Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu engine ya gari yangu Nissan winroad ilikua inagonga na kutoa sauti kama machine ya kusaga ya diesel. Nimenunua engine engine , sasa hii ingine mpya imefungwa leo lakini kwenye test haina nguvu kabisaa . ukikanyaga mafuta ndo kabisaa inapiteza nguvu. Pia inapoteza nguvu kwenye mlima na kuspeed up kwenye mteremko . tatizo litakua nini chief

Tukichukulia kuwa kila kitu kimefungwa vizuri, na wala hakuna bomba la hewa amabalo halikufungwa sawasawa, yaani hakuna leakage ya hewa, inawezekana kuwa injini uliyonunua imeshakula sana piston rings. Hebu waambie wafanye compression test; inatakiwa compression iwe kama 40-45 PSI yaani kati ya 28kPa mpaka 31kPa hivi. Kama compress ni chini ya hapo, basi piston rings zimekwisha utatakiwa kuweka nyingine.

Tatizo jingine ambao sielewe linaweza kuwa limejitokezaje ni pale fuel pump haipeleki mafuta ya kutosha; yaani ule mrija wa mafuta haukufungwa vizuri kwa hiyo kuna mafuta yanavuja, ila hilo unaweza kusikia harufu ya mafuta na kuna matoen ya mafuta yanadondoka chini, inawa mengi yanaveporate kabla ya kufika chini.
 
hebu nimbie kwanza tatizo lilianzaje; lilianza ghafla tu au lilianza pole pole.
Tatizo lilianza pole pole ambapo pia lilipelekea pia kupasuka flau wheel tukabadirisha.Mechanically hatukujua chanzo cha flau wheel kupasuka kwa kiasi kikubwa.Cha msingi tatizo hili halijatokea ghafla.
 
Nina wasiwasi kuwa transmission yake imekufa, kwa hiyo zile clutch plate zake zinateleza, ndiyo maana unakanyaga accelerator inajini inaunguruma spidi ya juu lakini magurudumu hayapati nguvu. Nenda kwa mafundi wa transmission wakuewekee torque converter na clutch plates mpya kama utawapata. Kuna viplates vingi sana ndani yatransmission ambavyo voyte vinatakiwa vibadilishwe kwa sababu vimeshasagika.

Ikishindikana ripea, basi tafuta transmission mpya.

Matatizo mengi ya transmission husababsihwa na kutokubadili transmission fluid wakti wake. Watengezaji wengi wanakuambia kuwa usibadili transmission fluid lakini ukweli ni kuwa baada ya muda transmission fluid insihiwa kwa kujaa vipande vya chuma vitokanavyo na vyuma kusagoka. Inabidi uweke fluid mpya na filter kila baada ya miaka kama kumi hivi kulingana na aina ya gari.
 
Nina wasiwasi kuwa transmission yake imekufa, kwa hiyo zile clutch plate zake zinateleza, ndiyo maana unakanyaga accelerator lakini magurudumu hapati nguvu. Nenda kwa mafundi wa transmission wakuewekee torque na clutch plates mpya kama utawaapta. Kuna viplates vingi sana ndni yatransmission ambavyo voyte vinatakiwa vibadilishwe kwa sababu vimeshasagika...
Ahsante mkuu nitaanzia hapo.
 
Tukichukulia kuwa kila kitu kimefungwa vizuri, na wala hakuna bomba la hewa amabalo halikufungwa sawasawa, yaani hakuna leakage ya hewa, inawezekana kuwa injini uliyonunua imeshakula sana piston rings. Hebu waambie wafanye compression test; inatakiwa compression iwe kama 40-45 PSI yaani kati ya 28kPa mpaka 31kPa hivi. Kama compress ni chini ya hapo, basi piston rings zimekwisha utatakiwa kuweka nyingine.

Tatizo jingine ambao sielewe linaweza kuwa limejitokezaje ni pale fuel pump haipeleki mafuta ya kutosha; yaani ule mrija wa mafuta haukufungwa vizuri kwa hiyo kuna mafuta yanavuja, ila hilo unaweza kusikia harufu ya mafuta na kuna matoen ya mafuta yanadondoka chini, inawa mengi yanaveporate kabla ya kufika chini.
Asante mkuu
 
What does 5W-30 actually mean? - Rymax Lubricants

Nipatie reference kutoka kwa manufacturers wa oil wanaosema 5W30 haina tatizo kwenye mazingira ya joto?
Mkuu manufacturers wa magari mengi siku hizi chaguo lao la kwanza la engine oil ni 5w30 au 10w30 bila kujali mazangira.

Hii elimu kuwa 5w30 ni ya nchi ya baridi sijui wabongo tuliitoa wapi..

