SoC02 Serikali ya Tanzania itumie magari madogo (small SUVs)

Stories of Change - 2022 Competition

Prospogi

New Member
Aug 13, 2012
3
6
Tanzania, nchi yangu nzuri, inayotajwa kufikia uchumi wa kati wa chini, imebarikiwa kuwa na rasilimali za aina mbalimbali kama vile ardhi nzuri ya kilimo, madini, misitu, n.k; bado inakuza uchumi wake taratibu sana kutokana na changamoto mbalimbali. Moja ya changamoto kubwa sana kwa miaka mingi, ni serikali kuwa na matumizi makubwa ya fedha inazokusanya kutoka vyanzo mbalimbali na kufanya shughuli zake za kila siku. Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa na za maksudi kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi kizalendo, pia imefikia hatua ya kuanzisha tozo kwenye miamala yote ya fedha inayofanyika kwa njia mbalimbali, kutokana na makusanyo kidogo ya kodi yasiyoendana na mahitaji ya fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kutoa na kuboresha huduma mbalimbali za umma. Baada ya tozo kuanza, wananchi wengi hatujaafiki pamoja na utetezi wa serikali juu ya malengo ya kukusanya tozo hizo.

Wakati huo huo, serikali haijaweka wazi ni kwa namna gani yenyewe inachukua hatua kupunguza matumizi yake ya fedha nyingi yasiyo ya lazima. Tunajua kwamba serikali hununua huduma na bidhaa kwa bei kubwa mno kuliko bei halisi ya soko kulingana na sheria yake ya manunuzi ambayo kimsingi inaongeza gharama zaidi za kuendesha serikali kuliko kupunguza. Pia kwa miaka mingi, serikali imekuwa ikihakikisha kiongozi wa umma, anaishi maisha ya kifahari sana kwa kutumia pesa zetu walipa kodi. Viongozi wengi wa umma wanaishi kwenye nyumba za kifahari za serikali, wanatembelea magari ya kifahari ya serikali, pamoja na kulipwa mishahara mikubwa na posho nyingi; mtindo wa maisha ambao hauakisi serikali yoyote yenye dhamira ya dhati ya kupunguza umaskini kwa wananchi wake. Mtindo huu wa maisha ya viongozi wa umma, umeshindwa kuleta tija kwenye kupambana na umaskini na kupelekea watu wengi kutamani kuwa viongozi wa serikali maana wanajua wakipata madaraka hayo, basi wataishi maisha ya kifahari. Marehemu Rais John Pombe Magufuli, kwa kiasi kidogo aliweza kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma kwa kubana matumizi yasiyo ya lazima.

Eneo moja ambalo binafsi nafikiri serikali ya Tanzania inafanya vibaya, ni hatua ambayo inaonekana kuwa sahihi (ingawa si kweli) ya kununua magari ya kifahari yenye injini kubwa ambayo yanatumia mafuta mengi sana na vipuri vyake ni ghali pia, kwa ajili ya matumizi ya viongozi wa serikali. Kwa miaka mingi, serikali imekuwa ikinunua magari hayo (maarufu V8) kwa ajili ya matumizi ya wakurugenzi wa halmashauri zote, wakuu wa wilaya zote, wakuu na makatibu tawala wa mikoa yote, wakuu wa taasisi za umma zote pamoja na baadhi ya wakurugenzi kwenye taasisi hizo, makatibu wakuu na manaibu wa wizara zote, mawaziri na manaibu waziri wote, majaji wote, n.k. Magari hayo mengi yananunuliwa kutoka kampuni ya magari ya Toyota, ni aina ya Landcruiser V8. Pia baadhi ya ofisi chache za umma zina magari kutoka kampuni za Nissan, Landrover, Ford, n.k ambayo pia yana injini za V8. Huenda kuna punguzo la bei kidogo serikali ya Tanzania hupata kutoka kampuni ya Toyota, ndiyo maana zaidi ya 80% ya magari ya serikali ni kutoka kampuni ya Toyota, lakini kitendo cha kununua magari ya V8 kutoka Toyota kwa wingi zaidi, kinadumaza kukuza uchumi wa nchi kwani serikali inatumia gharama kubwa sana kuyaendesha magari hayo ya V8.

