Nini Tofauti kati ya Mazishi na Maziko??

Mazishi ni mchakato mzima wa kuandaa na kumweka marehemu kaburini. Maziko ni sanda zinazotumika kumsitili marehemu kaburini.
 
Msiba ni kuelezea shuguli ya mfu.
Kilioni ni sehemu watu wanapo lia.
Matanga ni shuguli baada ya kutoka makaburini.
Kufa na kufariki naona ni maana moja.


Kwenye red si kweli, kufa ni kupotelewa uhai, kufariki ni kuondoka/kujitenga.... na kama kuondoka/kujitenga huko ni kwa kufa basi shurti isemwe fulani kafariki dunia. ukisema tu kafariki, weledi watauliza kenda wapi. Pia waweza sema tumefarikiana na ndugu au jamaa yangu(ambaye hamjaonana siku nyingi)
 
Wachangiaji wooote mmekosea!

Nimefuatilia namna wote mlivyo changia hii mada na kugundua kuwa wote mmekosea.

Maziko na Mazishi yote yanamaanisha kitu kimoja



Kwa Mujibu wa Kamusi ya TUKI



Maziko
nm [ya-] funeral, burial, interment, exequies:
Mazishi nm [ya-] funeral, burial.




Sasa kwa sababu kuna maswali mengine yameongezwa hapa ngoja niwajibu!



Msiba nm mi- [u-/i-] bereavement, sorrow, misfortune; disaster.
(ms) Hakuna matanga usiokuwa na mwezi - misfortune never comes singly;

Msiba mkuu - catastrophe.


Matanga nm [ya-] mourning period: Weka matanga - remain in mourning; Vunja/ondoa matanga - end mourning;


Kilio nm vi- [ki-/vi-] 1 wailing. 2 cry, shout. 3 mourning. 4 problem. Kilio cha maji water problem.




.
 
kwa kidhunun sijanyaka, tupe tafsiri kwa kamusi ya kiswahili kwa kiswahili
 
kwa kidhunun sijanyaka, tupe tafsiri kwa kamusi ya kiswahili kwa kiswahili

.
Mkuu, Hujaelewa nini? .. kwani hapo si kuna kidhungu na Kiswahili?

Haya kwa kiswahili!


1. Funeral n 1 mazishi; maziko

provide a funeral =
zika
attend a funeral = hudhuria mazishi
perform a funeral service (Muslims) soma talakini.​



2. Burial n maziko, mazishi; kuzika

requisites for burial =
vifaa vya mazishi.
3. Burial-ground n. makaburini, maziarani, mavani.

4. Burial service
n ibada ya kuzika; talakini

say burial service = soma talakini.

5. Interment
n maziko; kuzika.

6. Exequies n (pl) maziko.

7. Bereavement n 1 (tendo au hali ya) kufiwa. 2 msiba.


Na haya yote yanakujia kwako ni kwa HISANI ya watu wa KAMUSI ya TUKI!

.
 
Mi nadhani mazishi ni maandalizi (mpaka wakati wakufika makaburini) ya kumzika marehemu.
Maziko ni kitendo cha kuanza kuweka mwili makaburini.

Mazishi umepatia lakini Maziko sidhani kama uko sahihi. Maziko yasound ka nomino hivi yaani ni sehemu ambapo marehemu anazikwa.
 
Tuendelee na mjadala naona kumekuwa na hoja mchanyato
 
Msiba ni kuelezea shuguli ya mfu.
Kilioni ni sehemu watu wanapo lia.
Matanga ni shuguli baada ya kutoka makaburini.
Kufa na kufariki naona ni maana moja.
pamoja sana tz1, kwa kuongezea kufa inafaa zaidi ikitumika kwa wanyama
na kufariki kwa binadamu, sawa na kuzaa ni kwa wanyama na kujifungua ni
kwa binadamu....hii ni kwa ajili tu ya kutofautisha kati yetu na wanyama
 
Mi nadhani mazishi ni maandalizi (mpaka wakati wakufika makaburini) ya kumzika marehemu.
Maziko ni kitendo cha kuanza kuweka mwili makaburini.

Umesema kinyume cha mambo. Maandalizi YOTE ni MAZIKO, wakati MAZISHI ni kitendo cha kuweka mwili wa marehemu kaburini!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom