Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa

ahsante mkuu. next week bosi akinipa changu ntakutafuta unisaidie kununua Novel.
Ni vyema ukapata Kindle PaperWhite - Hii ni device maalum nzuli kwa walio addicted na novel /vitabu kwa ujumla.
kindle.jpg


kindle_paperwhite_2015.jpg


Ambapo utakuwa ukinunua vitabu toka amazon na instantly unakipata katika kifaa chako na kuanza kusoma hapo kwa hapo.
Screenshot_2016_08_22_11_54_40.png
 
mkuu mi nataka kununua domain ya .com kwa 0.99 USD je utanchaji sh ngapi?
Huduma ya PAY4ME, kwa kiwango cha malipo mtandaoni chini ya USD2.5, Huwa ni BURE, Hakuna service charge utakayonilipa.

Kwa domain ya .COM kwa usd 0.99, utalipia TSH 2,500 Tu, kwa utaratibu tajwa hapo juu.

domain.jpg

Kwa nini iwe tsh2,500 na si 2,186 tu? Sababu kuna makato kwa huduma ya kuhamisha fedha.
 
Huduma ya PAY4ME, kwa kiwango cha malipo mtandaoni chini ya USD2.5, Huwa ni BURE, Hakuna service charge utakayonilipa.

Kwa domain ya .COM kwa usd 0.99, utalipia TSH 2,500 Tu, kwa utaratibu tajwa hapo juu.

domain.jpg

Kwa nini iwe tsh2,500 na si 2,186 tu? Sababu kuna makato kwa huduma ya kuhamisha fedha.

asante mwalimu ngoja nikucheki
 
Mimi nahitaj taa za gari aina ya harrier head lamp na fog lamp za corolla Axio. Ebu nipe mchakato mkuu
Fuata hatua hizi ili kupata bidhaa unayohitaji

1. Fungua google .com

2. Kwenye serach box weka hizi keyword Fog Lamp Toyota corolla axio mfano.

3. Kagua links, utaona bei tofauti tofauti, chagua ile itakayofaa

4. Au waweza fungua moja kwa moja EBAY .com kisha ukaingiza hizo key word.

5. Baada ya kupata unachohitaji, Copy link yake iweke hapa au nitumia kwa njia tajwa hapo juu

6. Then ndipo mchakatop wa kuifikisha Tz bidhaa husika unaanza
FOG_LAMP.jpg
 
Duuuuuuh huyu ni yule yule wa Qsat na account za kichina za paytv ! tahadhari hawa watu wana maneno matamu sana but mwisho wake ni kilio kwa mteja!
Alikutapeli nn mkuu fungukaa i hv been known him for almost 4 years toka enzi za tunnelguru na huawei phone unlocking jamaa hana tamaa za kijingaa km unavofikir ww mkuu ungekuta malalamiko kedekede km angekuwa na tabia hizoo tena na wana jf wa sa hv wangemfungulia na uzi kabisaaa bt jamaa anajaribu kujijengea cv yake ya kibiashara since day one i saw him hana tatizo mkuu!
 
Duuuuuuh huyu ni yule yule wa Qsat na account za kichina za paytv ! tahadhari hawa watu wana maneno matamu sana but mwisho wake ni kilio kwa mteja!

Acha kufkiria mambo kwa kutumia makalio ndugu, usipende kukariri maisha kama unavyokariri kila siku dogo.

Kama umeingizwa mjini na watu wengine huo ubwege na ujinga ni wako lakini sio kwa Mwl.RCT coz nimeshanunua kwake kwa mtindo wa aina hii zaidi ya mara 2 na mzigo wangu nimeupata bila shaka.

Jamaa ni muaminifu na nampongeza kwa huduma zake kwa jinsi anavyozifanya tangu pdproxy, tunnelguru mpk online shopping jamaa anajua anachokifanya uspende kukariri maisha dogo coz maisha hayakaririwi kama unavyokariri wewe, bwege wee.
 
Mwl.RCT nahitaji kitabu hicho hapo chini. amazon nimeona paperback mpya zinauzwa dola 8+3.99 shipping. natakiwa kuwa na Tsh ngapi? nipo Mbeya.

9780330294911.jpg

nataka na hardcover ya hii novel nimeona amazon used ni dola 6.

