Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa

Kwa wanaotumia AMAZON kufanya manunuzi

- Uzito wameweka kwa Pound (LB)
upload_2016-10-1_14-31-15.png

- ili kujua uzito huo katika Kg tumia hii calculator

Link
: Convert lb to kg - Conversion of Measurement Units
upload_2016-10-1_14-33-4.png
 
Kwa wanaotumia AMAZON kufanya manunuzi

- Uzito wameweka kwa Pound (LB)
View attachment 410270
- ili kujua uzito huo katika Kg tumia hii calculator

Link
: Convert lb to kg - Conversion of Measurement Units
UTANGULIZI

Je Kuna bidhaa unataka kununua toka nje ya nchi kwa sababu hapa Tanzania umetafuta na umekosa kuipata?

Je kuna huduma unahitaji kulipiwa mtandaoni?

Kama jibu ni NDIO basi hii thread inakuhusu.

Thread hii ni maalumu kwa wanaohitaji kununua bidhaa yeyote toka nje ya nchi. Bidhaa ambazo
  1. Hazipatikani hapa nchini au
  2. Hata ukipata ghalama yake huwa ni kubwa mara mbili zaidi, ukilinganisha na ghalama ya Kununua nje + Ghalama ya usafirishaji + Kodi
Hivyo thread hii itajikita katika nyanja kuu mbili:

1. BUY4ME
: Manunuzi ya bidhaa mtandaoni toka mataifa 15: ITALY, UAE, CANADA, UK, USA, JAPAN, FRANCE, CHINA, INDIA, GERMAN, MALAYSIA, SINGAPORE, SPAIN & SOUTH AFRICA. Huduma hii nitaiita BUY4ME.

(a) Kupitia huduma hii ya Buy4me Utaweza kununua bidhaa kutoka katika masoko* yaliyo bora yasiyouza na kusafirisha bidhaa nje ya nchi zao.

(b) Pia ununuzi wa bidhaa toka masoko* ambayo yanaweza tuma bidhaa nje ya nchi zao, kuja huku Tanzania (Africa)

*Masoko = Online shopping site

Jukumu langu ni (i) KUKUNUNULIA (ii) KUKUSAFIRISHIA (iii) KUKUFIKISHIA mahala ulipo pindi bidhaa yako ifikapo hapa nchini.

2. PAY4ME
: Malipo ya dharula ya hapo kwa hapo kulipia huduma na bidhaa
Kutokana na kadi yako kuisha mda wake au kadi yako inashidwa kufanya miamala kwa wakati huo ambao unashida.
Yamkini upo safarini na unahitaji ufanyiwe malipo kwa haraka.
Na iwapo pia huna kabisa access na online payment system yeyote.
Huduma hii itajulikana kwa jina la PAY4ME .

Mfano:
Kulipiwa domain name, webhosting , licence keys kwa software au program yeyote uitakayo mtandaoni , Kulipiwa huduma au uanachma katika tovuti mbalimbali mfano Netflix au HBO n.k

UTARATIBU WA KUNUNUA BIDHAA - BUY4ME

Utafuata hizi hatua

1. Tafuta bidhaa unayoihitaji toka tovuti tofauti tofauti.

2. Chagua bidhaa husika unayohitaji katika tovuti uliyo chagua mfano kama ni ALIEXPRESS, SOUQ, AMAZON (.com, .in, .uk ) au EBAY (.in, .com, .uk)

3. Nipe link ya hiyo bidhaa unayohitaji na uliyochagua.
Utanipa link kupitia email au whatsapp au PM

4. Nitaikagua link husika na Nitakujulisha gharama kwa TSH inayotakiwa kulipwa.

5. Utafanya malipo kwa utaratibu wa malipo uliowekwa.

6. Ndani ya dakika 5 - 45 tangu ufanye malipo nitakuwa nimelipia bidhaa yako na kukupa ushahidi wa:
- Payment Invoice,
- Picha (Screen shot) ya Bidhaa yako baada ya malipo kufanyika.
- Uthibitisho wa email niliyopokea baada ya muamala kukamilika.
- Hatua hii nitahitaji email yako au namba ya whatsapp ili kukutumia hivi vielelezo.

7. Utasubiri ndani ya saa 24 – 72 ili kupata tracking number ya mzigo wako kwa mizigo yenye tracking number.

8. Mzigo wako utachukua kati ya siku 9 – 21 kukufikia mahala ulipo.
TRACKING.png

TIME_TAKEN.png


GHALAMA UTAKAZONILIPA

- Kwa huduma ya BUY4ME utanilipa kwa makubalino baina yako wewe na mimi kutegemea thamani ya mzigo wako. Kiwango utakacholipa ni kati ya USD 2.5(Minimum) hadi USD 25 (maximum)

- Kwa huduma ya PAY4ME hii utalipia kiasi cha USD 2.5 hadi USD 5 Tu.

- Viwango kwa TSH vitakokotolewa kulingana na EXCHANGE rate ya US dola kwa siku husika malipo yanafanyika.

MAKUNDI MAWILI YA TOVUTI MASOKO

KUNDI A
– Wauzaji wanatuma moja kwa moja bidhaa kuja Tanzania (East Africa) -
Ambapo ghalama ya usafirishaji inajumuishwa wakati wa manunuzi ya bidhaa husika. (Napendekeza masoko ya kundi A yatumike Zaidi ili kupunguza ghalama.)

KUNDI B - Wauzaji wake hawatumi bidhaa kuja Africa, Nitawajibika kupokea mzigo wako katika nchi husika (viz UAE, USA, CHINA, JAPAN etl) .
Na mzigo ukishapokelewa ndipo unatumwa kuja Tanzania (Africa)
  1. Ambapo ghalama ya kutuma Mzigo Tanzania (Africa) itatokana na uzito wa mzigo. Gharama HAZIKADIRI kwa mujibu wa mita za ujazo (Volumetric Weight W*L*H) (Angalia kipengele cha ghalama ya usafirishaji hapo chini)

  2. Tracking number utapewa mpya ambapo utaweza ku_track mzigo wako ukiwa Njiani kuja TZ (Africa).

  3. Waweza kutrack mzigo kwa njia Mbili (a) Kwa kutumia mfumo wa SMS katika simu yako, au (b) kwa kutumia tovuti kwa njia ya simu au computer.

GHALAMA ZA USAFIRISHAJI MZIGO – TOKA MASOKO KUNDI B

1. Iwapo umenunua bidhaa kutoka katika soko la kundi A. Ghalama ya usafirishaji hulipwa wakati wa ununuzi.
Pia kwa baadhi ya masoko kwa bidhaa zote au baadhi ya bidhaa wauzaji, hutoa FREE SHIPING, hivyo kunakuwa hakuna ghalama ya ziada baada ya ununuzi wa bidhaa yako.

2. Iwapo umenunua bidhaa toka soko kundi B – Ghalama ya kusafirishia hutegemea UZITO wa bidhaa husika katika KILO (Kg) au katika POUND (LB) na kiwango cha fedha hutokana na kila 0.5kg ya bidhaa yako. kwa huu utaratibu

Mfano
:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 15
b) 0.6 – 1kg Ghalama ya kusafirisha ni 27.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 38.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 50.74 USD

Hivyo pindi ununuapo bidhaa kwenye Soko kundi B – Hakikisha unaangalia uzito halisi wa bidhaa yako. Ili kujua kiasi cha fedha kitakacho hitajika kusafirishia mzigo.

Na gharama hii ya usafirishaji italipwa Pindi mzigo uondokapo kwenye nchi husika kuja nchini Tanzania.

NB:
1. Gharama ya usafirishaji yaweza kulipwa ndani ya SIKU 1 hadi 5 Tangu upewe taarifa ya ghalama ya usafirishaji, kutoka nchi husika KUJA TANZANIA. ( Ni vyema ukalipa mapema).

2. Tracking number utakuwa nayo tayari hivyo utajua wazi mzigo wako umefika wapi au hatua ipi ya usafirishwaji.

KODI UTAKAYOLIPIA PINDI MZIGO UKIFIKA
  1. Pindi ununuapo bidhaa toka nje kumbuka kuna swala la kodi pindi bidhaa ifikapo nchini. (Kuna baadhi ya bidhaa huwa hazina nakodi – Mamlaka husika ndio huainisha bidhaa zipi zisizotozwa kodi)
  2. Utawajibika kwa malipo yote yatakayohitajika na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa bidhaa uliyonunua na iwapo utatakiwa kuilipia kodi.
  3. Gharama ya kodi hujulikana baada ya kuwa mzigo umekaguliwa na maafisa ushuru wa forodha hapa nchini.
  4. Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.
  5. Malipo yote utakayofanya utapewa stakabadhi husika.
NJIA YA MALIPO (KUTUMA FEDHA)

MALIPO YOTE NI KWA NJIA YA MPESA / TIGO PESA KWA HUU UTARATIBU

1. Piga *150*00# AU *150*01# (kwa Tigo PESA)
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa na 4 kwa Tigo Pesa
3. Mpesa Chagua 4. Weka namba ya kampuni au Chagua 3 kwa Tigo Pesa
4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. 261122
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo No. (Nitakupa Baada ya kuwasiliana nami)
6. Weka kiasi (mfano: 50,000/=)
7. Weka namba ya siri.
8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
** (BAADA YA MUAMALA KUKAMILIKA, TUMA KWANGU UJUMBE UTAKAOPOKEA- KAMA UTHIBITISHO)

NJIA ZA MAWASILIANO

Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: +255 (0) 625 955 137 au 0784 496 856
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 784 496 856
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @mw1rct

MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram – utajibiwa hapo kwa hapo kwa hapo.
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.

Iwapo unamazungumzo marefu na unahitaji kupigiwa niandikie kwenye ujumbe “CALL PAY4ME” au “CALL BUY4ME” na nitakupigia bila gharama yeyote.

http://m.ebay.com/itm/2-5-7-10-15M-...%3A8fd56b021570a78846958137ffff853c%7Ciid%3A1
Itakuwa pesa ngapi za madafu kupata hiyo.
307m693.gif
 
Screenshot picha ya kitabu
au
Nipe jina la kitabu na mwandishi, then nitafanyia kazi.
Nina list vitabu ninavyovihitaji. Ndo mana nikauliza kwanza.. kingine mfano naona kwenye amazon wanasema buy new from lets say dola 1, lakin price list inaenda mpk lets say dola 50....
so hapo unasemaje icho cha dola 1 kinaweza kuwa sawa na dola 50? N.B hapo kwa mujibu wa description vyote ni NEW.
kingine ile PRIME wanasema free shipping ama dola 13 . Nieleweshe hapo
 
Screenshot picha ya kitabu
au
Nipe jina la kitabu na mwandishi, then nitafanyia kazi.
Kingine hapo kwnye new and used ni kuna tofauti kubwa kuanza bei ndogo hadi bei kubwa kuliko ma vyote wanasema ni new...sasa hapa inakuaje mana wengi wanaamini kua bei kubwa mdo bora zaidi na quality
1475929739499.png
 
Asante kwa jibu lako zuri. Je nikimumua vitabu kama 10 hivi napo pia hakuna kodi ama kimoja ndo hakina kodi? Mana unaweza kununua kama vitabu 10 ama 15 alafu wakasema unanunua kwa ajili ya biashara ili wakukate. Ufafanuzi apo
Tutapata ufafanuzi zaidi toka mamlaka husika.
 
Back
Top Bottom