Nipeni ufafanuzi wa Upendo wenu kwa Lema

Je ninyi walamba asali mnaovaa uniform za kishoga na kutembea mkinata mkishapewa vyeo hamtaki hata kusogelea tena watu, mnajifanya special miungu watu. Niko radhi kuwavumilia CDM miaka 25
 
Mkuu Emashilla ni nini kimekupata?? Au wewe ndio Maeda??

Back to topic.

1. Josh ni mbunge tangu 4th April mwaka huu ni miezi michache sana compared na uongozi ulokuwa jimboni kabla yake (CCM tokea Uhuru-1961).

2. Kwa miezi hii michache, Ngabobo wana Maji

3. Maroroni na Kitefu wana maji

4. January mwakani wanafunzi wasiojiweza kifedha zaidi ya 100 watalipiwa masomo yao (idadi itaongezeka)

5. Ubadhirifu wa pesa za wananchi umegundulika na kufuatiliwa. (Mfano ni wizi wa million 6 point something ulofanywa na diwani Zuberi na wenzie). Nasari kaugundua.

6. Kwenye ofisi za chama utaona ratiba isiyopuumzika ya Mbunge kuitwa katika mashule na sehemu zingine kuchangia, kusikiza na kujua kero zao.

7. KICHAMA; Mbunge amesaidia ufunguzi wa matawi na kuongeza wanachama.

Tuanotegemea hivi karibuni ni;
Kufufuliwa kwa ile Irrigation Scheme ya kunyeshea mashamba ya mpunga ya leki tatu. Ilitengezwa na wafadhili lakini ilikufa kukosa utunzaji.


Emashilla kamanda wangu. Je hao wengine waliifanyia nini Meru yetu kwa miaka 51 ilopita?

Usiniambie lami ya Nkoaranga (tunamjua aleijenga)

Usiniambie lami ya Tengeru Hospital (tunajua uoga ndio uliijenga na imeishia hosp)

Usiniambie lami ya Ngurdoto (Mrema na wamiliki wenzie wa kisiri wa the Lodge wanayo influence na wakajengewa, kuthibitisha hilo, Lami imeishia mwisho wa shamba).


Kwa miezi michache hii Joshua Nasari (MB) kwa kusaidiana na wapiga kura wake wameijenga Arumeru, tutegemee mengi mengine mazuri.
 
Ukiona mnyonge anaonewa kwa kupgania haki za wengi, wewe utasimama upande wa Mnyonge ama upande wa Mwonevu??
 
Mkuu kwani Arusha wakiamua kukiondoa kabisa chama cha mapinduzi na ofisi zao ina maana hawatapata maendeleo??ina maana fedha za watanzania wote zitabagua wapi wakajenge barabara au wanaangalia wapi chama cha mapinduzi kinakubalika?
 
Nyie Endeleeni Kuwadhihaki Hawa Wabunge wa CDM mkitegemea wananchi bado ni Mbumbumbu!! Ijulikane Mbunge ni Mwakilishi Anaekuwepo Kusimamia Kodi Zetu.

Sasa Nyie Kodi Zetu Mnakula mnategemea Tumlaumu Mbunge!! Ipo siku itabidi Tuwaulize Kodi zetu mlipeleka wapi? Mbona Mbunge Wetu alikuwa anasimamia Hewa?
 
Ameirudisha arusha miaka 20 nyuma, vijiwe vya majobless vimeongezeka, biashara ya mbege na bangi imeshamiri. Hayo ndio aliyo wafanyia wana arusha. Wanamshabikia kwasababu haya mambo ndio wanayataka.
 
View attachment 65583
Barabara za Arusha nasikia zimejengwa/Zinajengwa na Serikali ya CCM kwa kushirikiana na wapenzi wa CCM!

Enyi CHADEMA Arusha kuna nini kinachopelekea watu kukosa Imani kwa Chama Cha Matatizo na kuamua kumpenda Lema?

Tafadhali, nijulisheni aliyoyafanya Lema hapa Arusha na nchini Tanzania.

