Nini Nimejifunza kutoka Ze Utamu na RM/RA Saga

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Zeutamu:

1. Wengi walilalamika kuwa zeutamu inawadhalilisha na wakataka ifungwe - hakuna aliyerespond.

2. Wengi walilalamika kuwa zeutamu imevunja ndoa zao na mahusiano na wapenzi wao na wakataka ifungwe - hakuna aliyesikiliza

3. Baadhi wakaandika kuwa kuna watu wamejiua kwa ajili ya zeutamu na wengine wajijidhuru na hata kuathirika kisaikolojia hakuna aliyesikiliza . . . .

4. Na hatimaye Mkuu Wakaya akadhalilishwa . . . . Usalama wa taifa hakuna aliyekuwa na amani, vijana wote wakaingia kazini, Police Force wakaingia kazini, Intelpol wakaingia kazini na hatimaye zeutamu haipo tena. Yote hayo yalifanyika katika muda mfupi sana . . . . . . .

RM/RA Saga

1. Wananchi wameumia sana miaka mingi kwa ajili ya ufisadi . . . hakuna aliyewasikiliza

2. Wananchi wamekufa sana kwa ajili ya umasikini ambao wakati mwingine umesababishwa na ufisadi hakuna aliyeshtuka

3. Hatimaye List of Shame ikatajwa . . . . Matokeo yakaanza kuonekana

4. Hatimaye Mafisadi wakubwa wakaanza kutajwa . . . na sasa mengi yafichuka na yataendelea kufichuka na najua kutakuwa na matokeo.

Just wondering . . . Nchi hii mambo hayafanyiki hadi wakubwa na mafisadi waguswe.

Nimejifunza kuwa ili nchi hii mambo yaende sasa ni lazima kuwagusa wakubwa na mafisadi?

Kama si hivyo . . . Why things do not happen the way they should happen?
 
Since when haipo hewani Mkuu??
 
It is very frustrating, welcome to the club of the frustrated bro, welcome to the club. But one thing for sure , we won't be frustrated forever....that is for sure.
 
Since when haipo hewani Mkuu??

Nafahamu hoja ya msingi umeshaifahamu lakini lugha inaleta tabu.

Ni hivi: Maalbino wameuwawa sana, lakini je mpaka sasa kuna suluhu yoyote ya hili jambo? Je hawapo hewani? kama wapo ni nini wanafanya?

Mkku wa kaya alipoguswa speed ya utendaji na performance iliongezeka kuliko kawaida. Maboss walikuwa matumbo juu. Hawakulala.

Next question please . . .
 
Since when haipo hewani Mkuu??

Hiyo Website haipo hewani toka jana Mchana kwa saa za Tanzania,hapa Jamii pakiwa ni baadhi ya vyanzo vya habari ya wanaouendesha mtandao huo...Tusijisifu kwamba mtandao huo umekufa tuzidi kuendelee kutoa ushirikiano ili usirudi tena Hewani....Lakini baadhi ya watu walioulizwa nani anauendesha wanatoa ushirikiano mzuri......kwa taarifa tu watatajana wengi na hatimaye Kinara atashikwa.......Kizuri na kikubwa imejulikana ni wapi picha nyingi zinakuwa Posted...kwa maana hiyo inawezekana Kinara wa mambo hayo yupo Eneo hilo....Tuendelee kufahamishana yaliyo mazuri na yale yote mabaya tushirikiane pia kuyapiga Vita!!

Kikubwa ni kwamba tuwe na heshima na staha katika kuandika mambo humu..tusitumie uhuru huu kupakana matope na kuchafuliana majina...Usijipe faraja kwamba upo peke yako unapoandika hapa,na unaweza kuvurumisha kila namna ya kashfa...kufikiri hivyo tu ni upungufu wa uungwana...Tujenge tabia ya kupendana na kuheshimiana!!Huo ndio utaratibu na utamaduni tuliyouzoea...
 
It is very frustrating, welcome to the club of the frustrated bro, welcome to the club. But one thing for sure , we won't be frustrated forever....that is for sure.

Time will tell . . . . Let us wait and see.

However, something seriously need to be done.
 
The answer to your question is: THEY JUST DON'T CARE! Viongozi wetu hawajali, hebu kumbuka mabomu ya Mbagala, bunge liliendelea kama kawaida na Pinda alibaki mpaka saa 2 usiku bungeni hakuna hata kusimama kuwakumbuka wahanga wala nini! Unafikiri ni kwa kwa nini? THEY DON'T GIVE A DAMN!
 
Hiyo Website haipo hewani toka jana Mchana kwa saa za Tanzania,hapa Jamii pakiwa ni baadhi ya vyanzo vya habari ya wanaouendesha mtandao huo...Tusijisifu kwamba mtandao huo umekufa tuzidi kuendelee kutoa ushirikiano ili usirudi tena Hewani....Lakini baadhi ya watu walioulizwa nani anauendesha wanatoa ushirikiano mzuri......kwa taarifa tu watatajana wengi na hatimaye Kinara atashikwa.......Kizuri na kikubwa imejulikana ni wapi picha nyingi zinakuwa Posted...kwa maana hiyo inawezekana Kinara wa mambo hayo yupo Eneo hilo....Tuendelee kufahamishana yaliyo mazuri na yale yote mabaya tushirikiane pia kuyapiga Vita!!

Kikubwa ni kwamba tuwe na heshima na staha katika kuandika mambo humu..tusitumie uhuru huu kupakana matope na kuchafuliana majina...Usijipe faraja kwamba upo peke yako unapoandika hapa,na unaweza kuvurumisha kila namna ya kashfa...kufikiri hivyo tu ni upungufu wa uungwana...Tujenge tabia ya kupendana na kuheshimiana!!Huo ndio utaratibu na utamaduni tuliyouzoea...

Mwawado;

Ninachofahamu, next day baada ya kumdhalilisha mkuu wa kaya, haikupatikana tena. For sure I know Intelpol na vijana wa ICT Usalama wa Taifa waliplay role kubwa.

Maoni yako mengine nakubaliana nayo with a note kwamba: Je mambo hayatokei nchi hii mpaka tu watu wakubwa waguswe?
 
The answer to your question is: THEY JUST DON'T CARE! Viongozi wetu hawajali, hebu kumbuka mabomu ya Mbagala, bunge liliendelea kama kawaida na Pinda alibaki mpaka saa 2 usiku bungeni hakuna hata kusimama kuwakumbuka wahanga wala nini! Unafikiri ni kwa kwa nini? THEY DON'T GIVE A DAMN!

YES, they dont care! May be they care only wakiguswa!
 
Hiyo Website haipo hewani toka jana Mchana kwa saa za Tanzania,hapa Jamii pakiwa ni baadhi ya vyanzo vya habari ya wanaouendesha mtandao huo...Tusijisifu kwamba mtandao huo umekufa tuzidi kuendelee kutoa ushirikiano ili usirudi tena Hewani....Lakini baadhi ya watu walioulizwa nani anauendesha wanatoa ushirikiano mzuri......kwa taarifa tu watatajana wengi na hatimaye Kinara atashikwa.......Kizuri na kikubwa imejulikana ni wapi picha nyingi zinakuwa Posted...kwa maana hiyo inawezekana Kinara wa mambo hayo yupo Eneo hilo....Tuendelee kufahamishana yaliyo mazuri na yale yote mabaya tushirikiane pia kuyapiga Vita!!

Kikubwa ni kwamba tuwe na heshima na staha katika kuandika mambo humu..tusitumie uhuru huu kupakana matope na kuchafuliana majina...Usijipe faraja kwamba upo peke yako unapoandika hapa,na unaweza kuvurumisha kila namna ya kashfa...kufikiri hivyo tu ni upungufu wa uungwana...Tujenge tabia ya kupendana na kuheshimiana!!Huo ndio utaratibu na utamaduni tuliyouzoea...

Mkuu shukrani kwa hiyo reminder hapo juu.........ni muhimu sana kukumbushana ili kurudi kwenye mstari...........
 
Kikubwa ni kwamba tuwe na heshima na staha katika kuandika mambo humu..tusitumie uhuru huu kupakana matope na kuchafuliana majina...Usijipe faraja kwamba upo peke yako unapoandika hapa,na unaweza kuvurumisha kila namna ya kashfa...kufikiri hivyo tu ni upungufu wa uungwana...Tujenge tabia ya kupendana na kuheshimiana!!Huo ndio utaratibu na utamaduni tuliyouzoea...
aah usitutishe......kama kuchafuana haoo viongozi wako wameshatuchafua vya kutiosha watanzania.....kawaambie kwanza hao viongozi wako wache wizi....

