Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Nishawahi kukatazwa na dealer wa Toyota kutumia injector cleaner,yeye alisema once ukianza basi inatakiwa utumie kila unapojaza mafuta hasa kwa kuwa filling station nyingi kwa bongo zinauza mafuta machafu (ambapo sikumuelewa kwa kweli)
1. Je, kuna ukweli katika hilo?
2. Nikiweka mafuta kwenye vituo vya kawaida gari haina mis,lakini nikiweka kwenye vituo vya TOTAL then nikarudi kwa vingine mis hutokea na sometimes gari kuzima na kusumbua kuwaka,Je,ni formula ya mafuta kutofautiana au kuna sensor kwenye gari haipo sawa?.
Shukrani.

Huyo dealer alikudanganya, labda alitaka ukishakpata matatizo umrudie. Injector cleaner ukiitumia vizuri, hasa ukitumia ratio nzuri, chupa moja kwa full tanki labda mara moja kila baada miezi miwili unaongeza sana maisha na ubora wa injector zako; ndiyo maana hizo cleaner zipo madukani. Ni kweli kuwa kuna vituo siyo waaminifu, wanauza mafuta yasiyo na Octane number inayotakiwa. Kwa bahati mbaya sina jibu rahisi kukusaidia, kwani ubora wa amafuta ni kazi ya wachujaji. Labda sehemu nyingine huchanganya Regular na Super kwa sababu hizo zina octane number tofauti.
 
Nina RAV 4 KILL TIME kila nikiwasha na kurudi nyuma inatoa mlio wa Ka ka ka, na ikichanganya haitoi tena na mara nyengine hata nikiachia break kwenda mbele kuna mlio wa TI TI TI, nini tatizo nimeshapima sensor zipo sawa kwa mashine, msaada mkuu tafadhali hata kama nikuletee usikie ninachosema nipo Dar
 
Kuna original na genuine...
Hata za kichina huwa na original kutokana na standard zao..

Genuine ni kama iliyotoka na gari....hakuna tofauti na inafanana mpaka part number na sometimes inasoma mpaka chasis number..

Part kuandikwa tu Toyota au Nissan haitoshi kuifanya iwe genuine bali yaweza kuwa original huko ilipitengenezwa..
Jibu lenye akili sana vitu vyote vya China wanaandika original lkn ukishaweka kwenye gari Siku mbili nyingi imekufa
 
Mkuu, kuna mshikaji ana ford Taurus ya 05, ambayo ina tatizo wakati wa kustart. Anapata message ya 'low oil pressure', wakati oil iko full, tena na kuzidi kidogo. Hata baada ya kubadilisha 'oil pressure sensor' na kuweka mpya, bado hali hiyo inajitokeza tu. Tatizo linaweza kuwa nini?
Nb: cha kushangaza ni kwamba kwakati mwingine gari inastart hata ikiwa na hiyo message ya low oil pressure!
 
Mkuu nimefuatilia kwa karibu na Nimesoma kila post, hongera na Ubarikiwe sana maana ni shule bila ada, asante.

Mimi nina carina Ti, nikiwasha gari injili inaunguruma kama mashine ya kusaga ikiwa free ila nikiweka gia (D) mlio unaisha. Mafundi waliniambia nifanye overhaul, Nimefanya kwa gharama kubwa lakini bado iko vile vile.

Ishu nyingine ninapoanza mwendo gari huwa nzito kiasi muungurumo wa injini hauendani na spidi ya gari (yaani mtu wa nje anaweza kufikiri napiga ress). Mpaka speed ukifika 20-30 ndo muungurumo hushuka na kuenenda sawia na accelerator.

Kadhalika kama unapatikana TZ hasa hasa dar naomba nipm namba yako tafadhali.
 
Kuna sababu kubwa tatu zinazoweza kusababisha hali hiyo ijitokeza kwenye gari lako: Sababu ya kwanza ni iwapo kuna tundu kwenye bomba la hewa kati ya air filter na Intake manifold ya engine,kiasi kuwa hewa inayopita kwenye filter haifiki yote kwenye manifold, sababu ya pili, ni iwapo ile Idle Air Control (IAC) valve imekufa; hii hufanya adjustment ya hewa inayongia kwenye injini kusudi ilingane na kiasi cha mafuta kinachoingia wakati wa silence, halafu mwisho ni Exhaust Gas Recirculation (EGR) valve nayo ikifa hushindwa kurudisha hewa ndani ya injini na kuifanya injini ichome mafuta yasiyowiana na hewa iliyopo bila kuwa na mzigo wowote mpaka ukishaweka gear ndipo unapoip[a injini mzigo, na muunguruma unabadilika.
 
Mkuu, kuna mshikaji ana ford Taurus ya 05, ambayo ina tatizo wakati wa kustart. Anapata message ya 'low oil pressure', wakati oil iko full, tena na kuzidi kidogo. Hata baada ya kubadilisha 'oil pressure sensor' na kuweka mpya, bado hali hiyo inajitokeza tu. Tatizo linaweza kuwa nini?
Nb: cha kushangaza ni kwamba kwakati mwingine gari inastart hata ikiwa na hiyo message ya low oil pressure!
Nilikuwa na wasiwasi na Oil pressure sensor;. kama hiyo ni mpya basi huenda tatizo ni kubwa sana kuwa kuwa injini imeshasagika sana kiasi kuwa clearances za oil zimekuwa kubwa sana, na hakuna pressure yoyote inayojengeka tena.
 
