Nini tufanye kama JK atamteua e lowassa kuwa waziri mkuu?

Yaan huyo fisadi akirudi kwenye chat basi hamna rangi tutaacha kuona watanzania.
 
Tulianzishe sasa kama vipi.haiwezekani nchi yetu inachezewa tu halafu tunakaa pembeni tunalalama. akimleta tunaingia mitaani.hiyo ni haki yetu n kikatiba.
 
Kwani tutafanyaje zaidi ya kuchekelea. La kufanya lilikuwa Oktoba 31, 2010, tukasema anafaa. Hivyo tutasema zidumu fikra zake make tushakuwa watu wa ndiyo mzee kwa kila kitu. Tusubiri miaka mitano ya maumivu tena.
 
Lowasa si waziri mkuu mstafu wala hakujiuzuru bali alifukuzwa kazi na bunge.unapomtaja lowasa kumbuka kusema 'waziri mkuu aliyefukuzwa' sio aliyejiuzuru ok? Usiwe kimeo kama tbc1
 
hakuna kitu mtafanya zaidi ya kelele tuu na magazeti yenu ya shigongo....ila 2015 CCM must go!
 
Maswali haya ya ajabu sana! JK ni rais na anauwezo wa kufanya lolote lile!

JF haina uwezo wa kufanya chochote kile kwa namna yoyote ile zaidi ya kuandika tu humu.

Tunaposema jamani pigeni kampeni, waelezeni watu habari njema ya wokovu ya kuwa ccm IONDOKE MADARAKANI huwa hamfanyi, mnasubiri kuuliza maswali kama haya

JK ana dola, ana nguvu, ni rais-ebo!!! he can do anything in his capacity ili mradi amefuata katiba husika! kama EL na RA wamekuwa wabunge ndio mwazo wa kuwa mawaziri.....This time will never even dare to talk malicious about JK will sit down and ask myself---who voted for these people? ukipata jawabu utagundua ubaya wa hawa watu haupo kwa wala haujulikani kwa watu wote!!!

EL an uwezo wa kuwa waziri, na bado akawa rais 2015-2025!!!! inawezekana tu, CCM wakiweka jiwe bado litapita tu kuwa rais

we need to change NEC tell those who call themselves fighters to do this ASAP , au wakae kimya milele!
 
Kwani kuna tabu,ila wajue mwisho watanzania wataingia mtaani hata kabla ya 2015 kukomboa nchi yao kwa manyangau!
 
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............

Itakuwa hamna tatizo kama kati ya wabunge 230+ wa CCM hakuna aliyeko tayari ku-waziri mkuu au kama wote watakaopendekezwaku-waziri mkuu ama watakataa au kutokubaliwa na wabunge wenzao.
 
Nitafanya sherehe nyumbani kwa kuandaa mlo mzuri nifurahi na familia yangu. Kitakachonifurahisha ni namna ccm itakavyokuwa imejiandalia anguko kuu ifikapo 2015. Hakika hilo likitokea, hata mbinu ya uchakachuaji haitafua dafu mbele ya hasira za wananchi ambao wengi wao sasa wametambua kuwa shida na mateso wanayoyapata yamesababishwa na ufisadi.
 
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............

Jamani kwani katiba ya nchi inamzuia Lowasa kuwa waziri mkuu?. Kujiuzulu nafasi hiyo kipindi cha nyuma bado si kigezo cha yeye kutochukua tena nafasi hiyo. Mbona Mwinyi alijiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani tokana na kashfa lakini baadaye akaja kuwa raisi wa Tanzania?.

Na kwa kifupi Lowasa kama Lowasa hakuwa na kosa katika sakata la Richmond, kujiuzulu kwake ni kwa ajili ya kuwajibika kwa maana kwamba waliokuwa chini yake hakutenda kilichopaswa kutendwa kwa wakati ule.
Kwa mtazamo wangu mimi Lowasa ni kiongozi mzuri sana. Anafuatilia maagizo aliyotoa, anawapelekesha mawaziri walio chini yake kufanya kazi na wala si kuleta longolongo. Lowasa haoni haya kumfukuza mtu mzembe kazi hadharani. Mawaziri na watendaji wavivu serikalini hawampendi Lowasa kwa sababu ni kiboko yao. Na ndiyo hao wavivu wameweza kumpikia majungu kwa lengo la kumwangusha ili kuendeleza uzembe na longolongo serikalini.

Jakaya tafadhali nakuomba mrudishe Lowasa katika nafasi ya uwaziri mkuu na Pinda mpe wizara nyingine.
 
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............
nitanyamaza kimya kabisa kwani ile shughuli ya advocacy kwa wananchi kufahamu ubaya wa ccm itakuwa imepata mwalimu mwema wa vitendo.
Na kama kawaida wabunge wa ccm watampitisha kwa kishindo maana hawajui nini maslahi ya taifa na nini maslahi ya chama.
 
Back
Top Bottom