Manufacturers hakuna mahali anasema ukiwa Canada tumia 5w30 ila ukiwa nchi za joto kama Africa utumie oil namba 50 kwa gari petrol.

Kingine, uliposema hiyo 5w inawakilisha kiwango cha chini cha joto kuwa joto lisishke zaidi ya nyuzi 5 za centigrade, hapo si sawa mkuu...

Kwa mfano,samahani kwa hili lakini...niliishi jimbo moja huko marekani linaitwa Iowa...lipo Midwest....baridi ya hapa mahali December mapaka February huwa inagonga zaidi ya -20°C....na magari ya huko wanatumia 5w30..

Sasa kama hii 5w inasema joto lisishuke zaidi ya nyuzi 5, magari ya huu mji si yangegandisha oil..?

Hii oil 5w30 inaweza kutumika kwenye outside temperature inayoanzia -30°C mpaka 40°C+ mkuu...

Kwa hiyo oili hii mtu wa Dar na mtu wa Canada wotw wanazitumia bila shida kwa sababu nchi yetu hakuna mkoa wowote wenye joto linalozidi nyuzi 40 za C..
 
Mkuu manufacturers wa magari mengi siku hizi chaguo lao la kwanza la engine oil ni 5w30 au 10w30 bila kujali mazangira.

Hii elimu kuwa 5w30 ni ya nchi ya baridi sijui wabongo tuliitoa wapi...
Kuna watu wanajidanganya kuwa kuna nchi za joto na nchi za baridi; hawajui kuwa nchi ambazo zina baridi sana wakati wa Winter huwa pia zina joto sana wakati wa summer kuliko hata la Dar. Halafu hata nchi iwe na joto kiasi gani, haiwezi kufikia joto la injini.
 
ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler.
Huku Tanzania hatutumii CHRYSLER, GM and FORD

Labda diaspora wa Marekani

Lakini pia Waafrika wengi kwenye diaspora utakuta wana stick na magari wanayoyajua toka Afrika, Toyota Forunner, Corolla, Camry, Discovery, Avalon, na kidogo Nissan, Benz nk.

Na hicho cheti cha ASE Service Consultant ukifika lazima ulipeleke TCU ukakitafsiri mwenyewe na uwa convince kwa nini wakutambue ilhali umesomea CHRYSLER na FORD
 
Kuna watu wanajidanganya kuwa kuna nchi za joto na nchi za baridi; hawajui kuwa nchi ambazo zina baridi sana wakati wa Winter huwa pia zina joto sana wakati wa summer kuliko hata la Dar. Halafu hata nchi iwe na joto kiasi gani, haiwezi kufikia joto la injini.
Ni kweli mkuu...kwa sababu nakumbuka pale Iowa wakati wa summer joto lake hilo la Dar ni mtoto. Nadhani mleta hoja bado hajaelewa vizuri maana ya ile namba kabla ya W na ile namba baada ya W.
 
Mkuu manufacturers wa magari mengi siku hizi chaguo lao la kwanza la engine oil ni 5w30 au 10w30 bila kujali mazangira.

Hii elimu kuwa 5w30 ni ya nchi ya baridi sijui wabongo tuliitoa wapi...

Mkuu nimekuelewa vyema sasa tujiulize gari inatoka Japan ina Km 80,000 kwetu huku tunaiita mpya, hii hii gari kwetu ikija tembea 30,000 km utaishangaa. AC hazifanyi kazi, mlio wa engine ni tofauti inachoka sana (sisemei kwa zote) tatizo hapa linakua nini mkuu?

Kuna mji China unaitwa Harbin baridi inakua mpaka -6 huku ndio nilijua matumizi ya right oil to your car.
 
Kuchoka kwa gari kunategemea sababu nyingi sana..

Sababu ya kwanza mazingira...Gari limetoka Japan almost kila sehemu ni lami kwa hiyo gari linakuwa linatembea bila shuruba na mikikimikiki hivyo engine haitumii nguvu kulinganisha na huku kwetu..

Vipuri duni vya kufanyia service..Kwa mfano engine oil na oil filter..
Kwa mfano ukiagiza gari used Japan, likifika tu mafundi wetu hawa wanakushauri umwage oil iliyokuja na gari uweke SAE 40 eti ndiyo inayofaa Tanzania..
Hapo inakuwa ni sawa na wewe una damu group O, unalazimishwa kuwekewa group B ..lazima utaumia.

Hiyo oil yenyewe wakishaweka SAE 40, wanakuwekea na oil filter ya 3500/-..
Hapa lazima Engine ichoke mapema sana na kuanza kubadilisha milio..

Watu pia hawaweki spark plugs ambazo zimependekezwa...huwezi kuqmini mtu amenunua gari milioni 13, anaweka plugs za buku 4 kwa moja..hapa lazima Engine itakuwa ina... struggle ili kipata full combustion..

