Babumawe
JF-Expert Member
- Sep 12, 2014
- 2,556
- 2,560
Watu wawili wamepoteza maisha mkoani Njombe baada ya kuingia na jiko la mkaa ndani ya chumba cha kulala kwa lengo la kupunguza baridi Mkoani Njombe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililowakuta Benitho Mbatha (23) mpiga debe wa mjini Njombe na Jazila Said Mndendeule (27) mkazi wa Namtumbo.
Aidha amesema “Sababu ya kifo chao inaonyesha wakati wakiwa hai waliweka moto wa mkaa kwa ajili ya kujihifadhi na baridi na huu mtindo wa kuweka mkaa kwa watu wa Njombe ndio mtindo wao”alisema Kamanda wa Polisi Hamis Issa.