Nini tufanye kama JK atamteua e lowassa kuwa waziri mkuu?

kwa kweli sioni tabu sana kama kikwete atamteua lowasa. Ingawa lowasa amamekutwa na kashfa hizo ukichunguza kwa makini utagundua kuwa ni mtu anayeipenda sana nchi yake, ni jassiri na anachapa kazi. Kwa lowasa naona ni kitu. Pia naye ameshajifunza kutokana na upepo wa mabadiliko. Tuache kuhukumu kwanza maana nasi tutahukumiwa

lowasa ni mchapa kazi, ila kale kakashifa kaufisadi kanaudhi sanaa, lakini ni mtu makini katika utendaji,
kulingana na system ilivyo nitafurahi tuu kwasababu wote waliopo ni madudu tuu isipokuwa wachache sana. Akimteua is okay lakini tuwe macho anaweza kuja na hasira zake ..
 
Hapana hapana hapana huwezi rudia matapishi yako mwenyewe hata kama chakulahicho kilikugharimu mamilioni.
 
Bora Lowassa Mwizi mchapakazi kuliko mtoto wa mkulima mr Pinda muadilifu lakini muoga si jasiri.Fisadi mchapakazi ni bora kuliko muadilifu mzembe.

Unamaanisah kama analiingizia taifa shs 10 halafu anaiba shs 100 tuendelee kumkumbatia tu,haikubaliki!
 
sasa kama alimshika mkono monduli na kuomba wapiga kura wamchague kwasababu ni mchapa kazi na mtu makini kwann ashindwe kumteua kama waziri mkuu?na atafanya hivyo kwa kigezo wananchi wenyew wamemsafisha kwa kumchagua tena kuwa mbunge wao..siasa za Tanzania ni ngumu sana jamani,hazitabiriki!
 
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............

Mkuu mawazo yako kwako ni sahihi ila ulilowaza ni sawa na kusema ' hivi itakuwaje kama ukiamua kuchukua sindano uchome mwamba wa jiwe kwa ajiri ya kuvuta damu'
Ukipata jibu lake itakuwa umepata jibu la hoja yako
 
Wakubwa kwa CCM sio ajabu, inawezekana kabisa..... hawa jamaa ni uso wa kauzu mkavu...... wanaweza wakafanya hiii......na hata wanajua 2015 ipo....wakiwa na hakika Katiba bado itakuwa ni hii hii kwahiyo haitawazuia kuchakachua tena kama kawa.........
 
Jamani kwani katiba ya nchi inamzuia Lowasa kuwa waziri mkuu?. Kujiuzulu nafasi hiyo kipindi cha nyuma bado si kigezo cha yeye kutochukua tena nafasi hiyo. Mbona Mwinyi alijiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani tokana na kashfa lakini baadaye akaja kuwa raisi wa Tanzania?.

Na kwa kifupi Lowasa kama Lowasa hakuwa na kosa katika sakata la Richmond, kujiuzulu kwake ni kwa ajili ya kuwajibika kwa maana kwamba waliokuwa chini yake hakutenda kilichopaswa kutendwa kwa wakati ule.
Kwa mtazamo wangu mimi Lowasa ni kiongozi mzuri sana. Anafuatilia maagizo aliyotoa, anawapelekesha mawaziri walio chini yake kufanya kazi na wala si kuleta longolongo. Lowasa haoni haya kumfukuza mtu mzembe kazi hadharani. Mawaziri na watendaji wavivu serikalini hawampendi Lowasa kwa sababu ni kiboko yao. Na ndiyo hao wavivu wameweza kumpikia majungu kwa lengo la kumwangusha ili kuendeleza uzembe na longolongo serikalini.

Jakaya tafadhali nakuomba mrudishe Lowasa katika nafasi ya uwaziri mkuu na Pinda mpe wizara nyingine.

