Ablessed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 4,616
- 3,499
- Thread starter
- #21
Dah umeongea kiundani sana , kiukweli hiki ulichoandika ni sehemu ya ukweli dear. Ina maana mume anapaswa kuwajibika vema/ kutimiza wajibu wake. Unajua mimi nimeishi na mama wa kambo tulifanya kila lililojema juu ya mama huyu lkn alichoturudishia ni maumivu tu. Hata wanae walikua wakitusogelea basi wanapigwa utadhani wamesogelea kifo. Kumbuka yeye alitukuta pale home. Baada ya kua na maisha yetu tumemsomeshea watoto wake wote na sasa wengine wanafanya kazi. Nae alikuja na mwanae pia tulimtendea wema wote ikiwa pamoja na kumsomesha kwani tulijifunza kuwa usilipize kisasi. Sasa naelewa kumbe matatizo mengine yanasababishwa na baba kuwa either kumuamini sana mkewe na kutowafuatilia watoto.Sijalelewa na mama wa kambo na bado sijawahi kuwa mama wa kambo ila nimekuwa mama wa yatima.
Ila mama yangu keshalea mama wa kambo.
Kuna kipindi ilibaki kidogo tuletewe mama wa kambo wakati baba na mama walivyotengana.
Nakumbuka kaka zangu walikuwa wakiambizana jinsi gani watakavyomfanyia visa huyo mama akiletwa. Thank God it never happened.
Ninachoweza sema, kuna aina 2 ambazo zinamchango mkubwa sana wa mahusiano ya watoto na step parents zao.
1: watoto uliowakuta, mara nyingi chuki kwa watoto hawa huwa si kubwa sana unless the wife is a real monster.
2: watoto wakiokukuta, ingawa watoto ni honest hawana kosa lkn ni wamama wachache sana (mine included) wanaoweza ishi nao vizuri.
Sasa ni nini keinachochangia (in either cases) mama akamtreat vibaya mtoto wa mumewe.
1: mume kutukuwa na uwezo wa kuiongoza familia
2: mume kuabuse mkewe ambaye naye hutafuta mnyonge wake
3: mume kuwa malaya na kutoitimizia familia mahitaji
4: mawifi kuingilia na mara nyingi kuwapenda watoto wa kambo kuliko wa ndoa
5: tabia au roho mbaya ya mke.
Sasa nini cha kufanya.
Kabla ya kumuintroduce mtoto kwa mke na mke kwa mtoto, baba ongea nao kwa undani na kwa kutulia.
Baba uwe na muda wa kutosha na familia ikiwezekana hakikisha mnasali pamoja jioni.
Mtrust mkeo, na mwambie amlee mwanao kama wake; asiache kumkanya kisa si mwanaye.
Ongea na mtoto, amuone mama wa kambo kama mama yake na amuheshimu.
Msigombane mbele za watoto na muwashirikishe wote ktk mipango yenu ya maendeleo.
Onesheni upendo kwa maneno na matendo.
Ni hayo tu Ablessed
Kwa mtazamo wangu , sintakua mbali sana na wewe ni kwamba wababa muwe karibu na watoto wenu . Na hili la kua karibu na watoto lifanyike kwa hekima sana ili mama asijione kua anadharaulika. Pia si kila anacholalamika mtoto juu ya mama wa kambo/ mama basi kinakua cha kweli la hasha vingine vinachanganyika na utoto/chuki. So baba ajaribu kubalance.