Mafundi wetu wanatabia common ya kutoa thermostat, kisha wanakushauri usiingie gharama ya coolant, uweke maji ya bomba..

Kipato duni kinafanya magari yetu yachoke mapema...kwa mfano mtu anamiliki gari dogo kama Passo au IST, hilo hilo ndiyo la kwenye lami na tope, mjini na mashambani, milimani kama Upareni na Tambarare...kama ana duka hilo hilo gari ndiyo lakubebea bidhaa za dukani...lazima gari lichoke mapema.

Wenzetu kwenye nchi zilizoendelea utakuta ana gari zaidi ya moja...na mara nyingi huwa ni SUV, Gari ndogo na pick up kubwa kama Amarok, Takoma au Navara....kwa hiyo kila gari inakuwa na matumizi yake.

Mafuta ya petrol yenye kiwango duni...na hiki ndiycho kilio kikubwa, kikifuatiwa na SAE 40 pamja na maji ya bomba.

Mwisho Watanzania wengi hatuna desturi ya kutunza mali zetu, hatufuati kanuni zilizopendekezwa na manufacturers na tunaogopa bei ya spea genuine na hii ndiyo sababu watu wengi wameegemea kwenye Toyota vile wana uhakika wa spea feki za bei rahisi
 
Number zilizoko kwenye oil zinawakilisha mambo matatu
-Viscosity ambayo ni namba ya kwanza
- W ambayo inamaanisha Winter
- namba ya mbele ya W ambayo inamaanisha kiwango cha juu cha joto ambayo oil hiyo huweza kufanya kazi...
Mh! Mkuu hapa umechanganya mambo..
 
Kuchoka kwa gari kunategemea sababu nyingi sana..

Sababu ya kwanza mazingira...Gari limetoka Japan almost kila sehemu ni lami kwa hiyo gari linakuwa linatembea bila shuruba na mikikimikiki hivyo engine haitumii nguvu kulinganisha na huku kwetu...i
Mkuu naweza kupata FCC ID ya key fob kwa Toyota harrier toleo la 2005/9?
 
Du! Hii kitu inanipa shida sana. Nimeangalia kwenye fob niliyonayo sijaweza kupata. Nilikua na mpango wa kuagiza funguo mahali akaitaji hii kitu.
Kuna fobs ambazo ni programmable na kuna ambazo siyo programmable. Kama yako siyo programmable, una kazi kubwa sana ya kutafuta fob nyingine inayofanana kabisa, ila kwa sababu za kiuslama, unaweza kukuta fob inayofanana na yako iko continent nyingine kabisa. Programmable ni rahisi sana, wewe nunua yoyote ile umplekee mwenye computer ya kuprogram hizo fobs, holla!
 
Chief samahani, naweza funga engine ya Mercedes Benz 102 kwenye cresta gx 100?

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
Sijui kwa sababu inategema ukubwa wa ingini yenyewe, sehemu zake za kufungia na uzito wake; hayo ni mambo ya mtaani siyo ya kiufundi. Tafuta kijana wa mtaani anayejua kufanya modifications akusaidie
 
Sijui kwa sababu inategema ukubwa wa ingini yenyewe, sehemu zake za kufungia na uzito wake; hayo ni mambo ya mtaani siyo ya kiufundi. Tafuta kijana wa mtaani anayejua kufanya modifications akusaidie
Samahani, unakosea kusema mambo ya mtaani maana modifications ni professional pia watu wanaingia darasani na wanahitimu pia

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
 
Samahani, unakosea kusema mambo ya mtaani maana modifications ni professional pia watu wanaingia darasani na wanahitimu pia

Sent from my itel it1508 using JamiiForums mobile app
Kama wapo watu wanahitimu utaalamu wa kuhamisha injini kutoka gari model moja na kuiweka kwenye gari modeli nyingine basi sawa, onana nao. Mimi leseni yangu hainiruhusu kufaya mambo hayo kwa sababu kadhaa za kiusalama na kibiashara kwa makampuni ya kutengeneza magari.

Nina imani elimu ya kuswap injini za magari model tofauti itakuwa inavunja sheria za biashara za kimataifa. Huiwezi kujenga gari yako ya Nyumbu, halafu ukaweka injini ya benz bia idhini na kuanza kuuza hiyo Nyumbu yako.

Yeyote anayefanya hivyo anaitwa fundi wa mtaani, kwani hafuati sheria. Ingawa hata mimi nikiwa na shida huweza kufanya njia za mkato kutatua matatizo yangu lakini siwezi kutumia njia hizo za mkato kwenye garo ya mtu mwingine
 
Back
Top Bottom