Nini maoni yako Kuhusu Muungano?

Hakuna sababu ya kuwa na muungano kama hakuna serikali moja. Na hata wale wanaosema kuwa pawe na serikali tatu yaani sesikali ya mapinduzi Zbar, serikali ya jamuuri ya Tanganyika na serikali ya jamuuri ya muuanga ya Tanzania pia naona hawatakua na jipya kwani bado hapatakuwa na faida yoyote zaidi ya kuOngeza matumizi ya pesa za walipa kodi kwa ajili ya kulipa msururu wa viongozi kwenye serikali hizo. Kama ni mahusiano ya kiuchumi tutakutana kwenye East African Community kwisha. Kama Zbar wana katiba yao inayowatambua kama nchi kwa nini watanganyika na sisi tusiwe na yetu? why? TO ma side mi naona hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho, hakuna kinachozali kisichokufa so huu ndio wakati muafaka wa kuiua Tanzania na kubakia na nchi mbili i.e. Tanganyika na Zanzibar kwa kua hata wazbar wanataka hivyo.
 
Wao wanauzanzibari (utaifa wao) wakati sisi tumeuua utanganyika wetu halafu wanataka usawa katika masuala ya katiba. this is unfair
Maoni yangu,
1.Huu muungano wa nchi Mbili ni lazima uzalishe serikari moja(Serikari ya jamuhuri ya Muungano ya Tanzania)-ni kiini macho cha hali ya juu kuwa nchi mbili zilizoungana zinazalisha serikali mbili eti ya Muungano na ya Zanzibar,hata mtoto mdogo wa darasa la chekechea anaelewa kuwa ilitakiwa serikali moja tu au ilitakiwa serikali tatu.
2.Haki ya mtanganyika imemezwa na Muungano huu,ni lazima tuutafute utanganyika wetu(asili yetu) kwa namna yoyote ile,kila binadamu ana asili yake nasi kama watanganyika tunataka asili yetu ya kuwa mtanganyika mtanzania.
3.Mambo ya muungano yaelezwe kinagaubaga pasipo maficho yoyote yale,Tunaficha nini?
4.Ikishindikana kabisa ningependa Muungano uvunjwe na kila nchi ibaki na haki zake kama nchi.

nawasilisha
 
Mimi naona Wazanzibar waachwe waamue hatma ya nchi yao. Lakini sote tunatokana( kama wanadamu) na BABA wa BWANA yetu YESU CHRISTO. Wale tunaomwamini YESU kuwa alikufa akazikwa na siku ya tatu akafufuka kwa ajili yetu, tutakutana katika UFALME ujao wa MUNGU na wale wasioamini makao yao ni katika ziwa lile liwakalo moto na kiberiti.

Duh! mapambio utafikiri uko wapo radio..
 
Kila upande(Tanganyika na Zanzibar) upige kura ya maoni kuamua kama tuwe na muungano au hapana, na kwa kuwa ili muungano uwe imara bila mushkeli inabidi ipatikane ridhaa ya pande zote mbili,na kama kura ya maoni ya upande wowote itasema hapana itamaanisha hakuna haja ya muungano hata kama kura ya maoni ya upande mwingine itasema ndiyo, na kama kura za maoni za pande zote mbili zitasema hapana ndio itathibitisha zaidi haja ya kutokuwa na muungano.Sasa kama kura za maoni za pande zote mbili zitakuwa NDIYO kwa muungano,itabidi tuingie katika hatua ya pili ya kukubaliana ni aina gani ya muungano tuwe nao,hii aina ya muungano tulio nao sasa wa 'Nyerere na Karume' itabidi usiingie kwenye mchakato kwa kuwa umeleta manung'uniko na malalamiko mengi na zaidi ya yote unachanganya vichwa vya watu!tubaki na aina mbili tu za muungano kupigia kura ya maoni yaani muungano wa serikali moja na ule wa serikali tatu, na kwa suala hili pia itabidi kila upande upige kura kuchagua aina gani ya muungano kati miundo hiyo miwili, iwapo matokeo ya kura za maoni ya pande zote mbili yatasema NDIYO kwa muundo unaofanana, huo ndio utakuwa muungano wetu, na hatua itakayofuata ni kuandika katiba itakayoendana na muundo huo (hapa namaanisha kuwa hata mchakato wa katiba wa sasa hauna maana mpaka tupate kwanza suluhisho la muungano) na iwapo matokeo ya kura za maoni ya pande zote yatatofautiana kuhusu muundo wa muungano yaani upande mmoja ukubali serikali tatu na upande mwingine ukubali serikali moja hapo itabidi kila upande uchukue ustaarabu wake yaani hakuna haja ya kuwa na muungano,Tanganyika kwao na Zanzibar kwao kila taifa lijiongoze lenyewe kwa mujibu wa katiba watazotengeneza wenyewe! hayo ndio maoni yangu.
 
Muungano ulikidhi malengo ya wakati ulipo asisiwa,kwa sasa hauna faida yoyote zaidi ya kuwa mzigo kwa walipa kodi wa Tanganyika.MUUNGANO UFE NA WAZENJI WAONDOKE BARA.
 
Kama hakuna uwezekano wa kuwa na serikali moja basi Muungano ni bora ufe tu. Maana hata USA wameungana zaidi ya mataifa 40 lakini wameweza kuwa na serikali moja. Kwa nini kwa TANZANIA iwe nongwa?? No Single Government, No Muungano
Ni vema Wazanzibari wakiamua hatima ya nchi yao. Lakini ni bahati mbaya kwamba jambo hilo halitakuwa zuri kwao kwa kuwa baada ya hapo hoja za uunguja na upemba zitaibuka! Wataingia katika machafuko. Wapemba nao watataka kujitawala kwa kuwa na serikali yao lakini wasiweze. Zanzibar itapitia kipindi kigumu kisiasa na kiuchumi. Baadhi yao watatamani muungano lakini wakati huo watanganyika watakuwa na serikali ya chama kingine ambayo haitakubali kuwepo muungano na Zanzibar.

Kwa sababu ya hali ngumu ya kisiasa na kiuchumi, vijana wengi wa Zanzibar watarubuniwa na kujiunga katika makundi ya magaidi (sio Al shabab). Wakati huo Al shabab itakuwa imekwishatokomezwa lakini yatakuwa yameibuka makundi mengine yenye msimamo mkali wa kidini na Zanzibar itachukiwa na nchi nyingi duniani kwa sababu ya kuwahifadhi magaidi. Ni bahati mbaya vilevile kwamba kukosekana kwa amani Zanzibar kutaiathiri sana Tanganyika. Kutakuwa na uhasama wa kisiasa baina ya Tanganyika na Zanzibar.
 
Wazanzibar Vigeugeu sana,
Unataka kuolewa halafu bado unataka uendelee kuishi kwenu, ushaona wapi hiyo?
Ukishachanganya Sukari, Maji na Majani unachopata ni Chai sasa, sio kimojawapo kiendelee ku-exist tena!!
Bora uvunjike tu tujue moja!!!
 
kwa vile muungano huu hauna faida na upande wowote ule tokea ulipoanzishwa 1964 basi bora uvunjwe kila nchi iwe kivyake.
Watanganyika na Wazanzibar watakutana katika mambo ya uchumi na mengineyo katika East Afrika Community.
Ni bora Zanzibar wakae na nchi yao na Tanganyika kivyao kama hapo zamani kabla ya kuungana. ni nchi nyingi tu duniani ziliungana walipochoka walivunja Muungano na kukaa kila nchi kivyake na wamezidi kufanya maendeleo mazuri tu bila ya kuleteana matatizo.
 
Back
Top Bottom