Somo zuri kutoka uchaguzi wa Kenya ambalo watawala wa Tanzania na CCM hawataki kulisikia.

Shahed kamikaze

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
575
959
Mambo 10 yanayoutofautisha uchaguzi wa Kenya na nchi zingine Afrika
19 Agosti 2022

Na Yusuph Mazimu
BBC Swahili
Kenya elections

Kenya imefanya Uchaguzi wake mkuu Agosti 9, 2022, na kumchagua William Ruto kuwa Rais wa tano wa taifa hilo, akimuangusha mwanasiasa mkongwe, Raila Odinga, aliyekuwa anagombea kwa mara ya tano na aliyekuwa anaungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta, anayemaliza muda wake.
Ni uchaguzi wa saba wa mfumo wa vyama vingi na wa tatu tangu kuanzishwa kwa Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC). Waangalizi wengi wa uchaguzi huo wameusifu.
MATANGAZO

th

Nimeshiriki chaguzi 5 Tanzania kama mpiga kura, chaguzi 4 kama mwandishi wa habari, na uchaguzi mmoja kama msimamizi msaidizi wa kituo cha uchaguzi, katika jimbo la Moshi mjini, katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Lakini nimefuatilia kwa karibu chaguzi zingine kama za Uganda, Rwanda, DRC, Ghana, Afrika Kusini na Nigeria.

Hivyo kuwa kwangu karibu mwezi mmoja nchini Kenya kufuatilia na kuripoti uchaguzi wa mwaka huu nimejifunza mengi lakini haya 10, nayaona yakiutofautisha kwa kiwango fulani, uchaguzi wa mwaka huu Kenya na chaguzi za nchi nyingi za Afika.

1: Uwazi mkubwa usio wa kiafrika​

Kenya elections

Kila mmoja ameshuhudia uchaguzi wenye uwazi mkubwa kabisa katika historia ya chaguzi nyingi za Afrika.

Kulikuwa hamna namna nyingine yoyote ya kupunguza malalamiko, makasirik au ghasia zaidi ya kuwa na uchaguzi ulio huru na wazi.

Mauaji ya watu zaidi ya 1000 baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na maamuzi ya Mahakama ya juu baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 yamebadilisha kabisa mfumo wa uwazi katika uchaguzi wa Kenya.

Siku ya kupiga kura, nilitembelea vituo mbalimbali vva kupiga kura katika kaunti ya Nyeri kikiwemo cha shule za msingi Temple na kile cha Sagana alichopiga kura mgombea mwenza wa Kenya Kwanza, Rigathi Gachagua.

Mawakala walikuwa huru kutekeleza majukumu yao, uamuzi wowote wa jambo lolote ulikuwa wazi na kila mmoja alishirikishwa.
Kenya elections

Maelezo ya picha,
Kwenye simu yako ya Mkononi uliweza kufuatilia matokeo ya uchaguzi kupitia mtandao wa Tume auchaguzi, IEBC
Tume ya uchaguzi, IEBC ilifungua ‘Online Portal’ kuruhusu mtu yeyote kufuatilia matokeo ya Uchaguzi kwenye mtandao. Fomu 34A kutoka vituo vyote 46,000 vya kupigia kura kutoka kaunti zote 47 za nchi hiyo zilipakuliwa humo.

Siku moja tu baada ya uchaguzi (Agosti 10, 2022), IEBC ilianza kuweka Fomu 34B zinazotayarishwa na maafisa wa Uchaguzi wa majimbo wakianza na eneo bunge la Saboti.
Ruka Twitter ujumbe, 1

Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Kama ulikuwa na simu ‘janja’ ama kompyuta, hukuhitaji kusubiri matangazo ya maafisa ama Makamishna wa tume ya uchaguzi kujua kura yako inaendaje.

Vituo vyote vya habari, vilikuwa na uhuru wa kutangaza matokeo kutoka kwenye mfumo wa tume. Na tume ilisema wazi kuwa kutofautina kwa matokeo yanayotangazwa na vituo vya televisheni kusiwachanganye, ni kasi ya kujumlisha ya kila kituo cha habari lakini matokeo ya mwisho yatathibitishwa na Tume.

Mawakala wa vyama waliruhusiwa kupiga picha matokeo na kupewa nakala za matokeo, wananchi walitangaziwa papo hapo matokeo kwa vipaza sauti, kila mmoja alifahamu matokeo na namna mambo yalivyokuwa yanaenda.

Hakukuwa na kutangaza matokeo kwa kuvizia. Hili limepunguza malalamiko na migogoro mingi ambayo awali ilisababisha ghasia mpaka mauaji na uharibifu mkubwa wa mali.

2: Uwekezaji zaidi kwenye teknolojia ya uchaguzi​

Kenya elections

Kenya inatajwa kama nchi iliyowekeza zaidi kwenye matumizi makubwa ya teknolojia kwenye uchaguzi kwenye eneo la Afrika mashariki na kati.

Nilikuwepo katika Shule ya msingi Kerogoya, Kaunti ya Kirinyaga wakati maafisa 296 wa vituo vya uchaguzi 148 wa eneo bunge la Kirinyaga ya kati wakipewa vifaa vya kisasa kabisa vya uchaguzi.

Hawakuanza leo Kenya kuwa na vifaa vya aina hii. Ilianza tangu uchaguzi wa mwaka 2013. Uchaguzi wa mwaka 2017 nchi hiyo ilinunua vifaa vya kisasa vya uchaguzi, Kenya Integrated Electoral Management System (KIEMS) zaidi ya 45,000 kwa zaidi ya shilingi za kenya bilioni 6.8, kabla ya kuongeza vingine kama 10,000 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.
th

Ruka Twitter ujumbe, 2

Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 2
Vituo vyote 46,000 vya kupigia kura viliunganishwa na mtandano wa internet ili kuruhusu uwasilishaji wa matokeo kwa haraka. Hawakutegemea umeme wa kwenye mashule, taa za kisasa za sola, laptop na tablet za kisasa, zilirahisisha kuhesabiwa kwa kura wakati wa usiku na uwasilishaji wa matokeo kwa wakati.

Lengo la uwekezaji huu mkubwa ni kuhakikisha uchaguzi wao unakuwa wa uwazi zaidi.

3: Sheria na taratibu za uchaguzi ni rafiki kwa demokrasia​

Kenya elections

CHANZO CHA PICHA,CITIZEN
Maelezo ya picha,
George Wajackoyah, alinadi bangi katika kampeni zake za kuwania urais wa Kenya mwaka huu
Ukiacha kanuni mbalimbali za uchaguzi, mfumo wa uchaguzi Kenya unasimamiwa na sheria 7, ikiwemo Katiba ya nchi hiyo ya mwaka 2010, Sheria kuu ya Uchaguzi ya mwaka 2011; Sheria ya makosa ya Uchaguzi ya 2016, Sheria ya Vyama va siasa ya 2011, Sheria ya Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka ya 2011, Sheria ya gharama za uchaguzi ya 2013 na Sheria ya masuala ya uongozi namaadili ya mwaka 2012.
Katiba ya nchi hii imeruhusu tume huru ya Uchaguzi, tume yenye uhuru wa kiwango cha juu, licha ya misukumo na ushawishi wa wanasiasa iliyopo.

Ni tume isiyopokea ‘malekezo kutoka juu’.
Sheria kwa mfano ya uchaguzi, 2011 haitoi mianya ya wazi ya mgombea kupita bila kupingwa ama kukatwa kwa wagombea kwa makosa ya ‘kufikirika’, zaidi zinaleta fursa ya kuwa na wagombea wenye ushindani wa kweli kwenye uongozi.

Sijashuhudia wala kusikia mgombea amenyimwa fomu ya uchaguzi kwa sababu afisa uchaguzi anaumwa au yuko nje ya ofisi au amejifungia ofisini. Sijasikia wala kuona afisa anakataa kupokea fomu ya mgombea yeyote iliyojazwa au wagombea kuzuiwa kufanya kampeni ama mawakala kunyimwa vibali vya kuingia vituoni. Kwa sababu Sheria zinabana na zinasimamiwa kisawasawa.
Ruka Twitter ujumbe, 3

Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Twitter ujumbe, 3
Wagombea walikuwa huru kupita kwenye vituo kuangalia mambo yanavyokwenda, sikusikia wala kuona mgombea aliyekimbizwa kituoni, kujeruhiwa ama kuwekwa ndani.

Waangalizi wa kila upande waliruhusiwa, hakukuwa na mipaka yoyote kwao katika shughuli zao kisheria.

Sheria za Kenya zinaruhusu matokeo mfano ya rais kuhojiwa mahakamani. Raila Odinga, mgombea urais kupitia Azimio, amepinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Ruto, na anaelekea Mahakamani.

