naomba munisaidie wana JF

Mwaka 1975, Mwalimu Nyerere aliwaeleza viongozi wa TANU kwamba ulikua ni muhula wake wa mwisho kama Rais wa JMT,na kwa hiyo waanze kutafuta mrithi wake. Kama siyo vita ya Nduli Idd Amin,mwaka 1980 tungepata rais mpya. Mwalimu alikua amefanya kazi kubwa kujenga taifa jipya. Mwili ulikua umechoka. Alitaka apumzike. Ukiona mtu anakaa madarakani miaka mingi,ujiulize kama kweli ni mchapa kazi ama ni mbangaizaji na mroho wa madaraka.
 
nyerere alikuwa dictator wa mawazo,anachotaka yeye ndo sawa.kumbuka zidumu fikra
alijua hawezi ongoza kukuwa na vyama vingi watu wangesema udhaifu wake hadharani.aliongoza kirahisi wakati haki za binadamu haziko ktk katiba.bill of rights ilowekwa kwenye katiba 1985
 
Mandela hakuacha madaraka kwa kupenda, ulikuwa ni mkataba ili atoke jela, kuwa kwanza kuwe na national reconcilliation na aongoze one term.
 
Mandela hakuacha madaraka kwa kupenda, ulikuwa ni mkataba ili atoke jela, kuwa kwanza kuwe na national reconcilliation na aongoze one term.

Mkuu, njoo na facts jamvini usije na meneno matupu, hivi unaujua msimamo wa Mandela wewe?

Ebu tuambie huo mkataba aliufanya na kina nani? Unadhani Mandela ana akili za kushikiwa kama viongozi wenu wa CCM?

Ameishakataa masharti mengi tu wakati yupo kifungoni ili awe huru..
 
Shah wa wapi aliyenyongwa?l

Mtakufa mkimchukia Nyerere na hamtafanikiwa katika matamanio yenu! lol
Kinyungu umesema umemaliza yote. Ni sawa na kutaka kulinganisha Yesu na Muhamad, hawatafanana hata ukirudi nyuma au kusogeza mbele miaka elfu kumi.
 
Nyerere aliacha madaraka mara mbili bila kulazimishwa na mtu mwingine; uliza leo kama kuna kiongozi anayeweza kuachia madaraka kirahisi hivi hivi.

na mzee wa watu alianza kunenepa na kugain afya baada ya kutoka madarakani,hakuwa na uroho wa madaraka hata kidogo
 
  • Thanks
Reactions: Ame
kama ungekuwa mfuatiliaji mzuri wa hotuba za Nyerere ungekuwa ushawahi kusikia moja ya hotuba zake wakati anaachia madaraka; alisema si vizuri na wala si busara kwa kiongozi kukaa muda mrefu madarakani hata kama unafanya mambo mema kwa wananchi kwa kuwa kwa silika za binadamu itafika wakati watakuchoka tu, si lazima kwa kutaka mabadiliko ya sera bali wanaweza wakawa wanataka sura mpya tu, hata kama sera au utendaji utafanana na kiongozi wanaemtaka atoke, kwa kuwa binadamu hawawezi kuamini kuwa ni wewe tu mwenye uwezo wa kuongoza miongoni mwa wananchi wote. Hivyo Nyerere alikuwa ni mtu aliyekuwa anaona mbali kama kawaida yake na alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Africa waliokaa madarakani muda mrefu waige mfano wake, waondoke madarakani kwa heshima huku wakiendelea kuenziwa na sio kuondolewa kwa aibu!
 
Nyerere aliacha madaraka mara mbili bila kulazimishwa na mtu mwingine; uliza leo kama kuna kiongozi anayeweza kuachia madaraka kirahisi hivi hivi.

Kila kitu kinataka utaalam kukijua sio kila mtu ana uwezo wa kufahamu haraka kwanini Mwl nyerere aliamua kung'atuka. Kwa wajuzi wa mambo wanaamin kua Nyerere kuadopt siasa ya ujamaa kulimfanya ajjikute ktk presure kubwa na nchi za capitalism ikiwemo US.

Itakumbukwa kua hata jaribio la kumpindua linalo julikana kwa jina la coup lilifanyika. Ushahidi ni kua jaribio hilo lilifanyika ktk nchi nyingine nyingi na sio Tanzania tu, kwa maana nyingine ilikua ni kama political design ya wakati ule kwahiyo kama angekataa kuondoka angeondolewa tu kama walivyoondolewa wengine.
 
lakini huoni kama yeye alitumia busara kuondoka madarakan hadi leo watu bado tunamheshimu na kumkumbuka?
 
Back
Top Bottom