....kupendana tupendane vipi mkuu kama baba mama hawatupendani iweje watoto wawapende wazazi wao.....nawachukia raisi na watendaji wao woote....ndio siwapendi....nifungeni
 
YES, they dont care! May be they care only wakiguswa!

Superman...Maneno yako yana ukweli usiopingika,Lakini ni nani wa ku-act?.Tatizo la mambo yetu ya nyumbani kila mtu ni mwepesi kumtupia lawama mwingine...Naapa hapa kwamba kama kila mtu akiujua umuhimu wake kwa jamii Tanzania ni Bora kuliko tunavyoifikiri....baadhi ya masuala hayataki miongozo ya serikali bali ni kila mtu kujua wajibu wake kama Mzazi au Mtanzania!!

Naomba unielewe sitetei uozo uliopo serikalini,lakini nasi kama mtu mmoja mmoja tupende kujituma kwa manufaa yetu na wenzetu.
 
Hiyo Website haipo hewani toka jana Mchana kwa saa za Tanzania,hapa Jamii pakiwa ni baadhi ya vyanzo vya habari ya wanaouendesha mtandao huo...Tusijisifu kwamba mtandao huo umekufa tuzidi kuendelee kutoa ushirikiano ili usirudi tena Hewani....Lakini baadhi ya watu walioulizwa nani anauendesha wanatoa ushirikiano mzuri......kwa taarifa tu watatajana wengi na hatimaye Kinara atashikwa.......Kizuri na kikubwa imejulikana ni wapi picha nyingi zinakuwa Posted...kwa maana hiyo inawezekana Kinara wa mambo hayo yupo Eneo hilo....Tuendelee kufahamishana yaliyo mazuri na yale yote mabaya tushirikiane pia kuyapiga Vita!!

Kikubwa ni kwamba tuwe na heshima na staha katika kuandika mambo humu..tusitumie uhuru huu kupakana matope na kuchafuliana majina...Usijipe faraja kwamba upo peke yako unapoandika hapa,na unaweza kuvurumisha kila namna ya kashfa...kufikiri hivyo tu ni upungufu wa uungwana...Tujenge tabia ya kupendana na kuheshimiana!!Huo ndio utaratibu na utamaduni tuliyouzoea...

Yale yale ya Mussolini, Let their heads be seen but not their voices! Duuh, hawa katsa wa Tanzania bwana, kazi kwelikweli
 
Superman...Maneno yako yana ukweli usiopingika,Lakini ni nani wa ku-act?.Tatizo la mambo yetu ya nyumbani kila mtu ni mwepesi kumtupia lawama mwingine...Naapa hapa kwamba kama kila mtu akiujua umuhimu wake kwa jamii Tanzania ni Bora kuliko tunavyoifikiri....baadhi ya masuala hayataki miongozo ya serikali bali ni kila mtu kujua wajibu wake kama Mzazi au Mtanzania!!

Naomba unielewe sitetei uozo uliopo serikalini,lakini nasi kama mtu mmoja mmoja tupende kujituma kwa manufaa yetu na wenzetu.

Mwawado usitake nicheke mie, ukijituma kama mzalendo mengi ukasema jamani mafisadi wanao tumaliza hawa hapa, serikali wanakujia juu kama moto wa kifuu cha nazi kwamba wewe mamlka hayo kakupa nani? need more ndugu yangu?

Tanzania nadhani ni mwendo wa ze utamu tu.. yaani kuwalipua vigogo wakifeel inavo uma ndo mambo yanaenda!
 
