Mkuu, pole sana! Ndo maisha hayo . . . kua uvikute . . . walituambia wahenga wetu. Ndo hayo ya ukubwa. Hakika mama mtoto kakukosea sana. Kaa, utulie uone namna nzuri ya kumsaidia awe mtu mwenye utu, awe mke na si mpita njia, atambue kwamba vyote vilivyoko nyumbani ni vyake na si vya mwingine kiasi cha kutamani kuviiba. Anamwibia nani sasa? Msaidie atambue kwamba wewe ni wake tu hana mpinzani mwingine mtaani kiasi cha kumfanya akulishe madude ya madawa. Huyo mama hajatulia. Anahitaji tuisheni ndefu na iliyojaa upendo. Akikuelewa umempata mkeo asipokuelewa basi mzee beba huo msalaba, utafanyaje!!
Nakushauri usimwache ndoa. Unahitaji kumsaidia abadilike, akue na kukomaa katika maisha hayo. Akuamini!! Poles sana mkuu. Hiyo nayo ni shule ya aina yake. Liwe ni somo tosha kwako na kwetu wengine.
Nakushauri usimwache ndoa. Unahitaji kumsaidia abadilike, akue na kukomaa katika maisha hayo. Akuamini!! Poles sana mkuu. Hiyo nayo ni shule ya aina yake. Liwe ni somo tosha kwako na kwetu wengine.