39592125
 
Mwl.RCT nahitaji kitabu hicho hapo chini. amazon nimeona paperback mpya zinauzwa dola 8+3.99 shipping. natakiwa kuwa na Tsh ngapi? nipo Mbeya.

9780330294911.jpg

nataka na hardcover ya hii novel nimeona amazon used ni dola 6.

39592125
Nipe link zake kwa PM pls
 
UTANGULIZI

Je Kuna bidhaa unataka kununua toka nje ya nchi kwa sababu hapa Tanzania umetafuta na umekosa kuipata?

Je kuna huduma unahitaji kulipiwa mtandaoni?

Kama jibu ni NDIO basi hii thread inakuhusu.

Thread hii ni maalumu kwa wanaohitaji kununua bidhaa yeyote toka nje ya nchi. Bidhaa ambazo
  1. Hazipatikani hapa nchini au
  2. Hata ukipata ghalama yake huwa ni kubwa mara mbili zaidi, ukilinganisha na ghalama ya Kununua nje + Ghalama ya usafirishaji + Kodi
Hivyo thread hii itajikita katika nyanja kuu mbili:

1. BUY4ME
: Manunuzi ya bidhaa mtandaoni toka mataifa 15: ITALY, UAE, CANADA, UK, USA, JAPAN, FRANCE, CHINA, INDIA, GERMAN, MALAYSIA, SINGAPORE, SPAIN & SOUTH AFRICA. Huduma hii nitaiita BUY4ME.

(a) Kupitia huduma hii ya Buy4me Utaweza kununua bidhaa kutoka katika masoko* yaliyo bora yasiyouza na kusafirisha bidhaa nje ya nchi zao.

(b) Pia ununuzi wa bidhaa toka masoko* ambayo yanaweza tuma bidhaa nje ya nchi zao, kuja huku Tanzania (Africa)

*Masoko = Online shopping site

Jukumu langu ni (i) KUKUNUNULIA (ii) KUKUSAFIRISHIA (iii) KUKUFIKISHIA mahala ulipo pindi bidhaa yako ifikapo hapa nchini.

2. PAY4ME
: Malipo ya dharula ya hapo kwa hapo kulipia huduma na bidhaa
Kutokana na kadi yako kuisha mda wake au kadi yako inashidwa kufanya miamala kwa wakati huo ambao unashida.
Yamkini upo safarini na unahitaji ufanyiwe malipo kwa haraka.
Na iwapo pia huna kabisa access na online payment system yeyote.
Huduma hii itajulikana kwa jina la PAY4ME .

Mfano:
Kulipiwa domain name, webhosting , licence keys kwa software au program yeyote uitakayo mtandaoni , Kulipiwa huduma au uanachma katika tovuti mbalimbali mfano Netflix au HBO n.k

UTARATIBU WA KUNUNUA BIDHAA - BUY4ME

Utafuata hizi hatua

1. Tafuta bidhaa unayoihitaji toka tovuti tofauti tofauti.

2. Chagua bidhaa husika unayohitaji katika tovuti uliyo chagua mfano kama ni ALIEXPRESS, SOUQ, AMAZON (.com, .in, .uk ) au EBAY (.in, .com, .uk)

3. Nipe link ya hiyo bidhaa unayohitaji na uliyochagua.
Utanipa link kupitia email au whatsapp au PM

4. Nitaikagua link husika na Nitakujulisha gharama kwa TSH inayotakiwa kulipwa.

5. Utafanya malipo kwa utaratibu wa malipo uliowekwa.

6. Ndani ya dakika 5 - 45 tangu ufanye malipo nitakuwa nimelipia bidhaa yako na kukupa ushahidi wa:
- Payment Invoice,
- Picha (Screen shot) ya Bidhaa yako baada ya malipo kufanyika.
- Uthibitisho wa email niliyopokea baada ya muamala kukamilika.
- Hatua hii nitahitaji email yako au namba ya whatsapp ili kukutumia hivi vielelezo.