Mahakama nazo zina uhuru fulani usiolalamikiwa kwa upendeleo. Sheria inaruhusu na hivyo kuifanya haki za vyama na wagombea kutendekana na kuimarisha demokrasia.

4: Wagombea wanawake, Vijana, wagombea huru na wenye ulemavu ni zaidi ya funzo​

Kenya elections

Maelezo ya picha,
Mmoja wa wagombea mwenye ulemavu aliyeshinda uchaguzi wa Kenya mwaka huu
Wanawake wamenishangaza Kenya. Macho yao hayako kwenye viti maaalumu kama Tanzania.

Wanaingia kugombea. Kuna wawakilishi wa wanawake bungeni, wanaochaguliwa na wapiga kura wote kama mbunge mwingine yeyote.
th

Ukiacha hivyo nimeshuhudia uchaguzi wenye makumi kwa makumi ya wagombea wenye ulemavu, wagombea huru na wagombea wanawake wakichuana na kushinda kwenye nafasi za juu kabisa za kuchaguliwa kama ugavana, ubunge na udiwani

Play video, "Kutana na Linet Chepkorir ‘Toto’ mbunge wa kike mwenye umri mdogo zaidi Kenya", Muda 1,35

01:35
p0cthpb6.jpg

Maelezo ya video,
Uchaguzi wa Kenya 2022:Kutana na Linet Chepkorir ‘Toto’ mbunge wa umri mdogo zaidi Kenya
Nilipokuwa Kaunti ya Nakuru nilikutana na mgombea wa nafasi ya udiwani, (MCA), mwenye ulemavu wa miguu akipita kwa magongo nyumba kwa nyumba kuomba kura.

Martin Wanyonyi, yeye ameshinda ubunge wa eneo la Wabuye Mashariki na kuwa Mkenya wa kwanza mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kushinda ubunge.

Nilikutana pia kwenye makazi yake, Gavana mteule wa Meru, Kawira Mwangaza, ‘binti wa kazi za ndani (house girl)’ wa zamani, aliyembwaga mwanasiasa mkongwe Kiraitu Murungi. Ukiacha mwakilishi wa bunge mdogo kabisa mwenye umri mdogo zaidi Kenya, Linet Chepkorir ‘toto’ binti mwenye miaka 24.

Yupo George Nenem, kijana wa miaka 22, aliyeshinda udiwani kwenye Kaunti ya Nakuru, ambayo karibu nafasi zote kubwa wameshinda wanawake.
Hili linakuonyesha uwanja mwingine kabisa wa siasa za kidemokrasia kwenye uongozi.

Wagombea wengi tu wasio na vyama (wagombea huru) wameshinda kwenye nafasi walizogombea. Unapimwa kwa uwezo wako zaidi kuliko nguvu ya chama chako, jinsia yako ama muonekano wako.

Play video, "Fatuma Achani ashinda ugavana Kwale", Muda 2,58

02:58
p0cv2d8w.jpg

Maelezo ya video,
Matokeo ya uchaguzi Kenya:Fatuma Achani ashinda ugavana Kwale

5: Uhuru wa kuripoti na kupeana taarifa​


Maelezo ya picha,
Katika baadhi ya maeneo ya nchi, wananchi waliwekewa Skrini kubwa za kufuatilia matokeo
Hili ni jambo jingine lililonifunza kwenye uchaguzi wa mwaka huu wa Kenya.

Nilitumia siku 12 kuripoti taarifa za Uchaguzi katika Kaunti ya Nyeri ikiwemo kushuhudia zoezi la upigaji kura siku ya Agosti 9, lakini kilichonishangaza ni namna watu walivyokuwa huru kupeana taarifa.

Kufikia saa 2 usiku, watu wengi wenye simu za mkononi, redio na runinga katika maeneo nilikopita kama Mathira, Othaya, Tetu na Nyeri mjini walikuwa na taarifa za matokeo ya awali na picha za nakala za matokeo. Lakini sikuona mtu aliyekamatwa kwa kumpa mtu taarifa za matokeo wala kubughudhiwa.

Sheria zinatambua kwamba ni haki yao ya msingi. Ukiacha kupewa ruhusa ya kuchukua na kufuatilia matokeo kwenye ‘Portal’ maalumu ya tume ya Uchaguzi na kuripoti, waandishi na vituo vya habari tulipewa uhuru mkubwa wa kuripoti.

Bomas, kituo kikubwa cha kujumlisha kura ilikuwa kama kambi ya wakimbizi, vituo karibu vyote vya ndani na nje vilivyopewa vibali, vilikuwa na mahema na studio zao za muda, vikiruhusiwa kuripoti kila tukio.

Maelezo ya picha,
Afisa mkuu wa Uchaguzi katika Kaunti ya Nyeri, Anastacia Nduku (kushoto) alinipa muda wa kutosha kuzungumza nae kuhusu utaratibu wa majumuisho ya kura katika kituo kikuu cha majumuisho ya kura kwenye chuo cha Ufundi Nyeri.

Nakumbuka kutumia na kutangazia matangazo ya moja kwa moja kwenye moja ya kumbi za hoteli katika kaunti ya Nyeri, tena bure zikiwa huduma zote mpaka viburudisho, internet yenye kasi kubwa zilizotengwa kwa ajili ya wanahabari ili kusaidia kupashana taarifa.

Kwa hili, Baraza la habari Kenya, MCK limenifanya nione Baraza la habari Tanzania, MCT, lina safari ndefu ya kuandalia waandishi wa habari wa Tanzania, mazingira mazuri ya kuripoti habari za uchaguzi, kwa faida ya wananchi, na si upande wowote wa wanasiasa ama vyama.

Wagombea, wananchi wenyewe na hata watumishi wa Tume ya uchaguzi, IEBC, hawakufungwa mdomo, wakati wowote ulipowahitaji kwa mahojiano, ama ufafanuzi walitoa ‘ushirikiano wa ajabu’. Nakumbuka kufika katika kituo kikuu cha majumuisho katika chuo cha Ufundi Nyeri, Afisa mkuu wa Uchaguzi wa IEBC katika Kaunti ya Nyeri, Anastacia Nduku , alikutana na waandishi wa habari na kuondoka, lakinini alilazimika kuacha shughuli zingine na kurudi kunisikiliza nilichokua nahitaji kwa ajili ya kuwahabarisha wasikilizaji wa BBC.

Kwa muda wote niliyokuwepo Kenya sikusikia umeme ukikatika ama mtandao wa Internet kuzima ama ‘kuzimwa’ kwa lengo lolote la kiufundi ama kuzuia taarifa.

6: Polisi walikuwa walinzi wa usalama, hawakulinda kura za mtu au chama​


Jukumu la Polisi linafahamika ni ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Katika vituo vya uchaguzi wa Kenya, nilivyotembelea kulikua na walinzi watatu mpaka 6 kulingana na idadi ya vituo hasa kwenye shule. Kazi yao ilibaki kulinda tu usalama wala hawakumlindia kura mgombea ama chama fulani.

Hata katika baadhi ya maeneo palipoonekana kama kuna harufu ya mzozo kidogo, waliingilia kati bila kutumia mabavu, wakatuliza na kurejea kwenye nafasi zao.

Ni nadra kushuhudia hilo kwa nchi nyingi za Afrika. Zaidi Polisi wangeonekana kutumia nguvu kuhakikisha watawala wanashinda Uchaguzi. Kenya sikuona hilo mwaka huu na kama lilikuwepo katika baadhi ya maeneo ambayo sikufika, basi lilifanyika kwa kificho sana.

7: Wagombea wote wanapewa heshima na thamani sawa​

Hili ni jambo jingine usilotarajia kuliona katika nchi nyingi za Afrika. Julai 30, 2022, majira ya saa tatu asubuhi nikitoka chumbani kwenye moja ya hoteli niliyofikia, katika kaunti ya Nakuru, nakutana na ulinzi mkali na msururu wa walinzi zaidi ya 30 wakiwa na bunduki. Sikufahamu haraka, lakini nilipofika kwenye eneo la kunywa chai, nikamuona George Wajackoyah, mmoja wa wagombea wanne wa urais Kenya aliyekuwa na hoja ‘tata’ ikiwemo kuhalalisha matuizi ya bangi katika sekta ya viwanda.

Ulikuwa ulinzi kwa ajili yake, alikuwa anaongozwa na maafisa usalama na kulindwa kama alivyokuwa analindwa Naibu Rais, William Ruto. Ruto pamoja na kuwa na mikwaruzo na Rais Uhuru Kenyatta alipata huduma zote kama ilivyokuwa kwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga, aliyekuwa anaungwa mkono na Uhuru na Serikali. Haukuwa ulinzi wa ‘kujionyesha’, ulikuwa ulinzi wa kweli kweli kama kanuni na sheria zinavyotaka.