Duh mafundi walishauri oil hii kwa ajili ya kilitime yangu...
Madhara yake hasa ni nini? Maana ndio yaliyopo katika gari yangu.
Unawaamini mafundi warekebishaji kuliko kuwaamini waliotengeneza gari? Kama manual ya gari huna hata google pia ukose? Kiufupi kill time inatumia oil ya 5w30 na oil hii ni nyepesi sana kuweza kuhakikisha inapenye vizuri kwenye engine ya gari inaweza kufanya kazi katika mazingira ya hadi joto la -30c hadi 30+c lkn oil yako hiyo ya 20w50 ni oil nzito sana hivyo ili ivhanganye kwa haraka lazima engine ya gari ifike jotolid lake la ufanyaji kazi hivyo kipind chote ambacho engine haina joto vyuma vya ndani vinakuwa vinasagika kwani hakuna oil ambayo inakua inapitia hivyo vyuma plz plz nasisitiza gari ni ya kwako mwenyewe ukishindwa kusoma manual za magari waulize wamiliki wa magari oil sahihi kwa gari yako.
 
Na kuna fundi mwingine nilimuuliza kwa nn nimuuzie mteja oil no 50 kuliko no 30 kama ambavyo sina ya gari yake inataka majibu yake aliniambia tu gari zote za aluminium ndo zinatumia oil hiyo hizo zingine ni mbwebwe tu isipokuwa asitumie no 40 kwa sababu inagandisha oil kwenye engine nikauliza tena no 40 na 50 IPI ni oil nzito kuliko nyingine? Hakujib hadi hivi sasa sijaona jibu so wamiliki wa magari mpende kutuamini sisi tunaowapa oil na mkumbuke kitu sahihi na genuine huwa ni gharama wengi mnapenda oil za bei rahisi ndo maana mnaambiwa mchukue hizo 20w50 wakati unamiliki gari ndogo na je fuso atumie oil ipi? Tafakari chukua hatua gari ni yako na ipende gari yako kwa kuiwekea vitu sahihi
 
Mkuu ninavyofahamu namna bora ya kusafisha injectors ni Ultrasonically.

Hayo mafuta ya kusafishia injectors si yanachukua uchafu kwny tank yanapeleka kwny injectors then ule uchafu unaelekea wapi mkuu?
Ultrasonic ni njia nzuri sana kwa kusafishia parts mbalimbale zenye uchafu, lakini lakini siyo kila dereva au fundi analo karai hilo la ultrasonic. Mafuta ya injector cleaner hayachukui uchafu kwenye tanki na kuupeleka kwenye injector bali hulainisha na kuyeyusha ile carbon build up kwenye injector na kuzifanya zidondoke kwenye combustion chamber na kusukumwa nje pamoja na moshi wa exhaust. Fuel filter ni microsieve ambayo ni iko fine sana kublock particles zote za ndani ya tank, in fact kuna fuel filter mbili kwenye fuel system, moja ndani ya pump na nyingine ndani ya fuel pressure regulator, kwa hiyo hakuna particles za kwenye tanki zinazoweza kuingia kwenye na kuziba injector, kwani zikipita kwenye yale machujio basi zitapita pia kwenye inector..
 
Je 40w 50 inafaa kwa gari ndogo?
Hapana, oil hiyo ni nzito sana kwa injini ndogo; nakushauri usiweke oil inayozidi 10W-30 kwenye gari ndogo. Ushauri kamili ni 10W-20, 5W-30, 10W-30. Ukiweka 10W-40 au SAE40 kwa gari lenye milage kubwa sana utalisikia pia muungurumo wake ukibadilika kuwa kama wa trekta.
 
Mkuu habari na hongera kwa kazi nzuri.

Nina shida na engine ya IZZ. Muungurumo wake umekuwa juu na pia kunakuwa na mlio wa kkkkkkk.

Fuel consuption imeongezeka tofauti na kawaida. Nimebadili plug lakini shida haijaisha bado.

Pia kunakuwa na vibration sana.
Ni mambo gani natakiwa kufanya na tatizo linaweza kuwa ni nini?
Nina injini hii ya 1ZZ-FE, (1794cc), kwenye hii injini, vibrations ni kitu cha kawaida, ila ikizidi, mwambie fundi aangalie engine mounts, kama zile bushes zake zimechoka, ndani utapata mtikisiko mkubwa ukiweka drive na ukasimama kama ukiwa kwenye foleni.

Pili, muungurumo kuwa mkubwa kunaweza sababishwa na oil uliyoweka. Kama umeweka oil nzito mfano 20w 40, lazima injini itakuwa na mvumo mkubwa hasa asubuhi ukiiwasha. Na gari huchelewa kuchanganya.

Tatu, injini hiyo, muundo wake ni kuwa, hasa asubuhi, ukiiwasha, muungurumo huwa juu, na kadri inavyopata moto, muungurumo unashuka. Ukiwa ndani utaona mshale wa RPM unashuka taratibu, ukifika kwenye 650-700 kutoka kwenye 1500, utaona inakuwa calm kabisa, na unaweza kuondoka sasa.

Nne, safisha air filter mara kwa mara. Unapoenda kujaza upepo, toa air filter nayo ipigwe upepo kutoa vumbi.

NB: nimetumia gari yenye injini hii kwa miaka 5 sasa, hayo yote niliyoelezea nimeyapitia. Oil weka 5w 30. Leo nimenunua ya Toyota lita 4, elfu 75.
 
Ndugu yangu Toyota litre 4 iuzwe 75000? Badala ya 90? Kuwa makini umenunua dumu ila oil iliyomo sio ya Toyota
 
Back
Top Bottom