kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,332
- 12,647
- Thread starter
- #21
Huwezi kushika korodan* za baba yako kwa kisingizio cha demokrasia. Hakuna kisichokuwa na mipaka yake popote duniani, jamaa walitudanganya sana kwa maslahi yao. Wote tumepewa majina yetu bila ya kushirikishwa, mbona hatuandamani kuyapinga ili tuchague yale tunayoyapenda wenyewe? Kama muungano wetu uko hivi tukubali tu kuwa waasisi wetu akina Nyerere, Karume na wazee wengine walikosea au walipatia kwaajili yetu, dhamira zao zilikuwa nzuri na zenye faida kwa wakati huo hata sasa na kesho pia. George Washington na wenzake walikosea au kupatia kwa niaba ya wamarekani wote.uko sahihi ndugu kiongozi, nimekuelewa vema sana. Hata na hivyo..
ikibainika tatizo la misingi ni nini kwa hoja na ufafanuzi mujarabu hapatakua na tashwishwi yeyote kwa wananchi kuuangana bila kujali, dini, rangi, kabila au mirengo ya kisiasa na kufanya mageuzi wanayoyataka....
Kwa hali ilivyo nchini na pengine kwasabb ya malezi na itikadi za vyama ndio maana watu hupinga kila kitu na saa zingine bila hata hoja,
lakini pia hali hiyo imechochea tabia ya kudandia kila hoja, kitu ambacho kinadhihirisha dhahiri shahiri kwamba hakuna dhamira ya kweli ya kuongoza mageuzi na ndio maana kupuuzana na kubezana kumekua kwingi pia kwa viongozi wa kisiasa na vyama vyao 🐒
Mfano, UKAWA ndio chanzo cha kutokuwa na katiba mpya wanayoidai leo. Na kilichozuia mchakato wa katiba kuvunjika hadi leo ni watu kutaka aina ya muungano ibadilike, upuuzi huu ndio uliotufikisha hapa. Katiba ile ilikuwa na hata muundo mzuri wa tume huru ya uchaguzi kuliko hii iliyoko sasa, lakini wachwara wakaona muungano ndio kitu cha maana sana kwenye katiba. Hata wazanzibar lazima walidhike na muungano kama ulivyo sasa, wakiendelea kudai na kupewa wanaamsha hamu ya watanganyika nao kudai ili wapewe. Zanzibar itakuwa ya kwanza kuuvunja muungano huu kama wakiendelea na kuuchokonoa muungano kila siku. Maalimu Seif ndio aliyeongoza wimbi la kusitisha mchakato wa katiba mpya.