Je habari hii haina public interest? Mhariri gani asiyejua habari za maslahi ya kitaifa? Why not IPP media?
ebwana wee yaaani magazeti yote yawe yanaandika habari moja? na tv & redio zitangaze habari mamoja? tembea uone nchi zingine magazeti/media zinavyofanya kazi.
Mkuu,
Nadhani ungefanya utafiti kwanza na kujua kama ilikuwa ni habari gani kwa siku hiyo.
Kwa taarifa yako lile tukio ndiyo liliyokuwa habari kubwa katika habari za michezo kwa siku ile. Basi hata kama IPP ingeona kuwa haina umuhimu wa kuipa nafasi ya kuchukua uzito wa juu, basi ingeiripoti kama habari ya kawaida. Pia katika hali ya kawaida haiwezekani magezeti yote ya IPP, Redio na Televisheni hazikuona umuhimu wa kutoa taarifa ile ya kijamiii...KULIKOOONI?
Na sio habari hiyo tu,kuna mambo mengi hivi sasa sisi washabiki wa ipp tunakosa,hivyo inatubidi kuhaha na kutafuta pa kujikwamua na kupapata.nawaomba uongozi mzima,utufikirie sisi wapenzi wa ipp kwani,kupata habari na matukio makubwa yanayoendelea au kutokea duniani,tunawategemea zaidi wao.Huo ni mtizamo Finyu kwa IPP media wakati Tz hasa wasomaji wake ni pia waislam jee hawanyimi haki waislam kupata habri kama hizo?
Mkuu wangu chombo chochote kina uhuru wa kutangaza au kuto kutangaza habari fulani for whatever reason iwe personal au professional. Kinacho paswa kukemewa ni habari fulani kuwekwa kiupendeleo na si habari fulani kuto kuwekwa. Hawaja vunja sheria yoyote kwa kuto tangaza habari hiyo. Na kama vyombo vingine vili tangaza basi inatosha si habari ilifika? Au unataka kusema kisa ni Manji aliyetoa msaada ndiyo maana hawa kuweka hiyo taarifa?
Haya bwana mkuu.Mkuu,
Tuwe wakweli, ni nani hapa yuko huru kuandika habari mmiliki au editors wa vyombo vyote vya IPP?
Mbona sijaona hata siku moja vyombo hivyo havikuandika matokeo ya mechi ya ligi kuu yaliyofanyika siku ya pili yake ati tu kwa sababu vyombo vingine vilikwisha ripoti mechi hiyo? au mbona vyombo hivyo vya habari vimekuwa vina ripoti juu ya sherehe za may mosi ambazo tayari zimekwisha ripotiwa na vyombo vingine? Kama hujui ni kwanini IPP haikuandika habari za Yanga siku ile bora ukae kimya au ufanye utafiti kwanza.
Kuna uwezekano mkubwa kabisa mmiliki wa IPP ndiye anayeamrisha ni habari gani iende kwa wasomaji kwa kadri ya matakwa yake na wala siyo ya watumiaji wa habari. Hisia hizi zinajengwa na mafanikio aliyoyapata Yusuf Manji katika kusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi aliingia kuutatua lakini alishindwa. Hasira zake alikuja kuzimalizia kwa kukataza habari za mafanikio ya klabu ya wananchi yasitangazwe katika vyombo vyake. Upo hapo!