7. Utasubiri ndani ya saa 24 – 72 ili kupata tracking number ya mzigo wako kwa mizigo yenye tracking number.

8. Mzigo wako utachukua kati ya siku 9 – 21 kukufikia mahala ulipo.
TRACKING.png

TIME_TAKEN.png


GHALAMA UTAKAZONILIPA

- Kwa huduma ya BUY4ME utanilipa kwa makubalino baina yako wewe na mimi kutegemea thamani ya mzigo wako. Kiwango utakacholipa ni kati ya USD 2.5(Minimum) hadi USD 25 (maximum)

- Kwa huduma ya PAY4ME hii utalipia kiasi cha USD 2.5 hadi USD 5 Tu.

- Viwango kwa TSH vitakokotolewa kulingana na EXCHANGE rate ya US dola kwa siku husika malipo yanafanyika.

MAKUNDI MAWILI YA TOVUTI MASOKO

KUNDI A
– Wauzaji wanatuma moja kwa moja bidhaa kuja Tanzania (East Africa) -
Ambapo ghalama ya usafirishaji inajumuishwa wakati wa manunuzi ya bidhaa husika. (Napendekeza masoko ya kundi A yatumike Zaidi ili kupunguza ghalama.)

KUNDI B - Wauzaji wake hawatumi bidhaa kuja Africa, Nitawajibika kupokea mzigo wako katika nchi husika (viz UAE, USA, CHINA, JAPAN etl) .
Na mzigo ukishapokelewa ndipo unatumwa kuja Tanzania (Africa)
  1. Ambapo ghalama ya kutuma Mzigo Tanzania (Africa) itatokana na uzito wa mzigo. Gharama HAZIKADIRI kwa mujibu wa mita za ujazo (Volumetric Weight W*L*H) (Angalia kipengele cha ghalama ya usafirishaji hapo chini)

  2. Tracking number utapewa mpya ambapo utaweza ku_track mzigo wako ukiwa Njiani kuja TZ (Africa).

  3. Waweza kutrack mzigo kwa njia Mbili (a) Kwa kutumia mfumo wa SMS katika simu yako, au (b) kwa kutumia tovuti kwa njia ya simu au computer.

GHALAMA ZA USAFIRISHAJI MZIGO – TOKA MASOKO KUNDI B

1. Iwapo umenunua bidhaa kutoka katika soko la kundi A. Ghalama ya usafirishaji hulipwa wakati wa ununuzi.
Pia kwa baadhi ya masoko kwa bidhaa zote au baadhi ya bidhaa wauzaji, hutoa FREE SHIPING, hivyo kunakuwa hakuna ghalama ya ziada baada ya ununuzi wa bidhaa yako.

2. Iwapo umenunua bidhaa toka soko kundi B – Ghalama ya kusafirishia hutegemea UZITO wa bidhaa husika katika KILO (Kg) au katika POUND (LB) na kiwango cha fedha hutokana na kila 0.5kg ya bidhaa yako. kwa huu utaratibu

Mfano
:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 15
b) 0.6 – 1kg Ghalama ya kusafirisha ni 27.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 38.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 50.74 USD

Hivyo pindi ununuapo bidhaa kwenye Soko kundi B – Hakikisha unaangalia uzito halisi wa bidhaa yako. Ili kujua kiasi cha fedha kitakacho hitajika kusafirishia mzigo.

Na gharama hii ya usafirishaji italipwa Pindi mzigo uondokapo kwenye nchi husika kuja nchini Tanzania.

NB:
1. Gharama ya usafirishaji yaweza kulipwa ndani ya SIKU 1 hadi 5 Tangu upewe taarifa ya ghalama ya usafirishaji, kutoka nchi husika KUJA TANZANIA. ( Ni vyema ukalipa mapema).

2. Tracking number utakuwa nayo tayari hivyo utajua wazi mzigo wako umefika wapi au hatua ipi ya usafirishwaji.

KODI UTAKAYOLIPIA PINDI MZIGO UKIFIKA
  1. Pindi ununuapo bidhaa toka nje kumbuka kuna swala la kodi pindi bidhaa ifikapo nchini. (Kuna baadhi ya bidhaa huwa hazina nakodi – Mamlaka husika ndio huainisha bidhaa zipi zisizotozwa kodi)
  2. Utawajibika kwa malipo yote yatakayohitajika na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa bidhaa uliyonunua na iwapo utatakiwa kuilipia kodi.
  3. Gharama ya kodi hujulikana baada ya kuwa mzigo umekaguliwa na maafisa ushuru wa forodha hapa nchini.
  4. Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.
  5. Malipo yote utakayofanya utapewa stakabadhi husika.
NJIA YA MALIPO (KUTUMA FEDHA)

