Nyani Ngabu na Yo Yo enzi zao...

Status
Not open for further replies.
lol,
yo yo nimependa ki bag chake na malapa, hiyo suruali yake ni juu pima chini malizia kitambaa.

NN hiyo saa ndio anaturingishia au?..
 
Yaani, mmetachi my very soul kwa hizi picha.

Kama unakidate chako unasubiri siku ya mnada/soko, nao ulikuwa once per month
Unasugua ndala zako zinawaka, kanga yako ya njano, gauni vitambaa polyster au japan, umesuka tano kichwa
Kazi unafanya fasta ili uruhusiwe kwenda sokoni
Unakikuta kidate njiani, kama ni babu kubwa kina baskel swala au phonex
Kina radio ndogo almaarufu duduprufu, kimefungua BBC au dochiwele, full kingereza

Kinakupalift, mtazunguka siku nzima
Kinakupeleka for lunch
Ni chai na vitumbua, wakati mwingine vya unga wa mahindi, au maandazi
Matawi sana unanunuliwa soda na biskuti

Mnamalizia na desert lenu la maana la miwa
Na hiyo miwa haikatwi ni kila mtu wake mrefu
Ili msifike nyumbani mapema, mnarudu taratiibu huku yy anasukuma baskeli yake
Hizi mnazoitwa water and pillow fights, kwa enzi zetu ilikuwa ni anakunyangánya kanga
Sababu its a taboo kigori kutembea bila kanga kiunoni,
Unaanza kumkimbiza, anailaza baskeli yake pembeni mwa njia
Mtakimbizana kimbizana wee, mara akusubiri, unamshika unaanza kuivuta vuta kanga
Mara anakutishia kukutekenya kwapani, wewe unaona aibu unakimbia tena.
I can go ON and ON andON andON

The love was PURE, PURE, haya mashule haya yanaharibu vichwa tu, tukaja mjini kujijaza taka za wazungu, nataka desert ya pina pie

Hawa jamaa lazima atakuwa Wasukuma au Wanyamwezi maaana enzi hizo walikuwa wanapenda sana kutembea na radio na baiskeli..
 
Kongosho umenikumbusha mbali sana......
nakumbuka wakati huo ili dada atoke lazima aondoke na mtoto......basi ndo unachukuliwa hapo unasindikiza.....
wakati dada anaimbishwa anajidai yuko busy na nywele zako....saa hiyo ni kipilipili.......
basi zitavutwa weeeee.....ukirudi nyumbani una upara katikati ya kichwa......na ili nisiseme inabidi hongo ya double cola itembee.....
 
Kongosho umenikumbusha mbali sana......
nakumbuka wakati huo ili dada atoke lazima aondoke na mtoto......basi ndo unachukuliwa hapo unasindikiza.....
wakati dada anaimbishwa anajidai yuko busy na nywele zako....saa hiyo ni kipilipili.......
basi zitavutwa weeeee.....ukirudi nyumbani una upara katikati ya kichwa......na ili nisiseme inabidi hongo ya double cola itembee.....

tuwekee picha yako ya enzi hizo.
 
Ahsante sana Mkuu,

Hii ni attempt nzuri sana ya kuwarudishia jamaa makali yao ya enzi zile!!

DC
 
  • vijana wa zamani hao
    229306_10150190451807073_609802072_7530269_7068531_n.jpg

hehehe mjomba PAW naona kala sun glass halaf kafunga tambara la deki shingoni. Kulaleki!
 
ha ha ha....hapo lazima Yo Yo kapiga kile kitu cha VIP kwa ndani
hahahahahahahaha ehehehehe hiyo makitu ukiivaa bana haikuwa na adabu ukiwa mbele za watu unashangaa imeshapanda iko mabegani ahahahahahaha......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom