Njombe: Wapenzi wafariki wakiwa wamelala chumbani na jiko la mkaa

Watu wawili wamepoteza maisha mkoani Njombe baada ya kuingia na jiko la mkaa ndani ya chumba cha kulala kwa lengo la kupunguza baridi Mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililowakuta Benitho Mbatha (23) mpiga debe wa mjini Njombe na Jazila Said Mndendeule (27) mkazi wa Namtumbo.

Aidha amesema “Sababu ya kifo chao inaonyesha wakati wakiwa hai waliweka moto wa mkaa kwa ajili ya kujihifadhi na baridi na huu mtindo wa kuweka mkaa kwa watu wa Njombe ndio mtindo wao”alisema Kamanda wa Polisi Hamis Issa.
 
Mlikuwa mnakimbia madarasa ya kemia! Unaweza kufa kirahisi kwa ignorance yako. Hewa ya CO haina rangi wala harufu. Ukiivuta ya kutosha unakufa kiulaini kabisa. Mkaa ulivyokuwa unawaka ulitoa CO, wao wakaivuta.
mi sijaelewa hilo somo !

yaani unakufa ki'ulaini tu hivo bila hata kufurukuta yaani roho itoke kirahisi tu?
 
Mkaa, unavyowaka kwa kukosa oxygen, unazalisha carbon monoxide (CO) ambayo huvutwa na binadamu na kisha kuungana na hemoglobin (Hb) ktk mapafu. Kisha CO husambazwa sehemu mbali mbali za mwili (kwenye cell) na hatimaye kusababisha matatizo ya upumuaji (oxygen tension vs CO tension).
Kwa kifupi sana, hayo ndiyo maelezo.
R.I.P to them.
 
Haemoglobin huungana na oxygen kwa asili, ikitokea carbon monoxide imezidi kwenye damu kunakua na competition kwenye binding site ya haemoglobin. Haemoglobin ikiungana na carbon monoxide inakua sumu moja mbaya sana
 
Dah ... Nikusahihishe mkuu...mkaa unatokana na mimea ukiungua unatoa gesi ya kabondayoksaid (CO2)....hivyo kama umejifungia sehemu isiyo na madirisha...hiyo CO2 inarudi tena kuendelea kuungua bila kukamilika muunguo wake...na hivyo kufanya kuanza kujengeka kwa hewa kabonimonoksaid (CO) ambayo ndiyo sumu yenyewe ,

Mkaa, unavyowaka kwa kukosa oxygen, unazalisha carbon monoxide (CO) ambayo huvutwa na binadamu na kisha kuungana na hemoglobin (Hb) ktk mapafu. Kisha CO husambazwa sehemu mbali mbali za mwili (kwenye cell) na hatimaye kusababisha matatizo ya upumuaji (oxygen tension vs CO tension).
Kwa kifupi sana, hayo ndiyo maelezo.
R.I.P to them.
 
Hivi hakuna wasambazaji wa room heater zinazotumia umeme, au tatizo itakuwa kwenye bili.....mimi nina heater ya kupasha chumba joto niliyotoka nayo majuu lakini baridi la Dar halijanishawishi kutumia heater zaidi ya kulala na blanket......serikali toeni ruzuku kwenye heater ziuzwe maeneo yenye baridi kali na pia wapunguziwe bili za umeme ili waweze kumudu.
 
Back
Top Bottom