MALIPO YOTE NI KWA NJIA YA MPESA / TIGO PESA KWA HUU UTARATIBU

1. Piga *150*00# AU *150*01# (kwa Tigo PESA)
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa na 4 kwa Tigo Pesa
3. Mpesa Chagua 4. Weka namba ya kampuni au Chagua 3 kwa Tigo Pesa
4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. 261122
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo No. (Nitakupa Baada ya kuwasiliana nami)
6. Weka kiasi (mfano: 50,000/=)
7. Weka namba ya siri.
8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
** (BAADA YA MUAMALA KUKAMILIKA, TUMA KWANGU UJUMBE UTAKAOPOKEA- KAMA UTHIBITISHO)

NJIA ZA MAWASILIANO

Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: +255 (0) 625 955 137 au 0784 496 856
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 784 496 856
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @mw1rct

MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram – utajibiwa hapo kwa hapo kwa hapo.
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.

Iwapo unamazungumzo marefu na unahitaji kupigiwa niandikie kwenye ujumbe “CALL PAY4ME” au “CALL BUY4ME” na nitakupigia bila gharama yeyote.

307m693.gif


Hongera kaka kwa kuwaletea watu huduma hii wale wanaohitaji....mnaandika post hii kuwatoa watu wasiwasi wale wenye shaka na wewe.

Huyu jamaa ni mwaminifu 101% na i confidently vouch for him...so tumieni huduma zake kwa amani kabisa.
 
Hongera, lakini tunahitaji ushuhuda zaidi kwa watu uliowahudumia. Tumia verified user, na waombe mods kwa humu jf wakudhamini. Biashara na waafrica ni pasua kichwa, watu sio waaminifu kabisa na wengine ni wezi. Ungefungua kampuni na uwe na address inayoeleweka ingeongeza uaminifu kwako. Pili, jaribu kulink links zako na zile za TRA zinazohusu kodi kwa bidhaa kutoka nje. Nimeiona calculator ya TRA magari ni hatari. Kodi zinazidi bei za kununulia na shipping. Mwezi wa saba nilitaka kuagiza laptop moja kutoka Aliexpress, lakini nikakutana na wazungu furani waliingiza laptop tano waliipata usumbufu airpot. Sijui walitozwa kodi kiasi gani. Nikaghairi kununua
 
Hongera, lakini tunahitaji ushuhuda zaidi kwa watu uliowahudumia. Tumia verified user, na waombe mods kwa humu jf wakudhamini.
cc: Invisible ,
Nimepokea ushauri wako ndugu a4apple
Biashara na waafrica ni pasua kichwa, watu sio waaminifu kabisa na wengine ni wezi.
Hili nalitambua.
Kwa miaka mitatu nimekuwa nikiwahudumia wadau bila ya kuwa na official Thread, Ndipo nikaona ni vyema kuwa na thread ya rejea.
Uaminifu kwangu ni msingi wa huduma
Pili, jaribu kulink links zako na zile za TRA zinazohusu kodi kwa bidhaa kutoka nje.
Changamoto za TRA nazifahamu.
Pia huwa nawashauri wateja wa nini cha kufanya ili kuepukana na hizi changamoto
Kodi zinazidi bei za kununulia na shipping.
Hili ni kweli.
Hasa wanapo Uplift item price kutoka ile uliyonunulia na wao kuweka yakwao.
Nimetolea maelezo kidogo kwenye hii link.
>> Kukatwa kodi kwa mizigo
lakini nikakutana na wazungu furani waliingiza laptop tano waliipata usumbufu airpot. Sijui walitozwa kodi kiasi gani. Nikaghairi kununua
Wakati wowote ukihitaji msaada wangu nakukaribisha.

KARIBU
 
Mimi nahitaj taa za gari aina ya harrier head lamp na fog lamp za corolla Axio. Ebu nipe mchakato mkuu
Habari
Hii ni status ya mzigo wetu. Dated 17/09/2016
By Tuesday utakuwa mikononi.
feedback.PNG
 
Back
Top Bottom