Pia katika siku 15 nilizoshuhudia kampeni za uchaguzi na kukutana na wagombea mbalimbali wa nafasi za Useneta, Ugavana, Ubunge na udiwani, sikushuhudia wala kusikia mgombea amezuiwa kufanya kampeni kwa sababu ni mpinzani, ama alinyimwa ulinzi kwa sabau haiungi mkono serikali ama kwa sababu zozote zile.

Iwe mpinzani ama mgombea huru, huduma kwa mujibu wa sheria za uchaguzi unazopaswa kupata kama mgombea ulihudumiwa kwa thamani ile ile.

8: Kama huna pesa, uchaguzi utakuwa mlima mrefu usio na kilele​


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Sikatai uwepo wa wagombea wachache sana, walioweza kuchaguliwa kwa kutumia fedha kidogo, lakini wengi lazima uandae fungu kubwa zaidi la fedha kuweza kuchaguliwa. ‘mie sikuwa na pesa, nilitumia Ksh 750,000 tu’, (wastani wa dola 6,000 za Marekani au wastani wa shilingi milioni 14.5 za Tanzania) alinambia mgombea mmoja wa Udiwani katika eneo bunge la Othaya.


Utafiti wangu mdogo baada ya kuzungumza na wagombea wateule wanne wa nafasi mbalimbali, ili kuwania udiwani unahitaji angalau kuwa na kiwango cha chini cha dola 200,000 (zaidi ya 400mil za Tanzania, Ubunge uwe na mara mbili ya udinwani, angalau dola 400,000 huku Useneta uwe na angalau mara mbili ya ubunge.

Ndo maana haishangazi kuona wengi wa wanaowania nafasi za uongozi Kenya, ni watu wanaojiweza.

9: Uchaguzi wa mtu na sio vyama ama ushawishi wa mamlaka​


Maelezo ya picha,
Gavana mteule wa Meru, Kawira Mwangaza (kushoto), akiwa na mumewe aliyekuwa anatumia gitaa kumuombea kura mkewe. Mwangaza ameshinda bila chama, akigombea nafasi hiyo kubwa kabisa kama mgombea huru.

Nchini Tanzania, pamoja na nguvu ya mtu, chama cha siasa kina nafasi na mchango wa moja kwa moja wa ushindi au kushindwa kwa mgombea. Wapo wachache wenye majina anayojiuza kuliko chama, lakini wengi vyama Kauli ya ‘kuunga mkono juhudi, ilishamiri sana wakati wa uchaguzi wa mwaka 2022.

Sikuliona hilo sana kwenye uchaguzi wa mwaka huu Kenya.


Tangu natoka Kaunti ya Nairobi kwa njia ya barabara mpaka kaunti za Nakuru, Murang’a, Nyeri, Kirinyaga, Nyandarua, Meru na Laikipia sikuona bendera yoyote ya chama barabarani. Zaidi ni mabango mengi ya wagombea.

Chama ni msingi, lakini uwezo wa mtu, asili yake (kabila) na namna gani anaamika kwa wapiga kura, yalikuwa mambo makubwa zaidi waliyozingatia wapiga kura kuliko chama anachotokea.

Chama cha UDA, hakina hata miaka miwili tangu kutambulika kwake, lakini kimetoa mshindi wa urais, William Ruto na kujitolea viti zaidi ya 100 vya ubunge. Kiliweka wagombea 261 katika majimbo 290.

Jubilee, chama tawala anachotoka Rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyetta kimepata viti 23, huku chama kilichoasisi taasisi hilo, KANU kikiwa na viti 3 tu.

10: Kampeni kwa Kilugha​


Ilinipa shida katika baadhi ya maeneo, ambapo ilinilazimu kusikiliza kampeni kwa lugha ya kikuyu, hasa eneo la Mlima Kenya, kwa sababu ilikuwa rahisi zaidi kwa wagombea kujitangaza kwa lugha hiyo.

Ni jambo la kawaida katika maeneo mengi ya Kenya hasa za mikoa kusikia kampeni kwa kwa lugha za asili.
Kigooco FM, Gukena FM, Inooro FM, Kameme FM, Coro FM, Iganjo Fm, Rware FM ni radio maarufu nilizosikia zikiangaza kampeni kwa lugha ya Kikuyu.

Wapo wagombea walioandika mabango yao ya kampeni kwa lugha za asili. Na hili linaonyesha kwamba bado, kuna safari kwa nchi hii kuumaliza ukabila. Ukabila bado una mizizi mikubwa, pengine hili linaweza kuwa kasoro kubwa katika uchaguzi wa nchi hiyo.

 
Back
Top Bottom