Siasa inahitaji darasa,na njia pekee ya kulikomboa jimbo sio propaganda ni kutekeleza ahadi,mfano CCM si walitoa ahadi arusha ingawa mbunge ni wa CDM wanaweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kupitia serikali,mimi ningependa wananchi wachague wabunge wa upinzani na kupitia hilo serikali itaamka na kupitia harakati mbalimbali za kukomboa majimbo maendeleo yatapatikana tu,maana watu wakipewa madaraka wanajisahau sana na siku zote kupitia ushindani wa kupeana madaraka maendeleo yanakuja.
 
kabla ya kukujibi watakiwa kufafanua kuwa maendeleo tulio nayo kwa miaka 50 ya uhuru tuna stahili ili ujibiewe walicho fanya wabunge hawa muda mfupi walio kaa madarakani
 
Wanachadema wanakuwa wakali wanapoulizwa maswali critical kama haya, ila naomba watumie hii fursa vizuri ili waweze kuvutia watanzania ambao bado hawajawa na msimamo wa kiitikadi.

Ila vilevile wananchi nao wapate fursa ya kuona, kuchambua na mwisho kufanya maamuzi juu ya nafasi nyeti na yenye heshima hapa nchini walizopewa wapinzani, nafasi ya uwakilishi wa wananchi katika bunge tukufu la jamhuri ya muungano wa tanzania.

Tupunguze ushabiki katika kuorodhesha mambo aliyofanya mbunge huyu tangu wana-arumeru mashariki walipompa ridhaa.

yaani CCM baada ya miaka 50, ndo leo Tu mnapata msaada wa kujenga barabara Arusha? By the way, nampenda Lema kwasababu kwa muda mfupi aliokuwepo pale bungeni ameongea mambo mengi mema ambayo yamewafanya magamba muweweseke sana, hasa yule "mtoto wa mkulima, PM"
 
yaani CCM baada ya miaka 50, ndo leo Tu mnapata msaada wa kujenga barabara Arusha? By the way, nampenda Lema kwasababu kwa muda mfupi aliokuwepo pale bungeni ameongea mambo mengi mema ambayo yamewafanya magamba muweweseke sana, hasa yule "mtoto wa mkulima, PM"
 
CCM mtarukaruka, mtalia, mtafanya kila jambo kwa back up ya mahakama na polisi lakini arusha hatuwahitaji milele.
Lema katuletea ambulance nne mpaka sasa wagonjwa wetu wasio na uwezo wanapata huduma hii.
Lema kaanzisha mradi wa kusomesha watoto zaidi ya 400 wasio na uwezo wakiwepo yatima pamoja na wale waliopo kwenye mazingira magumu.
Lema amekua akisimamia haki za kina mama wanaosomesha watoto wao kwa kuuza nyanya na vitunguu pembezoni mwa barabara.
Lema amekuwa mwalimu wetu wa ujasiri kuanzia kwa watoto, vijana hadi kina mama ndio maana mpaka leo harakati zetu za kuupinga mfumo mbovu wa serikali hazitishi kwa mtutu wa bunduki wala mabomu ya machozi.

NB: ujenzi wa barabara arusha na maeneo mengine mengi tz ni mradi World Bank, pia hata pale panapofanyika miradi ya serikali fedha inayotumika ni kodi zetu tunazolipa kila kukicha, nakushauri hizo story kwamba barabara inajengwa na ccm nenda kawaadithie green guards wenzako ambao mko nao utumwani.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Dah!,cjui mi ndo sielewi au hailiweki!,mtoa mada kauliza aliekua mbunge wa Arusha mjini(Lema) kawafanyia nin wana arusha mpaka wampende,ila naona watu wanafanisha oo mara nagu oo lusinde yote yanatoka wap!,Tuachen siasa za kwenye khanga kama kuna mtu anajua au yeye mwenyewe arrespond!,tunapiga siasa kila mahali!!,duuuuuuu!!!!!!!!!!!!
 
Mimi ni mwana Arusha. Kwa kuamini dhamira njema ya swali lako mimi najibu kama ifuatavyo.