Hiyo Website haipo hewani toka jana Mchana kwa saa za Tanzania,hapa Jamii pakiwa ni baadhi ya vyanzo vya habari ya wanaouendesha mtandao huo...Tusijisifu kwamba mtandao huo umekufa tuzidi kuendelee kutoa ushirikiano ili usirudi tena Hewani....Lakini baadhi ya watu walioulizwa nani anauendesha wanatoa ushirikiano mzuri......kwa taarifa tu watatajana wengi na hatimaye Kinara atashikwa.......Kizuri na kikubwa imejulikana ni wapi picha nyingi zinakuwa Posted...kwa maana hiyo inawezekana Kinara wa mambo hayo yupo Eneo hilo....Tuendelee kufahamishana yaliyo mazuri na yale yote mabaya tushirikiane pia kuyapiga Vita!!

Kikubwa ni kwamba tuwe na heshima na staha katika kuandika mambo humu..tusitumie uhuru huu kupakana matope na kuchafuliana majina...Usijipe faraja kwamba upo peke yako unapoandika hapa,na unaweza kuvurumisha kila namna ya kashfa...kufikiri hivyo tu ni upungufu wa uungwana...Tujenge tabia ya kupendana na kuheshimiana!!Huo ndio utaratibu na utamaduni tuliyouzoea...

You are some how right ila tuu mkuu huwezi kueshimiwa kama ujiheshimu na unadhurumu wanyonge. Tanzania tunaogopana na ndio hicho kimetuangamiza kwanzia maradhi mbalimbali kama ukimwi na hata mafisadi kutuibia mchana mchana kwasababu no one is dare to talk.

Nchi za wenzetu mtu ambaye ni public figure inabidi awe mfano wa jamii kwa matendo bora na kuthamini utu wa watu na familia/ndoa yake. Asipofanya wananchi hawampi kura lakini tanzania mtu wa aina hiyo tunampa vote 110%!! mimi nafikiri utamu imesaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha tabia za watu na kuokoa maisha ya wale waliokuwa hawajui wameoa watu wa aina gani au wanawapenzi wa aina gani, kwa maana nyingine its is possible utamu imechangia kupunguza ukimwi na maradhi mengine tanzania.

haya ni maoni yangu binafsi
 
aah usitutishe......kama kuchafuana haoo viongozi wako wameshatuchafua vya kutiosha watanzania.....kawaambie kwanza hao viongozi wako wache wizi....

....kupendana tupendane vipi mkuu kama baba mama hawatupendani iweje watoto wawapende wazazi wao.....nawachukia raisi na watendaji wao woote....ndio siwapendi....nifungeni

That's it comrade!
 
vitu ambavyo nimejifunza kutoka kwenye ze utamu ni
1. viongozi wetu ni watu ambao wanajali maslahi yao tu na si vinginevyo, kinachokutokea wewe hakimuhusu mpaka kimpate na yeye
2. bado tuko mbali sana kwenye mapambano na watanzania hatupendani na ni wanafiki baadhi ya watu JF wanafuraia ze utamu kufungwa, huu ndio ulikuwa wakati wa kupandisha mashambulizi dhidi serikali lakini tunatumia muda huu wengine kufuraia na hichi ni kielelezo tosha kwamba mtu akimchafua tu mkulu atasulubishwa vya kutosha na wengine watafuraia.
3. mimi binafsi yangu naona utamu walivyoweka ile picha ya mkulu ni sawa sawa kwa ajili sisi raia wa kawaida hatuna kitu cha kumfanya wakati yeye na wenzake wanachukua chetu. utamu amepeleka mashambulizi pale yanapotakiwa kwenda
4. utamu itarudi tu very soon........

mtu anayegombana na mbaya wako ni rafiki yako na si adui yako
 
Ze Utamu imefungwa eti kwa vile mkuu wa Kaya kaumbuliwa?Hivi kuumbuliwa ni kitendo cha kusingiziwa au ni kuanikwa Hadharani watu wakuone jinsi ulivyo??Kuumbuliwa ni kubambikizwa mambo ambayo kamwe hujawahi fanya ni mwiko kwako, au ni kuweka wazi mambo unayo yafanya mafichoni kwa siri huku hadharani ukijifanya unamzidi hata kadinali Pengo kwa Utawa??? Imefungwa kweli??Ni vipi sisi wanachama wake mashuhuri tusioweza kwenda kulala bila kujivinjari kwenye Tovuti hii ya uchiuchi bado tunaweza kupata habari mototo za Ze Utamu bila shida?Kwani kuna Kuna Ze Utamu ngapi hapa Duniani??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom