Njombe: Wapenzi wafariki wakiwa wamelala chumbani na jiko la mkaa

Aisee,

Haya mambo miaka Fulani tumejifungia nyumba ndogo tukawasha moto na mafuta huku tumejifungia mama yuko chumbani ndio alituokoa mana lile jiko tulikua tumelelikata haswa na baridi ile.

Sijui ilikua vipi tulichomoka, Hapo tumesiz mama aka fungua mlango aisee dogo alikua kazima tayari mi nikambeba nikambwaga nje Huko mwagia maji sana jiko,ndo tukaanza kuongea kilichotokea.

Tungekufa kifo kibaya sana
 
Mkaa, unavyowaka kwa kukosa oxygen, unazalisha carbon monoxide (CO) ambayo huvutwa na binadamu na kisha kuungana na hemoglobin (Hb) ktk mapafu. Kisha CO husambazwa sehemu mbali mbali za mwili (kwenye cell) na hatimaye kusababisha matatizo ya upumuaji (oxygen tension vs CO tension).
Kwa kifupi sana, hayo ndiyo maelezo.
R.I.P to them.
Dah...haswaa....ndiyo muunguo usiokamilika....gesi ya ukaa inavunjwa oksijeni moja na kubaki moja....na ndiyo hiyo unayoita CO
 
Haemoglobin huungana na oxygen kwa asili, ikitokea carbon monoxide imezidi kwenye damu kunakua na competition kwenye binding site ya haemoglobin. Haemoglobin ikiungana na carbon monoxide inakua sumu moja mbaya sana
Kipi nilichokosea ktk maelezo yangu?
 
Hivi hakuna wasambazaji wa room heater zinazotumia umeme, au tatizo itakuwa kwenye bili.....mimi nina heater ya kupasha chumba joto niliyotoka nayo majuu lakini baridi la Dar halijanishawishi kutumia heater zaidi ya kulala na blanket......serikali toeni ruzuku kwenye heater ziuzwe maeneo yenye baridi kali na pia wapunguziwe bili za umeme ili waweze kumudu.

Dar kuna baridi?
 
Mwaka juzi wakati naishi Njombe, nyumba niliyokua nimepanga kuna Housegirl aliingiza ndani Kakijana Kake, Mama mwenye mtoto ni Kondakta kwahio siku hio Mama mwenye chumba walilala Makete, ndio Housegirl akaingiza MTU. Wakawasha na mkaa huku wako na mtoto mdogo (mtoto wa Boss wake)

Dah, sasa asubuhi Bibi mwenye nyumba anashangaa Housegirl haamki, bahati nzuri ile nyumba mpangaji mwingine alikua ni Nurse na siku hio alikua anaingia mchana. Baada ya kugonga mlango muda mrefu bila mafanikio wakafungua kwa nguvu.

Mungu mwema, wakawakuta wote wameanguka chini na wako taabani including kale katoto! Ila Housegirl na mchepuko wake wako naked!

Wakapata huduma ya kwanza wakazinduka. Njombe hapana aiseeee

Hata Mimi nilisurvive twice
 
Pole kwa ndugu wa marehemu.

Madhara ya kusahau somo la sayansi miongoni mwa jamii(wengi wamesahau aina ya hewa na jinsi hewa hizo zinavyopatikana na mifano yake).

Binadamu tunavuta hewa safi inaitwa " oxygen" na tunatoa hewa chafu aina ya "carbon oxide"

Mkaa unatoa hewa ambayo binadamu haihitaji("carbon oxide").Kitendo cha kujifungia na jiko ndani(mtu unakuwa umekubali kuondoa hewa safi inayohitaji kutumika na binadamu(" oxygen") na kutumia hewa isiyohitajika mwilini, lazima mwili uchoke na kuishiwa nguvu, hatimaye kulala usingi wa milele.
Usiwalaumu, usikute hawajasoma hawa marehemu
 
Back
Top Bottom