Unaposema hivyo tukuelewe kuwa ni mvivu wa kufikiri au una maslahi katika uwaziri mkuu wa Lowasa? unaijua Richmond ni mali ya nani? Lowasa alipoambiwa ajipime pale bungeni, alijipima akajiuzulu. kama alijuuzulu kwa makosa hata kama yalitendwa na mke wake si yalimchafua yeye? kurudi kwenye uwaziri mkuu kutatusaidia nini?
 
mtu atakaye weza kuthibitisha lowassa kaiba nini alete data , lakini kama ni longolongo tu lowassa atatoboa mbali sana . huyu jamaa ni mchapakazi wa hali ya juu hataki uzembe wa ujinga serekalini ndio maana wengi hawampendi , kila mtu anasema jamaa fisadi lakini hakuna hata mmoja aliweza kutoa ushaidi aliiba wapi . sio haki hata kidogo. akiwa waziri mkuu mambo mengi sana yatanyooka , wakenya wataacha kutuchezea kwenye mbuga zetu za wanyama kama wanavyotupinga sasa kujenga mahoteli npks zetu , natamani sana lowassa kurudi maana sio mwoga hata chembe.
 
:thinking:DDDuuuuuu???? itawashangaza wengi wasio mjua wahite hair, ila nawaambieni wana JF wenzangu, Lowassa ni shoka la chuma cha pua kwa maana ya utendaji kazi na kuleta maendeleo halisi yenye tija. Ni bhati mbaya tu alikuwa mbuzi wa kafara wakati ule ila JK akimrudisha tutajionea maendeleo ya ajabu na hata hao mafisadi pia watamkoma. wanaomfahamu watakuwa wamenielewa hapa
 
Wewe unaelewaje utendaji wa kazi, utendaji wa kazi ni pamoja na uadilifu. Nenda kawaone wafungwa wanavyolima kwa bidii, na vifungo vyao havikatizwi kwa sababu wanalima sana.

Ukishakuwa mwizi wewe si mchapa kazi. Watanzania tumezoea sana ubazazi mpaka tunahalalisha wezi ili mradi wanafanya mambo yao kwa bidii.
 
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............

je wewe una haibu?
 
Fukuza mkeo aliyempigia JK kura, Mwanza washashi waliwanyanganya wake zao shahada za kupigia kura.
 
jamani nimeomba mwenye data zozote za wizi wa lowassa aziweke hapa sio kuongea vitu ambavyo hujui tusiwe tunafata mkumbo kama wale nyumbu wa serengeti . hii itasaidia kukata mzizi wa fitina . tukijua anahusika na wizi wowote tutampiga chini kama hausiki tutamuunga mkono awe presidaa wa 2015
 
- Wakuu ninaomba kuuliza kama Mh. Lowassa leo akiamua amechoshwa na CCM na akaitosa in the public kwamba ni chama ambacho hakifai na kwamba sasa anahamia Chadema, maana ni chama kinachofaaa zaidi, je Chadema watamkataa?

William.
 
Jina la Lowassa limeshakuwa na taste mbaya mdomoni, kwani amefanya maovu mengi na amajijengea maadui wengi. Lakini ningependa ku-act as a devil advocate hapa, nadhani Tanzania inahitaji waziri mkuu mwenye calibre ya Lowassa ili kuweza kusukuma maendeleo katika nchi yetu. Pinda ni kiongozi mzuri kwa nchi zenye strong institutions na sio kwenye nchi yetu. Lowassa aliweza kuwapush wakenya around katika kupambana na trade imbalance katika EAC zaidi kwenye mambo ya tourism, aliweza kujenga shule nyingi katika nchi yetu. Kipindi cha uongozi wake kuna vitu vingi tangible vilifanywa na serikali.
 
- Wakuu ninaomba kuuliza kama Mh. Lowassa leo akiamua amechoshwa na CCM na akaitosa in the public kwamba ni chama ambacho hakifai na kwamba sasa anahamia Chadema, maana ni chama kinachofaaa zaidi, je Chadema watamkataa?

William.

William,

CHADEMA is the only party that is a threat to CCM in the mainland momentarily. (CHADEMA) is endowed with astute politicians, who will vehemently disagree with what you have suggested. To allow EL to join CHADEMA will be the end of CHADEMA, this will be a political suicide in the making. It is imperative to understand that EL comes with a bargage that will have detrimental effect on the party; to make a long story short , he is not worth the risk.
 
Back
Top Bottom