Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Salaam wakuu,weekend imeshatoboka tayari! Nipo hapa Rombo View ~ Sinza nang'ata Castle Lite baridi taaratibu huku nikisubiri kongoro na ndizi mchemsho kidogo. Nipo na mwanaJF mwenzangu.

Nimefikiria njia fulani za kuacha ulevi nikaona tushare pamoja ili tupunguze risks za kiafya na kifedha pia. Zifuatazo ni aina kuu za ulevi hapa duniani (hasa Tanzania):-

1. Uasherati /Uzinzi/Umalaya/Uchepukaji

2. Kunywa pombe (beer, wine, whisky, spirit,na mengine ya huko mtaani kwako)

3. Usengenyaji/ umbea/Unafiki

4. Kuangalia mpira, kucheza bao, kamali, karata na kunywa kahawa vijiweni

5. Kutamani kisichokuwa chako na usichoweza kukipata au kukinunua.

6. Kuvuta sigara, bangi, shisha nk

7. Kula mirungi nk

Sasa basi, mambo yote haya yamekuwa yakichangia ama kumkwaza mwenzi wako (bosi wako, rafiki zako), kukupotezea muda ambao ungeweza kufanya kazi kwa bidii, kukupotezea pesa, kukudhoofisha/kukuchosha kimwili nk.

Ili uepukane na haya yote, fanya yafuatayo:-

1. Minimiza idadi ya makundi ya Whatsap, ikiwezekana yafute yote

2. Ukitoka kazini, nyooka nyumbani kama mshale

3. Epuka makundi ya walevi wa aina nilizozitaja hapo juu

4. Penda kutumia muda mwingi kukaa na familia yako

5. Jitahidi upende kujifunza au kujua vitu vipya muda wote

6.Jitahidi kuwa busy na kazi au mradi wako mwingine baada ya masaa ya kazi.Mradi unaokuingizia pesa

7. Jitahidi kuivumilia kiu inayotokana na vilevi nilivyovisema hapo juu,kwani haufi

Asanteni sana.

Karibuni Rombo View Sinza,hapa Dsm.
 
Hii mambo kuanza ni rahisi ila kuacha ni Ngumu sana tena company za washakaji ndo huwa zinachangia, waweza kuwa huna kitu rafiki zako wakakupigia simu kwamba njoo upate mbili tatu, basi ukiienda ndo ziiii mpaka mida mibovu
 
Kama hivyo vitu ulivyovitaja vikitoweka kwenye jamii, nchi itafilisika kwa kasi ya mwanga.
 
Nimefikiria njia fulani za kuacha ulevi nikaona tushare pamoja ili tupunguze risks za kiafya na kifedha pia. Zifuatazo ni aina kuu za ulevi hapa duniani (hasa Tanzania):-

1. Uasherati /Uzinzi/Umalaya/Uchepukaji
Mkuu hii ya kwanza umetumia maneno makali sana......afadhali ungetumia kuchepuka kidogo wahusika wasijisikie vibaya.....
 
Ulevi ni sawa na nyumba, kuanza kutumia ulevi ni kuwa tayari umeingia ndani ya nyumba, ili uache kulewa unatakiwa kutoka ndani ya hiyo nyumba, unatoka kwa kupita mlango uleule ulioingilia kwenye huo ulevi(nyumba).
THINK
 
Endelea kunywa utupe mawazo mengine...yn ka beer kamoja tu umeanza ongea point...ukifika ya saba je..pls endelea ili tupate mafunzo.
 
Nmeacha Pombe kabisa kwa kutumia njia ulizo taja ila leo ndo nasherekea mafanikio kwa kugonga mbili tatu mkuu......!
 
Duuh, sasa mimi ntafanyaje niweze kuacha sababu mradi unaonisaidia kubadilisha mboga ni kuuza vilevi (pombe) na Guest house. Kibaya zaidi makundi yote uliyotaja wazinzi, michepuko, wacheza kamari na waangalia mpira ndo wateja wangu waliotukuka.
 
Back
Top Bottom