Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
Kuna haja ya kuweka mikutano kwenye YOUTUBE ili watu wasikie au sisi kama wadau wa JF tunaweza kufanya hivyo maana leo mambo mengi sana Chadema walisema na CCM walifanya hivyo na pia kuna sera nyingi sana ambazo CCM walikuwa wanaiga toka CHADEMAmchungaji maswali yako na nadharia yako ni tamu sana. Lakini sisi ni nchi ya amani, umoja, mshikamano na utulivu. Kutafuta majibu ya maswali hayo ni sawa na kupandikiza mbegu za chuki na mgawanyiko katika jamii hasa majibu yatakapotolewa kuwa serikali "iko mbioni", "ina nia", "imeanza mchakato" na "ina makusudio" ya kuyashughulikia masuala hayo yote "pindi wafadhili wakipatikana".
Sasa Chadema ikianza kuyapush maswali hayo inaweza kuwafanya waonekane wanataka kuleta mgawanyo na wao wenyewe siyo watu wanaopenda confrontation za kisiasa. Ni kwa sababu hiyo usitarajie kwenye OS kuona wakibeba mabango ya kuwapinga wabunge mbalimbali au CCM au wanachama wao kuandamana hadi kwa mbunge wa CCM kutaka asigombee tena.
Msingi wa OS (niko tayari kusahihishwa) ni hoja za kisomi za kwanini hali ipo jinsi ilivyo. Hoja hizi zinaendana na uanishaji wa hali halisi kwa kutumia takwimu mbalimbali, vielelezo mbalimbali na mifano mbalimbali ambayo inalenga kushawishi akili. Kwa kiasi kikubwa siyo "siasa proper" kama mifano ya karamu za Chai.
Kwa hiyo uelewa wangu wa OS imefanikiwa sana kuwavutia watu kujiunga na Chadema, sijui kwa kiasi gani watu hao watageuka kupigia kura hasa kama CCM itaamua kwenda full throttle kuwabana wapinzani na kuwavutia wananchi.