Kwa kuwa serikali ina magari ya aina hiyo mengi nchi nzima, na bahati mbaya bado inaendelea kununua mapya ya aina hiyo hiyo, nafikiri wakati umefika uongozi wa nchi (kuanzia kwa Rais Samia Suluhu) kuwa na mtizamo tofauti juu ya aina ya magari ambayo serikali inapaswa kununua. Huenda magari ya V8 yalifaa kipindi ambacho nchi yetu ilikuwa na barabara mbovu sana (hasa kipindi cha masika) ambazo zilikwamisha viongozi kufika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kutimiza majukumu yao. Sasa nchi yetu imepiga hatua kubwa sana kwenye kuboresha barabara mpaka vijijini, kwani barabara hizo nyingi sana zimeimarishwa vema na TARURA kuweza kutumika kipindi chote cha mwaka.

Nafikiri magari madogo (small SUVs) yenye mfumo wa Four Wheel Drive kama Rav4 (Toyota), X3 (BMW), X-Trail (Nissan), Forester (Subaru), n.k yenye ukubwa wa injini usiozidi 2000 CC; yanapaswa kuwa mbadala mzuri wa magari ya V8 ambayo serikali inaendelea kuyatumia na kununua mapya. Magari hayo madogo yana injini zinazotumia mafuta kidogo na pia vipuri vyake ni bei nafuu zaidi kuliko magari ya V8. Pia magari hayo madogo yenye mfumo wa Four Wheel Drive, yanaweza kupita vema hata kwenye barabara za vijijini nchini mwetu na kuwawezesha viongozi kufika maeneo ya vijiji bila taabu ya usafiri. Pia yana mifumo ya ufahari ambayo inawapa watumiaji wa magari hayo wakati mzuri wakiwa ndani yake.

Nashauri serikali isiendelee kununua magari ya V8, badala yake ianze kununua magari madogo (small SUVs) kama niliyopendekeza, maana kwa kufanya hivyo itapunguza sana matumizi ya pesa za umma yasiyo ya lazima kwenye matumizi ya magari ya viongozi (isipokuwa kwa viongozi wale tu ambao itifaki hairuhusu), pesa ambazo zinaweza kutumika kutoa huduma mahali pengine ambapo wananchi wanahitaji huduma bora zaidi. Pia, serikali ikianza sasa, itakuwa imeonesha njia kwa viongozi wajao kwamba kuwa kiongozi wa serikali, maana yake ni kujitoa kuhudumia wananchi, hivyo hakuna sababu ya kutumia V8 wakati gari ndogo yenye mfumo wa Four Wheel Drive inaweza kumfikisha kiongozi mahali popote nchini.

Jambo hili litawezekana tu endapo Mheshimiwa Rais wa nchi yetu na viongozi wenzake wa karibu (Makamu wa Rais na Waziri Mkuu), pamoja na Jaji Mkuu na Spika wa Bunge, wote kwa pamoja wataelewa mantiki ya kupunguza matumizi ya serikali kwa kuanza kununua magari madogo pekee kwa ajili ya matumizi ya serikali.

Nawasilisha,

Prospogi.
Mwananchi.
 
Naunga mkono hoja yako kwamba umefika wakati viongozi wa serikali kununuliwa mqgari ya kawaida uliyo taja hapo juu ikiwemo na hard top Landcruzer kwa safari ziara za vijijini. Kama ni issue ya starehe ndani waombe wawekewe hizo starehe. Nchi masikini viongozi kutembelea migari ya kifahari ni wendawazimu fulani hivi na kukosa aibu.

Mama Samia utakumbukwa kama utatuletea Katiba Mpya na kupunguza matumizi holela ya serikali kununua migari ya kifahari. Viongozi wanatakiwa kufanana na wananchi wanao waongoza ambaye hataki ajiuzulu. Pili mama punguza pesa wanayo lipwa wabunge na kupunguza viwango vya mikopo ya magari wanayo pewa wakisha chaguliwa/teuliwa. Ubunge ni uwakilishi kwa wananchi siyo eneo la kuchuma pesa. Watakao ona pesa ni ndogo waache na kujiuzulu hawatufahi wanefuata maslahi ya fedha bungeni.
 
kama alivyosema mdau hapo juu Land Cruser hardtop zipo makini sana na gharama nafuu kuzihudumia ukilinganisha ni L300 GR Sports.
images.jpg
 
Back
Top Bottom