1. Nimetumia haki yangu ya kikatiba kumchagua (kama ina maana ya upendo poa)

2. Nilipewa kuchagua kati ya CDM na CCM nikachagua CDM kwa sababu CCM ni chama chenye wenyewe na mimi si mmoja wao.

3. Kama serikali ya CCM na "wapenzi" wake wanajenga barabara ili wapendwe ni sawa ila pendo ni hiari si shinikizo.

4. Serikali kujenga barabari ni wajibu wake uliochelewa

5. Nilichagua taasisi ya kibunge ya jimbo kwa msingi ya kushawishiwa na kuchagua kati ya wagombea. Kati ya Matilda Buriani na Lema; Lema alijitenganisha kwa hoja, tabia na uwajibikaji.

6. Dogo janja usipime ni wakala wa mabadiriko
 
hata fisi wa serengeti hupewa dawa na wafadhili bila CCM.Arusha ni mikopo ambayo kila raia analipa wala CCM hawana cha kujivunia hapa.

Mkuu unajua ni wachache sana wanaojua wajibu wa serekali kwa raia wake. Ni wajibu wa serekali kujenga shule,zahanati,barabara na kila aina ya huduma kwa raia wake ni hawapaswi kujenga na kuacha ni wajibu wao pia kuhudumia hivyo vitu. Sasa kama serekali inakusanya kodi halafu ikijenga barabara inajisifu ni dalili ya serekali kukimbia majukumu yake. Kodi zetu ndio zinafanya haya yote kwani hata mkoloni alijenga shule na njia !
 
Na umasikini wa Wana-Arusha walio wengi umesababishwa na sera mbovu za CCM. Na wizi wa rasilimali za Arusha na Tanzania kwa ujumla unasababishwa na sera mbovu za Serikali ya CCM... Alichofanya Lema na anachoendelea kukifanya ni kushiriki harakati za kuikomboa Tanzania na watanzania dhidi ya mfumo dhalimu wa CCM.
Hivi wale twiga walibebwa wapi wakapelekwa Quatar?
Hivi ni nani aliruhusu DEGE la jeshi la Nchi nyingine kuja kukwiba Twiga wetu?
 
Wanachadema wanakuwa wakali wanapoulizwa maswali critical kama haya, ila naomba watumie hii fursa vizuri ili waweze kuvutia watanzania ambao bado hawajawa na msimamo wa kiitikadi.

Ila vilevile wananchi nao wapate fursa ya kuona, kuchambua na mwisho kufanya maamuzi juu ya nafasi nyeti na yenye heshima hapa nchini walizopewa wapinzani, nafasi ya uwakilishi wa wananchi katika bunge tukufu la jamhuri ya muungano wa tanzania.

Tupunguze ushabiki katika kuorodhesha mambo aliyofanya mbunge huyu tangu wana-arumeru mashariki walipompa ridhaa.

Hapo kwenye mstari una uhakika na unavyopaita? Maana km pako unavyosema ina maana na wakaao humo ni WATUKUFU, kitu ambacho hata kwa hali ya kawaida SI KWELI!
 
View attachment 65583
Barabara za Arusha nasikia zimejengwa/Zinajengwa na Serikali ya CCM kwa kushirikiana na wapenzi wa CCM!

Enyi CHADEMA Arusha kuna nini kinachopelekea watu kukosa Imani kwa Chama Cha Matatizo na kuamua kumpenda Lema?

Tafadhali, nijulisheni aliyoyafanya Lema hapa Arusha na nchini Tanzania.
Kama huna data usiongee kabisaa, barabara za Arusha na zile za Mbeya hazijengwi na CCM, tena wafadhili wa hizi barabara waligoma kuwapa pesa mkononi wanaserikali ya CCM maana wanawajua kwa uchakachuaji "Tumbo kwanza maendeleo baadaye". Waliamua kusimamia maswala ya pesa wenyewe na ndio maana unaona ufanisi wa kipekee
 
Back
Top Bottom